Kwa Watanzania wote.
Kwanza napenda kulishukuru Jeshi la Polisi Tanzania kwa kuanzisha website yake mpya hii ni hatua muhimu sana kwa Taifa. Kwa mujibu wa msemaji wa Jeshi la Polisi website hii itatumika kwa madhumuni ya kujua habari nyingi za Jeshi la Polisi na vilevile kutoa fursa kwa watanzania kutoa habari za wahalifu na wala rushwa kwa hatua za utekelezaji.
Lakini katika uzoefu wangu websites nyingi zilizofunguliwa kipindi cha nyuma karibu zote hazifanyi kazi kwa mfano Wizara zote za Tanzania hazina websites na kama zinazo hakuna kitengo kinachoshughulika kubadilisha taarifa mara kwa mara. Kwa mfano websites za Wizara za Maliasili na Miundombinu ambazo ni muhimu sana katika taarifa za Nchi kwamara ya mwisho zilibadilishwa mwaka 2006.
Ninashauri kama tunataka websites hizi zifanye kazi vizuri kuwe na webmaster aliyesomea kazi hiyo ambaye atakuwa anatoa habari na kupokea maoni kwa wasomaji kila siku tukifikia hapo ndio kutakuwa umuhimu wa kutumia teknologia hii.
Mimi kwa sasa nasoma hapa Ulaya navishukuru sana baadhi ya vyombo vya habari kwa kutoa habari za nyumbani za kila siku bila kumsahau ISSA MICHUZI ambaye kila Mtanzania aliyeko nje ya Tanzania anamfahamu kwa kutupatia picha nyingi za matukio ya nyumbani kupitia blog yake, kama Wizara husika zingekuwa zinaweka taharifa zao za kila mwezi kwenye websites hata baadhi ya wanafunzi wa elimu za juu wakati wanafanya Thesis zao wasingekuwa na haja ya kusafiri mpaka Dar es salaam kutafuta data za population ambazo ungeweza kuzipata kwenye websites za Wizara ya Mipango
Website yenyewe ya polisi ni hii www.police.go.tz
Reggy.R.M
UHOLANZI
MKEREKETWA UGHAIBUNI


Mawazo yako nayaunga mkono kwa 100%, kwani web yenyewe hata kufunguka haifunguki. Bado kuna safari ndefu sana, watu wapo kibao wana degree za website lakini hawana kazi wawtumie hawa sasa, sio kuweka hela kando kwa ajili ya vikao.
ReplyDeleteTokea walivyoizindua kila nikijaribu kufungua , haifunguki sijui inattizo gani
ReplyDeleteUnayosema ni kweli, maana hata hiyo website ya polisi hadi leo hawajai-update, inaonyesha kwamba IGP ni Omar Mahita. Hayo matukio ya ujambazi wataweza kuya-update
ReplyDeleteKweli kabisa kuhusu kuzi-update taarifa. Maana mpaka sasa website ya polisi ianonyesha kwamba IGP ni Omar Mahita wakati alishastaafu muda mrefu. Dada Joy
ReplyDeleteUnayosema ni kweli kabisa. Hizi website zinafunguliwa lakini hakuna up-dates zozote, mfano hiyo website ya polisi mpaka leo inasema kwamba IGP ni Omar Mahita.
ReplyDeletebwana Mwala Mzee wa Chapati Rosti wa Uholanzi nakupongeza kwa maoni yako mazuri kuhusu hili wimbi la websites za kumwaga ambazo as long as haziwi updated hafikiri zinakuwa hazikidhi malengo yake ya kutoa taarifa na kuelimisha umma kwa ujumla....Masomo mema na kata desa salama
ReplyDeleteMbona hiyo www.police.go.tz nayo haipatikani?....au wadau nyie mnaipata?...Mimi nimejaribu lakini Not available!
ReplyDeleteHii web haifunguki
ReplyDeleteShukuranu kwa kutupatia hiyp website Ya Tanzania Police.
ReplyDeleteKuna matatizo na hiyo website Link zake azifunguki au ndo wako katika harakati za kuikamilisha. Hebu nipatie ufunbuzi kama unao.
Toka
Toronto Canada
NB: Shukurani kwa Michuzi kwa taarifa utapashazo kila siku.
Habari ya Pasaka. Kwa kweli yanaunga mkono mawazo yenu kuhusu website nyingi hasa za taasisi za serikali yaani ziko dormant. Website ya jeshi la Polisi imehamia hapa http://www.cja.co.tz/police_new.htm by Zumba's
ReplyDeleteTanzania haijui tu ni aasilimia ngapi ya biashara inapoteza kwa kutokua na websites muhimu. Ulimwengu wa sasa hivi ni wa high tech.
ReplyDeleteWatu wengi wanaweza kufanya hizo kazi za uwebmaster ni ubahili tu kwa vile wanafikiri kuwa sio kila mtu anayo computer Tanzania sasa kuwa na webmaster ni upotefu wa hela.
Wangejua nchi nyingi ulimwengu huu zinajitangaza kupitia website.
Na watu wengi wanaopenda kutalii wakiangalia kwenye website kama hawaoni chochote wanaenda kwenye nchi yenye maelezo. Mtalii yeyote akitaka kutembelea nchi lazima anaangalia na official website za nchi hiyo kulikoni kujipeleka kichwa kichwa tu. Watalii tunaowapata tungejua tu kuwa ni marisk taker tu. kama tungeji advertise tungepata hata wasio marisk taker kama tungekua na official wesites. Tunge double au hata ku tripple watalii nchini kwetu.
