
kuna mdau kaniamuru nioneshe tena nondo zangu na pia nimburudishe kwa kile alichoita kukosa usingizi kutokana na kukesha kuangalia globu yetu hii. kwa kuwa mteja ni mfalme sina budi kumsujudia kwa picha hiyo nikimuonesha kaka charles kizigha na bernad rwebagira aliyeko masomoni berlin kwa sasa hizo nondo. kuhusu burudani mie naona mdau huyu apewe hii hapa chini ya Nyota Ndogo - Watu na Viatu - http://www.jambovideo.com/2007/06/11/nyota-ndogo-watu-na-viatu/
Duuh, hizo zana kambambe! Kweli mwezetu umejizatiti. Hongera.
ReplyDeleteNa hilo shati lako nalo...ni kiboko, sito sema mengi ila kusema ukweli linanikumbusha enzi za Mobutu na kofia yake.. lol, SteveD.
Kusema ukweli sijaufili huu musiki wa mtu na kiatu. Lete vitu vya uhakika bwana.
ReplyDeletemichuzi nakupa saa 24 toka sasa uombe radhi na kurekebisha kauli yako ya kumsujudia huyo mdau la sivyo yatakayokupata mimi simo. hasujudiwi ila ALLAH.
ReplyDeleteEngineer-Kilwa
Michuzi itakuwa vizuri utengeneze tovuti ya snaps zako maana picha zako ni nzuri profeshno, au vipi!!
ReplyDeleteBrother Michuzi naomba msalimie huyo Brother Benard,alikuwa jirani yangu pale kawe tanganyika packers,michuzi angalia jamaa huyo asije kukushusha kileleni kwa maana ni mbaya sana kwa picha na sasa kaenda kuongezea professionalism,hahahahha,tuwasiliane mkubwa mimi nipo Finland,email martinnako@yahoo.com.(nako)
ReplyDeleteMichuzi umekamilika!! si mchezo,safi sana,lazima nifagilie..!! ukiamua kuingia kwenye kitengo lazima uwe kamili.
ReplyDeleteMimi huo wimbo huwa unanikuna sana tatizo huwa sielewi kwanini unaitwa watu na viatu! wadau naomba nisaidieni kwanini ametumia neno Viatu hapo..
We Michuzi, hizo kemera ni zako binafsi au mwajiri wako (dele-nyuzi)???
ReplyDeletekama ni za kwako basi mimi sina wasi. ila kama ni za mwajiri wako basi unatakiwa kushitakiwa kwa matumizi mabaya ya mali ya Umma. Dele-nyuzi ni kampuni ya uma, utumiaji mbaya wa vyombo vyake ni ubaridhifu wa mali ya uma.
Michuzi ulitakiwa kusema mwanzoni kabisa kamera hizo ni za mwajili wako au wewe binafsi. Sababu kama ni za mwajili wako, nasi tumelipa kodi za kununua hivyo vitu ingawa ulitumwa wewe ukanunua. Ni vizuri ukafanya acknowledgement kwa employer wako kuwa anakuweka up-2-date.
ReplyDelete