wadau wanaendelea kututumia picha toka kila pembe. safari hii ni kijijicha mlangali, iringa, ilioletwa na obeid mgina aliye bulyanhulu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 21, 2007

    Mi naomba nitoe shilingi, hii sio sio IR labda tuelezwe vizuri ni sehemu gani.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 21, 2007

    aisee jamaa ananikumbusha mbali. hicho kijiji kinaitwa MALANGALI, sio Mlangali. Kipo njiani kuelekea Kidamali ambako pia kuna kiwanda cha "Maji Afrika". Ni njia hiyo hiyo pia inayokwenda mbuga ya taifa ya Ruaha.

    Sijui wale wagiriki wanaolima tumbaku Malangali bado wapo? Jamaa wanakata sana miti na kuua watu kwa kuwafanyisha kazi katika mazingira mabovu sana. Yaani wanaokausha hizo tumbaku wamesinyaa kwa moshi wa tumbaku, na wanaishi kama watumwa enzi za ukoloni. JK hebu wamulike hawa jamaa

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 21, 2007

    Michuzi hii sio MALANGALI Kweli?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 21, 2007

    NICE VIEW OOOOH!!!!!!!!!!!!!!!! LALALAAAAAA

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 21, 2007

    Aisee.. udenda unanitoka jinsi picha inavyo onyesha kimadhubuti hicho kijiji, shule, mashamba,kanisa n.k. truly postcard picture!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 21, 2007

    Jamani wala Michuzi na huyo mdau aliyeleta picha naye hajakosea, hicho ni kijiji cha MLANGALI na si MALANGALI, Kijiji hicho kama sijakosea kipo wilaya ya Njombe au Ludewa, lakini nina uhakika kuwa barabara ya kwenda Ludewa kwao marehemu Kolimba inapitia hapo, mimi binafsi nimefika katika Kijiji hicho. Na huyo jamaa aliyetuma picha hiyo yeye ni mzaliwa wa kijiji hicho.

    Obeid asante sana kwa kunikumbusha wakati nilipokuja kuhani msiba wa Mama.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 21, 2007

    Michuzi umenikumbusha kwetu i swear!!.....Nimeshaanza patwa na home sickness wow!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 22, 2007

    Asanteni sana yaani mnatufurahisha sana na kukumbusha mbali. Unajua tena ukishaishi huku ukija bongo sana sana you can afford ni for week na hizo four week ni baada ya miaka miwili au zaidi kuna sehemu nyingine hata iweje hatutaweza kuziona kabisa

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 22, 2007

    Malangali ni kijiji alichozaliwa mama yangu mzazi duh...nimeliona hilo kanisa la Lutheran ni la zamani sana.Hapo ndipo Isimikinyi bwana!!!
    Heko Michuzi

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 22, 2007

    stress free life.

    Unalala na kuamka wala hamna anyekudai bili ya umeme, maji, simu, motgage, bima ya nyumba na sehemu hizo wala bima ya mafuriko wasingeijua, security alarm hata hawaijui manake wote wanaaminiana...

    na hewa hapo ni so fresh

    Miss that life

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 22, 2007

    Sasa ngoja niwaeleze. Mimi nimezaliwa hapo Mlangali, nimekulia hapo MLANGALI na nikacheza mpira hapo Mlangali na timu moja iliyoitwa BADO SPORTS CLUB na kuwa mabingwa wa soka wa wilaya ya LUDEWA mwaka 1990. Mimi ndo yule kocha wao (Kocha KULANAO). Kanisa lionekanalo hapo ni ANGLIKAN na wala si Lutherani, kwa mbali ni Jengo la ustawi wa jamii (Jengo la LISHE) na kwambele yake ni Kituo cha Afya cha Mlangali. Milima yote hapo Mlangali ilikuwa mali ya akina MTIMAVALYE. Asante mdogo wangu Obed. Yune Ambwene Lunyamacho Mtimavalye Mgaya, somewhere in Europe, nitakuwa Mlangali mwishoni mwa July.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 22, 2007

    HAPO WOTE MMEKOSEA INAONEKANA MNABABAIKA NA HAYO MAJINA MAWILI NA MIMI NAWASAWAZISHA. MLINGALI NI KITONGOJI KIDOGO CHA IRINGA MJINI,UNAPITA MLANGALI UKIWA UNAENDA KIWANDA CHA MAJI.KUTOKA IRINGA MJINI(MANISPAA)KINAANZA KITONGOJI CHA MIYOMBONI,MSHINDO,MLANDEGE,MLANGALI,KIODOMBI UNAMALIZIA NA ITAMBA. MALANGALI NI KIJIJI NJIA YA KWENDA MBEYA UKISHAPITA MUFINDI. KUNA NJIA PANDA INAELEKEA HUKO NI KUNA MWENDO MREFU KUTOKA HIGHWAY.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 31, 2007

    WAAA DU NIMEFURAHI SAAANA JAMANI HAPO NI KUNYUMBA HAPO. NI MAHALI PAITWAPO MLANGALI SIO MALANGALI. NI KWA WAPANGWA ORIGINAL HAPO TUHONGICHE SANAAA. NI NJIANI KUELEKEA KWETU KABISA MAWENGI DU CHOZI LANITOKA MICHUZI NIKIKUMBUKA MAWENGI DU ULANJI DU . WAKINA LUNYAMACHO WOTE MPO PLEASE NAMIMI NI LUNYAMACHO MY ADD NI MLunya@hotmail.com

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 31, 2007

    WAAA DU NIMEFURAHI SAAANA JAMANI HAPO NI KUNYUMBA HAPO. NI MAHALI PAITWAPO MLANGALI SIO MALANGALI. NI KWA WAPANGWA ORIGINAL HAPO TUHONGICHE SANAAA. NI NJIANI KUELEKEA KWETU KABISA MAWENGI DU CHOZI LANITOKA MICHUZI NIKIKUMBUKA MAWENGI DU ULANJI DU . WAKINA LUNYAMACHO WOTE MPO PLEASE NAMIMI NI LUNYAMACHO MY ADD NI MLunya@hotmail.com

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...