ma-mac bobby na jokate sio tu walipendeza kwenye tuzo za muziki za kili bali pia waliimudu vyema kazi hiyo ambayo waliifanya kiprofeshno na bila kubabaikababaika

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 26, 2007

    Jamani sio siri Miss Tanzania mwaka jana walichemsha.... Jokate kila sehemu anakubalika lakini mwenzangu Wema mhhhhhhh!!! waliboogie Miss TZ committie...Jokate kiboko she is real n simple.... nakufagilia kip it that way

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 26, 2007

    Anon wa 3:18pm

    Hawakuchemsha Waandaaji miss TZ aliyechemsha ni Jokate mwenyewe hakuonyesha kama anakubalika kama ilivyo sasa. Na Wema alionyesha anakubalika tofauti na ilivyo sasa. Yaani ni kama football vile mambo dk 90 kipenga kikilia umepigwa bao ndio imetoka hivyo hata kama mechi zinazokuja ukimfunga 20 - 0 (mtungi) hautengui ushindi ulioupata. Mi naona mechi imepita tusubiri zifuatazo, AC Milan ( Wema) alibeba kombe basi Liverpool (Jokate) mkubali tuu si ndio maana ya kinyang'anyiro jamani!..

    Michu toa hii usi-i-trash... teh teh teh.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 26, 2007

    michuzi web site yake ni funga kazi, ipo up to date, ila rekebisha saa kaka, iko nyuma kwa bongo!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 26, 2007

    jamani kusema la ukweli jokate ni mzuri na alistahili kuwa miss tanzania sema kutokana na technicalities zilizotumika wema akapewa ule ushindi ila tukija kwenye swala la U MC yule mtoto hawezi kabisaa, kwanza anajaribu kuwa kama mtu flani lakini anashindwa kufika kwenye viwango vya huyo mtu, siku zote ninaposhudia akifanya U MC mahali nakuwa nasikia kama anaimba au anakuwa amekariri yale maneno thn anayaongea, kwa mfano jana alikuwa animba kwa sauti kubwa, yaani badala ya kufanya u mc alikuwa kama animba na sijui waliompa ile kazi walimwambia achangamke basi yeye akatafsiri kupiga kelele hili ndilo nalofikiria, sasa kama anaweza kujirekebisha afanye kama hawezi basi awaachie wanaoweza coz anaharibu kazi za watu na sisi tunaokwenda kwenye shows mbalimbali tunanyimwa haki yetu ya msingi ya kupata burudani kuanzia kwa MC na umaarufu haulazimishwi kiivyo, ni hayo tu.

    ReplyDelete
  5. Kwa kweli mimi nilifurahishwa pia na jinsi ma mc walivyoifanya vyema kazi yao,lakini tatizo lilikuwa kwa wale waliokuwa wakihusika na upande wa vipaza sauti kwa ajili ya sisi tuliokuwa tukiangalia tukio hilo tukiwa majumbani maana sauti ilikuwa inakatakata na hii ni kero ambayo sisi mafundi wa kibongo tutaimaliza lini maana mara nyingi sana baadhi ya mafundi wa bongo huchemsha katika hili hatimaye mtu anajaribu sauti wakati tayali yuko live,maana kulikuwa na maongezi mengine nilikuwa nikiyasikia ambayo hatukupaswa tuyasikie hewani pia matangazo yalikuwa yanakatikakatika hasa mwanzo ila BIG UP SANA KWA MA MC

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 26, 2007

    haswaaaaaaaaaa! anon wa hapo juu umeongea kitu amabcho kila siku mi huwa nakiona hicho. ni kweli kabisa na jokate yupo katika kila kitu. kuna vitu vingine wema alihitajika kuvifanya lakini sijawahi kumsikia zaidi ya kufungua vyoo vya shule ya msingi ya.... ila jokate amekubalika. hapo dj bobby na jokate mnavutia fanyeni mwe wachumba basi mpaka muoane. mnapendeza sana. NOPE

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 27, 2007

    Michuzi,
    Narudia tena kupost. Nilituma mara ya kwanza maoni yangu hukuweka katika blog yako. Najua umeegemea upande fulani.

