wadau hapa ndipo tutapokuja kuwafunza adabu senego watapokuja kurudiana nasi. lakini kwa matokeo ya kwao kidooooooogo naomba tujadili kifanyike nini ili tushinde maana kama wanja lipo, kocha mbrazil na pesa kedekede zipo. kifanyike nini twende ghana mwakani?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. Kwa maoni yangu,kiingilio cha mchezo huo wa marudiano kiwe poa ili wanja lijaze 60,000 halafu kwa umoja wetu tuishangilie stars kwa jazbar zote.Hiyo itawatia hofu wageni na kuwatia moyo Tstars..Naomba kutoa hoja,Allan.

    ReplyDelete
  2. Naunga mkono mawazo ya Allan, Ila Stars wapate mechi nyingine kama Tatu za kimataifa hasa nchi za ulaya ambako wachezaji wengi wa segenal wanachezea, itawaongezea confidence.

    ReplyDelete
  3. Hakuna haja ya kukimbilia Ghana. Mpira sio siasa. Suala ni kuendeleza timu za vijana kwanza,,then tutafika kwenye mashindano ya kimataifa. Hao ghana mnaowaona leo ni product ya vijana ya siku nyingi.Mpeni Maximo miaka mitano aendeleze vijana kwanza, na sio kumlazimisha kwenda Ghana.

    ReplyDelete
  4. Mimi naona timu ikae kwenye kambi muda mrefu kidogo ili waweze kupata mafunzo ya kutosha, ikiwa ni pamoja na kurekebisha makosa yaliyojitokeza. Mambo ya kukaa week moja yatawafanya wachezaji wasiweze kuelewana.

    ReplyDelete
  5. suala la soka la Tanzania linahitaji maandalizi na mikakati ya muda mrefu siyo kama ambavyo tunataka kufanya kwamba ndani ya miaka Mitatu tunataka tushiriki mashindano kama hayo. Tuwe na misingi ya michezo tangu mashuleni au utotoni, lakini sisi watanzania kila kitu tunakifanya siasa. Angalia wenzetu wa Zambia tangu timu yao ilipopata ajali hadi leo bado wanaijenga, lakin sisi tunataka miujiza itokee. Yungiz

    ReplyDelete
  6. Watanzania hatuna mikakaati, sie tunalilia kwenda Ghana tu? Lengo lisiwe kwenda Ghana tu, lengo liwe kukuza kiwango cha Soka nchini Tanzania ili kutoa timu bora. Ukishafikia hilo lengo utaenda Ghana, halafu Afrika Kusini na mashindano mingine.

    Nyie mnalilia kuonana matokeo ya leo tu. Sasa tukshafika Ghana kwa timu inayotia huruma kama hii ya kina Maxine halafu tufungwe mechi zote huko ghana itakuwa faida gani?

    Watanzania tunapenda sana short cuts, tusipende njia fupi. Hao Senegali hawakufika hapo kwa miezi sita kama sisi tunavyojaribu. Tusipende Mazingaombwe jamani. Kuwe na plan ya ushindi.

    Lengo lisiwe kwenda Ghana tu, tujipange kujenga Soka toka chini hadi juu.

    ReplyDelete
  7. Anony wa hapo juu umeongea point muhimu sana, kwani wiki hii nilikuwa nasoma magazeti ya bong online, nikaona waziri nafikiri wa michezo amesema kwamba uwanja utakuwa unaingiza Tshs. 90m/- kwa kila mechi, na hiyo figure ilikuja baada ya Waziri kusema kwamba kiingilio kitakuwa Tshs.15,000/- kwa kichwa.

    Hiki kiingilio ni kikubwa sana kwa baadhi ya watu kulipa kuangalia mechi, na kwa vile uwanja wa taifa uwezo wake ni watu kama 20,000-25,000, itakuwa vigumu sana kuujaza uwanja huu unaohitaji watu 60,000.