Ingawaje hata hii site ya police sijaweza kuifungua lakini I HOPE wanaandika kiswahili na kudhungu pia. Twajivunia kiswahili chetu lakini ukitaka kuvua samaki wengi ............
Nchi yetu inapoteza wasomi wengi tu nchi za nje kwa kutokuwa na site za information. Ni wasomi wangapi wana masters na PHD lakini wamezamia ughaibuni. Watu wengine hawajui kinachoendelea bongo kwa hiyo wanaogopa wasije wakaenda bongo wakajikuta wanalost tu.
ReplyDeleteKuna watu wako gizani waliondoka miaka ya 80 na hawajarudi mpaka leo. Hawaamini kuwa bongo iko hivi wakiangalia picha za michuzi.
Ingawaje hatutaweza kukubali lakini ukweli ni kuwa hii website ya Michuzi itasaidia sana kurudisha watu nyumbani mara baada ya kumaliza masomo yao.
Na Govt ingesisitiza wizara zake kuwa na website pia.....How much real does it cost to own a website per year? Miminafikiri sio kutokua na hela ya kufund hizo website ni kwa vile hatujui umuhimu wake.
Haturudi ng'o! nani arudi nchi ambayo wazee ndio wanayoiongoza akina Kingunge, tutaishia nchi matajiri na Elimu yetu na Tz kuendelea kubaki maskini kwani wangapi tumezamia? wengi sana, maslahi madogo lakini jitu halina elimu kipato chake kikubwa posho za vikao ndio usiseme! tunachapa kazi huku kwenye nchi za wenzetu.
ReplyDeleteUnalishukuru kwa nini? kma web yenyewe haifunguki na hakuna current news sasa hilo jeshi la polisi limefanya nini mpaka lishukuriwe? Na wasomi Tz haturudi ng'o kwani maslahi kidogo na unamkuta mtu hata elimu hana kipato kikubwa na posho za vikao ambazo ni kubwa. tunawaachia wasomi akina Kingunge waendelee kutesa na Tz yao.
ReplyDeleteKati ya watu wababishaji nchni Tanzania Polisi ni namba moja.Hakuna wanalofahamu!Mimi ningelikuwa serikali ningewarudisha wale vijana walioko nje ya nchi na wanaofanya kazi katika mahakam ya kimatifa ya Arusha ili walete ufanisi wa mambo ya upelelezi na ulinzi na maarifa ya computa ambayo wamejifunza huko.
ReplyDeleteJamani website hiyo haifunguki hata kidogo ni muda mrefu sio imeanzishwa leo.Yaani hata polisi wanagejua dunia iko wapi katika swala la uhalifu wangejitahidi kusomesha askari wake aktika hatua nyingine kabisa ya ulinzi.Polisi wanatumia nguvu tu katika kufanya mambo yao hawana ushawishi wa maneno ya kuwaingia raia na kutafuta wanachotafuta mahala phapahitaji nguvu hutumia nguvu bila busara.Asakri bado wanahitaji mafunzo ya kisasa!.Vijana wengi walioko katika mahakama hizi za kimataifa na marekani na uingereza wangerudihwa kazini wana ujuzi wa wa kutosha kwa huko waliko.
Lakini tunajua serikali haiwezi kwasababu tuna wivu na kuwakifiria mabaya wale wanaotafuta kwa wema.Tatizo letu watanzania hatutaki kuona mtu kapata.!Tuna matatizo we acha halafu sifa nyiingi halafu hakuna kitu.
Kati ya watu wababishaji nchni Tanzania Polisi ni namba moja.Hakuna wanalofahamu!Mimi ningelikuwa serikali ningewarudisha wale vijana walioko nje ya nchi na wanaofanya kazi katika mahakam ya kimatifa ya Arusha ili walete ufanisi wa mambo ya upelelezi na ulinzi na maarifa ya computa ambayo wamejifunza huko.
ReplyDeleteJamani website hiyo haifunguki hata kidogo ni muda mrefu sio imeanzishwa leo.Yaani hata polisi wanagejua dunia iko wapi katika swala la uhalifu wangejitahidi kusomesha askari wake aktika hatua nyingine kabisa ya ulinzi.Polisi wanatumia nguvu tu katika kufanya mambo yao hawana ushawishi wa maneno ya kuwaingia raia na kutafuta wanachotafuta mahala phapahitaji nguvu hutumia nguvu bila busara.Asakri bado wanahitaji mafunzo ya kisasa!.Vijana wengi walioko katika mahakama hizi za kimataifa na marekani na uingereza wangerudihwa kazini wana ujuzi wa wa kutosha kwa huko waliko.
Lakini tunajua serikali haiwezi kwasababu tuna wivu na kuwakifiria mabaya wale wanaotafuta kwa wema.Tatizo letu watanzania hatutaki kuona mtu kapata.!Tuna matatizo we acha halafu sifa nyiingi halafu hakuna kitu.
Waungwana,,, hata wanahabari pia wababaishaji maana hawakuchuja hiyo press release... wakapeleka hewani kama ilivyo kumbe website yenyewe sio www.police.go.tz, bali www.policeforce.go.tz, Michuzi umesameheswa ulikwa MWANZA hilo jina lingine bwana unatuboa....
ReplyDelete