pamoja na kwamba binti yetu flaviana matata amekuwa gumzo huko mexico lakini miss universe ya mwaka huu imeingia kiwingu baada ya mrembo wa uswidi kuamriwa na nchi yake kujitoa mashindanoni kwa kile kilichosemekana kuwa ni ukandamizaji wa kinamama na kuwa mashindano ya urembo yamepitwa na wakati. naomba tujadili kama uswidi wamefanya sawa na je na sie pia tuige mfano huo kwa kumuondoa flvaiana mashindanoni? kwa habari zaidi za mkasa huo na mengine kumhusu flaviana bofya hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 26, 2007

    JAMANI MNAOJUA KISPANIOLA TUTAFSRIENI HIYO ARTICLE HAPO CHINI YA GAZETI MOJA LA PANAMA. INAELEKEA MREMBO ANAMWAGIWA MASIFA.

    Miss Tanzania, rompe clichés de belleza
    --------------------------------------------------------------------------------



    Fuente: Agencias Internacionales
    Con sello propio, pero si de romper clichés se trata, los aplausos corresponden este año a Flaviana Matata, Miss Tanzania, quien es la primera participante del certamen en lucir la cabeza totalmente rapada. La africana, quien es modelo y técnica electricista en su país, espera que los jueces no consideren un inconveniente la ausencia de una larga cabellera, como la que caracteriza a la mayoría de sus compañeras. "Nunca le permito a nadie que me juzgue por mi ropa o por mi cabello. Creo firmemente que Dios me creó perfecta, una mujer africana pura y natural", advierte Flaviana a través de una entrevista que sirve de presentación en la página electrónica oficial de Miss Universo 2007.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 26, 2007

    Naungana na Sweeden, si hakihata kidogo wanawake kukaa uchi huku wanaume wakiwa wamevaa wanawafaidi kwenye swimsuit na vitakataka vya aina hiyo. Naamini huo ni mwanzo na wengine watafuata kupinga udhalilishaji huu. Kama tuna lengo la kuitangaza na Tanzania na kujisifia si kuwafanya mabinti hawa kutembea uchi. Mbona wanaume hawatembei uchi kuitangaza nchi. Huu ni udhalilishaji. Turejee mafanikio ya mamiss wa Kitanzania, sina hakika kama yapo na kama yapo ni kidogo sana, kubwa zaidi ni kuwashuhudia wakiwa uchi. Nani asiye yajua ya Wema Sepetu kuna blog moja ilimuonyosha uchi, sasa hii ni nini kama si mavuno ya Umiss.
    Naamini watajitokeza wengi kupinga lakini yale mataifa ambayo yanachukuliwa ndiyo kigezo cha Demokrasia yaani mataifa ya Scandinavia yameonyesha njia naamini tutafuata.
    Wale ambao wapo tayari kuwakomboa dada zetu na mama watarajiwa tuwaokoe wasichana hawa. Naamini Flaviana atapoteza muelekeo.
    Tumeshuhudia mashindanoya mamiss ya kiwafaidisha waandaji na kuwaacha mabinti hawa wakibakia kenye magazeti ya Udaku. Tunataka nini Watanzania?
    Chonde tusaidiane kuwaokoa watoto hawa

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 26, 2007

    Michuzi tafadhali usianze kuleta gundu hapa, kumuondoa Flav kwa nini? Baada ya kufika mbali hivo mtoto wa watu tafadhali acha kuanzisha hoja ambayo haina mpango, tumpigie kura na kumuombea ushindi ,thats it!
    Go Flavvvvvv,
    Nimempigia kura kila siku am doing my part, lets do it wabongo.... we know we can do it.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 26, 2007

    ee Mungu wangu
    hii mbona kali jamani.

    Ngoja niisublie kwenye taarifa ya habari.

    Sijazipata habari hizi.
    kwenye tv za hapa.

    Du inakera siyo siri.
    Wabongo tuendelee kudunda achana na hawa majamaa.

    siyo siri ni upuuzi huu.
    mh haya tuwaachie wenye nayo.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 26, 2007

    Hao watu wa Sweden wana siasa zao tu, mimi nafikiri hakuna haja kujiondoa. Maana hata hiyo Miss World iko kama hii ya Universe. Achana na Waswidi.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 26, 2007

    I read that article and I totally disagreed with Sweden decision.
    Firstly, Contestants were told before the competition what to expect and they agree with the terms.

