Home
Unlabelled
huduma
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Aisee hii biashara inataka ukomae kichwa kweli sio legelege.
ReplyDeleteWangeanzisha Funeral Homes tu. Hebu nipeteni habari bongo kuna Funeral Homes? Je ukitaka kuanzika unatakiwa uwe na kibali gani?
ReplyDeleteNGO yadaiwa kutapeli watu Mwanza
ReplyDelete*Pia yadaiwa kutapeli wengine wengi Kanda ya Ziwa
*DC Ukerewe, Afisa Elimu washituka na kuingilia kati
Na Mwandishi Wetu
WAKATI serikali ipo katika mkakati wa kuinua elimu nchini, shirika moja lisilo la kiserikali lijulikanalo kama Concern for the Elderly (Coel-Tanzania) linadaiwa kuwachangisha fedha wananchi kwa lengo la kuwapatia mafunzo ya ualimu wa chapu chapu wa shule za msingi bila ya kibali cha Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili, umebaini kuwa shirika hilo limekuwa likichangisha Sh 47,000 kwa kila mtu anayetaka kujifunza mafunzo ya ualimu katika shirika hilo, ambayo yanaendeshwa kwa muda wa mwezi mmoja katika mikoa ya Tabora, Shinyanga, Mara na Mwanza.
Katika Mkoa wa Mara, mafunzo yalifanyika wilayani Bunda katika Chuo cha Ualimu ambako waliojiunga walikuwa ni 220 awamu ya kwanza na baadaye watu 150. Mkoani Tabora mafunzo hayo yalihusisha watu zaidi ya 400 kutoka katika wilaya mbalimbali na katika Mkoa wa Mwanza,
mafunzo haya yalifanyika katika Wilaya ya Ukerewe ambako na watu zaidi ya 300 walihitimu.
Katika mafunzo hayo ya ualimu, kila aliyetaka kujiunga alilipia katika shirika hilo Sh47,000, fedha hizo zikijumuisha Sh25,000 kwa ajili ya ada ya mafunzo, gharama za malazi chuoni Sh 5,000, gharama za vitini vya mafunzo (handouts) Sh15,000 na Sh2,000 kwa ajili ya mahafali kumaliza mafunzo.
Kuhusu mafunzo hayo, mmoja wa watu walioshiriki mafunzo hayo wilayani Ukerewe, Sikitu Makene Matete ambaye alilipia ada sh 25,000 kupata mafunzo hayo ya ualimu kwa matarajio ya kupatiwa ajira Oktoba 9, 2006 na kupewa stakabadhi ya malipo, alidai yeye alilipia mafunzo hayo baada ya kuambiwa kuwa pia watapatiwa ajira ya ualimu katika shule ya msingi.
Shirika la Coel-Tanzania limesajiliwa Juni 2, 2000 chini ya sheria ya mwaka 1954 kifungu cha 337 kwa wakati huo na kupata hati ya usajili namba S0. No: 10448 iliyosainia na J. G. Maleko msajili wa mashirikaya kijamii wa Wizara ya Mambo ya Ndani (wakati huo), linajishughulisha na uzuiaji wa mauaji ya wazee vikongwe, ikiwa ni pamoja na kutoa elimu juu ya mila potofu za kishirikina zinazosababisha mauaji ya wazee.
Hata hivyo, kubainika kwa mafunzo hayo yanayotolewa na shirika hilo, kumekuja siku chache baada ya Mbunge wa Ukerewe, Balozi Gertrude Mongella, kupokea malalamiko kutoka kwa wakazi wa jimbo hilo ambapo aliwaomba kuyafikisha malalamiko yao kwa Mkuu wa Wilaya.
"Nilipata malalamiko kutoka kwa wananchi kuwa wamemaliza mafunzo ya ualimu lakini serikali imechelewesha ajira zao, wakiniomba nisaidiekuhakikisha wanapangiwa shule ili waanze kufunzisha kwa vile wamehitimu, baada ya kufuatilia mafunzo hayo nilivyoelezwa niliambiwa wamepewa na shirika hilo na walikuwa wakilipia fedha za mafunzo sh. 25,000, hivyo niliomba malalamiko haya kufikishwa kwa mkuu wa wilaya," alieleza Mongella na kuongeza kuwa tayarihatua zimekwisha kuchuklulia na Mkuu wa Wilaya.
