wiki ya utumishi wa umma inaendelea kwa maonesho mbalimbali ya taasisi na idara za serikali kama hii ya banda la mkemia mkuu ambapo mtaalamu wa dna anaelezea muundo wa teknolojia hiyo na namna ambavyo kitaalamu mtu unaweza kubainisha hata mambo ya uzazi ambapo mtu utapata uhakika kama mwana ni wako/si wako. wadau mnasemaje?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 19, 2007

    Kweli ni kiboko

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 19, 2007

    Kaunda hakutegemewa kuondoka madarakani, kwa hiyo alidhani anaimiliki Zambia na timu yao ya taifa. Kikwete atakaa madarakani miaka 10 tu, je akitoika tubadilishe tena jina la timu pia? Nadhani tulishaachana na kutukuza viongozi kiasi hicho hata kwenye pesa zetu hatuwaweki tena.

    Mimi nimeijua kama ni Taifa Stars tangu nadhani mwaka 1971 hivi. Mwaka 1980 ilifanya vizuri sana mpaka Dillunga na Sunday Manara wakachaguiliwa kuchezea timu ya Afrika.

    ReplyDelete
  3. Huu mjadala upo kule kwa Chemi Che-Mponda

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 19, 2007

    Hellow Mr michuzi nimeona habari za DNA hapo bongo kwa kweli nimefurahi sana.Sasa Mr Michuzi nakuomba sana unitafutie PRICE ya kupima DNA,yaani kucheck kama mwana ni wako au siyo wako kwani kama bongo ni cheap bora wazee tuje kupima HOME.Take care maan.

    ReplyDelete
  5. LOL! (Laughing Out Loud)

    Michuzi,

    Asante sana tena sana kwa andika kuhusu DNA. Maana wiki iliyopita niliblogu kuhusu hiyo hiyo DNA na jinsi wanaume washenzi wanavyokataa watoto wao. Wanaume DNA itawakomesha. Halahala mnapachika wapi! Raha ya sekunde... malezi ya miaka 18!

    http://swahilitime.blogspot.com/2007/06/halahala-mnaosema-mtoto-si-wako.html

    ReplyDelete
  6. Chemi,

    Wewe sasa MTU MZIMA sana,punguza matusi.Umetukana kule "kwako" umeona haitoshi hadi unayaleta kwa Michuzi.

    Kama wanaume "washenzi" watakomeshwa basi na wanawake "washenzi" wanaobambikia wanaaume watoto (hasa ktk ndoa au kisa mwanaume "anazo") nao pia watakoma.

    DNA Testing ni msumeno,unakata huku na huko.Angalau sasa watu watapata bahati ya kuwajua baba zao halisi.

    Je, kila mtu ana hakika baba yake ni baba yake "halisi"?

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 19, 2007

    Wewe dada uliebandika hii kitu ya DNA, it goes both ways--nasie wanaume hatuta lea tena vilivyo sio vyetu--did you ever think of that

    ReplyDelete
  8. DaChemi unajua huo ufeminist wako utakufikiosha pabaya kama bado haujakufikisha bado, manake wewe atiko zako nyingi nzuri lakini zinakosa objectivity na pia zinakuwa bayacidi.

    Sasa kuhusu DNA na wanaume kukataaa watoto unasema wanaume washenzi bila kusenma wanawake pia ni washenzi maana wap pia husingizia wanaume wamewatia mimba au hata kuwabaki wakati si kweli. utakuta mwanamke katembea na wanaume kibao kisha namchagua mmoja tu kuw andio Bamtoto wapi na wapi? Ndio mana wanaume wangine hukataa kwa sabu wanajua wataandamwa na chadi spoort kwa miaka 18 na watoto si wao!

    Hebu jirekebishe DaChemi, tumia utaaaluma wako wa uandishi wa habari kutuchambulia inshu nje ndani kisha sie washabiki wako tuinyambue tunavyotaka.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 19, 2007

    DNA ya mother nature kali kweli. Mtoto anafanana kama baba yake hata hubishi ukiambiwa huyu mtoto wako. Na nilivyokua mdogo nilikua nasikia kuwa ukikataa mtoto wako basi vitu vitakua havifanyi kazi tena.

    Hii scientific DNA hata haitakua na maana yeyote kwa vile jadi yetu hata kama baba anajulikana lakini wanawatelekeza watoto wao kila siku. Watoto mpaka wanakua wakubwa ndio wanaenda nda kutafuta baba zao. na mibaba mingine inasema atanitafuta akiwa mkubwa. Inatakiwa iwe crime na kwa vile hiyo ipo sasa hamna cha kukataa.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 19, 2007

    WHO IS YOUR DADDY...EHEEEEE

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 19, 2007

    Ni shilingi ngapi kupima? Michuzi mwaga basi vyote. Please...nataka kaka yangu apime yule wifi najua kamuingiza mjini kaka yangu. I doubt wale watoto ni wake. I need the proof kaka yangu kama kipofu vile.

