The following are Facts about two Countries
France- Area= 674,000 square kilometre
Tanzania- Area= 945,000 square kilometre
French Population= 64 Milion
Tanzania Population= 38 million France - Per Capita income =$ 30,100 Tanzania- Per Capita= $ 723
France- Cabinet= 15( down from 30- reasons given , to cut cost)
Tanzania- Cabinet 60( up from 45- reasons given - to increase efficiency)
Taking into consideration of above factors, Tanzania is larger to France 40%(if we measure number of ministers per area, we would need like 20-25 ministers)
Tanzanias population is only 60% of french's( if we measure number of ministers per number of people, we would need only 10 ministers).
Most importantly, look at the per Capita of the two citizens, since the government is run by moneys collected from its people, we do not have even 10% of what french people earn.
Tutaendelea kweli, kwa mabenzi haya, mawaziri 60, makatibu tawala, wakuu wa mikoa, wakurugenzi wa kumwaga na kadhalika.
By the way, this is my opinion, due to laymaniship.
Yangu machoooooooo
Have a good day


Duh! tunahitaji kufikiria na kuchukua uamuzi mapema iwezekanavyo!!
ReplyDeleteShida ni kwamba viogozi wanadhani kwamba watanzania wote ni wajinga! Wewe umewahi kusikia wapi baraza la mawaziri 60!! Marehemu Sokoine alikuwa akipendekeza idadi ya mawaziri iwe sawa wa idadi ya wajumbe wa CC (kwa wakati huo), yaani watu 21 tu!!!
ReplyDeleteWakati wenzetu wana-cut down the size of the cabinet by 50% we have increased ours by 36% and yet we expect Maisha Bora Kwa kila mtanzania! Bonge la analysis hili!
ReplyDeleteHuu ndio unaoitwa Ujinga wa Mwafrika, maliasili tunayo, lakini .... hatuna, ndio maana wazee wetu walisema penye miti, hakuna wajenzi. Inasikitisha lakini ndio hivyo, tunashabikia kuuza nji nzetu kwa rushwa na utawala mbovu
ReplyDeleteHakyanani kwa kasi hii na uongozi wa aina hii hatuendelei si leo, kesho wala miaka 100 ijayo hatutoki.
ReplyDeleteKibaya zaidi hawa viongozi wa sasa wanajenga tabia mbya ndani ya jamii. Tabia ya Rushwa, Ufisadi, Kulindana, Kujenga mitandao n.k.
Sometimes huwa najiuliza kama viongozi wetu wana akili au tope vichwani mwao. Kwa sababu naona majibu ya matatizo ya nchi yetu ni rahisi sana tu na yako wazi hata kwa mtu amabye hakusoma.
Bw. Michuzi hata Angela Markel wa Ujerumani hatua ya kwanza aliyochukua alipoingia madarakani ilikuwa ni kupunguza matumizi ya serikali ili kunusuru uchumi wa nchi. Sasa sie twalipana fadhila eti nani alifanya nini wakati wa kampeni na apewe madaraka!
Kituko kabisa. Nchi haiendi, bei zinafumuka, maisha hali ngumu, wanafunzi hawasomi, barabara hazijengwi, mashule bla bla hayana walimu wala vitendea kazi, rushwa kubwa zashamiri, nchi kazi kutegemea misaada tu na maliasili zachukuliwa hovyohovyo. Ni takataka tu kila kukicha. Nchi haina ajenda kabisa.
NA DITO YUKO HURU!
Cha kushangaza matumizi ya Ikulu yetu huenda yanazidi hata ikulu ya marekani.
ReplyDeletewe uliyetoa hiyo analysis kati ya france na tanzania ninakushukuru sana tena sana,hayo ndiyo mambo yakuwaeleza watanzania waliolala usingizi tororo.lakini dawa yake ina chemka.
ReplyDeleteTena kuna katibu mkuu na naibu waziri,wizara zingine manaibu wawili...haileti maana kabisa,sijui hawa wote wanafanya kazi gani?Mimi hata siioni,msisahau huduma lukuki wanazozipata kutoka serikalini...ujinga mtupu!
ReplyDeleteTutaendelea kuwa maskini tu,na hii ni kwa sisi maskini..sio wote,wachache wanapeta tu.
