
ujumbe huu umeingia punde tu toka ughaibuni...
MICHU!
NIMESOMA HABARI YA MAHANDAKI DAR, NA KUKERWA SANA NA JINSI JIJI LA DAR LIKIONGOZWA NA MEYA LINAVYOHARIBIKA LICHA YA WAFADHILI KUMWAGA MAPESA KILA KUKICHA. HIVI MAJUZI MH. PM ALIMKALISHA MEYA NA WENZAKE KITAKO NA KUWAFUNDISHA JINSI YA KUTENGENEZA TAA ZA BARABARANI KANA KWAMBA PM HANA MAJUKUMU MENGINE. MEYA WA JIJI ANAISHI DAR,HIVI KWELI HAJAWAHI KUONA KUWA TAA ZA BARABARANI ZIMEHARIBIKA KATIKA SAFARI ZAKE LICHA YA TAARIFA ZA KIOFISI.
1. HIVI KWELI HAJAWAHI KUPITA ASKARI MONUMENT NA PAMBA HOUSE KUONA MAHANDAKI NA MITARO ILIYOZIBA.
2. HIVI KWELI TUNAHITAJI MFADHILI WA KUKARABATI VISHIMO VIWILI VILIVYOKATWA KWA UZEMBE BILA UKARABATI.
3. HIVI KWELI KODI YA WANACHI WA DAR AMBAYO NI MABILIONI KWA MWEZI ZINAFANYA KAZI ILIYOKUSUDIWA.HIVI KWELI MEYA WETU ANAJIVUNIA NINI KATIKA KIPINDI CHA UONGOZI WAKE.
4. HAWA MADIWANI WANAJADILI NINI KATIKA VIKAO VYAO.
5. HIVI JK AU PM WANATAKIWA WASIMAMIE UZIBAJI WA MASHIMO NA KUWEKA BALB KATIKA TAA ZA BARABARANI.WADAU NISAIDIENI,MAANA MIMI SIELEWI JIJI ,MADIWANI NA MAMEYA WETU WANASHUGHULI GANI HAPO DAR.
NAMSHUKURU YULE MFANYAKAZI WA POSTA ALIYESHUGHULIKIA KIFURUSHI TOKA U.S.A NA KIKAPATIKANA MAANA AMEWEKA 'DIFFERENCE' KWA MAISHA YA MTANZANIA.
SIJUI WENGINE WANAWAJIBIKA VIPI.
KIMITO
ONTARIO, CANADA.
Hii inakera sana kwa kweli na sijui hayo maendeleoyatakujaje namna hii na still nimeona kwenye DARHOTWIRE jiji la Dar ndio ghali kuishi katika majiji hapo east africa.
ReplyDeleteNa kwa nini watu nyumbani wanapenda saana kutumia dola kununua/kufanyia biashara Tanzania? huu kama si ulimbukeni ni nini tulionao huuu?
Na kwa taarifa tuu kile kifurushi toka usa hakijafika bado,kilichopatikana ni cha jamaa kutoka malaysia nadhani.
meya wa dar hafahamu kwamba hiyo ni kazi yake kwa sababu anamanaibu wake ndio maana anakaa kimya akijua kwamba manaibu watafanya,kwa mfano meya wa ilala mtaa tu anao kaa ni mchafu kupita maelezo halafu kaanzisha mradi wa magari ya kuzoa taka,hizo gari zenyewe pia ni taka tosha halafu eti anazoa taka.sasa hizo hela za kununua hayo magari kazipata wapi kama sio kodi za wananchi?hapa maendeleo hakuna hata iweje,balb haziwekwi,mahandaki hayazibwi,na mitaro haizibuliwi.
ReplyDeleteNaungana na wewe kwa 100% nashindwa kuelewa huyu Meya wa Jiji anafanya shughuli gani jiji lote la Dar es Salaam limeharibika licha ya mahandaki, mifuniko yote iliyokuwa imebiwa kwenye mashimo ya kupitishia maji machafu haijarudishwa kila mahali upitapo mjini ni mashimo na haya ndio mojawapo yasababishayo follen zisizo na msingi. Pamoja na kwamba Tibaigana aliweka mkwara kwa wezi wote kurudisha mifuniko hiyo Meya hajachukua hatua yoyote pamoja na madiwani wake. Utamuona tu kwenye kipimajoto cha ITV kila siku kuzungumzia habari za wamachinga na usafikri wa daladala ndivyo alivyovishikia bango. Sijui nchi hii itafika wapi.
ReplyDeleteJK na PM wanapenda kufanya kila kitu. Kazi inayomhusu waziri fulani utaona rais au PM anaenda kufanya, sasa unategemea nini. Hii inawafanya watu wasijiamini, na hivyo kuamua kutofanya mpaka waambie. Na kwa kuwa wote wameingia madarakani kimtandao wananchi tuendelee kupata maumivu tu
ReplyDeleteAnonymous wa June 5, 2007 11:52:00 naomba nikuunge mkono kama siyo mguu. Kweli hawa viongozi wetu wawili wakuu wanapenda kutoa maagizo kwa kila jambo hata jambo la kushughulikiwa na katibu kata! Wamezidi sana mpaka wanawatia uvivu watendaji wengine serikalini.
ReplyDeletehayo mahandaki yako standby mkisikia vita msihangaike,
ReplyDeleteWenzenu wako bizi kutafuta vya kisasa: pazma ya kisasa, Tv ya kisasa, suti ya kisasa, soksi za kisasa, chupi za kisasa kwa wake na hawara zao, saa ya dhahabu ya kisasa, nk, ili waonekane hawavai vya Vingunguti...UKOGAJI!
