Home
Unlabelled
mkungu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Nakumbuka nta/asali ya kwenye mgomba ilivyokuwa tamu enzi za utoto. nilikuwa naenda nyuma kwetu kwenye migomba na kula nta hiyo. Ni hayo maua meupe yanatoa asali mmmm...kuna mtu yoyote alikuwa analamba hiyo? Come on be honest...
ReplyDeletedaa anony wa hapo juu umenikumbusha mbali sana, tena kwetu mbeya tukuyu, tulikuwa tunachomoa hivyo viua vina maji maji flani yenye sukari, basi mgomba ukianguka tu ili mradi na hivyo viua basi ilikuwa raha yetu kiukweli.
ReplyDeleteooh asante kwa picha nzuri
Mi sijawahi kula lakini jamaa unaonyesha jinsi gani ulivyokuwa mmelo (mroho) kiasi cha kula hayo majani meupe toka kwenye mgomba.
ReplyDeleteHata China nao hivi sasa wamekiri kwamba ulaji wa wanyama wenye sumu kali kama nyoka, nge, kenge au kula maua, si kwa sababu ni asili yao bali ilitokana na njaa kali. Na wewe anonymous wa hapo juu nadhani ni mmoja wao
Nta hiyo nami nilisha nyonya...he he, ila inabidi uwe makini, saa nyingine unakutana na inzi au sisimizi wamefia humo humo baada ya kuzidiwa uroda!!
ReplyDeleteKuhusu picha,ni bomba, ila ingekuwa bomba zaidi kama mpigaji ange onyesha kishina cha mkungu huo, kwani bado ingelikuwa inaonekana kwa ukaribu tu pia.
SteveD.
Hii ni kuhusu maoni yako wewe anon wa saa 11:49 AM EAT, sidhani kama umefanya uchunguzi wowote kabla ya kuyatoa. hata hivyo sito kulaumu kwani ni haki yako.
ReplyDeleteHata hivyo basi nakuomba ukumbuke Tanzania kuna hao kenge,mijusi,fukufuku,nyoka,fisi,n.k. kwanini watu kwa wingi hawali hao viumbe?!... pia kwa mantiki hiyo hiyo, huko japan watu wanakula karibu kila aina ya kiumbe na juzi juzi tu waling'ang'ania waruhusiwe kula nyangumi! italy wanakula farasi,vicheche n.k. je wananjaa au ni waroho kama usemavyo wewe.
naomba utoe link ya hiyo habari hapa.
watu wanakula senene,madafu,kumbikumbi n.k. ni kutokana na kuwa vitu hivyo vinalika, haviwadhuru,au kwa ajili ya imani, pia vitu hivyo vinapatikana kwa wakati huo au kwa ajili ya udadisi tu.
pia nakuomba ututajie angalau vichache unavyo ona si vyakula vya kiroho au njaa kama uonavyo wewe...
Ahsante. SteveD.
Anita umenikumbusha mbali. Huyo anayesema kula hiyo nta ni njaa hajui alisemalo. Hiyo ilikua one of the thing to do on our list tukiwa wadogo tunaenda kwa bibi.
ReplyDeleteWow those were the days....
Hiyo nyekundu inayotoa maua na hatimae ndizi inaitwaje kwa kiswahili?
ReplyDeleteSisi tulioko ughaibuni hatuwezi kusahau mgomba ulivyo labda mtu awe hajauona mgomba kabla.Ila twashukuru kwa vile watoto wa baadhi yetu kweli wanahitaji kuona mgomba ulivyo.
ReplyDeleteAsante sana kwa kutukumbuka kwa hilo.