Na chakusikitisha ni kuwa hata hao 60 waliopo 40% ndio wana vyeti au wameweka degree za kweli kwenye CV zao. Na 40% wana hawana hata high skull diploma.
ReplyDeleteNdio maana hawaoni hata umuhimu wa Elimi tena kwa vile wana believe kama wanaweza kuwa viongozi na elimu waliyonayo sasa kwa nini wasomeshe viongozi wa kesho?
Mbona umesahau kuwaambia wadau kwamba france was heavily involved in the exploitation of Africa and many other places across the planet .From Slavery to Colonialism..Acha utani bwana..France would not become what it is today without the suffering and exploitation of many..Ndio serikali yetu ovyo lakini thats not the reason behind our weak Economy and low quality of life...its deeper than that...next time compare Tanzania na Kenya may be that could be a fair comparison.
ReplyDeleteMwaziri 60 ni sera ya chama ya kuongeza ajira nchini....nyie mko wapi?
ReplyDeleteGood eyes, good catch. Excellent analysis!
ReplyDeleteSasa kama ni hiyo exploitation, what about Korea, Malasyia, Singapore just to mention the few, tuache India na Pakistani nao walitu-exploit??? Kama si ujinga wetu.
ReplyDeleteOr just compare ourselves na Nchi Jirani kila siki tutasema sisi tuna amani, hatuna ukabila kama , ardhi bora tunayo bora kuliko ya jirani, madini na utalii etc etc , lakini tupo wapi? Hata Check GDP ya Rwanda ni kubwa kuliko ya kwetu sasa sijui tatizo ni watu tupo wachache, eneo etc. Mpaka Juzu juzi nikasikia Mungai kaenda kujifunza alternative source of power rwanda, wanavyo tumia kwenye magereza yao, wakati kitu kama hicho Tz tulisha ki-discuss miaka ishirini iliyopita tuka tia kabatini huo mpango,
Ushaidi huo nenda CARMATEC Arusha utaukuta huo mradi au hiyo elimu ya Alternative source of power, JKT zilitaka kuanza lakini kama kawaida yetu ukaishi hivyo hivyo, matokeo yake badala ya muda mwingi ku-invest kwenye production sisi tunatafuta kuni, maji ya kunywa , kutibu malaria, cholera etc, halafu uta sema Mfaransa katunyonya
Mfano butu huo Huwezi kufananisha France na Tanzania:
ReplyDeleteUfaransa kwa ukubwa wa uchumi ni nchi ya sita duniani.
i)Ufaransa ina serikali za majimbo 22 ambazo zina uhuru mkubwa(autonomy) katika utendaji na maamuzi.Wenzetu infrastructure yao ipo juu sana na teknologia ipo mbali. Kazi kubwa ya serikali kuu ni coordination ya sera tu.
ii)Serikali ya ufaransa ina mawaziri 15 lakini pia ina secretaries of state 5 na idadi kubwa ya assistant ministers. Idadi ya mawaziri kamili kwetu ni 29 na manaibu 31.
iii) Hujasema pia kuwa ufaransa ina zaidi ya wabunge 923 yaani national Assembly 577 na senate 346. jaribu kucalculate gharama zao upate hali halisi kwa kulinganisha na kwetu.
iv)Wizara ni mjumuiko wa Idara mbalimbali. Ukipunguza mawaziri inabidi upanue wizara nyingine kwa kuziongeza hizo idara matokeo yake ni urasmu na utafunaji zaidi. Hata ukipunguza mawaziri 20 wenzangu labda mnajua utaokoa asilimia ngapi ya bajeti na utapunguza urasimu kwa kiasi gani katika nchi masikini kama yetu?
Toeni mifano inayolingana na hali halisi siyo ya kumlinganisha Tembo na sisimizi.
Anon. wa Tuesday May 22, 2007 5:12:00 PM unaongea kama msemaji wa serikali ya hawamu ya nne. Maelezo yako hapo juu hayana msingi zaidi ya kuhalalisha rushwa inayoendelea Tanzania. Ufaransa ni nchi kama Tanzania kwanini nchi mbili zisifananishwe? Kumbuka kuwa kuna globalization siku hizi, Ufaransa na Tanzania tunacheza katika uwanja mmoja. Ukisema Ufaransa na Tanzania sio sawa basi nenda ukaishi sayari nyingine kwani katika mashindano ya kibiashara na uchumi utakuwa mshika mkia milele. Your kind of thinking really makes me sick to my stomach. You are pulling us back man, don't talk for Tanzania talk for yourself.
