hawa ndo jk boyz waliowaliza bukina faso walipokuja kwetu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 37 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 17, 2007

    kaka michuzi
    jana umefanya kazi nzuri sana sana hongera,maana mimi ilibidi niacha kuangalia kwenye bbc nije kwenye blog yetu kumbe na sisi tunaweza kabisa kushindana na vyombo vya habari vya ulaya, jana wadau wote tumefurahi kwa kutupa ile mechi live endeleza libeneke mwanangu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 17, 2007

    Yaani mimi skuwahi mpenzi wa mprira lakini hii nimefurahi sana na support vijana wanyumbani jana watu tulikuwa tunapata txt msg kutoka kila pande ya dunia kuhusu ushindi huu hongereni sana sasa ndio kukaza mwendo zaidi

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 17, 2007

    JAMANI KAMA KUNA MTU AMEREKODI ILE MECHI YA JANA NA ILE YA MWANZA KATIKA FORMAT YA DVD AU VCD NAOMBA ANITUMIE HUKU UGHAIBUNI KUPITIA KWA MICHUZI NTAILIPIA GHARAMA ZOTE HUSIKA. MUHIMU: QUALITY YA KANDA LAZIMA IWE NZURI.

    ReplyDelete
  4. Hongereni Taifa Stars, kwa taarifa zilizopo hatujawahi kukwalifai toka miaka 80, toka katika mbio, Mungu akijaali tutafika.

    KWa wale watakao pendelea kuiona mechi ya Msumbiji na Senegali, kuna uwezekano mkubwa hii TV channel ya Senegal wanaweza kuenyesha live, lakini lugha ni kifaransa,


    http://sunuker.com/index.php?option=com_content&task=view&id=54&Itemid=1

    ReplyDelete
  5. ILANI..

    Hii ni qualification tu, bado mpira ni fainali huko GHANA.. na hiyo pekee ndio itaonyesha DIRA kwa dunia nzima, kwamba Tanzania iko kwenye GWARIDE la kuelekea Kombe la DUNIA...

    SIKU HIYO LAZIMA TULE NDAFU, MUNGU AKIJAALIA..

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 17, 2007

    KWAKO BWANA LEODGAR CHILLA TENGA,PRESIDENT,TANZANIA FOOTBALL FEDERATION:
    tupo katikati ya vita kali ya kutafuta nafasi ya kwenda Ghana,you are our Field Marshal,wewe ndo kamanda mkuu.please lead from the front.hebu ueleze umma wa watanzania crucial game kama la jana kwa nini hukusafiri na timu burkina faso?game la senegal dar ukaone bora ukale kuku Geneva kuliko kukaa mwanza utengeneze mikakati ya ushindi,matokeo?sare ya kijinga tu na senegal.sasa sikiliza beki hatuna costa hoi,nsajigwa red card,una mpango gani? wambie watu wako hapo ti ef ef waache upuuzi wamwite Pawasa haraka sana ili kocha apate nafasi ya kumuangalia,vinginevyo tukifungwa na msumbiji utatueleza!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 17, 2007

    chuki binafsi hazifai,TFF kwanini mnambania Boniface Pawasa?acheni hizo mwiteni azibe nafasi ya Nyumba na Fusso mwenye red card!!!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 17, 2007

    ktk kundi letu ni sisi tu ndo tulioshinda game ugenini!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 17, 2007

    SENEGAL vs MSUMBIJI

    http://www.rewmi.com/Live-Mozambique-Senegal-0-a-0-VIDEO-_a2033.html?PHPSESSID=d54c5cd5c1e2cba0934159a71836ed8d

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 17, 2007

    Michuzi bado una hangover... mbona hakuna picha mpya.. Nadhani jana umekunywa bure sanaaaaaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 17, 2007

    Michuzi leo uko wapi..Fungulia mbwa leo umefunga???

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 17, 2007

    Jamani kwani ninani aliyeibatiza timu yetu jina la JK? mbona hii ni timu ya watanzania wote na siyo timu ya JK?

    ni makosa kuiita timu ya taifa kwa jina la raisi katika kpindi hiki cha demokrasia ya vyama vingi. Na ijulikane pia kuwa, raisi wa nchi anaweza kufanya makosa makubwa sana na kuiabisha nchi, je hali hiyo ikitokea timu itabadili jina?

