
Ajali mbaya imetokea leo asubuhi katika eneo la Inyali, nje kidogo ya Jiji la Mbeya wakati basi la abiria la SABCO lililokuwa likitoka Tunduma (Mpakani mwa Tanzania na Zambia) kupitia Mbeya kwenda Dar es salaam lilipogonga roli kwa nyuma mteremkoni ambapo dereva alipotaka kulipita alikutana na pikap ikabidi arudi na kugonga roli kwa nyuma na kuua watu wawili papo hapo huku mmoja wa tatu ambaye alikuwa askari wa Usalama Barabarani akisindikiza basi hilo akifia Hospitali na kufanya jumla ya waliofariki mpaka sasa kufikia watatu.
Abiria kadhaa wamejeruhiwa, 15 wakiwa na hali mbaya sana.
Aziz.
Speed contol sheria na serikali iko wapi. yaani ajali zinaua kila siku na watu wala hawachukuliwi sheria yeyote.
ReplyDeletemaisha ya watu yanateketea tu. Wenye magari wanatakiwa wachukuliwe seheria ili wakiajiri madereva wawe wanaajiri madereva wenye usjuzi.
Mimi nilishapata ajali ya basi hapo TZ na I know how it feels na how much familia iligo through all that I don't even want to remember ...lakini kama ndio hivi ....inasikitisha sana...kila siku ni kuovertake....
Kwa mtindo huu madereva wa public vehicles mnatupeleka wapi?This is unprofessional kabisa na kutokuonyesha kujali maisha ya abiria wanaotegemewa na watu lukuki.polisi barabarani wanachangia kwenye hili pia kwani manasi yanayokwenda kasi zaidi wanayajua but wakishapewa chao basi tena haliwahusu.Nikiwa Bongo nimewahi kuwa ferried kwa basi dogo ili tuvuke mizani na baada yakuvuka tukarudi kwenye basi lililozidi uzito safari ikaendelea though niliprotest kitendo hicho sikupata support ya abiria wenzangu na askari wa barabarani wanalijua hilo.Okoeni maisha ya watu madereva na si kukimbia ovyo ili kupata sifa kwa tajiri na madereva wengine.
ReplyDelete