    Nafikri wangefanya viingilio tofauti kutokana na maeneo ya kukaa kama ilivyo uwanja wa taifa na hivyo kuweza kufanya watu wasio na uwezo mkubwa wa kifedha, basi waweze kua-afford kulipa labda kama Tshs6,000 - 8,000/-. Au basi wapunguze bei kwa pamoja ni iwe chini ya hiyo 15,000/- kwa wote. Lakini kwa vile kuna watu ambao wana uwezo wa kulipa hata zaidi ya 20,000/- kwa mechi moja, basi waweke sehemu ambazo ni maalum na nzuri halafu watoze hata 30,000/- kwa kichwa ili wafidie pengo la wanaolipa 6,000/- au 8,000/-.

    Lazima tukumbuke kwamba huu uwanja ni mkubwa sana kwa nchi yetu kwani ukichukulia mfano UK, ni Millenium stadium (abt 80,000)Cardif, Old Traford (78,000)Manchester, na Wembley (90,000)London na Emirates (60,000)London, pekee ndio vina uwezo wa kuchukua watu 60,000 za zaidi, na hii ni nchi iliyoendelea na wanapenda mpira kuliko bongo, kwahiyo swala la kupata nyomi ya kujaza uwanja wote wasilifanyie mchezo kabisa. Population yao ni zaidi ya watu 62,000,000, wakati Tanzania ina 34,000. London ina watu 5.5m wakati Dar es salaam ina watu 3m! Almost mara mbili ya Dar.

    Pia tusisahau disposable icome ya watu wa UK/London ukilinganisha na Tanzania/Dar es salaam. Av. Income per capita UK ni £12,000; wakati Tanzania ni £350. Tusubiri tuangalie mikakati itakayofanywa na viongozi wa michezo ili kuhakikisha uwanja huu unajaza na wanapata hela za kulipia deni la kuujenga pia

    ReplyDelete
  8. Mi nadhani uwezekano wa kuwapiga hawa senegal upo tu!tuhakikishe tunapata hizo mechi mbili na hizo timu za west africa 2 halafu vijana wetu wafanye mazoezi wzkati wa jua,siku ya mechi mchezo uanze saa nane kamili.unajua senegal wengi wanatokea ulaya ambako ndio kwanza winter inaishaisha,sasa wakichezeshhwaa ktk jua la bongo saa nane lazima watachoka haraka na kuwa dehydrated.hapo watalala tu.si uliona mbio za nyika kule mombasa?joto la pwani ya eeast africa kama hujazoea si mchezoi

    ReplyDelete
  9. point accepted

    ReplyDelete
  10. Nakubaliana na Allan hapo juu kuhusiana na bei ya viingilio.Kitu kingine ni kwamba mwalimu apewe wachezaji anaowataka mapema angalau wiki tatu kabla ya mechi ya marudiano ili waweze kuwasoma vyema hao Senegal kwa pamoja kwa kutumia mikanda ya video ya mechi mbalimbali.Kingine ni kwamba Maximo acheze kutumia mfumo ambao viwango vya wachezaji wetu vitaumudu.Nisingependa kumwambia ticha mtu wa kupanga lakini ukweli ni kwamba Mwaikimba hajui soka, yeye ni limwili tu, mpe Kaniki namba.Vile vile haya huu mpango wa kuvunja benki ili kuwaleta Madrid tuachane nao.Madrid ni timu kubwa lakini badala ya kupoteza mabilioni kuwaleta watali ni bora tukasaka mechi zaidi za majaribio na timu za hapa hapa Afrika kama nchi za kaskazini na magharibi mwa Afrika.Hata Ethiopia tukiwaomba itakuwa poa maana kiwango wanacho.

