majamboz kama haya yanapatikana http://www.marcusmusic.org/

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 08, 2007

    Kama mamabo ndio haya ...mimi yangu macho

    Hii so migoboli ya mapolisi hii kweli

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 08, 2007

    Bwana Michuzi habari yako.Hongera kwa kazi hii.
    Mimi ni Mtanzania ninayeishi Amerika,nitaendelea kuwa Mtanzania hata kifi kinichukue.Binafsi utaifa wangu haotokani na maandishi ta makaratasi bali uzao wangu kwa maana kitovu changu kilidondoka katika ardhi ya Tz.
    Pia ni mimi niliyetoa maoni kuhusu ukweli kuwa hali inavyokwenda si kesho wala si muongo mmoja ujao lakini naona hali ya usalama haielekei pazuri! haya ni mawazo yangu ambayo ni haki yangu ya kikatiba kama ambavyo wewe hukupenda kuyaweka hadharani! naliheshimu hilo kwani halikadhalika ni haki yako kimsingi.
    Tukiachana na hilo, naomba uanzishe hoja ama mjadala huu hapa chini:
    Mara nyingi sana watu hubishana kama si kusimangana kuhusu WAPI MAISHA NI BORA AMA NANI ANAFANYA NINI KATI YA WALE AWALIOPO NYUMBANI NA WENGINE WALIOPO NJE YA NCHI, HUSUSANI ULAYA NA AMERICA! Suala kubwa huwa ni kukejeliana na kuitana majina kama WABEBA MABOKSI(KWA WALIOPO ULAYA NA AMERICA)ama kejeli zingine zisizofaa kwa waliopo nyumbani pengine kwa kuamua kubali ama kwa kukosa nafasi na kuja(kwenda)nje ya nchi.
    Naamini kesi ya msingi ambayo wengi wetu pengine kwa makusudi au kwa kukosa ufahamu wa kutosha ni kuwa,WAKATI WOTE MAISHA YA ULAYA NI BORA KULIKO TZ(Ama Afrika kwa ujumla, lakini cha nizungumzie Tz)tatizo kubwa tunalolifanya ni kulinganisha makundi mawili tofauti kabisa! Hapa namaanisha kuwa,Maisha ya msomi wa Kitanzania hayaendani na elimu yake!
    Tunaposema"HUKO KAZI YENU NI KUBEBA MABOKSI, TUKUMBUKE HUYU NI MTU AMA MTANZANIA ASIYE NA ELIMU AMBAYE HATA HIVYO MAISHA YAKE KWA KWELI NI BORA KULIKO WASOMI WENGI WA NYUMBANI KWA NYANJA MBALIMBALI!
    Tunapofanya ulinganifu tufanye kwa makundi yanayowiana, kwa mfano:Linganisha Daktari Mtanzania aliyesoma na kufanya kazi America!hivi huyu utamlinganisha na mwenzake wa Kitanzania aliyepo Tz?
    Mhandisi wa Kimarekani mwenye shahada sawa na ile ta Kitanzania utawalinganisha?
    Kifupi, napenda tu kuondoa stigma iliyopo hasa kwa watu wa nyumbani kuwa Watanzania waliopo nje ni wabeba maboksi!hata hivyo MABOKSI hutumika kama SYNONYM kuelezea KAZI ZA HALI YA CHINI KWA TAFSIRI YA HUKU NJE KWANI HIZI KAZI ZINAZOITWA MABOKSI NDIZO ZINGEKUWA NI HUKO NYUMBANI NI KAZI AMBAZO ZINGEFANYWA NA WATU WENYE SHAHADA ZA VYUO VIKUU!Kwa mfano mimi binafsi nafanya kazi ya customer service, Watanzania wengi wanafanya kazi kwenye makampuni makubwa duniani kwa mfano Boeing,HP,lakini kwa vile hizi zinakuwa categorized kama unskilled laborers hivyo sisi Watanzania tumezipachika jina la MABOKSI kwa vile kwa mfano, unapo-assemble computer ni lazima utatoa parts kwenye boksi,unapo-assemble cellular phone ni vivyo hivyo! hi hapa ndipo jina MABOKSI tulilianzisha! Kifupi hakuna Mtanzania anabeba maboksi kama inavyotafsiriwa na wengi huko nyumbani!
    Pili, napenda kuzungumzia kitu kingine ambacho mimi binafsi nimejifunza hapa America tofauti na ilivyo huko nyumbani1 huku wenzetu wana-TAKE PRIDE na kazi yoyote anayofanya! hii kwa kweli ni tofauti na ilivyo huko nyumbani! wenzetu huko ni kawaida kukwambia kwa mfano "kazi yangu ni uyaya" ama mlinzi, ama NAOSHA MAVI WAZEE! najua ina-sound funny kwa utamaduni wa nyumbani lakini ndivyo ilivyo kwa wenzetu!Kwa vile sisi hatuko hivyo ndiyo maana kwa Tanzania mtu akiambiwa labda nafanya kazi ya KULEA WATOTO VICHAA, AMA KULEA WAZEE AMA ULINZI, kwa huko nyumbani hupata picha ya ajabu na picha kubwa hapa huwa"JAMAA HAWANA CHOICE NDIYO MAANA WANAFANYA KAZI KAMA HIZI" ukweli ni kuwa, haiko hivyo, na wengine huku nje(kwa mfano nilionao kwa uhakika ni hapa America)watu wengine hufanya kazi kama hizo kwa kujitolea na wanatoka familia zenye uwezo!
    Mwisho, nimelazimika kubainisha haya ili kueleweshana na si vinginevyo, popote mtu akinielewa vibaya si nia yangu!pia ni kutaka kuwaambia Watanzania wengine wenye nia ama nafasi ya kwenda(kuja)nje wazitumia nafasi hizo, kwani hakuna mahali popote duniani unapoweza kutimiza dream yako zaidi ya huku nje na hasa America!huhitaji kumjua MZEE FULANI wala kuwa MTOTO WA FULANI, huhitaji KIMEMO wala KINENO! ni wewe ni akili yako na subira!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 08, 2007

