Home
Unlabelled
chaaaz
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
BBC Swahili imeshapitwa na wakati, maendeleo ya TV yameshakua makubwa, kama wataweza kuleta BBC TV Swahili, hapo ndio watakua wamepiga hatua.
ReplyDeleteMiaka hamsini bila ya maendeleo ya Station, ukiambatanisha TV na RAdio, Radio yao haipatikani hata kwenye TV stations kama Radio nyingine nyingi.
Nini maendeleo ya BBC swahili mpaka hivi sasa ?
Huku BONGO, wengi hatusikilizi radio, maneno, news, football yote kwenye teli na mtandao.
I TOTAL AGREE with 9:49 Anonymous. OUTDATED type of station.
ReplyDeleteWewe Limbukeni hapo juu acha ushamba na utindiga, nani kasema BBC imepitwa na wakati? kama wewe hausikilizi BBC ni juu yako sio uanze ku generalize etI huku bongo wengi hatusikilizi BBC.
ReplyDeleteAcha kudanganya watu wewe usiye na jina hapo juu. Bongo wangapi wanaoingia kwenye mtandao eti kusikiliza Radio. Nadhani hata elfu moja hawafiki. Wabongo wengi tuishio bongo hata hizo email address hatuna, na wengi waliokuwa nazo hivi sasa zime expire sembuse wawe na muda wa kutafuta radio through internet!!!. Usichekeshe watu hapa. Kwa taarifa yako kwa upande wa news hakuna Radio inayosikilizwa na watu wegi Africa mashariki kama idhaa ya kiswahili ya BBC kwani ndiyo Radio pekee inayosikika kwenye nchi nyingi.Hivi bongo tuna radio ngapi zilizizo kwenye mtandao zaidi ya hao hao BBC?.Zote za hapa zilizojaribu michosho mitupu kwa kuwa offline kila wakati. ACHA HIZO. BRAVO BBC,BRAVO TIDO kwa kazi nzuri. Fanya kweli TVT pia. Bravo Charles Hilary, Tido atakapo retire itakuwa zam yako na wewe TVT
ReplyDeletetunahitajia Teli BBC.. naunga mkono kwa asilimia 100...
ReplyDeleteRadio inapitwa na wakati, nyau wewe.. wewe pekee mshamba umeng'ang'ania radio..
ReplyDeleteWewe unafikiri ushabiki wa timu za mpira za Bongo umekwisha siyo kama miaka ya 80s na 90s kwa sababu gani?
Waingereza/WAitali wameleta mpira wao kwenye TEli, CNN news, na TV nyingine nyingi, tu bongo.. unakua na muda wa kusikililiza Radio.. kwa news hizo hizo..
Ulimbukeni wako ndio umebakia na Radio yako mbovu.. hiyo..
Lazima ibadilike na wakati, radio yenyewe kwenye internet tu kwa sisi wa mbali....lakini mijitu mengine haielewi..
Nakumbuka vita ya Gulf war..., tulikuwa hatuondoki kwenye Radio kule kwetu Mwanza...., mtu kibao lakini hivi sasa vita hii hakuna mtu anayesikiliza nyuzi kwa radio, kwa kiwango cha wasikilizaji kama zamani..
ReplyDeleteRadio isiondoke..., lakini lazima ipatikane na TEli yake.. Acheni kurudishana nyuma ...lazima twende na wakati......
BBC yenyewe huku Uingereza na ulimwenguni siyo kama zamani....mambo yanabadilika kila siku wanawafukuza kazi wakurugenzi wao kwa vipindi vyao ovyo.....havina sura....
Ni lazima ifahamike kwamba wengi wa wasikilizaji nchini Afrika, hususan wa nchi za Afrika Mashariki na Kati, ambayo idadi yake hadi hivi sasa inafikia mamilioni kadhaa.
ReplyDeleteHii pekee ni radio ambayo, hakuna hata radio moja katika sehemu hizo yenye kufikisha ujumbe na habari kwa sehemu kubwa kabisa ya nchi hizo ukilinganisha na BBC.
Juu ya maendeleo yao, ina watu wakuripoti habari katika nchi mbali mbali, nchini Africa on the ground, ambapo pekee wanaripoti kwa ajili ya Radio BBC Swahili, pamoja na waandishi wa habari wa BBC kwa lugha nyingine. Ni mahisio yangu ushirikiano mkubwa upo baina ya hawa waandishi wa habari na maripota wa BBC.
Kwa hiyo basi, Radio BBC swahili inahitajika sana kuwepo.
Hata hivyo, ni muhimu ifahamike kwamba maendeleo haya makubwa yaliyoifikia hadi kufikia miaka hii hamsini, ni muhimu kama uwezekano upo BBC Swahili TV, itakuwepo kushirikiana na BBC Radio kutuletea habari muhimu, ikiwa kwa wasikilizaji wengi ikiwa ndani ya miji na vijiji.