    Secondly, I still don't understand why they waited for so long to withdraw that lady from the competition...if really they are concerned about women degradation then why they exposed her in those conditions at the first place? An environment that made her vulnerable

    Thirdly, They didn't support their allegations with circumstantial evidence which lead me to conclude it is just one of those empty rhetoric.

    Tanzania is a sovereign country and we are not going to make decision based on sweden view on certain issue. Unlike Sweden, Tanzania needs Miss Universe platform to promote itself...

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 26, 2007

    yoo bro michu, unauliza swali wakati jibu lipo wacha hizo weee. kila pemba ya duania yetu wakina dada zetu na mama zetu wananyanyasikia kijinsia, wamefanywa chombo cha starehe na burdani. kinachosikitisha na kushangaza na pia kukerehesha nafsi zetu nikwamba huko nyumbani nayoo mambo haya yapo.watu wanafagilia mafashion show, vipodozi sijui nini mara nini, badala ya kufagilia elimu. sisime kusoma ndo mtu unaonaekana wa maana sana na sisemi asiye soma ndo mjinga lakin elimu inasaidia jamani.
    wazungu wameliona zamani na nji kama sweden ndo kabisa upuuzi huo hawana wakiona wakina dada zao wanazalilishwa wanachukua hatua kama waliochukua. waachiyeni wakina dada zetu wadengue dengue tu wanaona la maana kumbe wapi.
    mchana kweupi dada zetu wanengua nengua juu za meza za majaji wa kiume halafu leo hii tunapiga vita ukimwi unadhani utakwisha hivi hivi, turekebisha tabia zetu na tutulizee ball katika ngono.
    mkuu wenu wa nchi alikuwa mkali wa totoz na bado pia sasa hata ukisema sheria itumika tumtoe mwana wetu flavia yatakuwa yale yale kesi kupelekea nyani na wakati tumbili ndoyo huyo huyo.
    poleni sana wakina dada zetu mungu atakusadiyeni mtakuja majuu msome mpate kuelimika. amen.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 26, 2007

    Kwanza kabisa binti wetu Flaviana Matata anawakilisha Bongo sio Uswidi na pia ndio nafasi yake kufanya kitu anachokataka kufanya Fashion well hawa uswidi wamemtoka mrembo wao kwa sababu zao minafasi na pia wameona kuwa mwaka huu sio wa kwako ndio wanatafuta sababu zisizo na msingi..
    Kwa mrembo wa uswidi kuamriwa na nchi yake kujitoa mashindanoni kwa kile kilichosemekana kuwa ni ukandamizaji wa kinamama na kuwa mashindano ya urembo yamepitwa na wakati sio kweli kama mambo ya kina mama yapo siku nyingi hasa third country so kwa nini leo waone kuwa na tena wakati wa mashindano yamefikiwa mwisho wake .... Please Flaviana Matata umekwenda kuwakilisha bongo yetu na mwenyewe pia so make you name as Flaviana matata and you come from Bongo.....
    take care na tupo na wewe pamoja ushindi wako ndio wa taifa letu na vilevile keept it

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 26, 2007

    Sweden wanoko tu. Lini wamepata a change of heart? Kwa nini wasingeacha kushiriki kabisa toka mwanzo? Why now? Why this late? Si mashindano yameanza kitambo tu kwanini wamesubiri mpaka saa hivi?

    Wamezoea kuona all blonds girls sasa wameona this time wengine wako dark and bold na wengine wako dark and rastafarian macho yanawatoka. Wamezidi segregation na hawataki kushindwa na mtu mweusi.

    Lakini hii news itasaidia watu wengi waangalie hiyo siku? Kwa upande mwingine ni hop hop to Donald Trump.

    Tumwache mrembo wetu asonge mbele. Mara ya kwanza na mara ya kwanza amekua noticed? Ameenda top 15. Hapa pamoja na kuwa ni ushujaa wake lakini tunamshukuru sana kwa kututangazia nchi yetu pia,

    YOU GO GAL

    Best of Luck

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 26, 2007

    Ajitahidi kubadilisha pozi la kichwa anaweka upande mmoja sana kitu ambacho hupingwa sana katika ulimwengu wa mapozi.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 26, 2007

    jamani wandugu naona mrembo wetu kaingia 5 bora..bonyeza iyo link...wawawa flaviana taji lako hilo labda wakubanie tu all the best http://www.pageant-almanac.com/miss-universe/playoffs.php

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 26, 2007

    waondoe huu ni nyanyasaji, wanawake wamefanywa mapambo ya dunia, well hawakulazimishwa!
    Ila nikiliangalia hili jambo kwa jicho la kifeministi nawapongeza waswidi!