ReplyDeleteMchangiaji wa juu yangu naona hata hesabu za kulinganisha zimekupita pembeni.
ReplyDeleteUnataka tukwambie Kikwete ni kiboko utuonyeshe magego yako ?Kaa nayo mwenyewe !!
i)Hivi hiyo Ufaransa kuwa ya sita kwa uchumi duniani iliumbwa hivyo au kuna kitu kilifanyika ?Ukiondoa mandeleo waliyofikia kwa kutumia colinialism.Je tuko nao sawa kwa yale waliyofanya bila hata kujumuishutumwa ?
ii)Kuhusu ufaransa kuwa na majimbo 22 ndiyo maana inafanikiwa,wewe ukiona kwako mambo hayaendi,kwanini usiige kwa mwenzako aliyefanikiwa na wewe ufanikiwe? au ukifanyahivyo utashitakiwa na kufungwa ?Kwanini na sisi serikali yetu isiwe na kazi ya ku"coordination" tu ?Anandika hayo una uzoefu au kwa kuwa kuandika ni rahisi ndugu yangu ?Coordination bila responsibility na accountability wapi na wapi ? Au ni mambo ya robot hayo ?
iii)Serikali ya ufaransa ina mawaziri 15 na secretaries of state 5,kwa hesabu zako hapo umepata jumla ya wangapi ?linganisha na idadi uliyotupatia ya hapa TZ !!Una halalisha ubadhilifu au na wewe ni kati yao ?
iv)Umetupatia idadi ya wabunge wa Ufaransa 923,lakini unatuambia ni mabunge yote mawili,antional assembly na senate,ujatuambia unafananisha hiyo na ukubwa wa serikali ya TZ au bunge letu .Kwa mantiki hiyo,bunge letu lina natioanal assembly na senate ?Kumbuka hapa tunalinganisha ukubwa wa serikali.
Unajichanganya kwa kutumbia tuangalie gharama za matumizi ya bunge lao,wakti umeshatuambia Ufaransa ni nchi ya sita kwa utajiri duniani,mbona unataka kutufanya wote hammnazo ?Au unatufunga ili upate kula zaidi ?Angalia,mwisho umekaribia haraka kuliko ulivyotarajia !!
v0Hiyo hadithi uliyomalizia hapo chini labda ukawaite watoto wako kama unao uwakalishe chini na uwatambie hiyo hadithi,lakini hapa siyo mahali pake mhishimiwa sana.Hayo yote yanawezekana kama kuna responsibility-- knowing what you are supposed to do,and accountability-- being accountable to what you do !!Au hilo nalo tukuandalie warsha na kungamano kukuelezea ?? Next time you need write something,do a critical thinking first,siyo kuwapigia makofi watawala wakati nchi inaangamia.
Nawakilisha !!
Wewe msemaji wa serikali muongo. Senate ya Ufaransa ina wawakilishi 321 na kila mjumbe anawawakilisha watu 150,000. Mwaka 2010 ndiyo litafikisha wawakilishi 346 kutokana ongezeko la watu. Unaona nyie mlivyokuwa wapambe na mnavyopenda uzushi. You can't even have your fact straight. Siku zenu zinahesabika.
ReplyDeleteHuyo either akili zake za tope au ni wale wako tayari kuuza utu wao kwa shs 10,000 za Tshs.
ReplyDeleteKwasababu amepewa mifano ya Malasyia, Korea, na Singapore, sio kwamba uchumi wao uko sawa na wa France kuwa wa sita Duniani, lakini wamepiga hatua kuelekea huko. Na ukiachilia mifano hiyo ya mbali , amepewa mfano wa Rwanda ambo GDP yao per person iko kubwa kuliko yetu, then angalia ya Kenya ambao only 1/3 ya ardhi yao ni arable, while Tz ni 3/4 and above, then utali tunasehemu nyingi, madini, etc, lakini kutokana na kuwa na wapiga kura kama yeye, wakipewa chumvi kopo mbili, anaanza anakuachia Dhahabu kopo Moja.
