Waziri Mkuu,Edward Lowassa na mkewe Regina wakimpa pole Mbunge wa Mbinga Mashariki na Naibu Waziri wa Mipango, Uchumi na Uwezeshaji, Gaudence Kayombo jana ambaye amelazwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa matibabu. Wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Afya na Mbunge wa Viti Maalum, dk. Aisha Kigoda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 25, 2007

    Mheshimiwa PM, tunafurahishwa sana na moyo wako wa kuwajulia hali viongozi wanapougua. Sasa tunakuomba ukamjulie hali Mh. Mbunge wa Viti Maalum Bi. Amina Chifupa wa Mpankanjia ambaye tumesikia hali yake sio nzuri na amelazwa katika hospitali ya jeshi.
    Na usisahau kwenda na mpiga picha wako.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 25, 2007

    ukiangalia hii picha unaona kweli nchi yetu inashindwa kuwapa hata wabunge huduma za class ya juu hospitalini. Ukiona utafikiri sio mbunge bwana aliyelazwa.....

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 25, 2007

    Kaka mbona maoni yanayotolewa kuhusiana na picha hii huweki.
    Nimepongeza hatua ya Mheshimiwa PM EL kuwajulia hali viongozi wanapokutwa na magonjwa. Sasa tunaomba aambatane na mpiga picha wake akamjulie hali Mheshimiwa Mbunge wa Viti Maalum Bi. Amina Chifupa wa Mpakanjia ambaye tumesikia amelazwa katika hospitali ya jeshi na hali yake sio nzuri.
    Ahsante Kaka Michu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 25, 2007

    Kaka Michuzi cha mno anachoumwa huyu mbunge ni nini?

    Nataka nimpe pole ila sijui nimwambie pole kwa kuumwa nini.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 25, 2007

    hali ya hospitali zetu bado inatisha! Tazama Waziri mzima analala na t-shati yake; hakuna nguo za wagonjwa za kulalia!

    Wakina mama wagonjwa na waliojifungua wanalalia kanga zao za nyumbani!

    Kunahatarai za kuleta kunguni na chawa hospitalini!

    Hii ni kwa Hospitali ya taifa...za huko wilayani, je?

    Pesa za semina huko Ngurdoto zinaweza kununulia nguo za wagonjwa za kulalia. Kinachotakiwa ni kuweza kuzishona hapa hapa chini. Kila Wilaya inaweza kushona nguo hizo na zifuliwe!

    Vijana wa kila Wilaya wenye kutafuta kazi, kwa nini msijiunge pamoja na kuomba hayo mapesa ya JK kuanzisha viwanda vua kushona na kufua nguo za hospitalini?

    Wakubwa wakizidiwa wanakwenda kutibiwa wapi!

    Lakini ukweli ni kwamba wote tunakufa, kama binadamu!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 25, 2007

    wabunge wakipewa huduma za class ya juu mnalalamika kwamba wanapendelewa,wakipewa huduma sawa na mwanachi mwingine mnalalamika...mnataka iweje???!! Eti bwana Mdau hebu angalia hilo kwa upana wake....

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 25, 2007

    Ndugu zangu, anaumwa nini mpendwa mheshimiwa Amina Chifupa?pole nyingi ziende kwake,Mwenyezi Mungu amsaidie apone upesi

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 25, 2007

    Ndio maana kila siku "viongozi" wenye mfuko mzito wanaenda tibiwa nchi za nje. Hiyo hospital!!!!????!!!! Hawana room special kwa ajili ya viongozi au first class??? hata kama ni kulipia mtu alipie. "NAIBU WAZIRI" yaani kalazwa kwenye room sijui gani tena...au kma hiyo ndio first class yenyewe basi hizo zingine ndio usiombe tena..

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 25, 2007

    Get well soon

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 25, 2007

    Huyo dakitari handsome ni nani? Hebu taja jina lake namezea mate. Pole kwa kuumwa mheshimwa mbunge.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 25, 2007

    Hiyo ndio first class jamani mnashangaa nini?Ndio Ari mpya,nguvu mpya,kasi mpya.

    Sasa huku kwengine usiombee.Kwa wanaomjua Kayombo hana makuu.Angeugua EL hapo ungesikia kaenda london.

    Michuzi Amina chibone katoka hospitali?Mbona mhe EL hajakwenda kumwona???

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 25, 2007

    Huyo ni professor Lema, ndio mkurugenzi wa MNH sasa, ni baunsa,mtemi na mnoko hakuna mfano.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 25, 2007

    wewe kila mtu unammezea mate kila siku ka!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 26, 2007

    I wish huyo mama ndio angekuwa waziri mkuu wetu....upendo, kichwa na busara kede...

    ReplyDelete
  15. Kama kweli Amina anaumwa Issa pls fikisha ujumbe wangu.

    I like the young lady's courage she is a potential woman leader she just needs to work (near)matured and good hearted women, then she will have a better approach on whatever she does. Get well soon Amina! you are in my prayers

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...