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 27, 2007

    Sipendi kuwakatisha tamaa wanafikiri kuwa haya mashindano ni ya maana. Kwa maoni yangu naungana na Wasweden kumwondoa 'mrembo' wao. Hivi wanawake wanapoongelea kujikomboa au wazo zima la 'feminism', wanategemea watajikomboa lini. Mambo wanayoshikilia ikiwa ni swala la urembo, kwa kutumia hela za nchi au wadhamini, wakati kuna mambo mengi ya kufanya kwaajiliya maendeleo ya nchi. Kuna maradhi, kuna njaa, ukosefu wa hudumu nyingi muhimu nk.
    Labda wangekuwa wanawakusanya wanawake 'warembo' kichwani kwa kuwashindanisha, kufanya mijadala ya kutatua matatizo ya kijamii, kuliko mavazi. Afterall, nikiwa mkristu, biblia inasema Mungu aliumba watu wote kwa sura na mfano wake. Kwa msingi huo, hakuna mwanamke mzuri wala mbaya, ila jinsi tu macho yetu yanavyoona kibinadamu, kuwa wengine wazuri zaidi. Simkandii Flaviana Matata, ila ninachoweza kusema ni kuwa, huyu binti ana 'GREAT SMILE' na meno yake yanang'ara kuliko ya Wazungu. Vinginevyo hana uzuri wowote wa kuwakilisha Taifa.
    Hebu tuache mambo ya mchezo kama haya na tujadili mambo ya kubadili hali za watu wetu. Vingineyo mwanamke ataendelea tu kubakia chombo cha kumburudisha mwanaume. Hata mkibisha wala sioni ajabu, maana wengine mtaniona waajabu.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 27, 2007

    Anony wa 2:03 Am, meno yake yamepakwa polish ya meno. Polish hizo zimejaa kila kona ughaibuni

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 27, 2007

    ANON WA KWANZA HAPO JUU TAFSIRI YAKE HAPO NI KAMA IFUATAVYO:

    Miss Tanzania, breaks beauty cliches
    ------------------------------------------------
    Source: International agencies With own seal, but if to break cliches it is tried, the applause correspond this year to Flaviana Matata, Miss Tanzania, that is the first participant of the contest in shining the head totally shaved. The African, who is model and technical electrician in his country, hopes that the judges do not consider a disadvantage the absence of one long hair, like that characterizes to most of its companions. "I never allow him to that it judges me by my clothes or my hair. I create firmly that God created to me perfect, pure an African woman and natural ", it notices Flaviana through an interview that serves as presentation in the official electronic page of Universal Miss 2007

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 27, 2007

    hao wa-Sweden wapuuzi tu. Bila shaka hawapendi kuona mtu asiyekuwa na nywele anawapiku manaake kule uzuri wao uko kwenye nywele (yaani wale wenye nywele za rangi ya dhahabu (blondes)) ndio wanaonekana wazuri.

    Sasa kupanda chat kwa Flaviana ambaye hana hata unywele mmoja kutakuwa kunawauma.

    Unajua hii ni kawaida. Hata state watu weusi wakihamia kwenye makazi ya weupe basi weupe huanza kuondoka taratibu

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 27, 2007

    THIS IS HER INTERVIEW WITH MYAFRICATODAY.


    What are your interests and what do you enjoy doing the most?
    I enjoy modeling. Fashion is my passion. Music is also something I am interested in.

    What is your career ambition?
    My ambition is to be an engineer as well as a top model and also a fashion stylist.

    Describe where you were raised and what your childhood was like.
    I grew up in the Shinyanga region in a normal family. Shinyanga is a region in Tanzania that is known for its minerals, especially diamonds, and is also reputed to be endowed with precious stones. I had a happy and fun-filled childhood where laughter and adventure were a part of every day life. I also frequently visited the mines in the area with my family and friends.

    LINK: http://myafricatoday.blogspot.com/2007/05/miss-universe-tanzania-2007-interview.html

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 27, 2007

    MICHUZI,
    Kuna mtu kajifanya kutafsiri Kihispania kwenda Kiingereza hapo juu. Kama tafsiri zenyewe ndio hizo ni hatari sana. Sijui Kiingereza hicho amesomea wapi huyo bwana. Sentence ameziandika si sentensi, ziko katika mfumo wa tungo tegemezi. Pili, ametafsiri neno kwa neno , na maana haiji katika ujumbe uliokusudiwa. Tatu, anatumia kiwakilishi au 'pronoun' - 'his' badala ya 'her'. Hivi Flaviana ameshakuwa 'he' mara hii.