Ndio maana kuna mtu moja kasema kuendelea Tz sio leo hii, ikiwa mtu na akili zake lakini kwa ujinga wake anaamua kuziwekea tope.
Na ndio hawa hawa wakiambia wadhini watoto wao wazazi wao wapate utajiri watafanya, au cheo atafanya maana hamna nazo, wanashindwa kuona hilo. Five years ago 1kshs was equal to 10 Tshs , baada ya kupata Dhahabu Bongo badala ya hiyo rate ku-karibiana ndio imezidi kuongezeka now it is approximately 18 tshs to 1 Kshs
Anoy wawili wa hapo juu asanteni saana kwa kumzodoa huyo mpiga debe wa mtandao.
ReplyDeleteMimi ni annon wa 5.12pm. nashukuru kwa maoni yenu kwani yamenipa somo kidogo kwa mabaya na mazuri pia. Lakini bado lazima tukubali ukweli kiuchumi hatuko sawa na ufaransa hivyo hatuwezi kujifananisha nao. Hatujiwezi bado tunajikongoja lazima tukubali hilo!Umaskini jeuri wa 1967 ulitufikisha wapi? Mimi nazungumzia hali halisi. Tumeona wangapi wakosoaji wakubwa kama nyie wakipewa nafasi wanavyogeuka kuwa wabadhirifu wakubwa?Angalia ripoti ya mkaguzi wa hesabu uone jinsi ubadhirifu kwenye halmashauri zilizo chini ya wapinzani ulivyo ngoma droo na zile za CCM. Point yangu ilkuwa ukubwa au udogo wa baraza la mawaziri unachangia parcent ngapi katika uchumi wa nchi?Hata wanaotubeba kwa misaada na mikopo ya masharti kwenye bajeti yetu ikiwemo ufaransa yenyewe wanaona hiyo siyo point muhimu. Niliweka idadi ya wabunge wa ufaransa maana kwa nchi hiyo serikali ni Rais, Bunge na Cabinet.Hivyo ukiangalia uwiano bado utaona gharama za kuendesha serikali yao bado ni kubwa sana kuliko kwetu. Coordination inamaanisha kuwa mambo mengi yanafanywa na serikali za majimbo kwa bajeti zao serikali kuu inawaunganisha tu ili kupata uwiano wa uendeshaji.Ikiwa kubwa au ndogo effect yake ni ndogo sana. Mimi kama nyiye ndugu zangu hata mimi kuna mabo siridhiki nayo na ila naona mfano wa ufaransa haupo mahala pake. tujilinganishe na watani zetu wa jadi Kenya ambao licha ya kuwa na mawaziri wengi kuliko sisi, ubadhirifu kuliko sisi, mishahara ya wabunge na mawaziri mara kumi zaidi yetu,miaka kadhaa waliendesha bajeti bila msada lakini bado wako juu kiuchumi zaidi yetu? Kwanini? Kwa sababu wenzetu wanajua kujituma sisi tunajua kupiga makelele tu. Nyiye watoa maoni hapo juu maoni yenu sawa ni kweli kuna matatizo makubwa ya kizembe kwetu lakini mnatoa ushauri gani? Uwekeni uwanjani tuujadili siyo kulaumu tu! Mpira rahisi kuuona ukiwa nje lakini ukiingia dimbani kuucheza kazi!Ukubwa au udogo wa serikali bado siyo point kwangu na vile vile kutoa mawazo mbadala haimaanishi kuwa mimi ni msemaji wa serikali. Wadau nashukuru sana kwa maoni yenu na tueendelee kupeana somo bila jazba
ReplyDeleteKwa wale waliosoma historia YA Ulaya nadhani mta agree with my little view..ignorance is pure bliss..yani watu mnaweza kabisaa kukaa hapa na compare France and Tanzania..Tanzania created 1964, France???And those who talk abt Korea and India..get serious..those countries have had a culture of Business wakati mababu zetu wanavua samaki nyasa na kucheza ngoma..India and China were Trading with the west even before Mjerumani hajakanyaga Tanganyika tuacheni upuuzi, next thing mtaanza kuongelea South Africa na maendeleo yao sio?? Unafikiri mzungu asingeamua kuishi pale ingekuwa vp??Waafrika watujawahi kuwa na culture ya umoja hata sikumoja..Ukweli Watanzania hatujawahi kuwa na culture ya kibiashara wala nini Mwarabu, Mhindi na Mzungu ndo wameleta hiyo