ili kuenzi mapenzi ya rais wa zamani wa zambia kenneth kaunda kutokana na kupenda kwake michezo timu ya taifa ya nchi hiyo iliitwa kk eleven
je kuna ubaya gani timu yetu ya taifa staaz kuiita jk boyz kama 'also-known-as' ama a.k.a kwa misingi hiyo hiyo?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 31 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 19, 2007

    Hallo Kaka Michu
    Mimi pia namuunga mkono huyo jamaa aliyetoa ilo wazo kuwa staaz ipewe jina la Jk Boyz ni sawa maana kiongozi wetu ameonyesha moyo mzuri wa kupenda michezo hususani Mpira wa miguu ana haki ya kumpa heshima hiyo

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 19, 2007

    Viongozi wengi duniani wanapenda Mpira. Kwa mfano, Tony Brair, John Mayor. Rais ya Bolivia (Evo Morales) juzi kacheza mechi na kupachika bao safi!!

    Waafrika tuache ulimbukeni!! Wale wote wanaoitwa J.K.Boys wanajikomba kwa rais. Hii siyo siri!! Hata wakati wa Kaunda waandishi wa habari walikuwa wakijikomba sana kwa Kaunda. Nimefurahi kuona hata yule muhutumiwa wa ujambazi sasa ni mfadhili wa JK.Boys!!

    Kila mtu anatafuta jinsi ya kujikomba. Hii ndio maana watani zetu wa jadi wanasema waandishi wa habari wa Tanzania WANAKAMBA miguu ya rais.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 19, 2007

    enzi ya Kaunda na Nyerere kulikuwa hakuna ukomo wa nafasi ya urais na ni mfumo wa chama kimoja. sasa kuna ukomo max miaka 10, na vyama vingi. Je kikwete akiondoka madarakani na timu nayo itabadilishwa jina na kuitwa Lowasa eleven or Mbowe eleven?

    ILI TIMU ETU IWE NA SURA YA KITAIFA IENDELEE KUITWA TAIFA STAZZ

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 19, 2007

    Zile enzi zilipita na sasa tuko karne ya 21. Viongozi wengi walitumia majina yao ilikujisimika madarakani (ni katabia kaudikteta) nchi jirani utaona viwanja vya mpira, mabarabara, shule na vyuo ni vinatumia jina la kiongozi aliyekuwepo.

    Na hata Saddam alikuwa hivyo mpa mji unaitwa kwa jina lake, pamoja na mafanikio ya timu yetu tusilewe na kumjenga dikteta JK nina imani hata yeye hatopenda JK Boys, hii ni Taifa Stars yaani nyota wa Taifa zima na sio rais tu.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 19, 2007

    hili swali linaonyesha uwezo wa watanzania wa kufikiri ni ziro!
    ynyewe hiyo ni reference au geza geza?The other time pia niliona ingine,watani wetu wa jadi wanamsemo ...Hakuna matata...
    "si vibaya na sisi tukisema bongo yetu haina noma wala nini"
    Unapoambiwa bloghii iko juu,mi napata maana nyingi,mojawapo ni kujaribu kushepu akili za watu katika mwelekeo mzuri.Inawezekana aliotoa hiyo rai anautani,lakini akili za wapitiao blog hii sio zote zawza pepeta bumba toka kwenye mchele.Niliingia kwenye peti shop moja,nikakuta samaki wa mapambo toka sehemu mbalimbali duniani.Waliotoka Lake Tanganyika hawana hata jina moja la kibongo, ila waliotoka lake nyasa(wao wanaita lake Malawi)Wanamajina mengi tuu ya kienyeji moja nilikumbukalo "Golden Chilumba".
    Tafadhali jamani hebu saidieni kizazi jacho kujisikia na utanzania wao.
    Kushinda mechi moja Bungeni!Timu ibadilishwe jina,acheni kumlewesha Muheshimiwa Rais,timu bado inanjia ndefu ya kutembea.
    Na pia nahisi ni busara hayo majina ya kuenziana yakatolewa wakati mtu hayupo madarakani,lengo aendelee kukumbukwa kwa mazuri alofanya.
    Michuzi huwa unanishangaza sana,comments zenye matusi huwa naziona ila maoni yangu yenye msisitizo huwa unayaediti,hwaaiii?
    Kwanini usiediti matusi ukaacha critical comments halafu wsomaji wako ndio wakajibu?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 19, 2007

