jk akizungumza na mabalozi waliokwenda kumuaga ikulu kabla ya kuripoti katika vituo vyao vya kazi. wa kwanza kushoto ni balozi ngilangwa anayekwenda kongo ya kabila wa pili shoto ni balozi juma maharage anayekwenda umoja wa falme za kiarabu na kulia balozi peter kalaghe anayekwenda canada na wa pili kulia ni balozi john kijazi anaeenda india

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 10, 2007

    Wa USA ni nani? Mbona hatumuoni akienda kuaga kwa vile site yao ina muda mrefu sasa toka nimeona kwenye staff page nafasi ya balozi iko "coming soon" Tanzanian Embassy DC au tumesahauliwa....au kesha kuja lakini ku update that site it will take ages?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 10, 2007

    Bwana michu, plz,plz sijue kama watu wengi wamengundua hii kwenye website ya JK http://www.kikweteshein.com/tanzania/ juu kuna bendera ya tanzania na upande wa kulia kuna bendera ya tz na pia ya zanzibar hii sijue maana yake kwa sababu ni rais wa tz so hakuna maana ya kuweka bendera ya zenj au kama ndio hivyo tutaka pia bendera ya bara pia sisi ndio watu aye haya ndio mambo hukiwa mtu wa bara uwezi kununua au kufanya biashara zenj lakini wao ndio rukhusa sasa kana kuna muungano wa east afrika je utawambia watu wa kenya au uganda wasifanye biashara , ndio maana utumwa bado upo kwa sababu zenj ni kwa zenj na bara ni kwa wote , mwambia JK asiweke hee bendera au kama unaweza kueleza kuwa nini ipo hapo maana hakuna logo au bendera yoyote ukaweka kwenye rais website isiwe na maana au hawa jamaa walidesign website hiyo ni wazenj ?????????? wanamaana gani lete hoja hii .plz michu...

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 10, 2007

    hapo emirates na canada wengine mate yanawatoka kuwatamania wenzao congo hakuna sana deal na india ndio buree waliozoe kuiba

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 10, 2007

    ukicheki hapo mabalozi wote wameshiba kuliko rais mwenyewe sasa sijui wataenda kutuwakilisha vizuri huko au ndo mambo ya Prof MAHALU?
    ni mtazamo tu

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 10, 2007

    wape somo JK ili waende kuwakilisha nchi vizuri. Tunataka tunataka Diplomasia ya uchumi bla bla za siasa zimepitwa na wakati. Hawa wote ni Career Diplomats. Lete wawekezaji safi sio wababaishaji na utalii tuongoze sio watu wanafikiri mlima Kilimanjaro upo Kenya.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 10, 2007

    Hawa mabalozi na wafanyakazi wengine wa serikali wawe wanafanyiwa review kila mwaka kuona mafaanikio yao. Hii itasaidia kuwafahamu na kuwaengua watendaji wabaya wanaotuingizia usiku. Michu, waambie wahusika mwana blogu wako anaweza akaandaa hii programme for free for the best interest of his country.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 10, 2007

    Kuna anoyny kasema India hakuna kitu watu wengine sijuhi hawaoni aibu kuongea utumbo kwenye blong inayosomwa na watu wenye elimu...for your information India,Mexico ,Brazil , Russia and China are leading countries in the world for economic growth....kuliko hiyo Canada unayoisema jitahidi kuangalia vitu kwa mapana.
    Kuhusu hao waheshimiwa hapo kila mmoja wao anafikilia jinsi ya kujenga nyumba masaki au mikocheni mambo yenu ya kutangaza kilimanjaro iko Tanzania mwachieni Mama Rose Migiro..
    Mkereketwa Ughaibuni..

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 11, 2007

    mtu mwenye elimu huwezi hata ku-spell blog (blong), and dont even tell me is just a typing error ndio maana wakenya wanatucheka.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 11, 2007

    India population growth not equal to economy growth...Canada population growth is less than economy growth...Think about that

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 11, 2007

    Jamani unayesema india mexico inaendelea uchumi wake kwa kasi usiangalie book value angalia wtu wake per capital yao ni ngapi...wachache sana ndio wana hela india na mexico kulinganisha na Canada per capital yake ni tofauti sana

    usisome tu vitabu tembelea hizo nchi uone pia. Anayesema anaeenda india tabuu tupu ni kweli...

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 11, 2007

    Anonymous June 10, 2007 10:38:00 PM EAT:

    Hapana! Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nchi za Kimataifa iwe inawachunguza. Kwa mfano, kwa nini hao ndugu waliprewa ubalozi. Kassim Mawado na Maharage. Wengi tunamfahamu Kassim Maharage.

    Lakini mdogo wake alipokuwa karibu kuamaliza shule na kuingia Mambo ya Nje, Kassim maharage akabadili kuwa Kassim Mawado!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 11, 2007

    Anon wa June 11, 2007 1:00:00 AM EAT na June 10, 2007 10:38:00 PM EAT ninakubaliana nanyi kwani mawaziri, mabalozi, wakuu wa jeshi, gavana wa benki kuu, wakurugenzi wa PCB, CID, TIS, na wengine wote ambao kazi zao ni za kitaifa na zinahusu usalama wa taifa, au maamuzi ya hao viongozi yanaweza yakawa na athari katika uchumi lazima wawe wanaenda bungeni kujieleza (parliamentary hearing) jinsi gani wanaweza wakatenda kazi zao kwa manufaa ya taifa.

    Watueleze resume zao, maafaanikio yao, mipango yao ya muda mfupi na mrefu na jinsi gani watafanya tofauti na hao jamaa waliopita ili kuleta maendeleo ya haraka Tanzania. Na kila mwaka warudi kuripoti bungeni.

    Na wabunge waulize maswali yenye manufaa kwa taifa siyo waikalie ubishororo kama malimbukeni.

    Tukianzisha utaratibu huu inaweza ikasaidia kuliko utaratibu wa sasa kila mtu anajibu kwa rais hatimae rais anajikuta anakazi nyingi kulikoni. Hajui aanzie wapi na aishie wapi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...