ideal..lasi ivyo watu wa pwani wangekuwa bado wanaota jua na kuvua samaki, wachagga wangekunywa mbege zao na kuchunga mbuzi na ng'ombe..France has had Kings for centuries even though oppressive but united the people and led to massive development. Did u know that France funded the Americans to fight off the British?? Get serious toeni maoni yenye maana..Wanatanzania hatupendi kukubali hali halisi kwamba its very sad but true kwamba we were not a nation to start with..China had a strong empire before a white man stepped in..and thats what defines them as chinese..what defines u as a Tanzanian?? Kama sio serikali ya nyerere??..Mmakonde na Mchagga got nothing in common and dont even try tell me that they used to trade or had anykind of Unity before the white man came. Sio tanzania tuu, nchi nyingi za kiafrika are going through the same problems. Im Tanzanian and Proud and its our generation that can change our poor country STOP POINTING FINGERS AND ASK YOURSELF WHAT HAVE YOU DONE FOR THE COUNRTY YOU DEARLY LOVE.
ReplyDeleteAnon. of Wednesday, May 23, 2007 11:53:00 AM you are missing a point. I don't think if the issue is unity although Tanzanian are united enough to overcome their obstacles. Also, the issue is not weither France funded US to fight British; Tanzania funded many Liberation Organization such as ZANU, FRELIMO, SWAPO just to name a few to fight colonialism. The issue was big government, spending, corruption, nepotism, taxation without representation and accountability. I think this was the issue with the first person who started this debate. I strongly believe that France was a fair game.
ReplyDeleteTatizo la CCM si kukosa watu wenye uwezo wa kuongoza
ReplyDeleteKitila Mkumbo
NITAENDELEA kukumbuka mambo mawili makubwa kuhusu Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005.
Mosi, uchaguzi ule ulionyesha kwamba Watanzania walikuwa wamechoshwa na utawala wa Rais Benjamin Mkapa, na kwamba walikuwa wana hamu ya mabadiliko katika uongozi wa kisiasa wa nchi yetu.
Pili, uchaguzi ule ulionyesha pia kwamba Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa anatosha. Kutosha kwa Kikwete kulithibitishwa na ukubwa wa ushindi wa kura alizopata katika uchaguzi huo.
Hakuna shaka kuwa ushindi wa Rais Kikwete ndani ya CCM na baadaye katika Uchaguzi Mkuu uliamsha matumaini mapya miongoni mwa Watanzania wa kada na jinsia zote.
Hata hivyo kuna kila dalili kuwa Kikwete aliyeanza urais wake kwa kuwapa watu matumaini makubwa atamaliza urais wake watu wakiwa wamekata tamaa na kunyong’onyea kuliko wakati mwingine wowote tangu nchi hii ipate uhuru.
Serikali ya Kikwete si tu kwamba inaelekea kushindwa kutekeleza ahadi zake, lakini pia inaelekea kushindwa hata kulinda yale mafanikio madogo yaliyopatikana wakati wa utawala wa Awamu ya Tatu wa Rais Mkapa.
Katika kipindi cha miezi 17 cha urais wa Kikwete, mfumuko wa bei umepanda, ukuaji wa uchumi umeshuka na thamani ya shilingi dhidi ya dola ya Marekani imezidi kuporomoka. Tukiachana na hivi vigezo vya kiuchumi, Watanzania walio wengi ni mashuhuda wa kuongezeka kwa ugumu wa maisha katika miezi 17 iliyopita.
Kama kawaida ya serikali ya CCM, huwa hawakosi sababu za kuhalalisha kushindwa kwao.
Wimbo maarufu sasa hivi wa kuhalalisha kushindwa kudhibiti mfumko wa bei na matatizo mengine ni ukame na mgawo wa umeme, kana kwamba nchi hii ndiyo imeanza leo kukabiliwa na matatizo haya.