    Sasa Jakaya si ndio Raisi wetu jamani,yeye anawakilisha nchi nzima internationally.Noma ikitokea hapa nchini yeye ndio watakaemhoji.Sasa tumpe advantage yake yakuwa Raisi.Kwanza kikwete ni mtu mpole sana halafu intelligent,hata Western countries wamesema hivyo.Hata kuna Rap group la Bongo Flava linaloitwa "JahKaya" ambalo ni babkubwa!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 19, 2007

    hayo mambo ya enzi za chama kimoja, huwezi kusikia england wanaitwa "blair boyz" hata siku moja.

    hebu piga picha 2010, kama maganga akiingia madarakani tutawaita "maganga boyz"?

    michuzi nakuunga mkono kwa mengi, lakini hapo ni patupu.

    fine kikwete apewe credit kwa kuiwezesha timu ya taifa kupata mwalimu na hamasa, lakini jina libaki hivyo hivyo - tuache kujipendekeza pasipo stahili.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 19, 2007

    Toka hapa.

    Taifa Stazz linatosha. Sasa unataka jk akiondoka akaja mwingine tuanze tena kuita timu yetu sijui xyz boys..? No way! Let Taifa Stars remain that way.

    Kweli tunamshukuru JK kwa kuipa priority timu ya taifa tofauti na watangulizi wake, lakini tusisahau kuwa resources zinazotumika ni za Watanzania wote, sio za JK binafsi. Sasa kwa nini tu-binafsishe timu kwa mtu mmoja?

    Kama anataka kumbukumbu, ajenge wanja lingine kama lile la BM, tutalipa jina lake kama kumbukumbu.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 19, 2007

    Kama ni hivyo basi Watanzania walikuwa na mapenzi ya hali ya juu kwa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi~AMIN kuliko kiongozi mwingine yeyote baada yake.

    Kwa sababu alikuwa na sera za kweli zilizolenga kuleta maendeleo kwa Watanzania wengi. Pia sera za IMF kama kushusha thamani ya shilingi alizipiga vita sana kwa sababu zilikuwa zinaongeza bei za vitu mbali mbali.

    Hakujitarisha alipokuwa Ikulu, hakukuwa na mikataba feki yoyote. Hao waliofuata baada yake...well I reserve my comments ili ujumbe huu utumwe hewani.

    Kwa kumalizia kama tunataka kubadilisha jina la Taifa Stars mimi naafiki ila tu waitwe Nyerere Boys na siyo JK Boys.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 19, 2007

    HAKUNA UBAYAAAAAAAA JINA LINAPENDEZA SANAAAA.WANAOKATAA NI CHUKI ZAO BINAFSI JK BOYS INAPETA PIGA UAAAAAAA.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 19, 2007

    Hiyo michuzi hapana. Huyu jamaa tumempa kuongoza nchi, kwa hiyo michezo kuipenda ni utekelezaji tu ya yale tuliyokubaliana wakati anaomba kura, na sisi kumpa ofisi pale Feri.
    Tuache kujigonga kusikokuwa na sababu. Sasa akimaliza miaka 10 tunabadili jina tena? TAIFA STARS, Finito!Mulioko ughaibuni, bei ya Lita ya Petrol imefika Tshs 1,500/=, mfumuko wa bei unapaa! O'C-Sinza.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 19, 2007

    Mimi naona bora iitwe JK & EL Heroes!!!!

    ReplyDelete
  13. Kama jina la Taifa Stars ni baya basi kuna mengine mengi (ya kitanzania) yaliyo mazuri kama vile Serengeti, Kilimanjaro,Selous au hata Nyerere.

    Lakini NAPINGA kuiita hii timu jina la JK.HAPANA. Hii ni timu ya watanzania sio ya Jakaya.Hata hizo pesa "anazotoa" ni zetu na sio zake za mfukoni.Yeye halipi kodi ila sisi ndio tunalipa kodi kwahiyo hata jina la timu liwe "letu" sisi walipa kodi wa nchi ya Tanzania.

    Tena tuache mambo ya kujipendekeza kwa rais kabisa.Yeye ni binadamu tu kama mimi na wewe, tusitake kumpa sifa kuubwa kuliko anazostahili.

    Hii timu inaitwa Taifa Stars;full stop.Kama yeye (JK) anaipenda sana hii timu na anataka iitwe jina lake mwambie sisi tunaipenda zaidi yake.Tumesapoti kwa mioyo yetu kwa miaka mingi na "tuliumia" sana wakati ule "wahuni" wa FAT walivyokuwa wanafanya "maigizo" na "mashindano ya kutafuna pesa" za chama.

