mh. frederick sumaye na mkewe, esther, wakisakata rhumba wakati wa mahafali ya mzee leo huko ughaibuni.....

Leo aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania kwa miaka kumi, mheshimwa Frederick Sumaye, amemaliza masomo yake na kuhutimu shahada ya juu ya Masters of Public Administration kutoka Chuo Kikuu cha Harvard, John F. Kennedy School of Government mjini Cambridge, Massachusetts, USA.
Mheshimiwa Sumaye alitoa shukurani kwa WaTanzania waliomsaidia akiwa masomoni. Alisema kuwa maisha yake chuoni Marekani yamekuwa tofauti na maisha aliyozoea Tanzania ya kuwa na wahudumu, walinzi, wapishi nk. Alisema alikuwa mwanafunzi wa kawaida tu na alikuwa anajipikia, kujifulia, kufanya usafi na kubeba backpack ya vitabu kwenda darasani.


Pia alikuwa na homework kibao na mwanzo aliona ni kazi kweli lakini alizoea.Alicheskesha watu alivyosema kuwa Tanzania alizoea kuitwa 'Mheshimiwa' lakini hapa USA hata mtoto mdogo anamwita, Fred.
Alitoa shukurani kwa waKenya pia waliomsaidia.Sherehe kabambe iliandaliwa na waTanzania chuoni Harvard ya kumpongeza mhesimiwa Sumaye kwa kuhitimu masomo yake. Sherehe ilihudhuriwa na waKenya, waGanda, waGhana, na waNigeria, na wazungu kadhaa pia.


Mhesmiwa Sumaye anatarajia kurejea Tanzania hivi karibuni.




zaidi nenda swahili times kwa kubofya hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 08, 2007

    Congrats Fred! Nuf jokes. Hongera Mh. Sumaye!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 08, 2007

    Kweli Afrika kuna mambo kwanza unakuwa Waziri Mkuu baadaye ndio unaenda kusoma.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 09, 2007

    Hi Fred go back to Tanzania and preach to those kids how important education is... and if they get the chance they must use it!! Shule uzeeni sio tamu kwani yes utabakiwa na elimu tuu but umri umekwenda sio rahisi kuitumia ipasavyo.. probably in the next few years utatakiwa kustaafu.. what the worse.. si bora hiyo chance angeitumia kijana damu mbichi...

    well hongera pia ni mfano wa kuigwa ni wachache sana especially wakifikia kwenye ngazi yako kimaisha wanakumbuka kuwa kuna umuhimu wa kujiendeleza... well done

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 09, 2007

    Hongera mheshimiwa!!! Nafurahi sana kuwaonyesha watanzania kuwa elimu haina umri..

    Nakuomba ukifika nyumbani uwaeleze hao wasomi wa nyumbani jinsi tunavyopata elimu yetu huku...na maisha ya huku yalivyo.

    Wewe umesoma na kujifanyia mambo yote peke yako kama kupiga, kufua, kusafisha unapoishi na hebu fikiria hawa nawafunzi wanaosoma full time na kufanya kazi full time......Waeleze wanafunzi watanzania wasichezee elimu wanayoipata mostly kama bure..

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 09, 2007

    Only and only in Africa, first u can become a Crime Minister(Yes Crime), then a student.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 09, 2007

    UMEULA KWANZA HALAFU NDIO UNAENDA KUPATA ELIMU. AMA KWELI!!! mHHHH

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 09, 2007

    We anony wa June 9, 2007 12:06:00 AM EAT acha ushamba nani aliyekwambia kuwa mtu ukishafikia umri wa kustaafu ndio inamaanisha huwezi kufanya kazi? Umri wa kustaafu manaake huwezi kuajiriwa, lakini unaweza kujiajiri.

    Na kwa mtu kama Sumaye hiyo ni poa kabisa kwa sababu Sumaye sio mtu wa kwenda kutafuta ajira. Huyu ni mtu wa kuja kuanzisha taasisi au kampuni na kuajiri wabongo wengine.

    Kwa hiyo elimu yake itamsaidia sana kuendesha miradi yake kisomi zaidi.

    Big UP Sumaye. Wale washamba wote waliokuwa wanakuita ziro sasa lazima wafyate.

