hii imeingia sasa hivi...
Kwako ndugu Issa Michuzi
Kwanza natanguliza pole na mchoko wa safari toka Dubai . Pili wasabahi wote huko nyumbani Dar-es-salaam. Tatu, naomba samahani kwa kiswahili changu kibovu.
Mimi ni mkazi wa Canada, si siku nyingi. Mimi ni mkongomani ambaye nimeishakaa Dar-es-salamm kwa siku kadhaa. Sehemu nyingi ninazijua, hata vichochoro vya Mbagala, Segerea, Tabata, Sinza, Kigira-gira lumo, Buguruni, Temeke, Mbezi,Gongolamboto... na penginepo. Mji huo, tumeuchezea.
Kwa kweli, Blog yako uwa inanifuraisha sana kwa sababu moja ao nyingine. Kila siku na kufata kwenye blog, unanitolea picha za leo-leo ambazo zinanikumbusha mengi, na zinanifanya niwe makini sana kwakuzifwatiliya. Unanivutiya sana kihasi kwamba kila mtu akifika nyumbani kwangu ( Canada ) anauliza: Michuzi anasema je?Blog ni yako, ila kuna picha ambazo utuahibisha ( kama picha ya yule baba mkubwa ya polisi, ambaye suruali imemfumuka yuma ), sio vizuri. Ila sasa kuna picha ambazo zinanipa hali na habari ambazo wewe mwenyewe umezitoa mbali sana, utafiti wako ni wajuu sana.
Kama usafiri Kinshasa, ambao unaaibisha, zimenifuraisha na kusikitisha, nchi kama Kongo... Ayasemeki. Ndo ulimwengu watatu huo.Umetoka Dubai, na madimbwi ya maji mitaani yakakuribisha nyumbani...huo ndio ulimwengu wa tatu.
Maisha ya nyumbani ayafuraishi ila ni nyumbani tu. Ndo cha muhimu. Jamaani, tufanyeje ili Afrika isonge mbele kama wengine ? Kuna profesa mtanzania kaandika kibatu: waafrika ndivyo tulivyo? Kwangu mimi, sio aulize swali, nakubali waafrika ndivyo tulivyo. Basi ndugu, lete raha na michuzi yako mitamu. Uko galerie Mavuzi, sio Kinshasa ? Kongo kuna lugha nyingi sana, usifikiri kama mavuzi ni mavuzi ambayo wewe unayajua, ni kitu kingine kabisa. Maswala ya lugha mwenzangu.
Nikuchekeche; nguo uwa ni mavazi sababu wanayavaa. Sasa, nguo wakizivua yanakuwa mavuzi, ao sio.Kuna kutakwa ( kama mtu mwenzie anamtaka= katakwa na mwenzie, matakwa , kiswahili cha kongo) na kutaka( kama mtu anataka= matako ), sio matako sehemu za mwili. Uko kongo, walokole wakiomba Mungu usema; Kwa matako ya Mungu pepo toka. Ndio lugha yenyewe.
Ebu nipe picha za leo-leo nzuri za mitaa ao vitongoji ambavyo vina nyumba za mjengo wa kisasa Dar. Nazitaka kwa hamu kubwa pitiya anwani yangu ao blog yako. Salam kwa mama watoto na watoto.
Tuwasiliane.
Papa Anzo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Kiswahili cha namna hii soyo kongo tu, hata zenji kipo; kufiwa wanasema...kufiliwa

    ile ile ya matako ya mungu .. na mavuzi! aah imenitikisa mbavu

    ReplyDelete
  2. Du hii kali

    ReplyDelete
  3. Hiyo ya matako nimeshawahi sikia na nilipigwa na bumbuwazi

    ReplyDelete
  4. Papa Anzo, nakupa zawadi kwa matako yangu, sina mavuzi ningekupa pia, umeipa utamu hii blog. tuambie maana ya avenue "korodani" pia kwenye hiyo picha chini kwenye hii blog.
    Kong'oli hapa http://haki-hakingowi.blogspot.com/2007/03/kabila.html

    ReplyDelete
  5. jamani
    mbona mimi hapa niko na wakongo wengi, na ukisema neno MATAKO kwao wanaliona ni tusi kubwa?

    sababu kuna siku nilisemaga MATAKO wakataka nimaliza, wanasema MATAKO si neno lakusemwa semwa, ni kali sana. sasa inakuwaje hapo PAPA ANZO?