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 17, 2007

    SENEGAL 0 MOZAMBIQUE 0 : Kocha wa MOZAMBIQUE Ameahidi kuipiga bao Tanzania, Leo Rais wao na Rais Mstahafu ---Kipenzi cha TZ Chissano alikuwa uwanjani

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 17, 2007

    RESULT: Mozambique 0-0 Senegal,
    Matokea haya yanafaida kwetu? au maumivu?

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 17, 2007

    Haya mambo hayo hapa mpira umeisha Msumbiji 0 and Senegal 0, kazi kwetu, Senegal anayo advantage ya magoli......

    ReplyDelete
  16. Bado Ngoma Ngumu SANA..lakini mategemeo yapo makubwa tu..
    Washindi wa Group ndio watakwalifai, ama ?

    P W P
    Senegal 5 2 8
    Tanzania 5 2 8
    Mozambique 5 1 6
    Burkina Faso 5 1 4


    Mechi Zilizobakia..
    07-09/09/07:
    Senegal v Burkina Faso, Tanzania v Mozambique

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 17, 2007

    kaka michu..
    nahis senegal wametoa droo na mozambique.. nafasi bado ipo maana bbc wanaonyesha ya kuwa senegal wana point 8 sawa nasi plz weka hii front page wadau waione

    2008 Nations Cup Group 7
    P W D L GF GA Pts
    Senegal 5 2 2 1 6 2 8
    Tanzania 5 2 2 1 4 6 8
    Mozambique 5 1 3 1 4 4 6
    Burkina Fas 5 1 1 3 4 7 4

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 17, 2007

    kama nilivyokutumia senegal na mozambique wametoka bilabila kaka cheki hapa kwa uhakikahttp://news.bbc.co.uk/sport2/hi/football/africa/6761279.stm wawekee wadau mkuu

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 17, 2007

    michu mbona huweki hii?

    Senegal struggle in Group Seven

    Tanzania coach Marcio Maximo was sent off during Saturday's game
    Senegal failed to go clear at the top of Group Seven when they were held 0-0 in Mozambique on Sunday in the 2008 African Cup of Nations qualifiers.

    The Teranga Lions are now only ahead of Tanzania at the top of the group thanks to their better head-to-head record between the two sides.

    Tanzania moved onto eight points on Saturday thanks to their 1-0 win in Burkina Faso.

    The encounter in Ouagadougou on Saturday saw the hosts comfortably in charge but failing to capitalise on their opportunities.

    Burkinabe frustration boiled over in the second half when defender Moussa Ouatara was sent off after head butting Amir Maftah.

    The visitors also had their fair share of trouble as Shadrack Nsajigwa and coach Marcio Maximo were also dismissed as tempers flared.

    The Taifa Stars punished the home side for being profligate midway through the second half.

    Henry Joseph beat the offside trap and chipped the ball over the keeper to give Tanzania a crucial win that sees their hopes of qualification given a major boost.

    Burkina Faso remain bottom of the table on four points while Mozambique are just two points ahead of them.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 17, 2007

    RESULT: Mozambique 0-0 Senegal,Group Seven

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 17, 2007

    RESULT: Mozambique 0-0 Senegal,Group Seven

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 17, 2007

    Senegal na Msumbiji ni 0-0. Msimamo wa kundi la saba sasa angalia jedwali hapa chini:

    2008 Nations Cup Group 7
    P W D L GF GA Pts
    Senegal 5 2 2 1 6 2 8
    Tanzania 5 2 2 1 4 6 8
    Mozambique 5 1 3 1 4 4 6
    Burkina Faso 5 1 1 3 4 7 4

    Tuombe mchezo ujao Stars waifunge Msumbiji na Bunina Faso waishinde Senegal.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 17, 2007

    Kaka Michuzi

    Naona kazi bado tunayo, maana Senegal na Msumbiji wametoa draw, kwa sasa Senegal anaongoza kwa kuwa na uwingi wa magoli ya kufunga akiwa na point 8 kama sisi. Hii inamaanisha nini kwetu. Tunaombea yafuatayo yatokee mwezi september. Senegal atoe draw na Burkinabe na sisi Tushide dhidi ya Mozambique. Ni gumu lakini ndo lililobaki. Maana Senegal atacheza kufa na kupona ukizingatia kuwa watakuwa nyumbani. Na pili watakuwa na hasira kwa vile Burkinabe waliwafunga kwao, kwa hiyo watataka kulipa kisasi. Kwa upande mwingine ni kuwa Burkinabe nao watataka kuwatoa kimaso maso mashabiki wao baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo. Kaaazi kweli kweli.