    Kuna sheria yeyote kuwa lazima mume na mke wakubali kupima huyo mtoto? najua kaka yangu hatakubali kuwapima wale watoto.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 19, 2007

    ooh, hii DNA ni nzuri mizozo itakwisha sasa kama yule dada sijui jina nimelisahau anaedai kazaa na former IG* si sasa waende huko kama uongo au ukweli itajulikana. maana wazee wengi wanapenda kula ma-HG bila kujua matokeo, yeye akirudi tu home mama hayupo basi anataka kuchapa cha haraka maskini ma-HG wasivyonaelimu ya binadamu wanakubali bila kutumia zana wakijua bosi hawezi kuleta madhara ya maradhi au mimba.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 20, 2007

    JAMANI...JAMANI...JAMANI....MSISAHAU BONGO KUNA USANII, WATU MPAKA KESHO WAKIENDA KUOA AU KUOANA WANAPELEKA VYETI KWA MA-PADRI VYA UONGO KUWA HAWANA NGOMA, WATU WANALIPA PESA KUPEWA MAJIBU KUWA SI WAGONJWA, I DOUBT KAMA HAO MAZEE HAWATATOA FEDHA, TENA WAKINA DADA WATALIZWA....MUNGU IBARIKI TANZANIA!!!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 20, 2007

    KUPIMA DNA BONGO NI AROUND TZS 120,000/= AMBOYO NI KAMA USD 100 HIVI.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 20, 2007

    HILI JIPYA KWANI UKIWA NA NGOMA HUOI AU KUOLEWA TANZANIA?

    mimi sioni sababu hata ya hao ma padri kujua kuwa mimi nina ngoma au sina. anayetakiwa kujua ni yule unayemuoa tu. kama wote manao sawa ..kama mmoja hana basi ndio hapo mwenye kutaka kwenda kuvua samaki wakati hajui kuogelea ni juu yake. ufaidi samaki huku unakufa ukijiona au ule ugali na harufu ya samaki wa jirani.

    bongo eaasy money itatumaliza watu wanapenda short cut sana tu.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 21, 2007

    CHEMI CHE MPONDA....HAHAHAAAAA. YAANI WEWE UNADAI WANAUME NDO WANAOKATAA WATOTO TENA UNAWAITA "WASHENZI!"
    HIVI UNA MTOTO WEWE. UNAJUA MACHUNGU YA KUSINGIZIWA MTOTO NA MWANAMKE ANAYEKIUKA NDOA NA KWENDA KULALA NJE?
    KAMA ALIVYOSEMA MDAU HAPO JUU KWAMBA WEWE UANDISHI WAKO UNA KASORO KUBWA. MWANDISHI HUSHUTUMU MTU UKIWA NA USHAHIDI AU VIELELEZO KAMILI.
    KWA JINSI ULIVYODAKIA HII ISSUE YA DNA, NADHANI UNATAFUTA UMAARUFU WA NGUVU. KUMBUKA TUMESHAKUSAHAU KIPINDI KIREFUUUU..TENA SANAAA.
    YAANI KWA SASA HUNA LAKO NA WALA HAKUNA MTU ATAKAYEKUPAPATIKIA ETI ULIKUWA MWANDISHI WA MAKALA KATIKA GAZETI LA SERIKALI. Just Sit Down And Shut It. You Are SHABBY LADY.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 21, 2007

    KUHUSU CHEMI:

    1.Huyu dada ana umri gani?
    2.Kaolewa au hajaolewa?
    3.Kuandika matusi, kwake ni sifa? tamaduni yake? au utovu wa kujiheshimu?
    4.Ana kaka au dada ambaye, kazaliswa na kukataliwa au kusingiziwa mtoto ni wake wakati mwanamke ni muongo?

    Naomba watu wajue kuwa kunawanawake wanaopenda kujishebedua na kuzaa hata na wanaume wa watu. utasika "baba yake waziri" so what?? wewe kama umeshajua mtu yupo kwenye ndoa unazaa nae ili?? wasichana tufikiri mara mbili, mtu kuw awaziri au na wadhifa ndio kitu gani?

    Afadhali hiyo DNA imekuja ingawa najua kuna machizi watahonga, lakini kama hao wapimaji watakuwa na msimamo kuna watu wengi tu wamesingiziwa, eti, "umefanana vidole, sijui pua"...pumba tupu wazee kapimeni watoto hao, mbakishe urithi wa mali kwa watoto husika.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 22, 2007

    Nakubaliana na Da Chemi maana kuna wanaume washenzi sana ambao wanadiriki kukataa wanao. Hawana adabu na ni wapumbavu wa mwisho dunia. Chemi kasema kweli kabisa. Semeni tu UKWELI UNAUMA. Kama hamtaki watoto wa nje acheni kusexi basi.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 22, 2007

    Anon wa 12:36PM, huyo Chemi kakukosea nini? Alikuchukulia bwana nini? Mbona unakuwa mkali sana kwake? Wewe ndo umetukana. Kama una shida na mwanaume wako wengi usiwe na wasiwasi ila usimsingizie kuwa kakupa mimba. Kama mungu amekuandikia utampata bwana. Hata hivyo old maids wako wengi dunia hii hutakuwa peke yako ukimkosa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...