mama akimhifadhi kuku baada ya mnwewe kuonekana akizengea angani. picha hii imeletwa na mdau toka kigoma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 21, 2007

    Michuzi!!!
    Kwa hiyo huyu mama si kuku?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 21, 2007

    Taaaa tantaaa tarararaaaa tantaaa taaaa tantaaaa ta-ra-ra-ra-ra-ra. mama na mwana!
    duh enzi zile wakati wa kipindi cha mama na mwana kilikuwa RTD. wadau mnakumbuka hiyo!
    NOPE

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 21, 2007

    Duh! Michuzi bwana.... eti mama akimhifadhi kuku!! Lakini sawa tunakubali kuwa hicho ni kikuku, lakini ungeandika kifaranga ungenisaidia kidogo miye kupunguza maumivu ya mbavu kutokana na kicheko!!

    Halafu hako kakifaranga kenyewe kanaonekana nuksi kichizi... cheki kanavyo dadisi anga!!! Vifaranga vya namna hii ndiyo huwa vinakua na kuwa KUCHI wapiganaji wasio na manyoya shingoni. kila kukicha ni ugonvi tu na jogoo wa jirani!! he he.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 21, 2007

    Mdau hapo Juu umenikumbusha zamani sana miaka ya themanini. Hicho kipindi alikuwa anakiendesha Sara Dumba, alikuwa anakimudu sana na hadithi zake kila Jumamosi. Hivi yupo wapi huyo Mama?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 22, 2007

    Utanifanya nilie kuna vitu vingine tukiwa home vya kawaida tu lakini huku ni kama kipofu akiona mbalamwezi.

    Hadithi za mama na mwana nilizikuta kwenye podomatic siku moja nilitoa macho
    mna kumbuka hadithi ya mtoto wa wafalme na chura? MAMA NA MWANA HADITHI HII HAPA

    ReplyDelete
  6. Umenikumbusha sana kipindi cha mama na mwana cha RTD (saa 8:02 mchana hadi 8:30 mchana) ambapo watoto tulikuwa hatukubali kutumwa dukani au nyumba ya jirani (hata kwa manati). Nammiss sana mama Deborah Mwenda na hadithi zake tamu.Yaani ilikuwa raha mtindo mmoja.

    Hadithi kama Binti Chura au Ua jekundu SITAWEZA kuzisahau kamwe.Michuzi "hutupendi" wewe,mbona sasa watukumbusha mambo matamu ambayo hayatakaa yarudi tena? Maskini mie!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 22, 2007

    Jama nisaidieni... huyo mama wa KUKU mwaweza fikiria ana miaka mingapi vile?!...maana naona kipara kimeanza kumpata kutokana na shida mbali mbali za kukwepa mwewe na vipanga na pia kukimbizana na wamiliki wake akikwepa kuchinjwa kwa kupaa na kukaa kwenye paa la nyumba...mimi nadhani ana miaka 3 na nusu hivi...
    nipe maoni tafadhali.. he he

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 22, 2007

    Mheshimiwa Issa..PICHA AINA YAKE HII HUYU "MTETEA" KAJITAHIDI SANAA KUNIFADHI "KIFARANGA" CHAKE.. FLASH YAKO INAFANYA KAZI MURUA..NA SIO " MWEWE " WALA " KIPANGA ". WIMBO..
    KUKU MWEUSI..
    KAMKARANGIZE NA MAPILIPILI..KAMKARANGIZE...
    KUKU MWEUPE..
    KAMKARANGIZE NA MAPILIPILI..KAMKARANGIZE...

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 22, 2007

    ETI WADAU KATI YA KUKU NA MAYAI KIPI KILITANGULIA NAOMBENI MNIELEWESHE WAUNGWANA!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 22, 2007

    Prince lee wew uko kwenye Scientology cult au????

    Mumgu uliona ameumba mayai au wanyama kwanza?

    Go figure

    jamani nimesikiliza hadithi za mama na mwana....mweee nikienda home nitasikiliza zote

    Michuzi thanks so much kwa vile kama sio weew haya yote tusingeyaona humu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...