ReplyDeleteUtamkoga nani na wewe huvitengenezi?
Haya yote ni matokeo ya uongozi wa rushwa. Wananchi hatuangalii competence na record ya kiongozi wakati wa kumchagua. Kweli Meya KIMBISA ni aibu kubwa. Jamaa ukimuona anaongea utadhani kichwani ni smart lakini wapi..very corrupt and irresponsible.
ReplyDeleteMwenyewe siamini kwamba PM au Raisi mpaka watoe directives ndo mambo yafanyike.Lakini inabidi wafanye kwa sababu Meya na watu wake ni kuiba tuu...wananchi tumechoka jamani..ibeni basi..lakini na sisi mtupe huduma..hata zile basic!
Hawa mameya na madiwani....ni hopeless kabisa. Mi nadhani ndo maana wengine wanasema hivi vyeo vifutwe kabisa!
Inasikitisha kuona kuwa watu hawawezi kuwa creative kwa vitu vidogo kama hivi ambavyo vina usumbufu katika maisha ya mtu wa kawaida ya kila siku. Its absurd. Harafu ukiangalia hawa hawa wanashinda ulaya..kufanya nini? ziara za kujifunza! wanajifunza nini? mimi na wewe hatujui!
asante sana mdau kwa kuleta hii mada nyeti.
ReplyDeleteMie nimetoka bongo hivi karibuni-swala la barabara kuu (main roads) wamejitahidi sana-tatizo kubwa lipo kwenye barabara za uchochoroni.Mnashangaa hako "kahandaki" hebu tembeleeni kwenye vitongoji mbalimbali mfano mlalakuwa, mikocheni, mwenge n.k., mtashanagaa wenyewe,Buguruni etc.
Ukiwa dar barabara kubwa mfano Morogoro Rd, Ali Hassan, etc-kwa kweli ni nzuri lakini ukishachepuka kutoka kwenye hizo barabara hapo ndio utaona "mahandaki ya kweli".
Swali langu zaidi ya hizo barabara kuu-je nani anahusika na kushughulikia barabara za uchochoroni-yaani zile zinazoenda kwenye maeneo ya watu wanapoishi (residential areas)?? wananchi wenyewe au Jiji??
Michuzi hebu piga picha jinsi barabara zilivyo kwenye residential areas...
Mimi kinachonishangaza zaidi kuhusu huyu meya ni sfari zake za mara kwa mara katika majiji ya nchi za wenzetu kujifunza na kujipatia uzoefu katika uendeshaji wa majiji lakini kumbe hizo sfari ni miradi ya kujineemesha wao wenyewe!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteAnyway,labda kwasasa amejikita zaidi katika mchakato wa uchaguzi ndani ya chama au labda majukumu aliyonayo katika Red cross which can not be an excuse kwani kama huwezi kitu bora ukae pembeni kuliko kuleta ubabaishaji kama walivyosema wenzangu hapo juu..
Meya yupi manake siku hizi jiji limekuwa kuuuuuubwa ati, na ma-meya ni wengi........ila hata kama ni mmoja tu nina mfano mzuri wa meya mmjawapo nyumban kwake tu majani mpaka mlangoni sasa mahandaki atayaona ni kero kweli?Waswahili wanasema jitoe kijiti jichoni kwako mwenyewe kabla ya kutoa kibanzi kwa mwenzio.These guys need a major phsychological overhaul. Kama alivyosema mwingine kny comment yake hawa jamaa wakisafiri wanatizama nini? Au wanawaza 'shopping' tu?Waheshimiwa kama mnasoma hizi wala msichukie mjue Watanzania 'wa kawaida' tumechoka na mambo haya yasioleleweka.Wataalam wapo kuwatumia hamtaki, kulikoni????
ReplyDeletemkogaji pumba out of point kalale kama umelewa
ReplyDeleteWatanzania wengi hatuelewi kwamba sisi ni nchi moja wapo ya nchi zinazoendelea. Kwa maana hiyo mambo yote bado yana kua. Unapolinganisha Dar es Salaam na jiji la London, Paris,or New York, you are absolutely wrong! Mimi niki tumia usafiri wa dala dala si tegemei kupata treatment ya Metro or city buses. Huku kwetu kuna mtu kabeba samaki, mwingine kikapu cha kuku etc. Uneshaona hayo Los Angeles?? Ni Watanzania na wanaendelea, wanajifunza. Maendeleo si kwa kazi ya radi, Tuwe na subira. We shall overcome. Hon. Kimbisa alishamuona babu yake akiwa Meya?? Si naye anajifunza? Tumsaidieni basi angalau kwa kusafisha sehemu zetu tunazoishi na kutotupa maganda ya machungwa na kupenga mafua barabarani bila hata aibu kidogo!! Guys come one, let's enroll our kids into schools!!!!Mungu ibariki Tanzania Na Africa.
ReplyDeleteKwako Mheshimiwa Mstahiki Meya... Tafazali tupe maoni yako kuhusiana na hali halisi iliyoleta mjadala huu na pia maoni yetu hapa juu... Asent
ReplyDeletekaka michuzi hii sasa ni aibu sijawahi kuona lami inazibwa na kokoto kama unvyojua blogu yako inasomwa na watu wengi sana kwa kuonyesha utanzania naonba pata ushauri kutoka ERB engineer registered board kama ni suitable kuziba hizo pot hole kwa kokoto idea hii aliyoileta ni nani mwanasiasa au engineer tunaomba utusitiri kwani madhara yake ni makubwa woote tutakuwa wapumbavu kumuacha huyo pimbi aliyeruhusu au kuagiza hivyo kama ni kubana matumizi si bora wasinunue mashangingi
ReplyDelete