    DAH LUGHA NYINGINE BWANA.
    NA UKISEMA UNAUZA KITU, KWA KISWAHILI CHA KONGO UNAMAANISHA UMENUNUA LOL!

    NA UKITAKA KUSEMA UMEUZA KW AKISWAHILI CHA KONGO USEME NIMEUZISHA EHEHEHE HENO HENO. ILA ANGALAU TUNAELEWANA.

    HAYA TUPE MAANA INGINE MAZEE.

    ReplyDelete
  6. Hawa jamaa zetu wa Congo walioishi Dar na kupata uraia wa "Bongo" wako wengi sana huku. Nimekutana nao New York mwaka jana na hapa Canada. Yaani uwezi kuamini kabisa Culture na tabia zao kama wabongo tu. Wakikutana na Wabongo huku wanajisikia raha sana, kama vile wamekutana na mtu wa nyumbani.

    ReplyDelete
  7. ...ahahaha ahah ahahah ahaha...sina mbavu!

    ReplyDelete
  8. Yaani huwezi kuchoka kuangalia picha za Michuzi. Keep it up na tunakufagilia sana. Ila suala la Avenue P***u linatisha lakini nikiri kuwa nishasikia 'Matako' mara nyingi likimaanisha 'matakwa'.

    ReplyDelete
  9. Papa Anzo, kamatilia hii zawadi hapo fasi ya kanada toka kwa Danny Engobo. Ni matako yangu.
    http://www.youtube.com/watch?v=MZIMjJSHd2U

    ReplyDelete
  10. Papaaa, ati ni kweli ukitaka kusemezana kuwa weka maji kwenye madumu makubwa makubwa wanasemezana "weka maji kumakubwa", au wakisemezana naomba nipande mbele wanasemezana "nitie mbele"
    au akiomba nipande nyumba bwana dereva wanasemezana "nitie nyuma shoferi"

    ReplyDelete
  11. Mwandishi SIO MKONGOmani bali ni mwongo na tapeli tu. anaigiliza kiswahili cha kikongo halafu anajisahau anaandika vizuri kiswahili sanifu na fasaha!!!

    ReplyDelete
  12. Mbona mnamfagili.... wabongo bwana. Mbona mimi nawajua wa congo wengi wanajua kiswahili kabisa...sasa nyie mnasema huyu sio mcongo ...mh.....

    Wewe tatizo lako nini kama sio mcongo ni yeye mwenyewe anajidanganya lakini katuelewesha vizuri. kwa hiyo cha maana nini amesema na sio nani ameandika...

    Wabongo tuache viswahili virefu..

    Mimi michuzi nachokuulizia ni wapi zawadi yake huyu. Mbona katoa point safi sana...au hii sio good kwako mpaka tutaje au tuwasifie viongozi wa CCM?

    ReplyDelete
  13. Lelo makambo lobi makambo nalembi ee
    Lelo bitumba lobi koswana nabayeee
    Naboyi kobebisa nzoto na manzaka nalembi eeee
    MAAARIO NALEMBI EEE
    MAAAARIO NABAYE EEE

    ReplyDelete
  14. PAPA AZO,Natafuta CD za FRANCO je huko zinapatikana,kama zipo tuwasiliane mimi niko WAsh,DC.

    ReplyDelete
  15. Ahhh! Papa Anzo umenivunja mbavu ndugu yangu. Canada uko mji gani? Hebu niambie si ajabu tuko mji mmoja na haitakuwa vibaya tukakutana ili kuyaongelea zaidi haya mambo ya mavuzi na matako ya mungu ha ha ha Mimi sikujua kama Mwenyezi Mungu naye ana matako, wabongo tunasema matakwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...