ukiondoa tatizo la mahandakizzz dar, kuna hii soo ingine ya wakola kuiba mifuniko ya mifereji ya maji machafu ambayo inasemekana wanauza kama skrepa kwenye vinu vya chuma. na mie hii nakula nayo kama mahandakizzz mpaka kieleweke. hapa ni nje ya mgahawa wa steers barabara ya ohio

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Kuna siku nilidumbukia ndani ya mfereji kama huo nikiwa Bongo. Kweli wazifunike maana ni hatari. Na kuna siku niliona kipofu andumbukia ndani ya mfereji. Jamani zifunike. Siyo wanangojee mtu afe ndo wachukue hatua.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 09, 2007

    Duu Da Chemi pole,mana napata picha mtu akidumbukia humo inakuwaje,Pole sana mamii

    ReplyDelete
  3. Da Chemi ni wanaharakati wa masuala ya watu wenye ulemavu nchini Tanzania pamoja na jumuia za watu wenye ulemavu wapo katika harakati ya kujenga weledi wa jamii pamoja na mambo mengine katika matumizi ya baadhi ya majina ambayo yamekuwa yakitumika kuwasiliasha aina za ulemavu miongoni mwao. Kwa mfano, badala kutumia neno 'kipofu' inapendekezwa zaidi litumike neno 'asiyeona'. Nitajitahidi nikutumia 'soft copy' ya kitabu kiitwacho "Mwongozo rahisi kuhusu kutanzua ulemavu na kujenga jamii ya wote.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 09, 2007

    Bongo kweli nchi ya kisanii, Hivi kwa mfano ikipitishwa sheria kuwa wanunua vyuma chakavu wote wasajiliwe na kuwa hakuna kununua skrepa, bila kukaguliwa na ikigundulika faini Shs 10,000 au kifungo miaka 10. Nafikiri watu watakuwa makini na ununuzi wa vyuma chakavu.

    kinachoonekana hapo wote muuzaji ambaye kaiba hiyo skrepa na mnunuzi wote lao moja kwa kuwa mwizi anataka hela bure na mnunuzi anataka malighafi cheap.

    Yaani hii sasa inatisha na inaweza leta maafa makubwa sana mbeleni ikiachiwa, mfano kuna vitu kama 'STEEL STRUCTURED BRIDGES', hawa jamaa wakipata vitendea kazi vya kufungua madaraja haya sijui kama kutakuwa na usalama, maana usiku wanaingia kazini asubuhi mtu anakuja speed mia anashitukia daraja halipo au nguzo moja imeng'olewa, too late.

    Sheria kali kuhusu ununuzi na uuzaji wa skrepa zipitishwe vinginevyo, tutakuwa tunarudi nyuma kimaendeleo.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 09, 2007

    KWA CHEMI KUDUMBUKIA HUMO WALA HAINISTUI. MLEVI KUMWINGIZA CHOONI NA KUMWAMBIA HUMO NDIYO CHUMBANI MWAKE, HALALI YAKE.
    UNALEWA SANA MWANAMKE NA KUJIVUNJIA HESHIMA YAKO. MWANAMKE KUWA MLEVI BADALA YA MNYWAJI...KOMBAAAAAA!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 09, 2007

    HIZI NJAA ZITAUA WATU WENGI!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 10, 2007

    Du Michu Ile faini pale juu isomeke Shs 10,000,000 na sio shs 10,000 ni ndogo sana hawatakuwa makini.

    Samahani: vidole vinamfupa

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 10, 2007

    ushauri wa bure kwa wahusika:achana na mifuniko ya chuma.tumieni mifuniko ya zege ambayo ndani mta reinforce kidogo tu halafu tuone hao wezi wa scraper watafanya nini?just a little bit of thinking u know?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...