BARUA YA WAZI KWA MWENYEKITI WA JUMUIYA YA WATANZANIA UINGEREZA
31.05.2007
Abubakar Faraji
Mwenyekiti
Jumuiya ya Watanzania Uingereza
Ndugu Mwenyekiti
YAH: USIMAMIZI WAKO WA KADHIA YA UKAGUZI WA MAGARI YAENDAYO TANZANIA
Nadhani barua hii itakukuta katikati ya shughuli za kawaida za kimaisha pamoja na kushughulikia masuala ya jumuiya.
Kama mmoja wa Watanzania waishio Uingereza napenda kukuandikia waraka huu kukuelezea masikitiko yangu juu ya namna unavyolishughulikia suala hili.
Nimelazimika kuchukua hatua hii licha ya ukweli kuwa na mimi ni mmoja wa wajumbe wa kamati mojawapo mpya zilizoundwa, hii ni kwa vile Mwenyekiti umeamua kulitolea kauli suala hili bila kufanya tafakuri na mtu yeyote ndani ya Jumuiya ya Watanzania waishio Uingereza.
Jitihada zangu za kukushawishi ujizuie kutoa tamko hadharani mpaka hapo utakapo kutana na wajumbe wenzako japo wa kamati ndogo ya Utendaji zimeshindikana, nimelazimika kuandika waraka huu kuelezea maoni yangu hadharani ili ieleweke wazi kwamba katika hili Mwenyekiti unaiongoza vibaya jumuiya.
Taarifa zako kuhusu kadhia ya WTM Utility Services na TBS zinaonyesha Mwenyekiti haupo katika upande WA Watanzania walio wengi, zinajikanganya na hazitoi picha halisi ya maumivu na dhulma ya dhahiri inayoonekana kufanywa kwa Watanzania:
Taarifa hii kuhusu mkataba huu usio na maslahi kwa Watanzania ilianza kujulikana kupitia tovuti yako binafsi www.tzuk.com tarehe 26.05.2007 ambapo uliitoa kama habari tu. Kama Mwenyekiti wa Watanzania mwenye jukumu la kusimamia maslahi yetu tulitarajia kwamba ungetoa maelekezo haya hata katika tovuti ya Jumuiya www.tzcommunity.co.uk ili watanzania wajue kuwa kuna utaratibu mpya wa ukaguzi. Ni taarifa ambayo inawagusa watanzania walio wengi kama sio wote waishio nchini hapa, hukuona umuhimu wa kuweka taarifa hii katika tovuti ya Jumuiya badala yake ukaweka katika tovuti yako binafsi ambayo kama mmoja wa waandishi wa tovuti hiyo siku za nyuma,nafahamu kwamba inaendeshwa kibiashara…
Kuna maswali mengi hoja namba moja hapo juu:
- Je ulipokea malipo yoyote katika kutoa taarifa hii kwa Watanzania waishio Uingereza?
- Kama Mwenyekiti wa Watanzania hukuona umuhimu wa kutaka kujua zaidi na kuwasilisha maslahi ya watanzania ikiwa ni pamoja na kutaka kuhoji baadhi ya matatizo ya dhahiri ambayo yamejionyesha katika taarifa yenyewe?
Baada kufanya mawasiliano binafsi nawe, tarehe 28.05.07 ulikiri kuwa umepokea malalamiko mengi kutoka kwa Watanzania, lakini hukuona umuhimu wa kuitisha mkutano wa wajumbe wenzako kujadili hili? Badala yake tarehe 30.05.07 ulitoa tamko kuwajulisha watanzania kuwa umepokea malalamiko yao na kama Mwenyekiti unafanya jitihada za kutoa tamko, ndani ya siku tano baada ya kukusanya ushahidi toka pande zote. Siku ya pili 31.05.07 umekurupuka na kutoa tamko kuelezea yaliyojiri katika mazungumzo yako na TBS, pekee!

Ukweli ni kuwa katika mazungumzo yetu baada ya tamko la kwanza, ulisema kikubwa ulichoongea na wadau husika [TBS] waliotoa zabuni kwa kampuni moja tu kufanya ukaguzi huu wa magari ni kutaka kujua vigezo wanavyoangalia katika ukaguzi. Licha ya kuwa hukushariana [kwa mara ya pili na kiongozi yeyote mwenzio ndani ya jumuiya na licha ya kukusihi sana usiendelee kutolea tamko hili suala mpaka hapo umekutana na wenzako wote] na yeyote, kwenye maelezo yako marefu ya tarehe 31.05.07, Mwenyekiti kipengele hiki kikubwa kilichotawala mazungumzo yako na TBS hukukiweka kwenye taarifa!
Badala ya kutuelezea vigezo vinavyotumika kwenye ubora wa magari, Mwenyekiti taarifa yako imeelezea kwa kirefu historian na umuhimu wa ukaguzi huu bila kugusa maswali muhimu ya watanzania.
Ndugu Mwenyekiti kukusaidia katika kujua ubaya na uonevu wa dhahiri unaofanywa na TBS ikishirikiana na Kampuni hii changa isiyo na nyenzo za kufanya zoezi zito na kubwa kama hii nakuomba uzingatie maelezo niliyoyatoa katika blog yangu hapo jana: http://saidiyakubu.blogspot.com/2007/05/utaratibu-wa-mpya-wa-kukagua-magari.html
Natambua wazi kwa kueleza msimamo wangu hadharani, nitakuwa sitendei haki nadharia ya uwajibikaji wa pamoja [collective responsibility] lakini kabla hujanisuta kwa hili nakuomba urejee vitendo vyako binafsi kuhusu kadhia hii ambavyo bila shaka kabisa si tu vinakiuka nadharia hii bali pia kuna wasi wasi miongoni mwa watanzania kuwa huenda ni mgongano wa maslahi [conflict of interest] ambayo ni dhambi kubwa zaidi.
Lakini pia nadhani kwa kukaa kimya dhamira yangu ya kukubali kuwa mjumbe wa kuteuliwa kwenye kamati hii kwa maslahi ya watanzania wote itakuwa inanisuta, mimi nawe tumejuana kwa miaka takriban mitano sasa na tumetokea kuwa marafiki wa karibu lakini katika hili Mwenyekiti nimejikuta sina budi kuuweka urafiki wetu kando kuangalia maslahi ya wengi. Ni matumaini yangu Mwenyekiti utakuwa na nguvu na uelewa wa kutambua kuwa ni tofauti katika hili ndio zimetutetanganisha na iwapo tukijirekebisha na kufanya kazi kwa maslahi ya wengi hakuna kitakachoharibika
Tunakuomba Mwenyekiti ili kuendeleza Jumuiya hii changa utoe maelezo binafsi kujiweka kando na mkataba huu vinginevyo utakuwa unapoteza sifa ya kuwa msimamizi mzuri wa haki na maslahi ya watanzania wote kwani msimamo wako katika hili unaonekana kuyumba sana hususan ukionekana kuvutia upande mmoja ambao ni dhahiri sio unaopendelewa na watanzania walio wengi.
Ahsante Sana.
Saidi Yakubu
Mtanzania aishie Uingereza.
Nakala kwa:
BI MWANAIDI SINARE MAAJAR
BALOZI WA TANZANIA UINGEREZA NA MLEZI WA JUMUIYA YA WATANZANIA WAISHIO UINGEREZA.
WAJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI YA JUMUIYA YA WATANZANIA.
WATANZANIA WOTE WAISHIO UINGEREZA.