    Michuzi vipi?? MAHUSIANO.COM wamekwenda likizo?? Mbona hatupeani taarifa kama tulivyokaribishwa???,

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 08, 2007

    Bunduki haishikwi hivyo baba...jamaa inaelekea hajapitia JKT huyu

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 08, 2007

    @£$~#@$?\!".... Backside....

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 08, 2007

    BREAKINGI NYUUUUUZI!!!
    LEO MANISPAA YA ILALA IMEANZA KAZI YA KUZIBA MASHIMO KWENYE BARA BARA ZINAZOZUNGUKA ASKARI MONUMENT,CITY CENTRE.HONGERA SANA MICHUZI,LOOKS LIKE UMEWAAMSHA!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 08, 2007

    Anony hapo juu try to make it short and simple ...Ujumbe wako unaweza kuwa mzuri sana lakini mtu akiona hii yote ...inakatisha tamaa ya kusoma...

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 08, 2007

    Anon wa pili hapo juu, You sound smart and understanding. Lakini, kifupi sio kwamba watu wa nyumbani hawaelewi. Wanajua sana kwamba maisha ya ughaibuni ni mazuri na bora kuliko nyumbani. Swala la maboksi mimi sioni taabu, labda sema kwa sababu sisi tumezoea uzembe na majungu, whats the problem kubeba box? As long as unakuwa compensated kulingana na kazi uliyoifanya?

    Again, tatizo la kwetu hatuna utamaduni wa kuthamini kazi, ndo maana utakuta YAYA anafanya kazi masaa kumi na manne au sita..lakini anapewa elfu kumi..Its sad na kwa mwendo huo, umaskini ndo utatuandama. Kwa hiyo wale wote mnaodharau watu..please take, heed, maisha hayana formula, na kila mtu anahaingaika kusudi aweze kupata chochote. Especially wasio na GOD FATHERS!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 09, 2007

    Tanzania kama wewe hubebi briefcase basi siyo kazi wakati huku NY city kila mtu ana bag pack na lunch box mkononi.

    Ukila sandwich kwenye park ni aibu kweli bongo.

    Tatizo la bongo wanaangalia sana TV na movie hizo ni movie tuu jamnai njooni huku muone the real life.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...