Home
Unlabelled
utalii
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Jamani hivi Tanzania wanaruhusu Watanzania kwenda kutalii nje ya nchi au wataruhusu lini?
ReplyDeleteMimi nilienda kuomba passport wizara ya mambo ya ndani nikajaza sababu ya kusafiri kwenye fomu ya maombi ya passport kuwa "KWENDA KUTALII MSUMBIJI" wakakataa kunipa passport,wakasema lazima nionyeshe barua ya mwaliko.
Hivi hawa uhamiaji wana matatizo gani kwani siwezi kwenda fikia Guest House?
Yaani Uhamiaji bado wana ukoloni wa kuamini mtalii ni mzungu tu,mtanzania hawezi kwenda kutalii nchi nyingine.Kutalii hakuhitaji hela nyingi kuna wazungu wengi nawazidi utakuta wanakuja na shilingi elfu 40 (dola 40)na kaptula Chafu na ndala,wanakula kwa mama ntilie na kula mahindi ya kuchomwa na maji ya shilingi 100.Hawa wanatambuliwa kama watalii hivi mimi nami siwezi hilo Msumbiji?
Kutalii kunasaidia. Kuna watu wanajua wawekeze wapi baada ya kutalii hata watanzania waweza jua cha kufanya katika nchi nyingine baada ya kwenda kutalii pia.Uhamiaji "wake up" huu ni wakati wa utandawazi.
safi sana Michuzi naona unatalii tu dumila heheheh. Hivi kuna nchi haujaenda ?naona imebakia Iraq tu
ReplyDeleteWewe hapo juu kwanini uende mambo ya ndani kuomba passiport kama huna hela au document yeyote inayokuonyesha unaenda nje?
ReplyDeleteKama sio barua ya mwaliko au shule ni lazima uonyeshe una hela za kuenda huko na kutembea bila shida. Wewe ni raia wa Tanznaia na nchi ina kila haki ya kuwaconcern na maisha yao. Ukipata shida huko nani watakurudisha bongo na kwa hela ya nani? Kwa hiyo kabla hawajakupa tuhiyo pass unatakiwa uoenyeshe kuwa unaenda mahali fulani.
Wewe unataka kutalii wakati bank huna hata ndururu? halafu msumbiji kuna kila kitu kama TZ sasa unataka kutalii nini huko?????... .Ndio nyie mnaoenda Cambodia kutalii au honeymoon nini???? lol
Ninaotakiwa kuwaonyesha kuwa nina hela za kutosha kwenda nje ni nchi ile ninakotakiwa kwenda kutalii.Siyo Tanzania.Msumbiji ndio walitakiwa waniulize kama nina pesa za kutosha kwenda na kuishi kwao siyo Tanzania.
ReplyDeleteTanzania wanajua ninazo ndio maana miaka yote nimeishi hapa bila kuomba kulishwa na wizara ya mambo ya ndani.
Pasipoti ni haki ya kila raia.Kila raia ana haki ya kuwa nayo ili wakati wote akijisikia kwenda kokote anaondoka hana haja ya kukimbizana kama mwanga "last minute" eti ana safari ya ghafla ndio asake pasipoti.Kwani nikiwa nayo nyumbani Uhamiaji kinawasumbua nini?
Tatizo Tanzania kuna uvunjaji mkubwa wa haki za binadamu Pasipoti inaonekana kama kitu cha wateule wachache jambo ambalo si sahihi hata kidogo.