kwa wengine pasaka si njema kiiivyo. mfano msemaji mkuu wa jeshi la polisi afande mugassa (mwenye kapelo) amepoteza baba yake mzazi na hapa ndio ametua minnesota asubuhi hii na mwili wa marehemu tayari kwa mazishi kijijini kwo. rpc afande zelothe (mwenye gogoz) na maafande wengine kibao walikuwepo kuwafariji ndugu jamaa na marafiki wa afande mugassa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Pole sana kamanda na wafiwa wote kwa ujumla. hiyo ni kazi ya mungu wote tutafuata njia hiyo hiyo, tumuombee mungu mapumziko mema

    Michu nawe pole kwa msafara wa kusindikiza mwili, ndio maana leo kidogo updates hazikuwa za kasi kama kawaida yako, halafu inaonekana kamanda mshikaji wako sana, mlikuwa nae tsj nini michu, maana mambo ya usemaji ni fani ya habari.

    poleni wote kwa ujumla

    ReplyDelete
  2. Poleni sana wafiwa tunajua hiki ni kipindi kigumu sana lakini mwombeni sana Mungu atawasidia

    ReplyDelete
  3. POLE SANA AFANDE MUGASSA, (Hakika sisi ni wa M/Mungu na kwake tutarejeja) Pole ndugu yangu ndio nimeona msiba huu sasa hivi, pole kaka.

    ReplyDelete
  4. KWANZA KABISA POLE SANA KAKA MUGASSA, KIFO KIMEUMWA NA HATUNA KIMBILIO KATIKA HILO, "KITAKUJA PINDI KITAKAPOTAKA KUJA"
    Ila bwana Michuzi nafikiri unahitaji kuwa makini kidogo, hapa umezungumzia swala zito,na gumu la familia ya afande Mugassa kuondokewa na baba yeke, lakini bado unaweka maneno ya ya utani utani kwenye jambo zito kama hili, *MINNESOTA* Sidhani kama ilikuwa ni halali kutumia neno hilo hapo, unawapa watu kazi ya kuanza kufikiria MINNESOTA ni wapi wakati umesha washtua kwa habari za msiba. Hizo picha nyengine za barabara, Air port nk sawa ungetumia neno hilo lakini kwa hii picha ya msiba ulitakiwa uweke mambo wazi ili kila atakaesoma apate ujumbe unaoeleweka tena kwa haraka. "WEMA NA MAHALI PAKE KAKA"

    ReplyDelete
  5. Bwana Michuzi Minnesota ndio wapi?Ile ya USA au unamaanisha sehemu gani huko nyumbani?Nadhani hayo matumizi mbadala ya majina yanapoteza ujumbe muhimu unaobebwa na picha unazotupatia.

    ReplyDelete
  6. Nyie washamba hapo juu mbona mna vichwa vigumu minnesota ni mwanza.Hio sio atomic science mpaka ukune kichwa ni lugha ya bwa michu na sisi tunaipenda sana.

    ReplyDelete
  7. Poleni wafiwa lakini Michuzi hacha kaujinga ka kuita sehemu za Tanzania majina ya Amerika au Ulaya inaonesha kwamba akili hauna na haupendi Tanzania bali unapenda mataifa mengineo.

    Kwa mtu uliye karibu na Serikali ungeona aibu kwa hayo unayoyafanya.

    Ata kama hautayatoa haya maoni lakini kaukweli kamefika na utajiuliza na kuacha huu upuuzi.

    ReplyDelete
  8. Mfiwa,
    Asante sana kaka Michuzi kwa kazi yako nzuri.Kwa upande wangu niko mbali na nyumbani.Nilipopata simu ya habari za mzee wangu sikuweza kupata muda wa kuwaaga ndugu zangu watanzania, ila badili yake nilikuwa natafuta tiketi ya ndege usiku mzima ili niwahi nyumbani kwa ajili ya mazishi. Nilifanikiwa kwa uwezo wa mwenyezi mungu, na niloporudi kwangu baada ya mazishi ya baba yangu, nilifarijika sana kupata simu na barua pepe kutoka kwa ndugu zangu watanzania za pole wakinieleza kwamba walipata habari kupitia kwenye website yako. Kazi nzuri sana, na Mungu akubariki.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...