    Tafsiri kwa Kiswahili bwana. Usijifanye kujua Kiingereza wakati unaandika meneno tu na si ujumbe. Vyote vinatakiwa ili tuelewe unasema nini.

    NAWAKILISHA.

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 27, 2007

    Aisee huyu mtoto mzuri bwana mmasai nini ila mbina hana jina la kimasai kama yoyo n.k

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 28, 2007

    Sasa wewe unayajua Kingereza you could translate for us! Acha ushamba bwana, someone tried to translate na wewe unajifanya unajua, wabongo vipi!!!!

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 28, 2007

    Hao wanaosema ni unyanyasaji wa wanawake mbona hiyo show ikianza ndio wa kwanza kufungua channel kuangalia?

    Halafu mbona kuna mashindano mengi ya kutafuta wanaume wazuri tu kila siku lakini haya pati watu wengi sana ndio maana hayajawa ya kimataifa pia. Kuna kumtafuta fireman mzuri , policeman mzuri, na mashow mengine mengi tu hata chippendale dancer kila kona.

    Tusubiri watu wengi wakishakua gay miaka inayokuja basi na hayo ya wanaume yatakua mengi. Kwa vile wanaume ndio wanauroho wakuangalia watu warembo sana kuliko wanawake. Sasa hapo yakija huko bongo sijui mtasema ni nini. Unyanyasaji wa wanaume...???? Let us show our talent and beauty.

    Mimi basi tu nimeondoka bongo ndio walikua sijui mwaka watatu toka waanzishe na nilikua mdogo obvious wazazi wangekua norma. lakini wakianzisha MRS TANZANIA mtaniona natinga.... Michuzi let me know wakianzisha hilo shindano. Mimi nitakuja kugombea.

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 28, 2007

    nyie mbwiga hapo juu huyo aliyetafsiri Kispaniola katumia electronic translator (mfano google translator). Inabidi uchambue hiyo tafsiri kupata idea ya ujumbe uliomo.

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 28, 2007

    WILLIAM,
    Acha ushamba na wewe. Unataka tusikosoe ili yabaki makosa kama yalivyo? Nadhani hukunielewa. Maana yangu ilikuwa ni kwamba, aliyetafsiri pale anajua Kiswahili, na wasomaji wengi hapa ni Waswahili. Mie sifagilii Kiingereza, na kikikosewa, ndio kabisaa, nakerwa mno. Kama mtu anajua Kiswahili, kwanini unasema 'kajaribu'wakati halazimishwi kutumia lugha ya kigeni? Nakijua sana na sikifagilii, maana najua kuna mahali kinahitajika. Hii blog wasomaji wake asilimia zaidi ya 90 ni Waswahili, kwanini utumie Kiingereza.

    Nampongeza sana bwana MICHUZI, kila akitoa habari kwa Kiingereza, huomba radhi kabisa, kwamba 'Inglish iz not richebo'. Sasa na huyu aliyetafsiri, ili kuwa safe, angesema kuwa 'hii najaribu kutafsiri' badala ya kujifanya anamsaidia yule mwandishi wa kwanza kwa kutoa Kiingereza, chenye makosa.

    ASANTE. WABONGO TUNAPENDA KUJIONA TUNAJUA KILA KITU, AFU TUKIKOSOLEWA ILI TUBADILIKE, TUKO WABISHI. Hasa watu kama William, uliyetoa maoni hapo juu.

    ASANTE.

    ReplyDelete
  24. Hao waswidi wanajidai wanajua haki za wanawake, wakati wao ndo wanaongoza kwa umalaya ulimwenguni na hasa hasa nchi za mashariki ya Afrika. Nani asiyejua wanawake wa Kiswidi ndo wanaongoza kwa kujiuza bure bure kwa vijana wetu mamba (marasta wanaowaza kwenda Mtoni-mamba kwake mtoni) wa DSM?

    Wanatengeza Filamu zaidi ya milioni kwa mwaka za Ngono za wanawake ndani ya nchi yao, na kuwachukua mabinti wadogo toka Estonia, Latvia, croatia, na Poland kwa ajili ya kutengeneza filamu hizo. Kwanini wasizuie biashara hii ya kudhalilisha wanawake, na wanaijua na wanaiacha iendelee ndani ya nchi yao kwa kusaidia ajira za vijana wao.