    Sele

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 17, 2007

    Mpira umeisha! Senegal na Wamakonde(Msumbiji) wametoka 0-0, so sasa tupo nafasi ya pili kwasababu ya magoli ya kufungwa (6) na machache ya kufunga (4). Iwapo Senegal watafungwa, ama kutoka sare ya aina yeyote na Wa-Burkinabi, na sisi tukamtungua Mmakonde (Msumbiji) ndani ya Bongo, then moja kwa moja tunaingia Ghana. Mungu Ibariki Tanzania.
    Msimamo wa kundi kwa sasa ni huu ufuatao:

    2008 Nations Cup Group 7
    P W D L GF GA Pts
    Senegal 5 2 2 1 6 2 8
    Tanzania 5 2 2 1 4 6 8
    Mozambique 5 1 3 1 4 4 6
    B. Faso 5 1 1 3 4 7 4

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 17, 2007

    ndugu zangu eh mambo yameharibika big time.wasenegali wametoa draw ya 0:0 sasa hivi na msumbiji,hivyo pamoja na kwamba wote tuko point 8 lakini wao senegal wana better goal difference.tarehe 8/sept sisi tunacheza na msumbiji dar na wao wanacheza na burkina senegal. wakishinda wamekwenda ghana na sisi tukishinda tuotee nafasi ya upendeleo ya best three losers ambayo ni ngumu kwani nchi kama sudan,uganda,zambia,guinea,mali wana better chance ya kupata nafasi hiyo.

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 17, 2007

    draw ya msumbiji na senegal leo bonge la hasara kwetu.wallah draw yetu na wasenegali dar tutaijutia!!!!!

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 17, 2007

    Msimamo Unaonekana hivi Sasa

    P W D L GF GA Pts
    Senegal 5 2 2 1 6 2 8
    Tanzania 5 2 2 1 4 6 8
    Mozambique 5 1 3 1 4 4 6
    Burkina Faso 5 1 1 3 4 7 4

    ReplyDelete
  28. AnonymousJune 17, 2007

    Michuzi can you pl stop this business of calling them JK Boys? Thanks.

    ReplyDelete
  29. AnonymousJune 17, 2007

    WHY YOU CALL THIS TEAM JK BOYS ????? IT MAKES MORE SENSE IF THE NAME REMAIN THE SAME TAIFA STARS

    ReplyDelete
  30. AnonymousJune 17, 2007

    jamani ila naomba tusibweteke kazi bado. Hakuna kulala mpaka kieleweke. Yaani piga ua tunahitaji ushindi mechi yetu na Msumbiji. Uwezekano wa kumaliza kileleni kundi 7 upo tukaze buti. Hata ikishindakana nafasi za washidi wawili naona zimebaki mbili moja itachukuliwa na Sudan au Tunisia sababu wote tayari wana point 12. Timu zilizobaki zote zinauwezo wa kumaliza na point 11 ambazo ni Tanzania, Zambia, Algeria na Eritrea

    Mechi za septemba ni kama ifuatavyo
    Zambia vs South Africa (SA)
    Algeria vs Gambia (Gambia)
    Eritrea vs Swaziland (Swaziland)

    Uzuri wake ni kuwa timu zote zinaWEZA kutubania zinacheza ugenini sisi tunacheza nyumbani.
    Mcheza kwao hutunzwa
    MUNGU IBARIKI TANZANIA
    MUNGU IBARIKI TAIFA STARS

    ReplyDelete
  31. AnonymousJune 18, 2007

    MICHUZI USIBANE HII
    NARUDIA TENA INGAWA MICHUZI UNANIBANIA,MUITENI PAWASA HARAKA SANA SIJAFURAHISHWA NA DEFENCE NITARUDI BONGO KUJA KUWAPA WAPIGA DEBE BUKU TANOTANO ILI WAANDAMANE KUMTAKA PAWASA STARS,HILO LIKITEKELEZWA GHANA KAMA KUMSUKUMA MLEVI WA GONGO

    ReplyDelete
  32. AnonymousJune 18, 2007

    STARS wanatakiwa washinde tu mechi yao na Mozambique. Hata kama Senegal wakishinda tutakuwa na pts sawa.

