chaaaaaaz hilari na trupu lake wakijiandaa na safari ya kuja bongo usiku huu kuhudhuria sherehe za miaka 50 ya idhaa ya kiswahili ya bbc zitazofanyika dar. nasikia mnuso wa nguvu umeandaliwa...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 24, 2007

    BBC Swahili imeshapitwa na wakati, maendeleo ya TV yameshakua makubwa, kama wataweza kuleta BBC TV Swahili, hapo ndio watakua wamepiga hatua.

    Miaka hamsini bila ya maendeleo ya Station, ukiambatanisha TV na RAdio, Radio yao haipatikani hata kwenye TV stations kama Radio nyingine nyingi.

    Nini maendeleo ya BBC swahili mpaka hivi sasa ?

    Huku BONGO, wengi hatusikilizi radio, maneno, news, football yote kwenye teli na mtandao.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 24, 2007

    I TOTAL AGREE with 9:49 Anonymous. OUTDATED type of station.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 24, 2007

    Wewe Limbukeni hapo juu acha ushamba na utindiga, nani kasema BBC imepitwa na wakati? kama wewe hausikilizi BBC ni juu yako sio uanze ku generalize etI huku bongo wengi hatusikilizi BBC.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 24, 2007

    Acha kudanganya watu wewe usiye na jina hapo juu. Bongo wangapi wanaoingia kwenye mtandao eti kusikiliza Radio. Nadhani hata elfu moja hawafiki. Wabongo wengi tuishio bongo hata hizo email address hatuna, na wengi waliokuwa nazo hivi sasa zime expire sembuse wawe na muda wa kutafuta radio through internet!!!. Usichekeshe watu hapa. Kwa taarifa yako kwa upande wa news hakuna Radio inayosikilizwa na watu wegi Africa mashariki kama idhaa ya kiswahili ya BBC kwani ndiyo Radio pekee inayosikika kwenye nchi nyingi.Hivi bongo tuna radio ngapi zilizizo kwenye mtandao zaidi ya hao hao BBC?.Zote za hapa zilizojaribu michosho mitupu kwa kuwa offline kila wakati. ACHA HIZO. BRAVO BBC,BRAVO TIDO kwa kazi nzuri. Fanya kweli TVT pia. Bravo Charles Hilary, Tido atakapo retire itakuwa zam yako na wewe TVT

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 24, 2007

    tunahitajia Teli BBC.. naunga mkono kwa asilimia 100...

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 24, 2007

    Radio inapitwa na wakati, nyau wewe.. wewe pekee mshamba umeng'ang'ania radio..

    Wewe unafikiri ushabiki wa timu za mpira za Bongo umekwisha siyo kama miaka ya 80s na 90s kwa sababu gani?

    Waingereza/WAitali wameleta mpira wao kwenye TEli, CNN news, na TV nyingine nyingi, tu bongo.. unakua na muda wa kusikililiza Radio.. kwa news hizo hizo..

    Ulimbukeni wako ndio umebakia na Radio yako mbovu.. hiyo..

    Lazima ibadilike na wakati, radio yenyewe kwenye internet tu kwa sisi wa mbali....lakini mijitu mengine haielewi..

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 24, 2007

    Nakumbuka vita ya Gulf war..., tulikuwa hatuondoki kwenye Radio kule kwetu Mwanza...., mtu kibao lakini hivi sasa vita hii hakuna mtu anayesikiliza nyuzi kwa radio, kwa kiwango cha wasikilizaji kama zamani..

    Radio isiondoke..., lakini lazima ipatikane na TEli yake.. Acheni kurudishana nyuma ...lazima twende na wakati......

    BBC yenyewe huku Uingereza na ulimwenguni siyo kama zamani....mambo yanabadilika kila siku wanawafukuza kazi wakurugenzi wao kwa vipindi vyao ovyo.....havina sura....

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 25, 2007

    Ni lazima ifahamike kwamba wengi wa wasikilizaji nchini Afrika, hususan wa nchi za Afrika Mashariki na Kati, ambayo idadi yake hadi hivi sasa inafikia mamilioni kadhaa.

    Hii pekee ni radio ambayo, hakuna hata radio moja katika sehemu hizo yenye kufikisha ujumbe na habari kwa sehemu kubwa kabisa ya nchi hizo ukilinganisha na BBC.

    Juu ya maendeleo yao, ina watu wakuripoti habari katika nchi mbali mbali, nchini Africa on the ground, ambapo pekee wanaripoti kwa ajili ya Radio BBC Swahili, pamoja na waandishi wa habari wa BBC kwa lugha nyingine. Ni mahisio yangu ushirikiano mkubwa upo baina ya hawa waandishi wa habari na maripota wa BBC.

    Kwa hiyo basi, Radio BBC swahili inahitajika sana kuwepo.