Utawala wa Kikwete utatukumbusha kwa mara nyingine kuwa tatizo la nchi yetu si kukosa watu wenye uwezo wa kuongoza. Wale waliokuwa na imani kwamba matatizo ya nchi yetu hayatokani na CCM bali viongozi wabaya katika CCM na kwamba kwa kumchagua Kikwete nchi ilikuwa imepata mkombozi itabidi wafikiri upya.
Ukweli ni kwamba ni vigumu kwa mtu yeyote mwenye uwezo kufanikiwa kuleta mabadiliko katika nchi hii kwa kupitia CCM ya leo. Yote hii ni kwa sababu CCM ya leo haina ajenda ya muda mrefu kuhusu maendeleo ya Tanzania, CCM ya leo haina uwezo wa kufikiri zaidi ya kushinda uchaguzi mwingine. Hiki ni chama ambacho kimsingi kimeishiwa ‘steam’ na kinahitaji kupumzishwa haraka.
Kwa hiyo hamu yetu ya kupata mabadiliko ya kweli katika utawala wa nchi yetu haitakamilika kama tutaendelea kubadilisha sura za viongozi pekee huku tukiacha mfumo wa utawala ukibaki uleule.
Tulianza na Mwalimu Nyerere. Mafanikio ya uongozi wake hadi leo ni mfano wa kuigwa. Kipindi cha Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa hawakufanikiwa sana kuleta mabadiliko ya uchumi, na sasa Jakaya Kikwete aliyebeba matarajio lukuki ya Watanzania kuondokana a umaskini.
Kinachohitajika sasa ni kuiweka CCM pembeni. Sababu ya kuiweka CCM pembeni tunayo. Sababu yenyewe ni ukweli kwamba Chama Cha Mapinduzi si tu kwamba kimeshindwa kupambana na vita ya kutokomeza ujinga, umaskini na maradhi, vita ambayo kilirithishwa na TANU, bali chenyewe kimebadilika kuwa sehemu na kiranja wa maadui hawa.
Hii inamaanisha kuwa hatua yoyote ya kujaribu kupambana na ujinga, maradhi na umaskini isiyohusisha kuindoa CCM madarakani imeshindwa kabla haijaanza.
Uwezo wa kuwashinda hawa maadui pamoja na CCM tunao. Uwezo wenyewe ni nguvu yetu ya kura wakati wa uchaguzi. Hata hivyo, ili kuweza kuing’oa CCM madarakani, tunahitaji jemadari wa kutuongoza.
Katika mfumo wetu wa siasa, hatuna jemadari mwingine isipokuwa vyama vya upinzani. Lakini vyama vya upinzani tutavikabidhi tu ujemadari wa kuongoza vita yetu dhidi ya ujinga, maradhi na umaskini pale vitakapoonyesha kuwa vyenyewe si sehemu ya adui, bali ni sehemu ya jawabu la matatizo yetu.
Vyama vya upinzani vinawajibika kuonyesha kuwa vyenyewe vikipewa nafasi ya kuongoza vitaweza kuihuisha na kuishinda vita iliyoanzishwa na TANU kwa kuwatokomeza hawa maadui watatu niliowataja.
Kwa maoni yangu, ili vyama vya upinzani vionekane kuwa ni sehemu ya jawabu na si sehemu ya adui na hatimaye viweze kuchagulika, vinahitaji kupitia hatua zifuatazo.
Hatua ya kwanza, wapinzani waonyeshe kuwa mbali ya kuwa waathirika, wao ni fursa.
Wataalamu wa saikolojia ya siasa (political psychologists) huvigawa vyama vya siasa katika makundi makuu manne. Kundi la kwanza ni la vyama vya siasa ambavyo vipo kisheria (de jure political parties) lakini havipo kihalisia.
Wataalamu hawa wa saikolojia ya siasa wanabainisha kuwa hivi ni vyama ambavyo ukiwauliza watu 100, si zaidi ya watu watano wanaoweza kuvitaja kwamba vipo.
Kwa kawaida hakuna mpiga kura ambaye hupenda kuvipigia kura vyama vilivyopo katika kundi hili kwa kujua kuwa kuvipigia vyama hivi ni sawa na kuipoteza hiyo kura. Bila shaka vyama vya namna hii tunavyo vingi katika nchi yetu.