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Peter Toima Kiroya, alipoulizwa juu ya suala hil,o alikiri kupokea malalamiko hayo na kuongeza kuwa alimwandikia barua Mwenyekiti Mtendaji wa shirika hilo kuomba ufafanuzi wa mafunzo hayo, ikiwa ni pamoja na kumwita katika kikao cha kamati ya ulinzi na usalama cha wilaya kutoa maelezo ya kina.
Kiroya katika kikao cha kamati ya ulinzi na usalama cha Novemba 30 mwaka jana, Katibu mwenezi wa Shirika hilo alitoa maelezo juu ya utendaji wa shirika hilo wilayani humo na utaratibu wanaotumia ikiwa ni pamoja na aina ya mafunzo wanayotoa na kikao kikabaini mambo mengi yaliyokiuka taratibu.
"Baada ya kupata maelezo ya Katibu Mwenezi na kufanya uchunguzi, tulibaini kwamba wananchi anaowaita watumishi wa Coel, walihadaiwa na kupewa matumaini kuwa watapatiwa mafunzo ya ualimu kusudi wakimaliza waajiriwe kama walimu wa shule za msingi," alisema mkuu huyo wa wilaya.
Aliongeza kuwa kwa vile mafunzo hayo yalikuwa yakifanyika katika Chuo cha Ualimu Murutunguru, wananchi pia walihadaiwa kuwa mitihani hiyo ilikuwa imetolewa na chuo hicho na kwamba yalikuwa yakitambulika na wizara.
Alisema mitihani hiyo ilikuwa imechapishwa maneno 'Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi; Chuo cha Ualimu Murutunguru¡' lakini walipomwuliza Mkuu wa chuo iwapo aliitambua, alieleza kuwa shirika hilo walikuwa wateja wao ambao waliomba na kulipia hapo kwa ajili ya kufanyia mafunzo ya watumishi wao na siyo walimu.
Alisema kutokana na hali hiyo, shirika hilo limepigwa marufuku kuendesha shughuli zake wilayani humo.
Naye Afisa Elimu Sekretalieti ya Mkoa wa Mwanza, Dora Ntundu, alipoulizwa kuhusiana na mafunzo hayo, alisema ofisi yake haikuwahi kupokea maombi ya maandishi, isipokuwa katika majadiliano, Mwenyekiti Mtendaji wa Coel-Tanzania, Jamathon Magodi, aliomba watumishi wake weweze kupatiwa nafasi za kufundisha katika shule za msingi ama elimu ya watu wazima.
"Mafunzo yanayotolewa na shirika hilo ni ya kijamii ili watu wake wakafundishe jamii juu ya mauaji ya imani potofu, hawana uwezo wa kufundisha wala kuingizwa katika ualimu. Watu wanatakiwa kuelewa kuwa jukumu la kutoa mafunzo ya ualimu lipo kwa vyuo vya ualimu tu ambavyo vina utaratibu wake na siyo kama linavyofanya shirika hilo," alieleza Afisa Elimu huyo.
Hata hivyo, Magodi alipoulizwa juu ya shirika lake kudaiwa kutoa mafunzo ya ualimu, alisema hayuko tayari kujibu kwa vile bado anaendelea na mazungumzo na Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe kuhusiana na mafunzo ya shirika lake.
"Nimeshatoa maelezo mengi karibu kila eneo ninakokwenda kutoa mafunzo yangu wananielewa, la Ukerewe siwezi kulisemea mpaka nimalize na Mkuu wa Wilaya, isipokuwa tayari nimemwandikia Katibu wa Wizara ya elimu kuomba waanze kufundisha, maelezo zaidisina," alijibu na kumwomba mwandishi wa habari kuondoka
ofisini kwake.