    Hata hivyo, ni muhimu ifahamike kwamba maendeleo haya makubwa yaliyoifikia hadi kufikia miaka hii hamsini, ni muhimu kama uwezekano upo BBC Swahili TV, itakuwepo kushirikiana na BBC Radio kutuletea habari muhimu, ikiwa kwa wasikilizaji wengi ikiwa ndani ya miji na vijiji.

    Tunafahamu, kwamba kuna influx ya matumizi ya tv, ndani ya majumba ya watu wengi huko Africa Mashariki na kati, ukilinganisha na miaka ya 80 na hata 90. Hii nasemea hasa katika miji na baadhi ya sehemu za vijiji ambazo zina access ya umeme.

    Ni matarajio yetu, kama maendeleo yaliyoifikia hapa UK, BBC TV na bbc Radio 5 na nyinginezo, tunataka na hayo yafanyike kwa Radio BBC swahili na BBC swahili TV. Tunafahamu fika hili ni shirika la Uingereza likidhaminiwa na watu wenye kulipa kodi na leseni za TV, lakini hata hivyo haya ni maendeleo ambayo wanaweza kuyaleta. Siwezi kutoa maoni juu ya hili zaidi sababu sina ujuzi huo lakini ni mahisio ya wengi, lazima pawepo na ushirikiano na hawa waandishi wa habari wa RAdio. Ni furaha iliyejo kumsikia Charles Hilary akitangaza Mechi ya mpira wa miguu nchini Uingereza kwa mfano FA CUP finali Arsenal na ManU, kwa lugha ya kiswahili badala ya kusikiliza kwa lugha ya kiingereza kupitia BBC 1, halafu Arsenal wakashinda..JOKI TU HII.

    Vile vile tunafahamu BBC inadhamini idhaa za Radio kwa lugha nyingine zisizopungua 30, lakini ukitizama katika hizo lugha ni lugha zisizopungua tano mpaka kumi, ambazo zinatumika zaidi ya nchi moja, kwa hiyo basi kwa kujipendelea sisi waafrika, lugha ya kiswahili ni lugha pekee ambayo inatumika kwa nchi nyingi na yenye kujitosheleza ukilinganisha na lugha nyingine Afrika. Kwa hiyo umuhimu upo wa kuwa na BBC Swahili TV.

    Munakumbuka Aljazeera TV channel uarabuni, imekuja baada ya BBC kusitisha huduma zao huko uarabuni, hatima yake Aljazeera walichukua nafasi hiyo iliyoachwa na BBC.

    By Mchangiaji

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 25, 2007

    let's talk facts here.in my view, radio is still the most used form of medium in Africa.it's the cheapest, it's the most mobile [ubiqutous] and above all it just works perfectly.

    bbc idhaa ya kiswahili inasikilizwa na watu milioni 20!inashangaza kuona wachache wanasema radio imepitwa na wakati.msisahau kwamba tanzania kuna tatizo la umeme, interenet connection ziko slow na expensive.

    na kwa mnaosifia tv, naomba mnitajie tv stations ngapi zinatoa vipindi vya kiswahili katika news and current affairs kwa quality inayokubalika.

    wengi wanaonyesha kwa kiingereza, tuna wazungumzaji wangapi wa kiingereza?mbali na hayo input ya watanzania katika cnn et al ni kiasi gani.

    of course radio inabadilika, kutoka shortwave to digital radio.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 25, 2007

    Nyie mnaosema hamna watu wengi wanaoingia kwenye mtandao, Mbona mnaanzisha jumuiya ya wanablog Tanzania? Sasa hao viongozi watakua viongozi wa nani kama hamna wanachama? Watu wanaingia kwenye net hata bongo sasa kama wewe huingii kila mara hiyo ni juu yako.

    Well, radio inaweza kusikilizwa na watu 20 million lakini ni Africa nzima au ni ulimwengu mzima wa nchi zinazosikiliza kiswahili. Na hao watu 20,000,000 hawajawaambia wanaisikiliza kwa kupitia njia gani....wengi wao ni hupitia kwenye mtandao na mfahamu wengi wako nje ya bongo au nje ya africa.

    Just be honest ni wangapi bongo wanasikiliza BBC london na ile sijui ya Ujerumani kila siku? Kwanza ni ya masafa marefu, Halafu ni swwaaaaaaa swaaaa mjeuze radio kila kona ndio muipate, pili ilikua ni saa kumi na mbili na mzee ndio alikua anafungua kusikiliza. Usiposikiliza at that time sijui saa moja au saa tano usiku tofauti na kwenye mtandao habari zinakuwa saved wew unasikiliza kwa muda wako.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 26, 2007

    Kitumbo hicho Mzee wa Macharanga fanya zoezi kinakutia uzee na taabu kufunga kamba za viatu angalia ulivyo poozi ile kikupe nafasi ya kupumua... (aDk)

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 01, 2007

    Saidi Yakubu nyie kuwa bongo ina maana hutuwezi kusikiliza redio tena?Jamani mbona ni mambo ya kihuni.Dira ya dunia naimiss

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...