
vingunge wa kamati ya muafaka wa kisiasa wa ccm na cuf katika picha ya pamoja kabla ya kuanza mkutano wao leo hoteli ya courtyard, dar. nyeti toka ndani ya kikao hicho zinadatisha kwamba mazungumzo yanakwenda vizuri na mwanga umeanza kuonekana baada ya kila pande kuendelea na muafaka kwa amani na uelewano. Mungu ibariki tanzania


Hamna kitu hapo, usanii mtupu, CUF wawe macho CCM inachofanya ni 'buy time and destroy tactic' kwani wanajua CUF wapo strong sasa wanachofanya kuwapumbaza ila wananchi wapoteze imani na CUF then hapo ndipo CCM itakapoibuka mshindi, kwani hakutakuwa na mazungumzo tena na CUF na watafanya watakavyo. Muafaka uliopita ungatekelezwa Maalim saa hizi angekuwa zake ikulu. Ila CCM ni kama wacheza mpira wakiona kuna dalili ya kupigwa mabao wanapanic na kusahau mafunzo ya kocha na kuanza kutembeza BUTI uwanjani, ukizingatia na REFA ni wa wao hata kadi nyekundu hawapewi, Sasa kazi kwako timu pinzani kuendelea na mechi ufungwe au kuacha mechi mwenzako apewe point 3 na magoli mawili.
ReplyDelete