wengi hatukona yanga ilivyofungwa kule tunis. hebu bofya linki hizo hapo chini ushuhudie mwenyewe goli moja moja. heri ya jumapili ya pasaka kwenu nyote

http://www.e-s-tunis.com/videos/fichiers/070406_EST-YAFC_1-0.ram

http://www.e-s-tunis.com/videos/fichiers/070406_EST-YAFC_2-0.ram

http://www.e-s-tunis.com/videos/fichiers/070406_EST-YAFC_3-0.ram

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Ukiangalia hayo magoli yalivyofungwa, kweli tunahitaji nguvu za ziada kuweza kufikia kiwango kinachiridhisha. Maana mabeki wanajikusanya pamoja kama wanamkaba mtu mmoja na kuwaacha washambuliaji wengine wakiwa peke yao "Poor Defence Positioning". Inabidi yanga tupewe pole. Zumba's

    ReplyDelete
  2. Michuzi,
    Asante sana kwa kututumia picha hizi. Kwa haraka mimi naona tuna (Taifa Stars) tatizo na kipa. Magoli yote matatu yanamwonyesha Ivo Mapunda akiwa katika wrong position. Nina wasiwasi juu ya uwezo wake wa kuwapanga mabeki wake. Ni ajabu, kuwa tuna kipa wa taifa aliyeruhusu magoli 9 katika kipindi cha majuma matatu. Huo ni wastani wa goli 3 kwa juma. Amefungwa na Waangola 2, Swnegal 4 na Esperance 3! Nani atamwamsha Maximo?!

    ReplyDelete
  3. HIVI TUTAENDA GHANA (NA TAIFA STARS,NAMAANISHA) NAMNA HII JAMANI? WACHEZAJI WETU HAWAJUI KUKABA NA WALA HAWANA MAARIFA YA KUTOSHA.YANGA NAIPENDA SANA ILA INANITIA HUZUNI SANA.

    PIA NADHANI SASA NI MDA WA KUMWEKA KASEJA GOLINI (KTK TIMU YA TAIFA)ILI ADAKE KROSI NA KONA ZEMBE AMBAZO IVO MAPUNDA ANAZIACIA ZIPITE KAMA MAJI YA MTO RUFIJI YAINGIAVYO BAHARINI BILA KUGUSWA NA MTU.

    LAKINI NADHANI GOLI LA PILI MAPUNDA ALICHEZEWA FAULU,AU WENZANGU MNA MAONI GANI?

    YANGA TUNA KIBARUA PEVU SANA MECHI IJAYO.NADHANI BAADA YA LIGI YA NYUMBANI HUYU KOCHA APEWE NAFASI YA KUSAJILI WACHEZAJI ANAOWAONA WANAFAA NA SIO KAZI HIYO IFANYWE NA VIONGOZI.PIA TUNAHITAJI YANGA "B" NA YANGA KIDS ZIFUFULIWE ILI TUWE NA YANGA NA TIMU ZA TAIFA IMARA.

    JK

    ReplyDelete
  4. Dah, magoli yote ni makosa ya mabeki..wamejazana kibao lkn wanamwachia mfungaji. Inasikitisha...cheki bao la kwanza na la tatu. poleni yanga

    ReplyDelete
  5. mimi kwa kweli magoli hayo naona karibu yote kipa amechangia kwa uzembe ni mzito mno huyo kipa pia nadhani kuna haja ya kumbadilisha hata katika timu ya taifa kwani haongei na mabeki na hata hayo magoli aliyofungwa kama la kwanza mtu amepiga nje ya kumi na nane na si shuti kali ule mpira ameuchop sasa pale kwa kipa ni timing inayotakiwa hata kuruka hutakiwi kuruka kwa kifupi kipa ni mzito na amevunja record ya kufungwa goli tisa katika mechi tatu za kimataifa

    ReplyDelete
  6. Bro Michu! Nipigie picha nzuuuri ya CCM Kirumba ukiweza kwa juu au ndani. Another thing kama ukiweza kila kiwanja cha hukomikoani. Usikunje Bro! We ndio kiboko.""Leo kuna bonge la party, jamaa wameniomba niwamichuzie picha zao"" hahahaha!!fanya hivyo basi!!

    ReplyDelete
  7. Asante sana michuzi kwa hizo webs!!! nachoona mimi kama wahenga walivyosema ng'ombe hazeeki siku ya mnada, mambo yameonekana yenyewe hapo uwanjani hamna kitu kabisa na wala hayo mashindano ya Africa haiwezekani tz kuingia hakuna haja ya kujidanganya wakati tunajua kabisa hatuendi tunahitaji maandalizi ya muda mrefu, hivyo basi tunahitaji kuwekeza nguvu zaidi kwa vijana wetu wadogo mf.watoto wa chekechea mnawapeleka kwenye wanja la nguvu hilo, somo la michezo liwekewe nguvu hasa soka kwa mf watoto wakue wakijua kwamba there is potential in that field...tunamshukuru sana Rais mstaafu BM kutupatia kitu cha kujivunia watz basi kwa sasa tulitumie kutengeneza manoti pesa na kulitangaza zaidi na zaidi kibiashara kujenga kitengo hicho cha michezo na nguvu zielekezwe kwa vijana wanaokua na watoto wadogo na nyie wazazi watz lazima muwasupport watoto wenu kwa kujitoa kiasi kikubwa ktk kuhakikisha wanafanikiwa ktk kitengo hicho NAWAKILISHA.