    Taifa Stars oyeeee! Naomba utuwekee wimbo wa Taifa Stars (audio) ulioimbwa na marehemu Mbaraka Mwinshehe!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 19, 2007

    Acha kujipendekeza wewe, nimeshasema hii timu inaitwa TAIFA STARS,sio JK Boyz kuweni watu wazima. Hiyo KK eleven haiitwi hivyo inatwa chipolopolo kwa taarifa yako kwa hiyo kila raisi ajaye ndio tuiite jina la Raisi timu ya Taifa? ACheni kuwa wavivu wa kufikiria

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 19, 2007

    mbona mnaabudu sana hao viongozi? siyo Mungu huyo unajua??? amewafanyia nini nyie waTZ mpaka mumpe huo wadhifa? Pesa zinaibiwa huko serikalini wala hawafuatilii. Bajeti inapangwa kubwa wala haimsaidii mnakaa kuongelea JK boyz, sijui flaviana. Mara chache tumieni akilini zenu

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 19, 2007

    Mpaka sasa jina ni zuri sana TAIFA STARS aka JK Boys, na hilo JK linakuja kwa kuwa rais ameonyesha uzalendo wa kutumia kafungu kadogo kwa ajili ya tifa stars kitu ambacho marais waliopita walishindwa kufanya hivyo.

    FC

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 19, 2007

    TUSIBWETEKE NA USHINDI...NGOMA
    BADO MBICHIIIII

    Michuzi, Nina rai kubwa kwa Watanzania na wapenda soka wengi ambao wiki hii walikuwa na furaha, nderemo zisizo kifani kufiatia ushindi wa Taifa Stars dhidi ya Burkina Faso.
    Ushindi wa 1-0 dhidi ya Burkinabe umepokelewa kwa shangwe ya aina yake kiasi cha kufikiri kwamba Stars ina tiketi mkononi ya kuelekea kwenye faina za Mataifa ya Afrika huko Ghana, 2008.
    Nimeshangazwa sana na mapokezi hayo kwani licha ya kutaka kujenga imani kubwa kwa wachezaji wetu, huenda ikawa sumu kubwa na kuwafanya washindwe kutimiza azma yao kwenye mechi ya mwisho dhidi ya Msumbiji.
    Nasema hivyo kwa sababu stars bado ina mtihani mgumu na cha muhimu ni kuimba dua kama tulivyofanya juzi, ishinde mechi yake dhidi ya Msumbiji huku Senegal nayo ikitoka sare dhidi ya Burkinabe huko Dakar.
    Ni kitendawili kigumu sana kwani endapo Stars na Senegal zitashina mechi zao, zote zitakuwa na pointi 11; hivyo ni Senegal ndiyo itakayopita kwenye kundi la saba na kuiacha Stars.
    Nafasi ya Stars kupata nafasi tatu za "bure" kutoka makundi yote pia inaoenakana ni finyu kwani kuna timu zilizo makundi mengine, zinaweza kuvuka pointi za Stars na hivyo kuitoa kwenye kinyang'anyiro hicho.
    Ukitazama msimamo wa kundi la nne, tayari timu za Tunisia na Sudan zimepata tiketi ya kushiriki fainali hizo na zitakutana kwenye mechi yao ya mwisho huko Khartoum kuamua mshindi wa kwanza kwa kundi hilo.
    Sudan inayoshika nafasi ya pili ina pointi 12 wakati Tunisia inaongoza kwa pointi 13. Endapo Sudan itailaza Tunisia huko Khartoum Septemba 7/9, Tunisia itakuwa miongoni mwa timu tatu zitazokapita kwenye tatu bora.
    Kundi la tatu, Uganda inayocheza leo Jumanne dhidi ya Lesotho huko Maseru, huenda ikafaidika na "tuzo" hiyo ya CAF kwani kama ikishinda itafikisha pointi 10 na inasubiri mechi yake ya mwisho dhidi ya Niger huko Kampala.
    Endapo Uganda itashinda mechi zote mbili na Nigeria kuboronga dhidi ya Lesotho, Nigeria yenye pointi 12, itakuwa ni miongoni mwa timu tatu za ziada zitakazopata nafasi ya kucheza fainali za Ghana.
    Lakini kwa vile mechi ya leo kati ya Uganda na Lesotho inachezeshwa na waamuzi toka Bongo, uzalendo unaweza kufanyika ili kuipinguza makali The Cranes na kuiweka Stars kwenye nafasi nzuri!
    Kwa maana hiyo hadi sasa Stars inalilia nafasi mbili kati ya hizo tatu kwani matokeo ya mchezo kati ya Senegal na Burkinabe, yanaweza kutabirika hasa ikitiliwa maanani kwamba Senegal haijawahi kupoteza mechi yoyote huko kwao katika kampeni hii.
    Zipo timu nyingine kama Eritrea, Guinea, Algeria, Zambia, zenye pointi nane kila moja kwenye makundi yao zinaweza kufanya maajabu na kuipiku Stars.
    Kundi la tisa halitii wasiwasi sana kwani mechi ya mwisho itakuwa dhidi ya wanaoongoza kundi hilo ambao ni Mali na Togo. Zote zina pointi tisa hivyo haliwezi kuathiri dhamira ya Stars kunyakua nafasi hiyo ya mbili bora.
    Wasiwasi mkubwa ninao kwa Eritrea kwenye kundi la nane ambao wanaweza kufikisha pointi 11 endapo watawalaza vibonde Swaziland na hivyo kuwa miongoni mwa timu zitakazochukua nafasi hizo mbili bora zilizobaki.
    Tuombe mungu timu itakayoshika nafasi ya pili kwenye kundi la nane ambalo zina timu za Guinea, Algeria, Gambia na Cape Verde, isifikishe pointi 11 ambazo huenda zikafikiwa na Stars.
    Kama mambo yatakuwa hivi kama nilivyotabiri wiki chache zilizopita kwamba Msumbiji ijitahidi kuichapa Senegal au watoke sare na sare kuilaza Burkinabe, basi Mungu siku hiyo ya Septemba 7, awe ATHUMANI angalau wabongo wafaidike na matunda ya kuwa mwanachama wa CAF!
    La msingi ni kwamba hakuna lisilowezekana. Jitihada zilizoonyeshwa na viongozi, wafanyabiashara, wananchi wote, zizae matunda.
    Na kwa vile mechi ya mwisho dhidi ya Msumbiji ni muhimu, SI VIBAYA KIINGILIO CHA MCHEZO HUO KIKAWA KIDOGO ILI WASHABIKI WAJAZE UWANJA NA KUISHANGILIA KWA NGUVU STARS IIBUKE NA USHINDI MKUBWAAAAAAA.
    NASEMA HIVYO KWA SABABU, KAMA NGOMA KIDEDEA IKIPIGWA HUKU WASHABIKI WAKISHANGILIA KUANZIA DAKIKA YA MWANZO HADI MWISHO, JAMAA WATACHANGANYIKIWA NA KUJIKUTA WANASHINDANA NA WACHEZAJI 22 BADALA YA 11.
    IPO HIYO NA HIYO NDIYO INAYOSAIDIA TIMU NYINGI KUSHINDA. WASHABIKIII NA KELELE UWANJANIIII.
    mpenda soka