    ReplyDelete
  11. ndo watafungwa mara nyingine wakati wanashangalia kiwanja kipya wenzao watakuwa wanapiga bao u.naona iko kiwanja kitaanza na historia mbaya.ilibidi kocha wa stars awe idd amin

    ReplyDelete
  12. Michuzi,

    Kazi ya kuwashinda Senegal ni kubwa, ushauri wangu ni huu:

    1. Huyu Mbrazili aambiwe kuwa hiki kwake ni kibarua lakini kwetu ni suala la utaifa, asifanye ujuaji kabisa, awasikilize wataalam wa Kitanzania pia. Kummweka Ivo golini ni balaa, huyu kipa hawezi kuzuia krosi na kona, angalia, katika mechi tatu mfululizo za nje amefungwa magoli tisa, (mengi ya krosi na kona), halafu anamng'ang'ia wa nini? Sawa Kaseja ni mfupi, lakini anadaka zaidi ya Ivo! Sawa anajenga timu ya baadaye, lakini safari ya Ghana ni mradi wa zimamoto, huwezi kutumia wanaojifunza, weka wazoefu.

    2. Huyu huyu Mbrazili aambiwe mpira wa Afrika siyo mchezo, asifikiri kuwa Afrika kila mtu ni mjinga, jamaa wanacheza soka la kulipwa Ulaya, huwezi kuwafunga kama huna mfungaji. Aweke wafungwaji wenye vipaji, siyo miili mikubwa tu inayotuliza mpira kwa ugoko. Mwaikimba wake hawezi kupachika mabao, amweke bwana mdogo wa Mtibwa, na Golota na Mrwanda. Awaulize akina Msolla wamsaidie, asiwafanye wajinga. Yeye anapata mafanikio makubwa kwa sababu ya support na mwamko ulioletwa na Rais mpenda michezo, asifikiri makocha wa Tanzania ni wajinga kabisa.

    3. Aaache kujaza wachezaji wa Yanga kwa sababu tu wana rangi kama ya bendera ya Brazil. Yanga ni sugu wa kufungwa kwenye michezo ya kimataifa, wataawaambukiza wachezaji wa Stars. Hili ni suala la saikolojia ya mchezo. Awapange wachache, au awapunguze kwenye timu. Kuna sababu gasi ya kuwaacha akina Swedi benchi na kumweka mtu kama Nsajigwa? Si anakumbuka alichofanya Senegal, unafikiri Swedi angefanya utani huo? Na kwanza Swedi anaweza kushambulia na kufunga bao. Mwambieni aache Uyanga-Yanga. Toka lini Yanga ikajaza wachezaji Stars halafu tukafanikiwa? Mwambie aongee na Sunday Kayuni, ingawa jamaa ni Yanga lakini anakumbuka wakati fulani alipata mafanikio makubwa kabla ya Oliviera hajamtibulia kwa kuwatumia Simba. Muulizeni kama kasahau nitaitaja timu, ilikuwa na Juma Bakari Kidishi Na. 7 na Lunyamila Na. 11, waliobakia wote Msimbazi. Mimi ni Yanga wa kutupwa lakini kwenye hili lazima ni mkweli.

    4. Mazoezni yaanze mapema, siyo ya wiki mbili kama wanavyotaka kufanya. Mwezi Mei wote wapige zoezi na mechi za kweli za majaribio. Huyu kocha ana tabia ya kukataa mechi za majaribio, ajifunze sasa. Asifikiri ana uwezo wa miujiza, soka ni ile ile. Mbaya zaidi sasa hivi Tanzania hatuna bahati ya wachezaji kama akina Marsha, akina Mogella, akina Tino, akina Salim, akina Adolph, akina Mwameja na upuuzi wake, akina Nteze, akina Madaraka, akina Lenny, tuna shida kidogo.

    5. Mwisho ni kama alivyosema mwenzangu hapo juu, ushangiliaji wa siku hiyo uwe balaa. Weka kiingilio poa washikaji wajae. Ikibidi hata wafungwa wote wa Tanzania waingie bure kuona mechi kwa miadi ya kushangilia kama vichaa ila lazima wawe na pingu miguuuni wasije wakaishia.

    Michuzi pokea hiyo, msogezee Maximo kwa Kimombo ingawa unadai wewe iz noti richabo.

    Mobhare Matinyi,
    Washington, DC.

