saa nane mchana leo...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 05, 2007

    Jama, kama $1 ilikuwa inanunuliwa kwa sh.1265 saa nane mchana, lakini saa nne asubuhi ilikuwa ina nunuliwa kwa sh.1260, Je, shilling imeshuka thamani au imeongezeka?!! nisaidieni jamani:-( steved.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 05, 2007

    Steved aisee,hapo shilling imeshuka thamani maana inahitajika amount kubwa zaidi ili kupata $1,mfano hapo inabidi kutoa sh.5 zaidi ya ambayo ungetoa asbh!! inaonekana ndogo lkn kama unahitaji dola nyingi inakuwa maumivu matupu!! inaelekea matumizi ya dola yameongezeka sana bongo kuliko shilling!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 05, 2007

    shillingi imeshuka thamani ok.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 05, 2007

    Hiyo maana yake asubuhi shilingi ilikuwa na thamani kuliko mchana. Kwa lugha nyingine ni kuwa mchana shilingi ilikuwa imeporomoka zaidi kuliko asubuhi.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 05, 2007

    HIVI KWANINI SERIKALI HAIPIGI MARUFUKU MATUMIZI YA DOLLAR TANZANIA? KWANINI MAHOTELI, MAKAMPUNI YA SIMU,INSURANCE COMPANIES(TRAVEL INSURANCE), N.K WANAWEKA BEI ZAO KWA DOLLAR? KWANI TUPO MAREKANI? HII INASAIDIA SANA KUPUNGUZA THAMANI YA HELA YETU,N AKAMA INA FAIDA TUELEZWE. KWANINI SERIKALI HAILIFANYII HILI KAZI? WAZIRI MEGHJI UPO?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 05, 2007

    Ama kweli wachumi tunao, hapa siyo jambo la kushuka ama kupanda kwa thamani ya shilingi ya tanzania. Kama shilingi ingekuwa imeshuka basi hiyo bei ya kuuzia US dolla (selling rate) ingekwenda juu. Hapa ni suala la "supply and demand" ya US Dolla. Inaonekana jana kulikuwa na wauzaji wachache wa dolla wakati huo huo wanunuzi ama hawajaongezeka au wamepungua pia. Lakini kwa kuwa hawa watu wanataka tengeneza faida kufanya uamuzi wa kushusha bei ya kuuzia inachukua muda sana kuliko ya kununulia. Inaonekana kama vile kuna wasiwasi wa dolla kupungua kwenye mzunguko hivyo wanaongeza bei ya kununulia kuvutia wauzaji ili baadaye waje waziuze kwa faida kubwa kama wasiwasi uliopo utakuwa kweli

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 05, 2007

    HIVI NYIE MAMBUMBU MNAOLALAMIKA ETI KWA NINI DOLA ILIKUWA CHINI ASUBUHI NA SAA NANE MCHANA IMEPANDA MNAJUA MNACHOONGEA?
    MNAFAHAMU KWAMBA BONGO HUWA YA KWANZA KUONA JUA KABLA YA UK NA US?
    MNAFAHAMU KWAMBA BEI YA FEDHA ILIYOACHWA JANA USIKU BONGO HUENDA WAKAAMKA NA THAMANI NYINGINE ASUBUHI NA BAADAYE MCHANA WAKAJA NA BEI MPYA?
    TATIZO LA WENGI WANAOTOA MAONI ELIMU NDOGO. HAWAJUI BIASHARA, FTSE,NASDAQ,DOW NA MAKAMPUNI MENGINE YANAYOSHINDANA KWENYE SOKO LA FEDHA.
    HIVI HUKO UK AU US KWELI NYIE MNAANGALIA BLOOMBERG AU CNBC NA KUONA JINSI GANI PAUNDI INAVYOKUWA IMARA WAKATI MAREKANI HAWAJAAMKA.
    UMBUMBUMBU KITU KIBAYA SANA. IMAGINE WENGI WANAOLALAMA UKICHUNGUZA WANAISHI UGHAIBUNI... MABOX BWANA, HATARIII. (MWANAMASOKO)

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 06, 2007

    Bwanamasoko, cha hatari nikuwa umbumbumbu mwingi hapa duniani unatokana na wale wanaojua kutotaka kufundisha au kujibu maswali ya wasiojua...oni la kwanza hapo juu lilikuwa swali,jibu lake sidhani litapatikana kama mbeba mabox ambaye anahitajika kwa uchu na uvumba katika nchi nyingi ambako CNBC au Bloomberg inarushwa kirahisi ataishia kuitwa mbumbumbu. SteveD.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...