    ReplyDelete
  8. goli la kwanza kipa alitoka mbele,zaidi credit kwa mfungaji.....goli la tatu, beki wa kulia alizembea.

    ReplyDelete
  9. Du, yaani Yanga haikunufaika kwa kuwa na wachezaji 7 Taifa Stars waliocheza na timu za Brazil, Angola, Senegal na South Africa na bado wanafungwa magoli ya kirahisi namna hiyo, kweli hata ndoto za Taifa Stars kwenda fainali za kombe la Afrika Ghana inabidi tuzitupe jalalani. Yaani Maximo, Micho na Taifa zima yabidi tuanze mkakati wa soka la juu mwaka 2017 ndio ni mwaka Elfu mbili na kumi na saba.

    ReplyDelete
  10. siamini yanga wanafungwa magoli easy [rahisi] namna hiyo, japo la pili ni kama kipa alibanwa mbavu - lakini all the same marking ilikuwa zero.nina mashaka na goalkeeper kama hakuna alternative - huyu pazia, lazima apange defence yake siyo?

    huenda ni kwasababu naangalia sana premier league, hata hivyo walikuwa na uwezo wa kuzuia zaidi - japo wangefungwa moja, matumaini ya ushindi mwanza yangekuwepo.


    kwa hivi ilivyo, matumaini ni asilimia kumi [10 per cent], si zaidi ya hapo.

    ReplyDelete
  11. Dah wee ni simba usilete mambo ya kishabiki hapa mbona hujaweka magoli Ya taifa

    ReplyDelete
  12. Asante kaka michuzi kwa kutuonyesha ayo magoli tuliyo fungwa na hao waalabu ila naona katika magoli mawili ya mwanzo naona tatizo ni la kipa Ivo Mapunda na naamini ata wale makocha wazalendo walipo toa ushauli ata timu ya taifa inabidi apumzishwe kwa nafasi yake kuchukuliwa na Juma Kaseja yale si magoli ya kufungwa kwa golikipa anayedakia timu ya taifa na nazani ata magoli tuliyo fungwa na senegal yatakuwa kama ayo tu kwa kweli inabidi apumzishwe uko timu ya taifa atuangalii umbo la mtu tutaangalia uwezo wa mtu tu

    ReplyDelete
  13. Lile goli la kwanza mtu unabidi utoe pongezi kwa mfunganji, lilikuwa ni goli murua na hata kama kipa angekuwa ni Buffon,Cech au Kaseja bado tu wavu ungetikiswa. Lile bao la pili ni 50/50 yaani ingeweza kuwa mfungaji alimfanyia madhambi kipa au ni goli halali, hata hivyo siku zote mtu ukicheza ugenini lazima matukio kama hayo yakuumize.Hata hivyo kulikuwa na mabeki watatu kwenye mstari wa goli na wote walikuwa wakikodoa macho tu.Bao la tatu ni kosa la kipa. Hata hivyo hii inaonyesha ya kwamba timu zetu zina matatizo makubwa katika ushindani.Mosi kila klabu zetu zikienda kucheza mechi nje ya nchi ni lazima mchezaji angalau mmoja atolewe nje kwa kadi nyekundu, hii inaonyesha upuuzi na utovu wa nidhamu wa wachezaji wetu. Pili, katika hizi mechi tatu za kimataifa zilizopita timu zetu zimekuwa zikiraruliwa kipindi cha pili, hii inaonyesha ya kuwa wachezaji aidha hawana stamina ya kutosha au kisaikolojia wanapotea na kusahau maelekezo ya walimu mara baada ya mapumziko.Hapa Yanga wameshatolewa kwenye mashindano haya maana hata waloge vipi hawawezi kumfunga Esperance angalau bao 3 za kuipeleka mechi kwenye penalti. Vile vile hata hawa CAF walivurunda kweli, mtampangaje mwamuzi kutoka nchi ya Afrika Kaskazini achezeshe mechi ya Esperance Tunisia, hapa hata wao wanastahili lawama kutoka na visingizio vya hujuma.

    Mwisho Tanzania ina vipaji vingi na bora zaidi ya vile vinavyoonekana Yanga na Simba.Kuna viungo hatari kule Zenji ambao Maximo amewafumbia macho.Vile vile kuna wachezaji wengine kedekede Kagera, mwanza, Kigoma, AFC na timu nyinginezo ambao wanastahili nafasi.Achana na hawa vichwa maji ambao wanajiona wameshakuwa akina Drogba na Adebayor (aka Mwaikimba,Mgosi n.k)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...