    ReplyDelete
  13. tunachotakiwa ni kuanza na soka la watoto ili tupate wachezaji sahihi. hata kama mkikasirika, ukweli ni kwamba uwezo individual wa wachezaji tulionao ni mdogo. kama hatukuweza kutisha (1981) tulipokuwa na Peter Tino au wakati wa kina Gaga, mnategemea nini toka timu hii dhaifu ? Hata tukienda Ghana, itakuwa aibu tupu ktk TV. well nawatakia maandalizi mema , hope tutaenda Ghana angalau kupata ladha ya Fainali za Africa, nothingelse .

    ReplyDelete
  14. Michuzi kama nilivyokwambia hapo awali, hao jamaa wakija tuwategashee nyama yenye riftvaley, kwa sababu kwa mambo ya vibuyu sidhani kama tunawaweza hao jamaa, pia maombi ya dini zote.
    Pamoja

    ReplyDelete
  15. wacahawi wote wa tanzania sumbawanga mwanza ukelewe tanga wawe kitu kimoja walete ile dawa kubwa tusiseme dawa sema sindano kubwa kuliko zote kama ile ya ngómbe wachanganye ili tushinde akuna pesa swala ni hilo tuuuuuuuuuuuuuu

    ReplyDelete
  16. Naomba Kocha Maximo na benchi lake wawe huru hasa kuhusu kikosi cha timu wasibanwe na mwelekeo wa vilabu ili tupate kikosi imara cha mashambulizi. Angalia takwimu za vilabu vyetu na timu ya taifa ya 80's utapata picha halisi. Futbol ipo lakini hatuiendelezi kwa kuwa hatuna committed futbol leaders. Lakini Juni tutafurahi.

    ReplyDelete
  17. Kwa maoni yangu hatutafika popote tukianza kuingilia kazi ya kocha hasa katika uchaguzi na upangaji wa timu. Tatizo letu watanzania wengi wetu kila mmoja anajifanya yeye ni kocha.Kufungwa mechi moja tu ndiyo imekuwa tabu!mbona Manchester na Arsenal zimebamizwa jana ina maana wapangue timu upya?
    TFF mwacheni kocha afanye kazi yake zile zama za kupanga timu ofisini zimepitwa na wakati. Ushauri huwa unatolewa lakini haulazimishwi.Mwamuzi wa mwisho ni kocha maana yeye ndiyo mwajibikaji.
    Wadau mnaonaje?

    Soma taarifa ya gazeti la lete raha hapo chini:

    TFF wataka Maximo aunde upya kikosi Stars

    08 Apr 2007
    By Mwandishi Wetu

    Baadhi ya viongozi wa shirikisho la soka, TFF, wanataka kocha wa timu ya taifa, Taifa Stars, Marcio Maximo apangue kikosi hicho kwa madai kuwa wengi wa wachezaji waliopo wana uwezo mdogo.

    Taifa Stars ilifungwa mabao 4-0 na Senegal katika mchezo wa tatu wa michuano ya awali ya Kombe la Mataifa ya Afrika wiki-endi iliyopita na tiketi ya kwanza ya kwenda kwake kwenye fainali za Ghana za mwakani inashikiliwa na ushindi katika pambano la marudiano baina ya timu hizo Juni 2, jijini.

    Habari za uhakika zilizopatikana jijini zinasema viongozi kadhaa wa TFF wanaona upo umuhimu wa kuunda upya kikosi kilichofungwa 4-0.

    Chanzo kimoja cha habari kilisema viongozi hao wa TFF (majina tunayo) wanataka Stars iundwe na wachezaji chipukizi ambao watakuwa na ari ya kusakata soka, ``tofauti na wa sasa ambao wengi wao ni wazee.``

    ``(Viongozi wa TFF) wanasema wakisema mapungufu yaliyo katika hiki kikosi Maximo husema anaingiliwa, sasa njia watakayofanya ni kupeleka malalamiko yao kwa (Naibu Waziri wa Michezo) Joel Bendera,`` alisema mjumbe mmoja wa kamati ya utendaji ya TFF ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini.