    ReplyDelete
  8. Hongera sana Fred. Umeonyesha mfano mzuri, elimu haina mwisho. Keep it up

    Toka Vienna!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 09, 2007

    Nimfano mzuri sana kwa taifa hasa kwa wazee ambao wako maofisini lakini hutaka madaraka bila ya kuwa na shule kazi kubwa wanaoifanya ni kuwachukia vijana waliosoma.kwahiyo wazee nafasi bado mnayo yakuweza kwenda shule badala yakupoteza fees kwa waganga wa jadi.Mfano mwingine ni huyu mzee michael looney ali graduate mwaka jana ktk chuo cha southwark-london nakuwa the oldest person to graduate on the planet 76yrs.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 09, 2007

    Hahahhah!Pesa na madaraka ni kila kitu. Jamaa Kaingia u PM akiwa na Diploma, mara tukasikia degree ya open University, sasa Masters ya Havard.
    Haya!hongera Mh. Sumaye

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 09, 2007

    SASA MIMI NAJIULIZA SUMAYE ANASOMA ILI AJE AWE NANI?AU NDO ZILE MALI WALIZOCHUMA MIAKA ILEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE YA NEEMA NDO AMEZITAFUTIA ELIM YA JUU?KULIKONI WABONGO?MADARAKA MATAM NYIE.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 09, 2007

    Jamani Elimu haina Mwisho! Bado hamuelimiki tu, kwa nini lakini? Nani kasema umri ukiwa mkubwa huwezi kusoma? Ebo!Afadhali ya Fred kaenda kusoma na tumemuona, je hao wanaojiita akina Dr Nchimbi, Mzindakaya, Malecela mbona hatukuwaona wakienda kusoma?
    Changieni hoja za maana, sio kuponda watu wanaotafuta kuelimika.
    Michuzi naomba maoni mengine yasiyo na kichwa wala miguu uwe unayatupia kapuni, tumechoka kuletewa pumba kila mara hapa kijijini. Nampongeza sana Fred, najua elimu yake itasaidia wabongo kibao, iwe moja kwa moja ama kwa namna nyingine!

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 09, 2007

    Congrats Fred, aka Mh bongo. Lakini najiuliza hapa, ulikuwa sponsored na nani, manake Havard University sio mchezo. Sio university ya kusoma na kupiga mzigo kusort fees etc

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 09, 2007

    Jamani acheni mzee wa watu hii ni changa moto kwa wavivu wa bongo na pia wengine walioko nje ya nchi... Wabongo hawataki kwenda shule kwa vile umri umesogea...Especially wanaume wetu wanatabia hii sana...wengi tunawaona shule hawataki kwa vile wako above 30 yrs old...Someni acheni mchezo, taifa la kesho tutakuja ongoza sisi wasichana tu.

    USA amegraduate mwanamke ana miaka 92 na walio na miaka 80 and above ndio usiseme wako wengi sana sana. Sasa hapo sijui mtasemaje?

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 09, 2007

    Hao mnaosema alikua waziri kwanza halafu shule. Atleast alikua na degree ni wangapi hapo wasio hata na O level education? Na bado wanaitwa waheshimiwa?

    Na pia USA raisi alikua ni a gentleman's C person na anaongoza huyu mtu wakuja kufanya master na umri wake huu basi alikua smart sana...na especially Harvard sio mchezo. Hawaangalii background yako kama vyuo vyetu vya bongo.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 09, 2007

    nilidhani wale wajinga watamponda Sumaye kwa kuja kusoma Ughaibuni na 'kupiga box'. .... au huwa mnapiga debe kuwachanganya watoto wa walala hoi ambao wengi wako huku kusoma at same time kutatua matatizo madogo madogo uswahilini ?
    Acheni ujinga na chuki. I hope na mimi ntagraduate soon , kisha niwatafute wanoachonga wanionyesha walichonacho.
    HONGERA MHESHIMIWA SUMAYE !

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 09, 2007

    mwizi tu huyo hana lolote!

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 09, 2007

    Hahitaji ajira huyo alishaiba tani yake toks serikalini.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 09, 2007

    Nadhani amekua humble kishenzi. Huku heshima ni kwa wote haijali wewe ni nani au unahela kiasi gani.

    Heshima za kitanzania sijui ni za wapi. Mwalimu akiingia darasani mawafunzi wasimame, akipita nje hata kama mmekaa chini kwenye majani baada ya kufagia yale mavumbi na kudeki darasa bila maji lakini lazima msimame.

    Mtu anahela kidogo basi kila mtu wanamwita mzee...mzee...heshima yako mzee...Na wengine wakubwa kuliko huyo mtu...

    Heshima inatoka rohoni na si kwa kulazimishwa...unaweza ukasimama sana, ukamwita mtu majina yote yaliyopo lakini kama rohoni humthamini haina maana yeyote.

    Maisha ya marekani yanafundisha mengi sana tu. Sio elimu tu tunapata huku bali maisha ni nini. Na nini n more valuable in this life na jinsi ya kuishi na watu pia. Yote haya tunajifunza huku.

    BINADAMU WOTE NI SAWA - Tanzania tunatakiwa tukumbuke hilo.. kwa vile mtu ana nyadhifa, ni boss au ana hela basi heshima yake ni tofauti kuliko yule asiyenayo au ni mlemavu.

