

WATU WAWILI INASADIKIWA WAMEKUFA NA TAKRIBAN 30 HIVI WAMEJERUHIWA BAADA YA BOMU KULIOPUKA JIJINI NAIROBI MILANGO YA SAA 2 ASUBUHI LEO KARIBU NA HOTELI YA AMBASSADOR ILIYOKO MTAA WA MOI AVENUE. KAMA KAWAIDA GLOBU YENU HII IMESHAPATA SNEPU AMBAPO JUU NI MOJA YA MAITI IKIINGIZWA GARINI NA CHINI NI UMATI WA WATU UKIUSHUHUDIA VARANGATI. HADI NAPOSTI HII HAKUNA UHAKIKA KWAMBA HILO BOMU NI LA KUJITOA MUHANGA AMA NAMNA GANI. ILA INASEMEKANA KUNA JAMAA ALIZUIWA NA WALINZI KUINGIA HOTELINI KUTOKANA NA KUVAA KIAJABU AJABU HIVYO ALIPORUDI CHUMA KIKALIA.
EH MUNGU IFUNIKE TANZANIA KWA DAMU YA YESU!!!!!!!!!
ReplyDeleteWABONGO KAENI MACHO! Kama wameanza upuuzi huo Nairobi na Dar lazima watajaribu. Bora usalama Kenya unafanya kazi maana angeingia ndani ya hiyo hoteli wangekufa watu zaidi.
ReplyDeletemungiki hao, na hii ni kugombea keki ya taifa jamaa wamepigwa stop kupiga debe matatu. hii inatoka na watu kukata tamaa ya maisha anaona bora kufa tu.
ReplyDeleteSasa na wafalme wetu bongo wafunguke masikio sio kuwaandama wamachinga na wapiga debe bila kutafuta ufumbuzi wa jinsi ya kuwawezesha nao angalau waambulie hata chenga za keki ya taifa. Wakikata tamaa hao ni salaha kali kuliko nyuklia, MUNGU IEPUSHE TANZANIA watu waishi kwa matumaini.
wewe unaewatupia zigo wapiga debe matatu ndo inabidi ufunguke kichwa, ubongo umeweka tope, very shallow thinking.
ReplyDeleteMichuzi Unalripoti ya Nairobi unaacha ya Dar Es salaam!
ReplyDeleteAliyekuwa mkurugenzi wa Uhamiaji kwa Muda mrefu Herbert Chilambo kafariki kwa kile kinachoitwa ajali!!!! Hivi kafa au kauawa na mamluki............
Nairobi wanatuhumiwa wasomali toka Somalia isejekuwa na Chilambo naye kauawa na mamluki wa kisomali ambao uraia wao una utata!!
Wewe ndio shallow thinking hujui adhari ya kunyanyaswa.yeye katumia tu mfano wanaoteseka bongo ni wengi wanaofaidi wachache. Ipo siku watu watachoka na ahadi. Hapo...
ReplyDeletedamu ya yesu ifunike taifa letu la tanzania,jamani mnaona lakini bado mnataka shirikisho!watanzania tuliangalie kwa kina maana huko kwa wenzetu mh!mungu tusaidie
ReplyDeletehapo Michuzi unanifurahisha, unaonyesha namna gani upo aputudeti na blog yako, yani zile habari motomoto kabla hazijapoa ushazirusha kwa wanablogu wako,! Safi sana! keep it up!Mungu Boresha AMANi AFrica Mashariki na Dunia Nzima Amen.
ReplyDeleteKwa style hii inabidi kujiunga na shirikisho tufikirie mara mbili mbili maana sijui itakuwaje maana najua hali kama hii tuliisha wahi kui-experience mara moja tu ambapo ni ubalozi wa marekani tanzania uli lipuliwa MUNGU IBARIKI TANZANIA
ReplyDeleteAnon 9:03
ReplyDeleteMasahihisho, Herbert Chilambo hakuwa Mkurugenzi wa Uhamiaji ila ni msemaji wa Uhamiaji. Hakuwahi kuwa Mkurugenzi wa Uhamiaji.
ANON WA 4:35 AM EAT,
ReplyDeleteM brain Thinks 300K more than yours. kama ungekuwa fast and accurate critisizer usingerukia gari kwa mbele. Soma nilichoandika elewa halafu ndio critisize tena sio kwa destructive but constructive critisization. Iam a free man to give up my views regardless will be against your shrinked brain and Low IQ. Remember always try to think and analyse before typing critical comments, otherwise it's going to turn agaist you
Mi najua wewe utakuwa ni mmoja wa watunga sera ambao kila siku mnafikiria kujizidishia ninyi na kuwakamua wabongo sasa nakwambia beware, msipo badili mtazamo, sooner or later things will be worse.
michuzi, picha ya maiti inayobuluzwa ya nini kwenye blogu?
ReplyDeletekwa hiyo ili bomu limepigwa na watuwaliochoka kunyanyaswa !? duh ! ...kweli wameonyesha kuwa wamechoka kunyanyaswa, ujumbe umefika .
ReplyDeletemkikubali shirikisho na hivi vitu lazima mvikubali kwa sababu silaha zitakuwa nje nje tu.
ReplyDeletema anonymous mnaosema watuwakichoka au kunyanyaswa watafanya hivi acheni unafiki.
ReplyDeletejisemee wewe kuwa ipo siku utafanya hivi kwa vile umechoka kunyanyaswa, usipandikize akili yako kwa wengine. ....inawezekana mpo wengi wenye mpango wakujilipua kwa sababu ya kuchoka na maisha,
si sahihi kusema watu wata...., sema mimi fulani ntafanya ... ,ukijilipua shauri yako,kama unadhani utakuwa umesaidia watoto wako...
Hii hadith mbona sijaisikia kabisa kwenye CNN au kulikoni
ReplyDeleteLeo beirut bomu limeua mmoja na kujeruhi kumi ...nimeona kwenye more than three new broadcast station...Sasa hii imeua wawili na kujeruhi 30 lakini wala hamna habari
Au wandishi wa habari hamna huko nini...??? Michuzi changamkia tenda ...kama Jeff Koinange kaachia ngazi...wahi ndugu yangu...habari hamna kabisa kutoka huko