    ``Wanaona Naibu Waziri ataweza kumshawishi kocha.``
    Pia, chanzo hicho cha habari kilisema, viongozi wa TFF wanaona Maximo ni muoga wa mechi za kirafiki za kimataifa ``kwasababu kila wakati amekuwa akizikataa bila sababu za msingi`` na kutolea mfano wa michuano ya Kombe la Chalenji iliyofanyika Ethiopia mwishoni mwa mwaka jana.

    Aidha, mjumbe huyo wa kamati ya utendaji alisema kuna fununu kuwa Maximo amekuwa akichaguliwa wachezaji na wanamichezo ambao wamejiweka karibu naye.

    Mtazamo huo wa viongozi wa TFF unaendana na mawazo ya katibu mkuu wa Pan African Omar Kapera ambaye katika maoni yake kwa Lete RAHA juu ya mchezo huo alisema Taifa Stars inastahili kupanguliwa upya kwa kuongeza wachezaji warefu katika nafasi ya kiungo, ambao watakuwa na uwezo wa kucheza mipira ya juu.

    Hatahivyo, Maximo tayari amekiri baadhi ya wachezaji wanaounda timu hiyo hawastahili kuwemo katika kikosi hicho kutokana na uwezo wao kuwa mdogo, na ameahidi kuangalia wachezaji wengine katika ligi kuu ndogo ya Bara itakayoanza Jumamosi.

    Stars iliyokuwa ikiongoza Kundi la Saba la michuano ya awali katika raundi ya pili, ni ya tatu sasa nyuma ya Burkina Fasso,zote zikiwa pointi mbili nyuma ya vinara wapya Senegal wenye pointi sita.

    Wachezaji wa kikosi cha kwanza cha Taifa Stars ni Ivo Mapunda, Juma Kaseja, Mecky Maxime, Salum Sued, Nadir Haroub `Canavaro`, Hamis Yussuf, Shadrack Nsajigwa, Victor Costa, Said Sued, Abdi Kassim, Amir Maftaha, Nizar Khalfani, Shaaban Nditi, Henry Joseph, Athumani Iddi, Jerry Tegete, Gaudence Mwaikimba, Said ‘SMG’ Maulidi, Danny Mruanda na Joseph Kaniki.

    * SOURCE: Lete Raha

    ReplyDelete
  18. UKUTA WA MAXIMO UNA WALAKINI. NDUGU WATANZANIA WENZANGU NAJUA TUNA NAFASI KUBWA YA KWENDA GHANA LAKINI HUU UUNGWANA UTATUPONZA!! YASIJE YA KATOKEA YA MIAKA ILE YA TISINI NA ILE STARS NZURI YA KINA ISSA ATHUMANI. TULIANZA VIZURI KWA KUIFUNGA TOGO NA DRO MOJA HIVI MARA TUKALETA YULE MBRAZIL. NAKUMBUKA JAMAA HADI TUNACHEZA MECHI YA MWISHO BADO ANADAI OOH TUTAKWENDA BUKIRNA FASO. NINACHOTAKA KUSEMA NIHIVI HUU UKUTA WA YANGA AMBAO PIA NI WA TAIFA STARS UNA WALAKINI. UKIONDO BEKI MMOJA AU WAWILI UTAKUTA SAFU NZIMA NI ILE ILE INAYOCHEZA STARS. UTAFUNGWAJE 4 HALAFU WIKIMBILI ZIJAZO UKUTA HUO HUO UNAFUNGWA 3.??? MAXIMO HAS TO DO SOMETHING. SAWA TUNAWEZA KUWA NA WASHAMBULIAJI BUTU BASI HATA DRO? AU BASI HATA 1 AU 2. TUTAFUNGWAJE NNE KILA SIKU?? KAMA FEDHA MNAPEWA SASA HII NINI. WATANZANIA TUACHE UMWINYI HAPA MSIDHANIHUKO NIGERIA ,IVORY COAST NA GHANA MAMBO YANAKUJA KIURAHISI.KUNA ZENGWE ZA NGUVU NANDIO MAANA WACHEZAJI WANAKAZA MAKALIO KULE. WAKILETA USHENZI SASA BAKORA TU! WATU WANAKUFA NJAA HUKO VIJIJINI MADAWA HAKUNA NYIE MNAFUNGWA FUNGWA MARA 4 MARA 3. NA HAO WENGINE AMBAO KUCHEZEA STARS WAMESHAANZA KUJIONA MASTAA SIJUI MWAIKIMBA SIJUI NANI WAANHALIE TUTAWARUDISHA HUKO KWAO WAKALIME VIAZI. SASA ZENGWE TUU TUSHACHOKA!! SI HAMINI KAMA HAO NDIO BEST DEFFENDERS TULIONAO SASA HAPO TANZANIA. WHERE IS CHRISTOPHER ALEX, LUBIGISA, AMRI SAID NA WENGINEO. TUMECHOKA MAXIMO BE CAREFULL TANZANIANS ARE SO COOL BUT CAN BE "CRAIZE" SOMETIME.

