ujumbe huu umeingia punde tu toka ughaibuni...

MICHU!

NIMESOMA HABARI YA MAHANDAKI DAR, NA KUKERWA SANA NA JINSI JIJI LA DAR LIKIONGOZWA NA MEYA LINAVYOHARIBIKA LICHA YA WAFADHILI KUMWAGA MAPESA KILA KUKICHA. HIVI MAJUZI MH. PM ALIMKALISHA MEYA NA WENZAKE KITAKO NA KUWAFUNDISHA JINSI YA KUTENGENEZA TAA ZA BARABARANI KANA KWAMBA PM HANA MAJUKUMU MENGINE. MEYA WA JIJI ANAISHI DAR,HIVI KWELI HAJAWAHI KUONA KUWA TAA ZA BARABARANI ZIMEHARIBIKA KATIKA SAFARI ZAKE LICHA YA TAARIFA ZA KIOFISI.

1. HIVI KWELI HAJAWAHI KUPITA ASKARI MONUMENT NA PAMBA HOUSE KUONA MAHANDAKI NA MITARO ILIYOZIBA.

2. HIVI KWELI TUNAHITAJI MFADHILI WA KUKARABATI VISHIMO VIWILI VILIVYOKATWA KWA UZEMBE BILA UKARABATI.
3. HIVI KWELI KODI YA WANACHI WA DAR AMBAYO NI MABILIONI KWA MWEZI ZINAFANYA KAZI ILIYOKUSUDIWA.HIVI KWELI MEYA WETU ANAJIVUNIA NINI KATIKA KIPINDI CHA UONGOZI WAKE.

4. HAWA MADIWANI WANAJADILI NINI KATIKA VIKAO VYAO.

5. HIVI JK AU PM WANATAKIWA WASIMAMIE UZIBAJI WA MASHIMO NA KUWEKA BALB KATIKA TAA ZA BARABARANI.WADAU NISAIDIENI,MAANA MIMI SIELEWI JIJI ,MADIWANI NA MAMEYA WETU WANASHUGHULI GANI HAPO DAR.
NAMSHUKURU YULE MFANYAKAZI WA POSTA ALIYESHUGHULIKIA KIFURUSHI TOKA U.S.A NA KIKAPATIKANA MAANA AMEWEKA 'DIFFERENCE' KWA MAISHA YA MTANZANIA.

SIJUI WENGINE WANAWAJIBIKA VIPI.

KIMITO

ONTARIO, CANADA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 05, 2007

    Hii inakera sana kwa kweli na sijui hayo maendeleoyatakujaje namna hii na still nimeona kwenye DARHOTWIRE jiji la Dar ndio ghali kuishi katika majiji hapo east africa.
    Na kwa nini watu nyumbani wanapenda saana kutumia dola kununua/kufanyia biashara Tanzania? huu kama si ulimbukeni ni nini tulionao huuu?
    Na kwa taarifa tuu kile kifurushi toka usa hakijafika bado,kilichopatikana ni cha jamaa kutoka malaysia nadhani.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 05, 2007

    meya wa dar hafahamu kwamba hiyo ni kazi yake kwa sababu anamanaibu wake ndio maana anakaa kimya akijua kwamba manaibu watafanya,kwa mfano meya wa ilala mtaa tu anao kaa ni mchafu kupita maelezo halafu kaanzisha mradi wa magari ya kuzoa taka,hizo gari zenyewe pia ni taka tosha halafu eti anazoa taka.sasa hizo hela za kununua hayo magari kazipata wapi kama sio kodi za wananchi?hapa maendeleo hakuna hata iweje,balb haziwekwi,mahandaki hayazibwi,na mitaro haizibuliwi.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 05, 2007

    Naungana na wewe kwa 100% nashindwa kuelewa huyu Meya wa Jiji anafanya shughuli gani jiji lote la Dar es Salaam limeharibika licha ya mahandaki, mifuniko yote iliyokuwa imebiwa kwenye mashimo ya kupitishia maji machafu haijarudishwa kila mahali upitapo mjini ni mashimo na haya ndio mojawapo yasababishayo follen zisizo na msingi. Pamoja na kwamba Tibaigana aliweka mkwara kwa wezi wote kurudisha mifuniko hiyo Meya hajachukua hatua yoyote pamoja na madiwani wake. Utamuona tu kwenye kipimajoto cha ITV kila siku kuzungumzia habari za wamachinga na usafikri wa daladala ndivyo alivyovishikia bango. Sijui nchi hii itafika wapi.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 05, 2007

    JK na PM wanapenda kufanya kila kitu. Kazi inayomhusu waziri fulani utaona rais au PM anaenda kufanya, sasa unategemea nini. Hii inawafanya watu wasijiamini, na hivyo kuamua kutofanya mpaka waambie. Na kwa kuwa wote wameingia madarakani kimtandao wananchi tuendelee kupata maumivu tu

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 05, 2007

    Anonymous wa June 5, 2007 11:52:00 naomba nikuunge mkono kama siyo mguu. Kweli hawa viongozi wetu wawili wakuu wanapenda kutoa maagizo kwa kila jambo hata jambo la kushughulikiwa na katibu kata! Wamezidi sana mpaka wanawatia uvivu watendaji wengine serikalini.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 05, 2007

    hayo mahandaki yako standby mkisikia vita msihangaike,

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 05, 2007

    Wenzenu wako bizi kutafuta vya kisasa: pazma ya kisasa, Tv ya kisasa, suti ya kisasa, soksi za kisasa, chupi za kisasa kwa wake na hawara zao, saa ya dhahabu ya kisasa, nk, ili waonekane hawavai vya Vingunguti...UKOGAJI!

    Utamkoga nani na wewe huvitengenezi?