Japokuwa kuna vyama zaidi ya 15 vilivyoandikishwa kisheria, ni wananchi wachache wanaoweza kuvitaja vyama zaidi ya vitano.
Kundi la pili ni vyama athirika. Hivi ni vile vyama ambavyo wapiga kura huviona kuwa ni sehemu ya kundi la watu wanaoonewa na kuathiriwa na mfumo wa utawala uliopo.
Hivi ni vile vyama ambavyo huvuta hisia na huruma ya wananchi. Kwa hiyo wananchi huhesabu vyama hivi kuwa ni sehemu ya waathirika, lakini si lazima wavione kuwa ni sehemu ya jawabu la matatizo yao!
Kundi la tatu ni vyama adui. Hivi ni vyama ambavyo kwa nje vinaonekana vina nia ya kupambana na matatizo yanayoikabili jamii. Lakini ukweli ni kwamba kwa ndani vyama hivi ni sehemu ya adui na pengine ndiye adui mwenyewe anayesababisha matatizo yanayoikabili jamii.
Hivi ni vyama ambavyo kwa kiasi kikubwa kuwapo kwake kunategemea nguvu ya dola na mali kuliko nguvu ya ushawishi katika umma.
Kundi la nne ni la vyama fursa. Hivi ni vyama ambavyo vinajipambanua kiitikadi, kifalsafa, kiuongozi na kimkakati kuwa ni vyama vyenye malengo thabiti ya kukabiliana na matatizo yanayoikabili jamii.
Kwa hivyo wananchi huviona vyama hivi kuwa ni fursa ya kutatua matatizo yao na hutumia nafasi ya uchaguzi kuvichagua ili vipate nafasi ya kutekeleza ajenda zao za kimaendeleo.
Kila mtu anaweza akavinyambulisha vyama vyetu vya siasa katika makundi hayo manne niliyoyataja hapo juu kwa kadiri uelewa na utashi wake unavyomtuma.
Kwa maoni yangu, vyama vyetu vya siasa tulivyo navyo vinaweza kuingia katika makundi matatu ya mwanzo. Wasiwasi wangu ni kwamba hatuna vyama vyenye kuingia katika kundi la nne.
Ni maoni yangu kwamba CCM ya leo imo katika kundi la tatu kwa maana kwamba chama hiki si sehemu ya majibu ya matatizo yetu, bali ni sehemu ya adui.
Mfano dhahiri unaothibitisha uadui wa CCM ni matumizi mabovu ya kodi zetu yanayofanywa na viongozi wa serikali ya CCM. Serikali ya CCM ipo tayari kufumbia macho upotevu wa shilingi bilioni 900, lakini wakati huohuo ikaona ugumu kuwalipia masomo wanafunzi wanaosoma vyuo vikuu kwa gharama isiyozidi shilingi bilioni 111.3!
Ni maoni yangu pia kwamba vyama vya upinzani vinaangukia katika kundi la pili, yaani waathirika. Vyama vya upinzani ninavyoviongelea hapa si zaidi ya vinne, ambavyo ni CUF, CHADEMA, TLP na NCCR-Mageuzi.
Vyama vingine vya upinzani vipo katika kundi la kwanza. Vyama hivi nilivyovitaja kwa kiasi kikubwa vimekwisha kufanikiwa kujitambulisha kama sehemu ya watu wanaoathriwa na utawala wa CCM, na hivyo vimefanikiwa kupata huruma ya wananchi walio wengi.
Hata hivyo vyama hivi havijafanikiwa kujitambulisha kama sehemu ya jawabu na fursa ya kutatua matatizo yaliyopo.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba vyama vya upinzani havijawapa wananchi mbadala wa yale yanayofanywa na CCM. Viongozi wengi wa vyama vya upinzani bado wanalalamika badala ya kutueleza wanachotaka kufanya wakiwa madarakani.
Kwa mfano, katika mgogoro wa hivi karibuni wa wanafunzi wa vyuo vikuu, walichofanya wapinzani ni kuungana na wanafunzi kulalamika na kulaani maamuzi ya serikali.
