mkurugenzi mkuu wa clouds 88.4 fm pamoja na prime time promotions jesph kussaga akimkabidhi zeze na ngoma jah rule ofisini kwake mara alipotua jijini dar kwa onesho la fiesta 2006. kuna tetesi kuwa safari hii tena atashuka mwingine saizi ya jah ruyle kutumbuiza ndani ya tamasha la fiesta 2007 mwezi ujao. stei tyuund....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 06, 2007

    Si walisema Fiesta ya 2006 ni la mwisho? Sasa lipo tena?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 06, 2007

    MICHU PELEKA HUU UJUMBE CLOUDS. NI HIVI, SIKU HIZI POWER BREAKFAST HAINOGI TENA KAMA ZAMANI. TIMU YA WATU WATATU ILIKUWA NI FINA, GERALD NA MASUDI KIPANYA. SASA SIKU HIZI UNAKUTA MARA MASUDI HAYUPO MARA GERALD KACHELEWA MARA SIJUI KUNA WATU GANI AMBAO KWA SAUTI TU HAWAVUTII. MFANO HUYO BONGE WA SASA, SINA HAKIKA KAMA UNAUSIKIVU MZURI MASIKIONI MWA WATU. WAJARIBU KUFANYA UCHUNGUZI JUU YA HILO.HALAFU SIKU HIZI MNAOGOPA KUSSEMA VITU DIRECT SIJUI KWA NINI AU SERIKALI ILIWAPIGA MKWALA? MI ZAMANI POWERBREAKFAST NILIKUWA NAITUMIA KAMA SEHEMU YANGU YA KUNIJULISHA TANZANIA KUMETOKEA NINI LAKINI SASA KILA NIKITEGA SIKIO NAKUTA MNALIMUMUNYAMUMUNYA TUU JAMBO. ANGALIENI MSIJE MKAPOTEZA UMAARUFU WENU. CLOUUUUUUUUUUDDDZZZZZZZZZ FMMMMMMMMMMMMMM.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 06, 2007

    Mnaosikiliza hii redio kwenye net manasikilizia wapi? Niliwahi kuipata mara moja tu kwenye bongo5 lakini nilibahatika mara mbili tu . Baada ya hapo haifunguki tena.

    Naomba mnieleze au kuna redio nyingne ya Tanzania inayosikika kwenye internet? Radio ya talk shows and news sio ya misiki tuuuuu. Miziki nasikiliza kwenye mahusiano.com na hiyo inanitosha kabisa

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 06, 2007

    Kazi ipo kama wanajisahau wakasema 2006 ndio mwisho wa Fiesta inakuwaje tena au kuna utamu gani?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 07, 2007

    radio maria tanzania inapatikana live, ni radio ya dini, 1100 na 1800 hours GMT inajiunga na radio tanzania dsm kwa taarifa ya habari

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 07, 2007

    naomba hiyo website ya radio maria. Nimegoogle zinakuja maeleze ya huku niliko tu...sioni hiyo yao. Thanks

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 08, 2007

    www.radiomariatanzania.co.tz

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 08, 2007

    WEYE MICHUZI NINI NOMA SANA , TUMETOA MAONI YETU NYETI NA WALA SI MABAYA .. UMEAMUA KUMINYA HUKUYAPUBLISH. NDIO MAANA WADAU WENGINE TULIONA HAPA BULOGUNI WANASEMA UNAPENDELEA WATU KAZAA. HASA HAO WAKURUGENZI TULIOWATAJA

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 08, 2007

    Jamani mkumbuke michuzi hawezi kuweka kila comment kwa vile anafanya kazi serikalini..
    Pili anaishi tanzania
    tatu mnataka aweke kila maoni akipotea mtamuuliza nani?

    Mnajua nchi yetu ukiwasema vigogo unatumiwa popobawa ..

    Tanzania tunajidai nchi ya demcrasy lakini bado sijui ni ucommunist au ni kabepari kadogo tu hako kanchi kwtu there is NO FREEDOM OF SPEECH AT ALL.

    Watu ni waoga oga tu...heshima nyingi za kinafiki tu

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 08, 2007

    Asante sana sana.....

    sasa kama radio maria kwanza ya dini wanaweza kurusha habari zao kwenye mtandaonini kinaowashinda hao wengine? Wangejua ulimwengu wa leo ni wa mtandao...

    ReplyDelete
  11. Jamani Joseph umevimbaa...!angalia usipate maradhi mwenzangu,japo najua mawazo ya huko bongo kuwa mtu ukiwa na wadhifa lazima uvimbe!Fanya mazoezi si nasikia Dar kuna gym tele.Au agiza vifaa vya gym toka kwa jamaa zako abroad.
    Hata hivyo hongera sana umeendelea sana.
    Good luck!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...