    ReplyDelete
  19. Kandanda ya kisasa ni mchezo wa sayansi na si kubahatisha kama tombola. Kuna kandanda na siasa lakini si siasa na kandanda. Siasa haiwezi kuinua kandanda lakini kandanda inaweza kuinua siasa na hata uchumi. Safari yetu ya Ghana ilianza na mguu mbaya. Tulianza na siasa. Tumebaki kucheza kandanda ya mdomoni, propaganda kwa wingi. Turuhusu si wataalam tu, bali hata wananchi watoe fikra zao huru juu ya namna ya kuendeleza soka yetu kama unavyofanya Michuzi kupitia blogu yako. Hii ni nchi yetu,tunaipenda nchi yetu, mchango wetu kwa nchi yetu ni pamoja na fikra zetu, zipewe nafasi hata kama kuna wanaokerwa nazo.

    ReplyDelete
  20. NAONA KUNA WATU HAPA WANALETA TUU MAMBO YA UNAZI BILA KUJUA MPIRA WA BONGO UKOJE.TENA CAH AJABU WENGINE NI WAANDISHI WA HABARI!! AMA KWELI WABONGO HATUNA PROFFESSIONALS.. MAKOSA YA UWANJANAI HAKUNA HATA MCHEZAJI MMOJA HASIYOKUWA NAYO.. KINACHOTOKEA NI KUJISAHAU KIDOGO TUU UNAPIGWA BAO KWANI UNACHEZA NA WATU WAZOEFU AMABAO WANATAFUTA TUU UFANYE MAKOSA HAYO KITU AMABACHO WACHEZAJI WETU KARIBU WOOTE WA SASA HAWANA. KUSEMA KASEJA HAFANYI MAKOSA NI UONGO MKUBWA , MBONA WAMSUMBIJI(TEX PUNGUE) WALIMFUNGA BAO LA MBA TENA LA KIJINGA KULIKO HILO LA IVO NA SIMBA IKATOLEWA MAPEMA SANA KOMBE LA SHIRIKISHO TENA AKASHINDWA ZUIA PENALTI AMBAZO TUMEZOEA KUMWONA AKIDAKA?? ACHENI UNAZI AKINA MATINYI.. NYINYI NI WAANDISHI TUNAOWATEGEMEA NDIO MAANA MKIWA WAHARIRI MAGEZI YENU NI YA KINAZI TUU. TEAM YA TAIFA INA MATATIZO MENGI SANA, KUANZIA MAUMBO YA WACHEZAJI ,LISHE , INTELLIGENCE YA WACHEZAJI (HAWAFUNDISHIKI) ,DHIKI (PESA KIDOGO HAZIKIDHI MATATIZO YAO) , MIPANGO DHAIFU YA USHINDI. TUMESHAZOEA TEAM KUSHINDA NYUMBANI KWA MBINU ZISIZO ZA UWANJANI. KWA WENZETU HASA NORTH AFRICA HATUTAWATETEMESHA UNLESS TUJIDHATITI KWA MUDA MREFU TUKIANZIA NA VIJANA. MAWAZO YA KITOTO YA KAMA YA KUJAZA SIMBA PALE UWANJANI KAMA TAIFA STARS (MAONI YA MWANDISHI..!!) NI UJINGA MTUPU. UMEONA WAPI WACHEZAJI WOOTE WA WAHISPANIA WA MARDID WAKAWA NATIONAL TEAM YA SPAIN?? KILA KOCHA ANAONA WATU ANAOWATAKA KWA MFUMO WAKE, HUWEZI KUMLAZIMISHA. HAYO NI MAPENZI YAKO KWA SIMBA TUMEKUELEWA KAKA... TEAM NI YA WATANZANIA WOOTE KAMA SIMBA INGEKUWA BORA BASI INGEKUWA BINGWA WA LIGI KWANZA NYUMBANI NA ISIFUNGWE HOVYO NA KUTOLEWA RAUNDI YA KWANZA. SIKU ZOTE KUMBUKA MPIRA NI MCHEZO WA MAKOSA NDIO MAANA KUNA MAGOLI YAWE YA UZEMBE, KUCHOKA AU VYOVYOTE. MANCHESTER WALIJIFUNGA KIZEMBE JUZI INAGWA WALEWALE NDIO MABINGWA WATARAJIWA. IT HAPPENS!!