    Narudia tena. Kwa mawazo yangu, japo najua wengi hawatakubaliana nami, mashindano haya hayana maana kabisa endapo watu wanaongelea ukombozi wa mwanamke. Kuna mengi ya kufanya kujikomboa kifikra, kiuchumi nk, na si kupoteza fedha za wadhamini au serikali kutuma mtu ashindanie urembo. Na kwanza urembo ni nini? Ni dhana pana mno. Ukiangalia maandiko kwa wakristu, Mungu aliumba watu wote kwa mfano wake. Hivyo wanawake wote ni warembo. Kama mtu akipinga dhana hii, basi na aendelee kuwakandamiza wanawake kwa kuwafanya wao kiburudisho cha wanaume kwa kutembea nusu uchi majukwaani. Haya ndio maendeleo tunayotaka, si ndiyo? Je, yanaongeza nini kwa kizazi kijacho cha watoto wetu?

    Nasema tena, Michuzi, usipotaka kuweka wazo langu, baki nalo tu mwenyewe, bila shaka unaguswa sana!
    Nawapongeza Wasweden kujiondoa. Hawawezi kuendelea kuwa washabiki wa vitu vidogo kama hivi. Kuna siku tutaambiwa tushindane kutembea uchi na kwasababu ni wazo la nchi zilizoendelea nasi tutaona ni maendeleo.
    ASANTE, NAWAKILISHA BWANA MICHUZI.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 28, 2007

    We anoy hapo 8:04 unaongea nini? Mbona kuna mashindano ya kutafuta mwanaume mzuri kila siku NY City? Kila siku wanaweka mashindano ya kutafuta a cute fireman in NY city. Na kila siku wanaweka calenda ya the top 12 men. Na hiyo utasema nini? Acheni hayo...

    ReplyDelete
  9. WEWE FEMINIST (anony 8:04) HAPO JUU UNA MATATIZO GANI? WE UNA MAKOVU MAPAJANI NINI? nenda kajichubue yatoke, maana una wivu sana na watoto wazuri, eti unajidai mashindano yanakukera.

    Kwa taarifa yako hao warembo siku hizi woote skonga imelala vichwani, na wasiosoma ni kama wewe. Urembo ni elimu pia. kama huna elimu ya kujua ngozi yako uitunzeje, nguo zako ziweje, na rangi yako iweje, na chakula chako na mazoezi yaweje huwezi kuwa mrembo. We unadhani kukaa Darasani pekee ndiyo elimu? Acha zako. Maprofessor wangapi walevi, makahaba, malaya, vicheche, wabaya kwa sura, hawatunzi familia zao, hawafundishi vizuri wanafunzi wao etc. HAO KWAKO NDO WASOMI?

    JIFUNZE MAMA...kama siyo...BABA, kwani najua ungekuwa BABA USINGEPINGA MAMBO YA UREMBO.

    SAMAHANI WANA BLOG AMENIUDHI NA USHAMBA WAKE WA KARNE YA 20.

    Hivi hujui kwamba kila Decade ina mambo yake? femists walimamaliza mambo yao miaka ya 70 kule SWEDEN katika FLOWER-POWER, sasa wewe unayaleta leo hii miaka ya 2007. SOMA HISTORY ujifuzne, MSOMI WE!!!!

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 28, 2007

    I like her dress,its very simple and beatuful.Is that "the famous kanga" material?

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 28, 2007

    JOKATE IS PRETTY BT SHE CANT MC!! mbona anapewa post kubwa mtoto huyu wakati bado hajakomaa kumaster>> kwakweli she CAN NOT MC! uzuri tumeukubali wa sura na shepu ila ku-MC ahh ahhhhhhhh! nimekataa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...