Jk na mkuu wa mkoa wa Mwanza dk. james msekela wakati akivuka kwa pantoni kutoka Bunda kuelekea UK (ukerewe ya mwanza) ambapo alifanya ziara ya siku mbili kukagua miradi ya maendeleo ikiwemo kufungua shule mpya ya sekondari na mradi wa maji nansio.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 04, 2007

    Duh!! Hii pantoni ilivyochakaa..yaani sio salama kabisa kwa RAISI kupanda. Isije kuwa mambo ya MV Bukoba

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 05, 2007

    When you see a head of state wearing sunglasses you should know that you are in trouble.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 05, 2007

    Kweli siasa inaua vipaji vya wataalum. Dr. Msekela ni Mtaalamu mzuri sana wa High Voltage, kanifundisha pale UDSM Facult Of Engineering kipindi hicho. Jamaa ni kichwa sana Ila tatizo la Bongo Wataalam hawathaminiwi kama wanasiasa na ndio maana wataalamu wengi wanajikita kwenye siasa ambapo panalipa vizuri. Huyu alianzia na Ubunge wa Tabora vijijini sasa mkuu wa mkoa sijui kama anakumbuka tena mambo ya HYSTERESIS na LOOPING, zaidi ya Kidumu chama.

    Ushauri: Serikali iwape kipaumbele wataalam ili waendeleze nchi vinginevyo tutageuka taifa la siasa maana kila mtu atawaza kuwa waziri au mbunge kwa kutumia vyeti vya Taaluma ya juu ya kama sayansi na biashara wanayopata kwa gharama kubwa sana., La sivyo tuanzishe chuo kikuu cha kivukoni tutoa Masters na PhD za siasa, maana inalipa kuliko za sayanzi na biashara.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 05, 2007

    Sir Issa NAONA RAIS WETU HARD WOKING HUYU SAFI SANA...ANATESTI ZARI..SHIKILIA VIZURI JK..HALAFU USICHEZE MBALI NA BOYA...

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 05, 2007

    Nchi itabadilika pale wanasayansi watakapolipwa zaidi kuliko wanasiasa na waendesha mitambo ya uzalishaji watakapolipwa zaidi kuliko maafisa utawala,wahasibu,na wachumi.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 05, 2007

    Jk kazi hizo waachie wengine,Unamaliza pesa.Shule imjengwa kwa milioni 20,safari yako wewe na wafuasi wako milioni 5.Wastage of money.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 05, 2007

    Sasa wewe unon hapo juu ulitaka hilo pantoni apande nani?Mjinga kabisa wewe Rais ni kama binadamu wengine.Pantoni libadilishwe si kwa sababu ya Rais.

    Ujinga tu umetujaa watanzania.Huyo Jk analipanda hilo mara 1 kwa miaka 5 or 10.Je watanzania wanaolipanda hilo kila siku.

    Tuwe na akili za akili.Na si akili za kijinga.

    Na kama siasa inalipa tutajibana huko huko.Prof Sarungi yupo wapi???

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 05, 2007

    Anoni wa Saturday, May 05, 2007 2:42:00 AM sio sunglasses, miwani hii ni photocromatic, inaonekana nyeusi kukiwa na jua. Lakini hata kama angekuwa na sunglasses, si ni za jua, na kulikuwa na jua. Au huwa zimeandikwa presedent asivae? Kila president na kielelezo chake. Mkapa alivaa cheni shingoni, na Nyerere alitembea na kifimbo, Mwinyi nimesahau!

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 07, 2007

    Kama jamaa anavaa miwani au havai ukweli ni kwamba with this guy in office, we are in big trouble. Wee kaa ukichonga tu with your photocromatic.

    Mungu Ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 08, 2007

    Mtoa Saturday, May 05, 2007 7:10:00 PM. Umejuwaje kama hiyo miwani ya Mheshimiwa Rais ni photocromatic au wewe ndiye unayemfanyie shopping? Hiyo miwani inaoneka kama ile inyouzwa $12.00 pale Mall of America, Minnesota. Are you going to dispute this again?

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 11, 2007

    WEwe Anonymosu hapo juu umeona mie linikjuwa nasema hivi boti Raisi Asipande sasa soma hii habari chini:

    Diallo, Ngeze, Kundya
    wanusurika kufa maji
    * Ni baada ya boti kuzama ziwa Victoria
    NA PETER KATULANDA, MWANZA

    VIONGOZI waandamizi wa serikali na CCM, akiwemo Waziri wa Maendeleo ya Mifugo, Anthony Diallo ni miongoni mwa watu 10 walionusurika kufa maji, baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama katika ziwa Victoria, wilayani Ukerewe, mkoani Mwanza.
    Wengine walionusurika ni Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Mwangi Kundya; Mwenyekiti wa CCM wa mkoa huo, Pius Ngeze na Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Peter Toima.
    Habari zilizopatikana jijini hapa na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Zelothe Stephen na Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wa mkoa huo, Barnabas Esau, zilisema ajali hiyo ilitokea jana kati ya saa 4:00 na saa 5:00 asubuhi, katika kisiwa cha Mabibi, Ukerewe.
    Akizungumza kwa njia ya simu jana kutoka Ukerewe, Esau alisema ajali hiyo iliwapata wakati wakitoka Mwanza kwenda Ukerewe, kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo, Edward China.
    Alisema viongozi hao walikuwa wakisafiri kwa boti ya idara ya maliasili Mwanza, ambayo ilikumbwa na dhoruba iliyoizamisha.
    Kamanda Stephen aliwataja wengine waliokumbwa na ajali hiyo kuwa Katibu Mwenezi wa Chama wa Mkoa wa Mwanza, Simon Mangelepaa; Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe, Ally Mambile; Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Maria Hewa na Mkurugenzi wa Hoteli ya Monarch ya Mwanza, Osward Mwizarubi.
    Kamanda Stephen alisema majina ya watu wengine wawili hayakupatikana mara moja, na kwamba boti hiyo ina uwezo wa kubeba watu 10, ambao ndio waliokuwemo katika chombo hicho.
    “Wakiwa katika kisiwa cha Mabibi boti yao ilipigwa na dhoruba na kuzama, lakini taarifa za awali tulizopata, wote wameokolewa na kupelekwa katika hospitali ya wilaya ya Ukerewe,” alisema Kamanda Stephen.
    Taarifa za kuaminika zilizopatikana kutoka Ukerewe kwa njia ya simu jana wakati gazeti hili likienda mitamboni zilisema viongozi hao waliokolewa na wavuvi, baada ya kukaa saa nzima ziwani.
    Kwa mujibu wa habari kutoka Ukerewe, waliokolewa na wavuvi na baadhi wakitumia maboya hadi walipofikishwa eneo la Nansio.
    Taarifa hizo zilisema nahodha wa boti, Herman Lubala na msaidizi wake, Nchuma Marwa ni miongoni mwa watu hao 10.
    Habari zilizopatikana baadaye zilieleza kwamba, viongozi hao walitoka hospitali na kushiriki mazishi ya China, na baadaye kurejea Mwanza kwa ndege ndogo.
    China alifariki dunia mwanzoni mwa wiki katika Hospitali ya Rufani Bugando, alikokuwa amelazwa kwa matibabu baada ya kupata shinikizo la damu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...