    ReplyDelete
  21. Watu wasifikiri kandanda ni sayansi si ajabu hata mechi ya marudiano tukafungwa kwasababu ya kushangaa uwanja mpya maana wao wameisha zoea viwanja tena vyenye kuchukua hadi watu 90,000 lakini pamoja na hayo wao huko kwao si walituchezesha usiku si wakija huku tutapanga mechi ichezwe mchana jua kali an joto kali lazima hapo watachoka ile mbaya na tutaweza kuwapiga hata bao sita halafu nilikuwa natamani hata uwanja wa taifa usingekuwa umerekebishwa tungewachezesha kwenye huo uwanja wenye mbinyuko wangekoma au tuwapeleke uwanja wa jamhuri morogoro lazima tutawapiga bao

    ReplyDelete
  22. Hao akina Matinyi ndio sampo za waandishi wa habari wa Tanzania. Na bora huu mswada wa sheria wa habari bora upelekwe haraka bungeni ili tupunguze utitiri wa waandishi wa habari uchwara. A,B, C,D za mambo ya mpira mtu hayajui lakini ndo wa kwanzaq kuparamia mambo asiyoyajua.

    ReplyDelete
  23. "Sisi ni watu wa sifa tu.Tuendelee kucheza mpira wa mdomoni.Hatuatkwenda popote pale katika soka. sisi ni sifa tu bila vitendo sifa zimetutawala unafikiri sifa bila vitendo kuna lololte litafanyika!."You get what you pay for"

    Msema ovyo

    ReplyDelete
  24. Mazoezi mapema, Kiingilio nafuu na Kujutuma kwa saana kwa hao wachezaji wetu waache ubishololo wapige ndinga kwanza ubishololo wakaufanye baadae Celta Vigo na Roma. Ila aa hao wanaanza ubishololo wakati bado wapo Yanga tutafika? Saula la "Dual Citizenship" liruhusiwe upesi ili Kalingonga Ongara na kina sisi tunaopiga soka ya kulipwa nje ila wazee wametoka bongo tuje kufanya saidia(wenzenu Senegal walirudi).
    Renatus Njohole aitwe kipa arekebishe makosa au abadilishwe upesi. Senegal wakitua tu ni kuwafanyia vurugu tu hotelini usiku kucha wasilale af kudadeki zake mechi ipigwe saa tisa kwenye ile jua ya kuchoma upara ndani ya umati wa watu elfu waliopagawa kwa kelele.

    Mkereketwa, lazima tuende Ghana!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...