Tunafahamu, kwamba kuna influx ya matumizi ya tv, ndani ya majumba ya watu wengi huko Africa Mashariki na kati, ukilinganisha na miaka ya 80 na hata 90. Hii nasemea hasa katika miji na baadhi ya sehemu za vijiji ambazo zina access ya umeme.
Ni matarajio yetu, kama maendeleo yaliyoifikia hapa UK, BBC TV na bbc Radio 5 na nyinginezo, tunataka na hayo yafanyike kwa Radio BBC swahili na BBC swahili TV. Tunafahamu fika hili ni shirika la Uingereza likidhaminiwa na watu wenye kulipa kodi na leseni za TV, lakini hata hivyo haya ni maendeleo ambayo wanaweza kuyaleta. Siwezi kutoa maoni juu ya hili zaidi sababu sina ujuzi huo lakini ni mahisio ya wengi, lazima pawepo na ushirikiano na hawa waandishi wa habari wa RAdio. Ni furaha iliyejo kumsikia Charles Hilary akitangaza Mechi ya mpira wa miguu nchini Uingereza kwa mfano FA CUP finali Arsenal na ManU, kwa lugha ya kiswahili badala ya kusikiliza kwa lugha ya kiingereza kupitia BBC 1, halafu Arsenal wakashinda..JOKI TU HII.
Vile vile tunafahamu BBC inadhamini idhaa za Radio kwa lugha nyingine zisizopungua 30, lakini ukitizama katika hizo lugha ni lugha zisizopungua tano mpaka kumi, ambazo zinatumika zaidi ya nchi moja, kwa hiyo basi kwa kujipendelea sisi waafrika, lugha ya kiswahili ni lugha pekee ambayo inatumika kwa nchi nyingi na yenye kujitosheleza ukilinganisha na lugha nyingine Afrika. Kwa hiyo umuhimu upo wa kuwa na BBC Swahili TV.
Munakumbuka Aljazeera TV channel uarabuni, imekuja baada ya BBC kusitisha huduma zao huko uarabuni, hatima yake Aljazeera walichukua nafasi hiyo iliyoachwa na BBC.
By Mchangiaji
let's talk facts here.in my view, radio is still the most used form of medium in Africa.it's the cheapest, it's the most mobile [ubiqutous] and above all it just works perfectly.
ReplyDeletebbc idhaa ya kiswahili inasikilizwa na watu milioni 20!inashangaza kuona wachache wanasema radio imepitwa na wakati.msisahau kwamba tanzania kuna tatizo la umeme, interenet connection ziko slow na expensive.
na kwa mnaosifia tv, naomba mnitajie tv stations ngapi zinatoa vipindi vya kiswahili katika news and current affairs kwa quality inayokubalika.
wengi wanaonyesha kwa kiingereza, tuna wazungumzaji wangapi wa kiingereza?mbali na hayo input ya watanzania katika cnn et al ni kiasi gani.
of course radio inabadilika, kutoka shortwave to digital radio.
Nyie mnaosema hamna watu wengi wanaoingia kwenye mtandao, Mbona mnaanzisha jumuiya ya wanablog Tanzania? Sasa hao viongozi watakua viongozi wa nani kama hamna wanachama? Watu wanaingia kwenye net hata bongo sasa kama wewe huingii kila mara hiyo ni juu yako.
ReplyDeleteWell, radio inaweza kusikilizwa na watu 20 million lakini ni Africa nzima au ni ulimwengu mzima wa nchi zinazosikiliza kiswahili. Na hao watu 20,000,000 hawajawaambia wanaisikiliza kwa kupitia njia gani....wengi wao ni hupitia kwenye mtandao na mfahamu wengi wako nje ya bongo au nje ya africa.
Just be honest ni wangapi bongo wanasikiliza BBC london na ile sijui ya Ujerumani kila siku? Kwanza ni ya masafa marefu, Halafu ni swwaaaaaaa swaaaa mjeuze radio kila kona ndio muipate, pili ilikua ni saa kumi na mbili na mzee ndio alikua anafungua kusikiliza. Usiposikiliza at that time sijui saa moja au saa tano usiku tofauti na kwenye mtandao habari zinakuwa saved wew unasikiliza kwa muda wako.
Kitumbo hicho Mzee wa Macharanga fanya zoezi kinakutia uzee na taabu kufunga kamba za viatu angalia ulivyo poozi ile kikupe nafasi ya kupumua... (aDk)
ReplyDeleteSaidi Yakubu nyie kuwa bongo ina maana hutuwezi kusikiliza redio tena?Jamani mbona ni mambo ya kihuni.Dira ya dunia naimiss
ReplyDelete