mhariri wa gazeti la msemakweli akiuliza maswali juzi jk alipokutana na wahariri ikulu. jk alitangaza pia kwamba kuna tovuti http://www.jakayakikwete.com/tanzania ambayo inampa ruksa kila mmbongo kuuliza swali kwake ama kutoa kero inayomsibu na kuahidi kutoa majibu chap chap

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 09, 2007

    Hiyo si ndio ile tovuti waliyoikana siku za karibuni na watu kuanza kumtupia mawe bwana mdogo Mike Shirima?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 09, 2007

    Michuzi tovuti za kutoa kero bado haziko hewani. Zitakuwa za serikali na anuani zake ni kama ifuatavyo
    www.mwananchi.go.tz na
    www.kero.go.tz

    Hiyo jakayakikwete.com ni tovuti ya mtu binafsi siyo ya umma inawezekanaje maoni ya wananchi yapitie kwenye tovuti binafsi

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 09, 2007

    kumbe haka kajamaa nako ni ka*hariri* duuuu..

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 09, 2007

    Jamani jamani hivi mbona uraisi unashushwa hadhi hivyo? Urais ni taasisi na sio mtu. Sasa tuna JakayaKikwete.com na Statehouse.go.tz ni upuuzi gani huu?

    Nina uhakika watu wa PR wa Raisi wamepitwa kushoto kidogo na maswala ya IT, lakini hio isiwe sababu ya kufanya mambo kiholela. Kama wamependa uendeshaji wa website anaofanya Webmaster wa JakayaKikwete.com basi si wampe tu ajira ya kuendesha StateHouse.go.tz (ambayo ndio website ya kiofisi zaidi).

    Na kama Kikwete kama Kikwete anataka kuendeleza u-popularist wake basi afunguliwe www.jakayakikwete.go.tz

    Ikumbukwe kuwa domaini ya serikali ya jamhuri wa muungano wa tanzania ni ".go.tz". na sio ".com" ambayo ni domaini ya kibiashara

    Kwa mtazamo wangu kutumia .com kunashusha hadhi ya Rais na hadhi ya Tanzania. Tanzania inabidi iwe kwenye .tz ili kuimarisha taswira yake kwenye mtandao.

    Kaanzeni upya nyie watu wa PR wa Rais. Hapa Mumechemsha

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 09, 2007

    Michuzi, muombe bwana Makwaiya(MK) akusaidie kutoa hiyo nafasi tupu hapo juu.. naona unapoteza sehemu ya picha kama mbili hivi. Kama utashindwa tuombe tukusaidie.

    Kingine, kama inawezekana pia,mwombe akuwekee navigation bar chini ya kurasa kwa ajili ya blog zilizopita, ili iwe rahisi kuzipitia mtu akisha scroll mpaka chini. By the way, blog yako is the most visited site in Tanzania according to google takwimu. Hongera! SteveD.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 09, 2007

    Nchi hii Wasomi wengi wamejazana katika sehemu ambazo zinaleta umaskini kwao na kwa watanzania.

    Elimu inabidi ipambane na Mazingira.Tanzania elimu hiyo hatuna ya kutosha.

    Sehemu kubwa ya wasomi wetu wamejazana katika sekta ambayo kitaalamu inajulikana kama sekta ya kuandika (WRITTING SECTOR). Sekta ambayo kwa sehemu kubwa inatumia kalamu,peni,komputa, makaratasi katika utendaji wa kazi za kila siku.

    Hakuna nchi yoyote duniani ambayo imeedelea kwa kutegemea sekta ya kuandika.Mjapani mmoja aliwahi kuniuliza akasema karibu kila duka ninalopita miotaani huwa linauza peni za kuandikia hivi watanzania huwa mnaandika nini? Inaonyesha peni ni bidhaa muhimu sana hapa kwenu!Kuna waandishi wengi sana wenye vitu vingi sana vya kuandika!!!

    Mazingira yetu ni ya Kilimo,Ufugaji,,Madini na Biashara.Ungetarajia wasomi wengi wawe wamejazana katika fani hizo na vyuo na shule zetu zijazane katika mkondo huo.Lakini wengi wa wasomi wamejazaana katika digrii za Sanaa.Bachelor/Masters etc of Arts akiwemo Raisi wetu.Na arts ni sanaa na anaye-practice arts ni artist au msanii.Kwa hiyo nchi yetu imejaa wasanii wengi sana wanaotoka vyuo vikuu.

    Lakini utakuta Kilimo ambacho ndio kinaitwa uti wa mgongo wa Tanzania kinaendeshwa unaendeshwa na watu waliomaliza darasa la saba au ambao hawakusoma kabisa.

