maria sarungi anazidi kutuhabarisha kinachojiri mexico
Hello!

Asanteni kwa ushirikiano wenu mzuri!

Jana (tarehe 24) warembo wamerekodi introduction zao wakiwa wamevaa vazi la taifa. Flavia kama mnavyoweza kuona ameva vazi lililobuniwa na Farouque Abdela wa Zanzibar na ameshika kibuyu. Vazi lake ni Maasai-insipiration kwani ina mshono wa kisasa lakini imechukua elements za Kimaasai. Kwa kweli mrembo wetu alipendeza sana!

Leo tarehe 25 alianza siku na interview ya waandishi wa habari wa kimataifa n ni kati ya warembo ambao wamefanyiwa interview kupita wengine wote! Yaani nimefurahi sana, kwani anamudu vyema interview, anajiamini na majibu yake ni mazuri. Waandishi wengi walimwuliza kuhusu nywele yaani kwa nini amekuja na nywele fupi. Flavia aliwaeleza waandishi kwamba mwanamke wa kiafrika asili yake ni nywele fupi za kusuka lakini nywele ndefu zilizonyooka mgongoni ni nywele zilizowekwa dawa au/na kuwekewa extension. Lakini yeye amekuja na uasili wake. PIa aliulizwa kuhusu Tanzania, nchi yake kwamba iko wapi na ina vivutio gani na pia aliulizwa kuhusu ushiriki wa Tanzania kwa mara ya kwanza. Flavia alieleza vivutio vya Tanzania akiwa anatumia makabrasha na taarifa alizopata kutoka Tanzania Tourist Board.

Kwa kweli Flavia amekuwa balozi mzuri sana wa nchi yetu na anazidi kuitangaza nchi yetu. Tuzidi kumwombea!
Asanteni

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 25, 2007

    Keep it up Flava

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 25, 2007

    Michuzi link nyingine ni hii watu wavote kama kawaida
    http://news.yahoo.com/photos/ss/events/en/051007missuniverse/im:/070525/ids_photos_en/r120841975.jpg;_ylt=Ahgwr8arvKxjx2ovPVQO1V3BaMYA?sp=3000&auto=yes
    Nadhani iko clear ni ya reuters baada ya interviwe ya leo

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 25, 2007

    Michuzi link nyingine hii
    http://news.yahoo.com/photos/ss/events/en/051007missuniverse/im:/070525/ids_photos_en/r3728023131.jpg;_ylt=AosP71fo3IQpdpJTHLXeOdd.KcMA

    Hii ni kali zaidi

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 25, 2007

    Jamani si kuna wambulu na wairaq wenye nywele ndefu za asili? au sio watanzania? ahahahah..just saying. In all I voted her and i will continue..she is great. Bwana awe nawe!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 26, 2007

    Nilijua tuu! Nweyele fupi za asili + kujiamini kama muafrika bila kuiga= black is beautiful! Hata kama asiposhunda zaidi, yeye ni Alek Wek wa TZ.. atapata modelling contracts! Way to go girl!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 26, 2007

    Miss Tanzania, Flaviana Matata, an electrical technician whose country is participating for the first time, is also challenging stereotypes of beauty with her shaved head. "I never let anyone define me neither by hair nor clothing as I believe God made me perfect as a pure, natural African woman," she said.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 26, 2007

    NINGEPENDA KUONA COMMENTS KUTOKA KWA YULE MODEL WETU CINTHIA MASASI HAPA..NI UCHOKOZI TU..

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 26, 2007

    jamani shime tumpigie kura huyu mtoto anatutia moyo sana. Hivi sasa anaongoza kwenye kumi bora anafuatiwa na USA muwe makini hakikisheni adui yake mmarekani awe mbali naye kama tulivyofanya venezuela. Ana kura nyingi mungu anaweza kusaidia miujiza Tanzania mwaka huu. Mhamasishaji

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 26, 2007

    Hebu tujifunze vizuri kuhusu makabila yetu Tanzania. Sasa haya mambo ya kuchanganya watu hayafai. Misupu naomba kuwaelimisha watanzania kwamba hatuna kabila linaloitwa Wambulu!tuna Wairaqw. Wairaqw wanapatikana katika Mkoawa Manyara,katika Wilaya za Mbulu,Babati,Hanang'(Hanang'wakiishi kwa ukaribu na majirani zao Wadatoga)Karatu ambayo imebakia Arusha nayo ni moja kati ya wilaya wanakopatikana kwa wingi.Kwahiyo tuna wairaqw wa Mbulu, lakini si Wambulu kama kabila,ama sivyo utakuwa na wababati nk!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...