    Sioni how sisi tutaku less favorite ktk kuchagua Best runners, tutakuwa na pts 11, plustume tie na kiongozi wa kundi letu.

    Most important clue,nasema funga Mozambique goli nyingi sana.

    ReplyDelete
  33. AnonymousJune 18, 2007

    Kwanza, Michuzi, ninyi waandishi wa habari ndio mara nyingi mnaobadilisha mambo. Hii timu ni 'TAIFA STARS' hili ni jina lake halijabadilishwa na kuwa JK Boys ni kama vile Chipolopolo, Lions of Terrenga, Ondomitable Lions, Uganda Cranes, Harambee Stars, Black Stars n.k. Tusipige debe kubadilisha jina la timu yetu bila makubaliano, haya majina hayabadilishwi hovyo hovyo tu kwa mapenzi ya baadhi ya watu.

    Pili, Pia Boniface Pawasa anafaa sana kuimarisha ngome nyuma. Timu yetu inaweza kuwa na benki/akiba ya wachezaji wapatoa 50 hivi wakiteuliwa k.m Brazil inavyofanya. Endapo baadhi ya wachezaji watakuwa na red cards au majeraha, kocha anaweza kuchukua wachezaji toka katika benki/akiba ya wachezaji wa Taifa Stars.Pawasa nafaa kuwa katika benki/akiba ila aache ubishoo. kama si ubishoo wake angekuwa anacheza daraja la kwanza Ulaya.

    ReplyDelete
  34. AnonymousJune 18, 2007

    Michu na wanablog wote, kuna possibility kubwa ya kwenda Ghana as long as tutashinda mechi yetu ya mwisho kwa atleast three clear goals. Tathmini ndogo inaonyesha kundi ambalo lina timu za Sudan na Tunisia ndo ambalo litatoa timu mbili kwa maana ya group winner and best looser as well kwa sababu Tunisia na Sudan wana points 13 na 12 respectively point ambazo hakuna mshindi wa pili wa kundi lolote mwenye uwezo wa kufikia ukiondoa Uganda mwenye 7 points with 2 games in hand, what does this mean? Ukweli ni kwamba timu karibu zote ukiondoa Sudan wenye 12, ni Uganda pekee wenye uwezo wa kufikisha 13 points kama wakishinda mechi zao mbili za mwisho, timu nyingine zote zilizobaki zina uwezo wa kufikisha points 11 tu kama sisi, kwa hiyo ni jukumu letu kuandaa mikakati ya kushinda goli nyingi against our neighbours Msumbiji ili tuwe na goal difference nzuri na hatimaye safari ya Ghana ikamilike!

    ReplyDelete
  35. AnonymousJune 18, 2007

    Ni kweli tumeshinda ila kuna haja ya kuandaa timu zetu tangu wadogo kwa sababu what happended in Burkinafaso was just a fluke! We just got the results but the quality of football was frustarting! We need to nurture our players before they mature other wise we will be waiting for miracles like what happened in Burkinafaso.

    ReplyDelete
  36. AnonymousJune 18, 2007

    Nakubaliana na wazo la kumuongeza Pawasa, ila tusiwe tunashadadia mambo bila kuwa na facts, napata wasiwasi kwamba hao wanaompigia Pawasa debe wanadhani Pawasa yule wa Simba ndo huyo huyo wa sasa hivi inawezekana ameshajiishia au kiwango kipo juu zaidi. Mpeni mwalimu muda amuone then kama ana msaada ataitwa, yasije yakawa yale ya miaka ya nyuma FAT walimuita mchezaji aliyedaiwa kucheza soka ya kulipwa Ujerumani kumbe alikuwa anameacha mpira na kitambi juu!Tuliona kwa Renatus, sio kila mchezaji anayecheza nje ana uwezo mkubwa wengine wanacheza mabonanza tu huko walipo!!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...