    Sasa kunakuwa na mgongano wa sera na vitendo. Nchi inasema inategemea kilimo hivyo ungetegemea mkazo uende huko wa kielimu lakini unakuta mkazo hauendi huko unakazia kuzalisha wasanii waliojaa digrii za sanaa.Nchi haiwezi endelea kwa kutegemea bachelor,Masters,au Doctors of arts.Nchi siyo sawa na chuo cha sanaa bagamoyo.

    Nyerere aliwahi kusema wasomi wakiingia katika kilimo, kilimo kitabadilika.Na kweli tumeanza kuona sekta kama za ufugaji kuku ambayo wasomi mijini wanaufanya kuna mabadiliko. Ilikuwa si rahisi kuona mtu akiwa anafuga kuku 1000 lakini sasa ni kitu cha kawaida.

    kwenye upande mwingine Mazingira yetu yana madini.Sasa ungetarajia ungetarajia kuona vyuo kibao vya madini hata vya VETA kama vile vya kufundisha kutengeneza vidani,n.k Lakini unakuta watu wanafundishwa umakenika wa magari ya Wajapani!!! (Import Oriented Education)na utengenezaji mashine za kutoka nje ya nchi!

    Matokeo yake madini tunayo elimu ya madini hatuna wala haipewi kipaumbele! Wakati madini ndiyo yako kwenye mazingira yetu na Elimu tupewayo ilistahili iwe ile ya kutusaidia kuyashughulikia mazingira ya madini ili tuondokane na umaskini.

    Biashara ni eneo lingine ambalo lingetiliwa mkazo lakini bahati mbaya Wafanyabiashara wengi wazawa ni darasa la saba na waliofeli sekondari.Wakati sekta hii ni pana na muhimu mno katika uchumi.

    Upande Wa Biashara umebakia mikononi mwa wahindi kwa kuwa wamegundua siri ya Kusoma.Hivyo wengi wao wamesomea biashara barabara ndiyo maana wanawashinda wafanyabiashra waswahili ambao kusoma wanaona kama kituo cha polisi. Kutwa wafanyabiashara wetu wanashinda kwa waganga wa kienyeji!

    Umaskini ni mkubwa Tanzania sababu elimu hii yetu ni mbovu sana haisaidii mtu apambane na mazingira.

    Mfano uuna Pamba kwenye mazingira yetu ungetarajia watu wengi wawe wamesomea mambo kilimo cha pamba,utengenezajinyuzi na nguo na mambo ya viwanda vidogo na vikubwa vya vitumiavyo pamba.Lakini unakuta elimu hiyo haipo watu wamekazana kuandika na mashule yanaendelea kuzalisha wasanii wa masomo ya arts.

    Nikiwa mkereketwa wa maendeleo ya nchi yangu naomba mfumo wa Elimu na mkazo wake ubadilike.Elimu Iwezeshe mtu kuwa na uwezo wa kupambana na mazingira na kuibuka toka kuwa maskini na kuwa tajiri.

    Na ili hili liwezekane elimu bora inayoshughulikia mazingira ni muhimu sana.

    Kama hatutawapa watu wetu elimu ya kuwasaidia kushughuklikia mazingira tutaendelea kuona wageni wakija wakichukua hizo fursa na sisi tutabaki tumetoa macho na kuishia kuwa maskini.

    Napendekeza wapanga sera badilisheni mfumo wa elimu ulenge hasa kwenye kilimo,ufugaji,Madini na Biashara,Na viwanda vidogovidogo vya bidhaa na mazao ya madini kama vidani n.k Tuwe na wakulima wengi wasomi badala ya kuwa na maafisa kilimo wengi wasomi.

    Ili nchi yetu iendelee haitoshi nchi kuwa na maofisa biashara wa serikali wengi wasomi bali nchi inahitaji wafanyabiashara wengi wasomi,pia nchi ili iendelee haihitaji tu maofisa wa madini wa serikali wengi wasomi bali inahitaji wachimba madini wengi wasomi.

    Hayo ndiyo maoni yangu. Wanakijiji mnaruhusiwa kutumia ninayoandika popote.Naona wengine wananiandikia kuomba ruksa kwenye mail yangu.

    Natoa ruksa ya jumla.Ukitaka kutumia makala zangu tumia tu popote upendapo.Niwe nakujua au sikujui ruksa.

