nafurahi na kushukuru kwamba wadau wameana kuleta picha mwanana tufaidi sote. huyu aliyeleta hii na huo ujumbe anaitwa agata anatokea kilimanjaro

Bwana Michuzi!
Najua vijana wetu wengi walio mamtoni wamesahau hata mgomba unafana vipi wape hiyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 21, 2007

    Nakumbuka nta/asali ya kwenye mgomba ilivyokuwa tamu enzi za utoto. nilikuwa naenda nyuma kwetu kwenye migomba na kula nta hiyo. Ni hayo maua meupe yanatoa asali mmmm...kuna mtu yoyote alikuwa analamba hiyo? Come on be honest...

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 21, 2007

    daa anony wa hapo juu umenikumbusha mbali sana, tena kwetu mbeya tukuyu, tulikuwa tunachomoa hivyo viua vina maji maji flani yenye sukari, basi mgomba ukianguka tu ili mradi na hivyo viua basi ilikuwa raha yetu kiukweli.

    ooh asante kwa picha nzuri

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 21, 2007

    Mi sijawahi kula lakini jamaa unaonyesha jinsi gani ulivyokuwa mmelo (mroho) kiasi cha kula hayo majani meupe toka kwenye mgomba.
    Hata China nao hivi sasa wamekiri kwamba ulaji wa wanyama wenye sumu kali kama nyoka, nge, kenge au kula maua, si kwa sababu ni asili yao bali ilitokana na njaa kali. Na wewe anonymous wa hapo juu nadhani ni mmoja wao

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 21, 2007

    Nta hiyo nami nilisha nyonya...he he, ila inabidi uwe makini, saa nyingine unakutana na inzi au sisimizi wamefia humo humo baada ya kuzidiwa uroda!!

    Kuhusu picha,ni bomba, ila ingekuwa bomba zaidi kama mpigaji ange onyesha kishina cha mkungu huo, kwani bado ingelikuwa inaonekana kwa ukaribu tu pia.

    SteveD.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 21, 2007

    Hii ni kuhusu maoni yako wewe anon wa saa 11:49 AM EAT, sidhani kama umefanya uchunguzi wowote kabla ya kuyatoa. hata hivyo sito kulaumu kwani ni haki yako.

    Hata hivyo basi nakuomba ukumbuke Tanzania kuna hao kenge,mijusi,fukufuku,nyoka,fisi,n.k. kwanini watu kwa wingi hawali hao viumbe?!... pia kwa mantiki hiyo hiyo, huko japan watu wanakula karibu kila aina ya kiumbe na juzi juzi tu waling'ang'ania waruhusiwe kula nyangumi! italy wanakula farasi,vicheche n.k. je wananjaa au ni waroho kama usemavyo wewe.

    naomba utoe link ya hiyo habari hapa.

    watu wanakula senene,madafu,kumbikumbi n.k. ni kutokana na kuwa vitu hivyo vinalika, haviwadhuru,au kwa ajili ya imani, pia vitu hivyo vinapatikana kwa wakati huo au kwa ajili ya udadisi tu.

    pia nakuomba ututajie angalau vichache unavyo ona si vyakula vya kiroho au njaa kama uonavyo wewe...

    Ahsante. SteveD.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 21, 2007

    Anita umenikumbusha mbali. Huyo anayesema kula hiyo nta ni njaa hajui alisemalo. Hiyo ilikua one of the thing to do on our list tukiwa wadogo tunaenda kwa bibi.

    Wow those were the days....

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 22, 2007

    Hiyo nyekundu inayotoa maua na hatimae ndizi inaitwaje kwa kiswahili?

    ReplyDelete
  8. Sisi tulioko ughaibuni hatuwezi kusahau mgomba ulivyo labda mtu awe hajauona mgomba kabla.Ila twashukuru kwa vile watoto wa baadhi yetu kweli wanahitaji kuona mgomba ulivyo.
    Asante sana kwa kutukumbuka kwa hilo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...