
nipo na mai nanihii wangu tukijidai baada ya kampuni ya wakala wa simu mpya za mkononi za mtandao wa bol waitwao 'kiboko super dealers' kutupatia vifaa hivyo vya kisasa leo makao makuu ya ofisi za 'big tv' yaliyopo jengo la nedco karibu na ymca.
simu hizi za bol tumezikubali kwani bei ni poa kichizi. yaani ukilipa alfu 36 kwa mwezi unaongea utakavyo kwa bol-t-bol bila kujali muda wa maongezi, wakati bei ya kupiga kwenda mtandao mwingine haizidi shilingi 150 kwa dakika.
kwa maelezo zaidi mpigie ali oki kupitia simu namba +255 754 788 098 -kazi kwenu wadau...


Brother Michuzi,hawa jamaa wa bol wameanzisha network yao bongo??I mean wamefunga BTS(Minara) Tanzania nzima au ni mtandao wao ni kupitia Satellite Comunication.
ReplyDeleteNi vizuri kusema kweli bol kuleta mapinduzi ya mawasiliano kwani Tanzania ni mojawapo ya nchi inayoongoza kwa kuwa na gharama kubwa za mawasiliano.
This is a challenge for big companies such as Voda,Celtel which are the leaders in high tarriff rates.
hii itaondoa gharama za simu za mitandao bongo, mana hawa tulifikiri celtel licha ya kubebwa na ttcl ingekuwa nafuu ,,wapii...
ReplyDeleteni bomba sana, inakuwa kama mamtoni vilee,,comviq kompis,,pwa pwa pwaaaaaaaaa----
Eeee bana eeeee. Michuzi huyu ndiyo mai waifu wako kumbe. aisee umeukata. kumbe una mtasha! tehe tehe tehe. Halafu hizo simu za BOL kama ni kweli zinacharge rate hizo makampuni mengine yameumia. Sasa mbona hujasema hizo huduma zinapatakanaje na wapi. Ama wote tuje hapo jengo la NEDCO? Ahh noma hiyo waambie. Wasambaze huduma kama wenzao basi. Hata mie nimewakubali hata kabla sijapata huduma zao. Nisalime huyo mai nanihii wako, mwambie nitanunua BOL lazima kwa heshima yake...
ReplyDeleteSafi sana nilishachoka watu kuni-beep kila mara...hii itakuwa kama mamtoni mwana...Ila ubaya wake watu wote watahamia huko halafu hii kampuni Bol mitambo itashindwa ku handle heavy traffic na itakuwa usumbufu mtupu..but lets wait and see..
ReplyDeletemambo ya contracts za simu taratiiiibu uswahilini!!!
ReplyDeleteTasha that ring one your finger girl- wats the score???
ReplyDeleteSir Issa... Mmependeza,reception inakubalika, japokuwa picha nusu.
ReplyDeleteMICHUZI TUNAOMBA BEI YA HIZO HANDSET MAANA ISIJE IKAWA MAMILIONI! INGAWA KUPIGA NI KARIBU NA BURE..
ReplyDeleteMisoup siku hizi umekuwa Modo?
ReplyDeleteTunashukuru BOL kwa hizo huduma,maana itatuletea nafuu sana.Lakini,mbona huyo wa maelezo zaidi yeye anatumia Vodacom,au namba zao za kuanzia zinafanana?maana kama ni hivyo anatupa wasiwasi wateja,hata yeye msambazaji mwenyewe hatumii?!?
ReplyDeleteMakampuni yote ya simu za mkononi ni sawa tu hakuna cha voda,celtel,zantel labda tigo kidogoo ndio wako cheap hao BOL wanavutia wateja tu hawa jipya
ReplyDeletemichuzi,
ReplyDeleteulitaliki kwanza au amekuwa ndo wife no.2? maana unaruhusiwa kufanya sub 4 eti? ehe ehe he heee
Nikaija Bongo naona nitatumia hiyo simu. Inaelekea ni deal safi sana.
ReplyDeletehuyo derrick, si wa tmk bondeni,yeye ni double r. napenda kutaadhalisha, mana watu hawachelewi kuvunjiana heshima humu.
ReplyDeleteMbona mmefanana? kasoro yeye mweupe. Issa unafaidi kila kona wacha weee
ReplyDeletesimu za BoL ni poa kichizi. Ni technoljia ya VoIP (Voice over IP) yaani kupiga kupitia internet. Handset ni USD 200 tu. Sema kuna ishuz chache bado mfano bado Tigo wanabana kwa hiyo ukiwa na BoL unaweza kupiga mitandao yote ila mtu wa Tigo hawezi kukupigia. Lakini ni ishu ambayo wanaisort out muda si mrefu. Kwa anayehitaji tuwasiliane. e-mail fredmboma@gmail.com
ReplyDeleteMzee Fredrick unaweza kutumia huo mtambo popote pale dunian au ni ndani ya bongo Tu..?
ReplyDelete