    Asanteni


    koloboi@yahoo.com

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 10, 2007

    wewe koloboi ni mpuuzi. hivi unajua kila fani ni muhimu? na kwa taarifa yako unapoanzisha biashara ni lazima ujue masoko yako wapi. Sasa unafikiri bila watu kusomea biashara watawezaje kupata mbinu za kutafuta masoko? Bila masoko ndio utakuwa katika hali tuliyo nayo sasa kwamba tunalima mazao mengi lakini yanaishia kuoza kwa sababu hakuna wajanja walioplan kuyapeleka sokoni kitaalamu

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 10, 2007

    Weee Koloboi jinga kabisa na umeongea pumba sana,yaani mie nikasomee kilimo wakati mwenzangu kasoma Arts na ameajiriwa TRA na kila siku anakomba rushwa halafu unataka mie niende nikakae kijijini kwa vile tu naipenda nchi yangu,kwenda kule haipo kila mtu anataka maisha mazuri ndo maana wengine wananunua rada na madeal fake ya richmonduli.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 10, 2007

    Koloboi hongera na mimi nakuunga mkono una mawazo mapya.

    Ungekuwa huku Marekani ungelipwa mamilioni mtu kama wewe.Sababu watu na serikali hutafuta sana independent thinkers wanaoweza toa mawazo mapya yenye mwelekeo mpya.

    Tanzania wasanii wengi mno wanatisha!

    Mimi naona tofauti ya Chuo Cha Sanaa Bagamoyo na vyuo vingine hapo Tanzania NI:

    1.Chuo cha Sanaa Bagamoyo hutoa wasanii wa kiwango cha Cheti wakati vyuo vikuu vinapigilia msumari kwa kutoa wasanii wa kiwango cha digrii.

    2.Wakati wasanii toka Chuo Cha Sanaa bagamoyo huendesha usanii wao kwenye kumbi za Starehe,Wasanii wenye digrii za sanaa huendesha usanii wao kwenye maofisi ya serikali ambaye ndiye mwajiri mkubwa wa hao wasanii.

    Lakini wote ni wasanii.Ndiyo maana nchhi hii haiendelei na hadi wengine tukaone tuikimbie! Usanii mwingi sana iwe kwenye Siasa,Tenda,Serikalini n.k

    Koloboi kama huko Tanzania hawakutaki kukusikiliza nitawasiliana na wewe njoo huku mwanangu.Huko wasanii hao hawawezi kukusikiliza.Nitakuandikia kwenye E-Mail yako hapa siwezi weka e-mail yangu.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 10, 2007

    Tatizo la hii nchi haijawahi kupata mwanasayansi akawa Raisi au waziri mkuu.

    Watu wa Sayansi ni watu serious hawapendi porojo kama watu wa arts! Nadhani nchi sasa ifike mahali angalau ijaribu wanasayansi ambao hawajasomea hayo masomo ya porojo tuone nini kitatokea.

    Wasanii wa arts mmetawala nchi hii muda mrefu mno na hatuoni matokeo.Ni porojo tu! Na usanii usioisha! Wekeni wanasayansi wengi na watambueni na kuwalipa vizuri zaidi kuliko watu wa sanaa muone kivumbi cha maendeleo!

    Lakini kama trend ya Kuendelea kuthamini wasanii ikiendelea watu watakimbia sayansi na kujazana kwenye sanaa baadaye taifa litajikuta hata mgawa vidonge itabidi aagizwe nje ya nchi.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 11, 2007

    Tatizo la huyu Rais wenu anaongoza kwa kutumia "majungu" yaani watu leo wanasema nini na yeye ndio anakurupuka kujibu au kufanyia kazi.

    Anatakiwa awe na serikali yenye dira na yenye mtazamo wa kututo sehemu moja na kutupeleka sehemu nyingine bila ya kusikiliza pet rumours za mtaani.

    I think the guy is not serious, a total mismatch na "chinga". Hata hotuba zake za mwezi ni upumbafuu mtu. Eti Rais anatangaza matangazo madogo madogo kama ya Ukimwi kupima, eti utoro shule ya msingi huku akiwa na baraza la mawaziri 60 ??

    Ninakerwa sana.

    Jafar

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 11, 2007

    Anon wa June 11, 2007 10:59:00 AM EAT ninakubaliana nawe, lakini ukimwi ni swala kubwa inabidi aliongelee ila utoro wa shule na mimba amechemsha. Sheria za kuwapa mimba watotot wadogo zipo tayari kwenye vitabu tatizo ni law inforcement. Na kama sheria hazitoshi ni swala la bunge kutunga sheria zaidi kutokana na wakati. Haina haja ya rais kwenda jukwaani kurudia rudia mambo wakati wahusika wapo, wanafanya nini? FIRE THEM!

    Tatizo la viongozi wetu inaelekea hawajui kudelegate majukumu yao. Wanataka wafanye kila kitu matokeo yake kazi inakuwa ngumu kutekeleza, at the end of the day, they accomplish little or nothing.

    Mr. President, please get serious a lil' bit. People who elected you expect more rather than less, sooner rather than later.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...