Nilitarajia kwamba vyama vya upinzani vingekwenda mbali zaidi ya kulalamika na kulaani; vingetumia fursa ya mgomo huu kuwaeleza wananchi sera mbadala ya elimu ya juu.
Ili kuweza kuishinda CCM katika chaguzi za mbeleni, vyama vya upinzani lazima vipige hatua kutoka kuonekana kuwa ni vyama athirika au vyama hurumiwa kwenda katika hatua itakayovionyesha kuwa ni vyama fursa.
Ni muhimu kwa vyama vya upinzani kutambua kuwa wapiga kura walio wengi hawapendi kupigia kura mgombea anayeonekana kuwa ni mnyonge na anayehitaji huruma.
Wapiga kura hupenda kuchagua vyama na wagombea wanaoonekana wana nguvu za kukabiliana na matatizo yanayoikabili jamii.
Kwa maana nyingine, ingekuwa ni barabara, kila mtu anajua kwamba barabara ya CCM ni mbovu, ina mashimo na ni hatari kupita. Lakini je, kuna barabara mbadala ya kupita?
Vyama vya upinzani vinawajibika kuonyesha kwamba barabara yao ni salama zaidi kuliko ile ya CCM.
Itaendelea wiki ijayo.
kitilam@yahoo.com
+44 7942 027067
Mimi naona tusiweke u-ccm au Uchadema etc, kwa sababu wote tunaishi humu humu Tz au interest yetu ni Tz, kwa ujumla wake.
ReplyDeleteLicha ya kuwepo, kwa sheria mbali mbali ili kuimarisha controls , kama kwenye kuto tender, kuratibu ubora wa kitu , kama ni ujenzi haya , kama ni bidha vipo.
The biggest problem ambayo inasikitisha na kukatisha tamaa ni pale wana siasa wanapo twa jukumu la mtaalamu na kujifanya wanajua zaidi na wanauchungu na nchi kumbe , wana uchungu wa kuiba, sasa matokeo yake ni mlolongo wa ubadhirifu, na wakumshika mtu anakuwa hayupo, maana baba au mama mwenyewe mwinzi , sasa amtaweza mfokea mtoto kwa kuleta mali ya wizi.
Ndio mana miaka nenda miaka rudi, report za mkaguzi mkuu hazi fanyiwi kazi, ukienda kwenye ujenzi wa barabara mbovu utakuta hayo hayo kaanza baba au mama kuchukua chake mapema, sasa na Afisa Utawala asie na chama, muhandisi, muhasibu, mtunza ghala nae anachukua chake, sema kinacho tofautiana ni kiwango cha pesa, mwingine ndio wanaishia ku-forge vyeti , kwa hiyo mfumo mzima unakuwa mbovu.
Mimi nimejaribu kufuatilia wakati wa Mashirika ya Umma iwe NBC au Bima au lolote walipokuwa wakijenga Nyumba za Wafanyakazi, sio kwamba walikuwa wanawapenda hao wafanyakazi bali ndio njia ya kutolea mchuzi, inaweza kuwa sio vibaya ikiwa 10% lakini ikawa ni 90% matokeo yake mradi hauishi, kila siku Project variation due to raise of cement, fuel etc etc, na Vijana kwa wazee mchuzi haukauki, na kamati ya bunge wakipita pamoja na wakaguzi nao wanapewa chao hadithi inaendelea hivyo hivyo, na hata akitoke mwenye moyo wakukemea, basi yeye ataondoka na wezi wata baki.
Sasa Solution nini hapa? ni Usimamizi mzuri toka juu kwenda chini.
Mfano mwingine kila mwaka Vyama vya Ushirika na Vilabu vyetu vya mpira angalau mara moja kwa mwaka
lakini kitu hiki hakifanyiki, na mrajisi yupo na waziri wake yupo, na waziri mkuu wakee yupo. Sasa kwanini rungu la waziri mkuu lisimuangukie waziri ambaye naye atamkumbusha mrajisi wajibu wake kama sio kumwajibisha, naye mrajisi atawalima viongozi husika, ambo nao watalimwa na wanachama wao.
Lakini kwa sababu tumezoea huyu ni mwenzetu ndio maana tunaacha kufanya yalio endelevu.
Kwa hiyo kama awe JK au Chadema etc etc hivi ndicho cha kufuatilia