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 05, 2007

    Haya yote ni matokeo ya uongozi wa rushwa. Wananchi hatuangalii competence na record ya kiongozi wakati wa kumchagua. Kweli Meya KIMBISA ni aibu kubwa. Jamaa ukimuona anaongea utadhani kichwani ni smart lakini wapi..very corrupt and irresponsible.

    Mwenyewe siamini kwamba PM au Raisi mpaka watoe directives ndo mambo yafanyike.Lakini inabidi wafanye kwa sababu Meya na watu wake ni kuiba tuu...wananchi tumechoka jamani..ibeni basi..lakini na sisi mtupe huduma..hata zile basic!
    Hawa mameya na madiwani....ni hopeless kabisa. Mi nadhani ndo maana wengine wanasema hivi vyeo vifutwe kabisa!

    Inasikitisha kuona kuwa watu hawawezi kuwa creative kwa vitu vidogo kama hivi ambavyo vina usumbufu katika maisha ya mtu wa kawaida ya kila siku. Its absurd. Harafu ukiangalia hawa hawa wanashinda ulaya..kufanya nini? ziara za kujifunza! wanajifunza nini? mimi na wewe hatujui!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 05, 2007

    asante sana mdau kwa kuleta hii mada nyeti.

    Mie nimetoka bongo hivi karibuni-swala la barabara kuu (main roads) wamejitahidi sana-tatizo kubwa lipo kwenye barabara za uchochoroni.Mnashangaa hako "kahandaki" hebu tembeleeni kwenye vitongoji mbalimbali mfano mlalakuwa, mikocheni, mwenge n.k., mtashanagaa wenyewe,Buguruni etc.

    Ukiwa dar barabara kubwa mfano Morogoro Rd, Ali Hassan, etc-kwa kweli ni nzuri lakini ukishachepuka kutoka kwenye hizo barabara hapo ndio utaona "mahandaki ya kweli".

    Swali langu zaidi ya hizo barabara kuu-je nani anahusika na kushughulikia barabara za uchochoroni-yaani zile zinazoenda kwenye maeneo ya watu wanapoishi (residential areas)?? wananchi wenyewe au Jiji??
    Michuzi hebu piga picha jinsi barabara zilivyo kwenye residential areas...

    ReplyDelete
  10. Mimi kinachonishangaza zaidi kuhusu huyu meya ni sfari zake za mara kwa mara katika majiji ya nchi za wenzetu kujifunza na kujipatia uzoefu katika uendeshaji wa majiji lakini kumbe hizo sfari ni miradi ya kujineemesha wao wenyewe!!!!!!!!!!!

    Anyway,labda kwasasa amejikita zaidi katika mchakato wa uchaguzi ndani ya chama au labda majukumu aliyonayo katika Red cross which can not be an excuse kwani kama huwezi kitu bora ukae pembeni kuliko kuleta ubabaishaji kama walivyosema wenzangu hapo juu..

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 05, 2007

    Meya yupi manake siku hizi jiji limekuwa kuuuuuubwa ati, na ma-meya ni wengi........ila hata kama ni mmoja tu nina mfano mzuri wa meya mmjawapo nyumban kwake tu majani mpaka mlangoni sasa mahandaki atayaona ni kero kweli?Waswahili wanasema jitoe kijiti jichoni kwako mwenyewe kabla ya kutoa kibanzi kwa mwenzio.These guys need a major phsychological overhaul. Kama alivyosema mwingine kny comment yake hawa jamaa wakisafiri wanatizama nini? Au wanawaza 'shopping' tu?Waheshimiwa kama mnasoma hizi wala msichukie mjue Watanzania 'wa kawaida' tumechoka na mambo haya yasioleleweka.Wataalam wapo kuwatumia hamtaki, kulikoni????

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 06, 2007

    mkogaji pumba out of point kalale kama umelewa

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 06, 2007

    Watanzania wengi hatuelewi kwamba sisi ni nchi moja wapo ya nchi zinazoendelea. Kwa maana hiyo mambo yote bado yana kua. Unapolinganisha Dar es Salaam na jiji la London, Paris,or New York, you are absolutely wrong! Mimi niki tumia usafiri wa dala dala si tegemei kupata treatment ya Metro or city buses. Huku kwetu kuna mtu kabeba samaki, mwingine kikapu cha kuku etc. Uneshaona hayo Los Angeles?? Ni Watanzania na wanaendelea, wanajifunza. Maendeleo si kwa kazi ya radi, Tuwe na subira. We shall overcome. Hon. Kimbisa alishamuona babu yake akiwa Meya?? Si naye anajifunza? Tumsaidieni basi angalau kwa kusafisha sehemu zetu tunazoishi na kutotupa maganda ya machungwa na kupenga mafua barabarani bila hata aibu kidogo!! Guys come one, let's enroll our kids into schools!!!!Mungu ibariki Tanzania Na Africa.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 08, 2007

    Kwako Mheshimiwa Mstahiki Meya... Tafazali tupe maoni yako kuhusiana na hali halisi iliyoleta mjadala huu na pia maoni yetu hapa juu... Asent

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 10, 2007

    kaka michuzi hii sasa ni aibu sijawahi kuona lami inazibwa na kokoto kama unvyojua blogu yako inasomwa na watu wengi sana kwa kuonyesha utanzania naonba pata ushauri kutoka ERB engineer registered board kama ni suitable kuziba hizo pot hole kwa kokoto idea hii aliyoileta ni nani mwanasiasa au engineer tunaomba utusitiri kwani madhara yake ni makubwa woote tutakuwa wapumbavu kumuacha huyo pimbi aliyeruhusu au kuagiza hivyo kama ni kubana matumizi si bora wasinunue mashangingi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...