wadau nafurahi kusema kwamba blogu yenu hii imeanza kuwa na meno. soma waraka huu pia...
Ndugu Michuzi,
Nafurahi kutumia blog yako kwani ina saidia kutatua matatizo lukuki.Kumbuka kwamba nilituma malalamiko kuhusu utapeli uliofanyika kwakuwapokonya kikundi cha ngoma za asili kiitwacho MACHOZI haki yao walioitolea jasho na kuwapa MANDELA THEATRE ambao wala hawakushinda.
Leo kuna taarifa kwamba baada ya wale matapeli kusoma kwenye blog hiiwame wapigia simu MACHOZI na kuwaambia kuwa waandae vijana wa kwendaZambia. Hii imeniacha mdomo wazi!!! Walipoambiwa hawaendi waliambiwakienyeji bila ya barua. Hata sasa hivi, kuambiwa kuwa waende wameambiwa kienyeji.
Suala la kujiuliza ni kwamba nini kilitokea katika kona zenyekiza? Tunapenda kufahamu. Kama wiki iliyopita waliambiwa wamechelewa,imekuwaje hawajachelewa wiki hii?!!Baada ya mashindano, waliambiwa watapewa pesa zilizopatikana kutokana naviingilio ili waweze kufanyia maandalizi.
Pesa hizo hawajapata hatasenti moja na bado wanaambiwa waende. Hawajaonyeshwa mkataba na walahawaja ambiwa watalipwa kiasi gani. Hawajuwi wanakwenda kufikia wapi nawanakaa kule siku ngapi. Yote hayo yamefanyika kwa haraka ili watu fulani waweze kujiokoa angalau kidogo.
Machozi wamepigiwa simu Jumatano 16/05 wakati walisha jiingiza katikakazi zingine baada ya kukatishwa tamaa. Walisha pokea pesa na wanatakiwakuanza Jumatatu. Siku iliyo baki kwa maandalizi ni leo na inaonekanakiongozi wao anatakiwa kuomba ruhusa kazini, kama akishindwa itakuwavigumu kwa kuwa safari ni Jumatatu 21/05.
Wadau nawauliza, hivi wakubali kuondoka au la? Naomba maoni yenu.
M. Chifu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 18, 2007

    Hiyo simu ya kitapeli. Kama wanataka kweli kujua Baraza la Sanaa wanaweza kuwapa jibu. Wanatakiwa kujua mkataba kabla kwenda manake wasije uziwa mbuzi kwenye mfuko wa sulfeti

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 18, 2007

    Mungu ni mwema, kama wamepata nafasi ya kwenda waende!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 18, 2007

    waende tu wawakilishe nchi yetu vizuri. hao wengine ambao hawakushinda hawatatuwakilisha vizuri.
    ndio maana kila tukienda kwenye mashindano ya kitaifa haturudi na kombe lolote. kwavile wanaopelekwa ni ndugu au rafiki za wazito tu

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 18, 2007

    Napendekeza kuwe na makubaliano ya kiofisi, kwa maana ya barua na mkataba halali unaoonyesha kuwa Machozi wanakwenda Zambia kwa muda gani na watafikia wapi na mwenyeji wao ni nani. Isije wakaenda Zambia na kuanza kuhangaika kwa kutelekezwa na hawa wasanii. Pia Baraza la sanaa Tanzania litumike ipasavyo kuwadhibiti matapeli hao, wanatia aibu taifa! Suala la kwamba muda unatosha ama hautoshi mi naona si la msingi sana, hili zigo wabebeshwe hao hao waliovuruga utaratibu. Nakuomba sana Mr Chifu fuatilia hatima ya Kundi la Machozi hadi uhakikishe haki inatendeka, hata kama hakuna kundi litakalokwenda Zambia. Tumechoka na usanii!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 19, 2007

    Anony wa kwanza kabisa kalonga utamu sana, Inabidi kupata mkataba wa shughuli nzima watalipwaje na wanalipiwa malazi nk, kwani jamaa hawa wanaweza wakawatosa kule si mmeng'eng'ania kuja mtajiju!!! si unajua mambo a kibongo, mi naona waende ila wawasiliane na Wazambia pamoja na baraza la sanaa kujua mustakabali wao huko.
    Wabillah Tawfiq

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...