    Huku ukijifanya wewe boss zaidi kuliko wafanyakazi wenzako utakuwa unamaliza kila project peke yako.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 09, 2007

    wewe anon hapo juu mjinga wa mwisho.huyo hata hicho cheti kapewa tu.

    labda akuajili wewe na familia yako.

    too late Sumaye,sasa ukajibu wizi uliofanya ulipokuwa madarakani.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 10, 2007

    Hongera Fred Sumaye!

    Habari za kuaminika zinaeleza kuwa sasa hivi Matthew Olusegun Aremu Obasanjo (Jenerali na Rais mstaafu wa Nigeria) naye kajiunga na shule moja ya Religious Theology kuchukua diploma ya mambo ya dini huko kwake Abeokuta!

    Labda Jenerali huyu anataka kuanzisha kanisa lake au anataka kuwa mchungaji wa roho baada ya kuchunga bundunki na kuchunga siasa!

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 10, 2007

    hongera sana mheshimiwa sumaya kwa ku graduates naomaba usirudi nyumbani jiendeleze zaidi kielimu na upate PHD yako ili uwakate kilimi limi wabongo wote waliotoa comment zao za pumba katika blog hii. maana master siyo big deal big deal PHD yako babakee wee na wanakuonea wivu maana wao waliosoma au wanasoma wanasoma katika viji college au university vya kishenzi shenzi tu hata havi tabuliku wala kusaminiwa, big up my man. Harvard si mchezo kaa baki bado piga PHD yako ukimaliza unatua bongo ukawaonee wajinga wajinga huko.
    haters kill your self, elimu haina mwisho na elimu ni power, kama sumaye kaiba mali ya umma, kaficha hizo mali au vyovyote vile wacha ni haki yake wajinga nyinyi mmeambiwa msiibe? au chance hamjapata ndo maana mnalala ma hapa.
    ongeze elimu babake sumayeeee nakufagilia piga PHD, tuwe mimi na wewe tunakimbizana sawa babake.
    all the best to you and to your family and friends and love one. usijali na mimi nikiukona nitakupigia saluti na heshima ya mheshimiwa msomi wangu humambo na marekani yetu. chao mwangu big up.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 10, 2007

    We Fred kwanini Uwe waziri mkuu wetu ndipo uende kusoma na siyo kusoma kwanza ndipo uwe waziri mkuu? Ina maana watanzania ulitugeuza vichwa vya wendawazimu?

    Unatuongoza bila elimu na kututumbukiza shimoni? Anyway ongera sana hila washauri wenzako wapate elimu ya kutosha ndipo wawe viongozi.

    Halafu we anonymos wa (June 10, 2007 4:53:00 AM EAT) suala siyo chuo suala ni elimu unayoipata inasaidiaje jamii yako na wewe mwenyewe? Unaweza soma havard kusiwe na cha maana mzee.

    Unaweza kusoma santa joseph-(mbagala) ukawa moto kweli.Siku hizi ni utanda uwazi kila kitu kinapatikana popote pale leo hii resources ziko kila mahala, siyo kama zamani wewe tatizo lako ujapata nauli ya kurudi bongo tangia ulipo ikimbia wakati akina Fred wakiwa watawala.

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 10, 2007

    Anon wa June 9, 2007 6:19:00 PM EAT inaelekea Cultural Anthropology imekupita mkono wa kushoto au hukuelewa. Every culture has its own, values, standards, and customs. Watoto wa kiafrika kumuamkia mwalimu ni utamaduni wetu, kwasababu katika jamii zetu unapokuwa mkubwa nafasi yako katika jamii inaongezeka umuhimu. Hata wa asia kama Japan ni sawa nasi, mkubwa anaheshima tofauti na mdogo. Lakini utamaduni wa magharibi ni tofauti nasi, hiyo ndiyo tofauti ambayo Mh. Sumaye amejionea mwenyewe…lakini angeenda Japan asingeiona hii tofauti ya kuitwa Fred na mtoto mdogo. You must have heard the term cultural relativism; this is what has an impact to Mh. Sumaye.

    Kuhusu tajiri kupata heshima hiyo ipo sehemu yeyote duniani. Mh Sumaye alikuwa waziri mkuu. Alikuwa ana power, authority, prestige and he has access to resources. Kwahiyo, watu kumuheshimu na kumnyenyekea siyo ajabu.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 12, 2007

    every guerrilla fighter can be a president, but not every president can be an academician. uacadenmician unahitaji subira, uvumilivu, na kutokata tamaa katika kujenga basics za ujuzi. we unafikiri kila president anaweza kuwa lecturer? sio field ya usanii.Basi bwana sumaye hongera sana umeonyesha virtues za uacademician ambazo ni basic in life. Now u have a good CV not only because u have graduated form havard lakini kwa sababu umejifunza virtues.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...