    Anaeitetea Sweden anaijua vizuri au anatetea ujinga wa vyombo vya habari na kujiita Feminist? Ishi ndani ya Sweden uijue.

    Kama kweli ni udhalilishaji kwanini kuna mashindano kibao ya urembo ndani ya Sweden mpaka muda huu?

    Sababu kubwa ya wao kujitoa ni u-mangi meza tu na ukiritimba kwa kuwa wabaguzi wa rangi na kujitangaza ulimwenguni kwamba hawana ubaguzi, kumbe wanaongoza kichini chini. Sweden hata kupata nyumba ya kupanga mpaka jina lako liwe la kiswidi, na kwa muundo huo vijana wajanja hubadilisha majina yao ili yaishiwe na ....SON, kama JOHANSON, OLSON, AKESON etc ili uweze kupata nyumba za kupanga Stockholm, Skovde, falkoping, Jonkping, Malmo, Umea, Upsalla na Gothernburg.

    Flaviana anawatingisha sana, na huu ni mwanzo. mashindano ya urembo si lazima, kama hutaki kuangalia, lala. sisi wapenzi tutaendelea kushangilia. Kwanza mi ninavyojua katika kumkomboa mwanamke hasa wa kiafrica, mashindano haya yamesaidia sana kwani yamewatoa matongo tongo akina dada zetu na kuwafanya wajiamini na kujitokeza kuongea mbele za watu, pia kuwa na IQ, kwani majaji hawaangalii uzuri wa mapaja yako tu, wanaangalia na IQ yako pia. Na kuhusu mapaja mazuri wanaangalia, je wazazi wako wamekuleaje tangu utoto, na si wakawa wanakufinya mapajani na kukuachia makovu tu bila kujali uanamke wako, na urembo wako kama mwanamke.

    ACHENI MAJUNGU, MNAOJIITA FEMINISTS, NA KAMA MNATAKA LIGI, MIMI NI MPINZANI MKUBWA WA WALE WANAOJIITA FEMINISTS, NIKIANZIA NA BAADHI YA TAMWA, TGNP, etc.

    Kwanza naomba nitoe neno ambalo liko nje ya mada. Kuna mkurugenzi wa TGNP (Mtandao wa Jinsia Tanzania) alitoa neno, eti swala la Amina Chifupa ni la kibinafsi kwahiyo waandishi wasiandike. Nilimshangaa sana kiongozi kama yule kuongea ujinga kama ule. Hajui kama Amina ni mbunge wetu sisi vijana wooote Tanzania (ingawa si wote tunaomkubali), sasa akiwa msemaji wetu na mwakilishi wetu katika kutunga sheria zinazotetea vijana, akikosea tuna haki ya kujua, na kuhoji, au akisingiziwa jambo ambalo liko nje ya maadili ya uongozi tuna haki ya kuhoji kulikoni. leo Hii unatuambia ni mambo ya kibinafsi? Hawajifunzi kwa Clinton, alipofanya mambo ya kibinafsi, wananchi walihoji na mpaka wakapima DNA?

    Hawa wanaojiita viongozi wa kutetea Jinsia, wanadhani JINSIA NI MWANAMKE TU, na kwamba chochote anachofanya mwanaume ni kudhalilisha mwanamke, hawajui kama wanaume pia wanadhalilishwa? ACHENI kujidai FEMINISTS kwa manufaa yenu, teteeni haki kikweli kweli tena kwa pande zote. WAONGO WAKUBWA, mkisaidiwa na misaada toka huko SWEDEN.

    NAWAKILISHA

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 28, 2007

    ANON WA KWANZA HAPO JUU TAFSIRI NI KAMA IFUATAVYO:
    Source: International agencies
    In her own way, yes this contestant has managed to break the rules, the applauses in this year Miss Universe go to Flaviana Matata, Miss Tanzania who is the first participant of the contest with a shining head a complete skin head. The African who is a model and an electrical engineer in her country, hopes the judges would not consider an inconvenience regarding the absence of long hair, which characterizes most of her colleagues. "I would never allow anybody to judge me for my clothes or for my hair. I firmly believe that God created me perfectly, a pure and natural African woman", said Flaviana during an interview which serves as a presentation in the official electronic page of Miss Universe 2007.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...