wadau waliosoma kitabu cha faraji h.h. katalambula cha 'simu ya kifo' kaeni mkao wa kula maana keshokutwa kuna uzinduzi wa filamu yake ambayo imeongozwa na mkongwe hammie rajabu na muongozaji wa picha ansary msangi na kuchezwa na kina riyama ali (kama agnes), hashim kambi (Inspekta wingo), fundi mzee a.k.a mzee upara (mzee jacob) na thecla mjata (mke wa mzee jacob). mwenzenu nimealikwa kwenye uzinduzi na mipango inafanywa filamu hii kuzinduliwa na kisha kusambazwa ughaibuni. kwa habari zaidi wasiliana na tripodmediaco@yahoo.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 03, 2007

    Bado pre-print editing watanzania tuko nyuma. Mtu ana design na kutoa kadi peke yake bila kuomba mtu wa pili aione na kuihakiki. Kuna makosa yafuatayo katika hii kadi:
    1. wanafuraha, je hakuna space hapo inatakiwa? au nachemka?
    2. kama ni uzinduzi = utakaofanyika, na sio "itakayofanyika"
    3. apartments = appartments
    4. St likitumika kifupi then ni St. yenye kituo mbele yake
    5. Hakuna umuhimu wa capital letters kwenye maneno Tarehe na Kumi

    ReplyDelete
  2. Michuzi, utupe scoop kuhusu hiyo filamu. Wish I could be there sounds interesting. Mpe Hammie Rajab na wengine wote hongera kutoka kwangu! Tafadhali mwambie Dada Thecla kuwa namtafuta. E-mail yangu chemiche3@yahoo.com

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 03, 2007

    nawapongeza wote walioshiriki ktk zoezi hilo la kutengeneza hiyo video movie (presumably)
    natumaini watatengeneza sinema japaokuwa ni video lakini yenye mtiriirko wa kiufundi wa feature film hasa na siyo kama za wanigeria
    LAKINI
    hiyo kadi ya mwaliko inanipa wasiwasi na kuhusiana na the entire production ya hiyo movie
    hivi ni kweli wameshindwa kutengeneza walau press kit ya kitaalam iliyojitosheleza hasa kwa ajili ya mtu kama michuzi amabaye ni mwandishi wa habari mwenye inluence michuzi hastaili kadi kama hiyo ya kibabaishaji huyo ni sehemu muhimu sana ya media ya tanzania na kwa serious film makers walipaswa wampe press kit yaani yenye habari zoote muhimu juu ya hiyo film.kuiona hiyo movie pek yake kwa michuzi haiwasaidii publicity hao jamaa wanpoteza a very readly available resource kama michuu
    raceisnobar media co

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 03, 2007

    Anonymous wa 5:39OM, hebu acha ushamba. 'apartments' ni sawa kabisa. Na kwenye kadi wamteumia 'justify' format ndo maana unaona nafasi!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 03, 2007

    AMA KWELI COMMENTOR NO.1 unaongozwa na stress tu.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 04, 2007

    big up waandaji wa filamu ila next time mjitaidi jamani kadi iyooooo kuirekebisha

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 04, 2007

    Hongera Tripod Media kwa kuja na something special.Simu ya kifo ni kitabu maarufu ambacho wazazi wetu walikisoma mashuleni, mpaka sasa hivi kitabu hiki kinatumika mashuleni nchini kenya. Kwa taarifa nilizonazo movie hii imetengenezwa Tabora kama mtunzi wa kitabu alivyokiandi, kwa wale waliosoma kitabu hiki wanaelewa.
    Am sure it was a big challenge for the production crew, but at the end of the day kazi yao imefanyika.
    Nadhani ni movie ya kwanza Tanzania inayotokana na kitabu chenye mafunzo kwa jamii.
    Keep it up Tripod Media. Critics will always be there,but they shouldnt stop you,coz i see you raising a bar for the Young film Industry in Tanzania.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 04, 2007

    Hongereni Tripod Media,U seem to know what u are doing. Kwa kweli mimi ndio mara ya kwanza kusikia movie inazindulia kwenye Theatre hapa Tanzania. Movie karibu zote hapa bongo ni kwenye kumbi za maharusi na pubs....
    Only professional movie makers would think of this.
    Hope this wont be the first and last movies from you...
    All the best

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 04, 2007

    Wote mliohusika kutengeneza hiyo video hongereni sana.Natumaini mtakuwa mmejitahidi kuleta mambo tofauti na tunayoyaona kwenye hizo filamu nyingine.

    Najua huenda ikawa si tofauti sana na hizo video nyingine tunazozifahamu hivyo tungependa tuione. Jambo moja tafadharini muache kuchanganya Tv drama na filamu jamani maana siku hizi kila mtu oh nimetengeneza filamu ukiangalia ni tv play tena mbovu mbovu tu inakuwa imebandikwa bandikwa vipande havina hata mahusiano na mwendelezo.
    Kaka michu mpe salamu zangu mzee Hammie Rajabu.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 04, 2007

    We anoni wa Thursday, May 03, 2007 8:52:00 PM, hivi mtoa comment wa kwanza ameongelea lolote kuhusu allignment ya kadi? unalipuka tu "justify" format. Uko sahihi kuwa apartment ni sawa, lakini mtoa maoni wa kwanza yuko right kuhusu vitu vingine vyote. Hata wewe unahitaji editor, neno "WAMTEUMIA" haliko katika kamusi. Nakubaliana na anoni namba 1, hii kadi ina makosa, na wala sio kubebana hapa.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 04, 2007

    we Mumu acha ushamba na wewe pia, anoni wa kwanza kagusia mambo ya nafasi au allignment format hapo? usilipuke, una ji expose.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 04, 2007

    Michuzi, good job. Blog yako ni very exciting. Mie ndo nilitoa comment namba 1. Sikudhihaki kuwa walioandaa kadi hawajui, bali nilitaka kuonyesha tu kuwa pre-press editing ni nzuri ikafanywa na watu tofauti tofauti. Unaona, hata mie hapa nilidhani aPPartments si aPartments. Hii inaonyesha jinsi tunavyoweza kujifunza toka kwa wengine. Lakini sijafurahishwa na watu wanapoona mtu kakosea, wanaanza kwa kusema "mshamba huyu". Elekezeni au kosoeni kwa upendo. Anoni alosema nimeongozwa na stress kutoa maoni yangu kanichekesha sana. Ni kweli niko stressed, nafungasha fungasha vilago vyangu. Naondoa stress zangu kwa kuja kwa Michuzi, au kwenye zile blogu mbili ambazo watu wanaomba zijadiliwe. But, tabia ya ku cross check kabla ya ku print kitu au ku click send ninayo sana maana bosi wangu hapendi kosa hata dogo vipi. Na hii imenifanya niwe hivyo katika chochote nikiandikacho. Alikuwa ananiambia, even perfect is not enough!

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 05, 2007

    Bro Michu kuna mtaalamu wa mambo ya filamu na TV anaitwa Mwanga kapotelea wapi huyu bwana maana najua ni mmoja kati ya watu ambao wamechangia kwa kiasi kikubwa mambo ya filamu hapo Tanzania na vijana wengi wameanzia kwake hizo kazi ningependa kuwasilianana naye maana nahitaji darasa kidogo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...