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 19, 2007

    Hivi kwani nani kakuambieni kwamba timu ya Taifa ya Tanzania inaitwa JK Boys? Mbona mnakuwa wavivu wa kufikiri? Hivi hata vitu vidogo vidogo vitumie muda wetu kuvijadili. Timu ya taifa inaitwa Taifa Stars.

    Sasa kama kuna mwenye shida na hilo hayo ya kwake. JK Boys ni kama jina la utani tu. Kama ambavyo kuna "richmonduli", "ukapa" (kwa maana ya ukata, enzi za Mzee Ben) n.k.

    Nakumbuka kabla ya ujio wa Micho pale Yanga, vijana walikuwa wanaitwa "Jack boys" (kocha mkuu wa Yanga alikuwa Jack Chamangwana). Nafikiri sasa wataitwa "Micho boys"

    Kwa hiyo akija "Maganga", "Lipumba", "Mbowe", bado tutakuwa na Taifa Stars a.k.a "Lipumba", "Mbowe" au "Maganga" boys!! kama watakuwa wanajishughulisha na michezo, lakini.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 19, 2007

    Kwanza kabisa kumfananisha Kikwete na Kaunda ni matusi kwani kikwete ni mwizi yeye na baraza lake lote la mawaziri---kaunda is one of the few presidents wa Africa waliofanya kazi kwa mapenzi halisi yakutoka moyoyi wakiamni wanatusaidia wa-Africa wote.
    Kwahiyo basi huyu alipendekeza to name the team aftre kikwete, aache unafiki humundani mimi napendekeza amzalie mtoto huyo kikwete na amuite mtoto wake JK. Zaidi ya hapo , kikwete hajafanya lolote to deserve to even have a kichochoro named after him in TZ

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 19, 2007

    Hapo kaka michuzi naomba tutofautiane kabisa kwenye hilo jambo. Enzi za akina Kaunda nchi nyingi za kiafrika zilikuwa zinaongozwa kibabe sana na hakukuwa na transparency kabisa. Hiyo timu ni mali ya watanzania wote hata mtoto aliyezaliwa sasa hivi na JK hatumii mshahara wake kuihudumia bali pesa za walipa kodi.
    Kwa hiyo itakuwa vyema timu ikawa na jina linalomuhusu kila mtanzania at least tungeiita Tanzanite Stars (coz ni madini pekee yanayopatikana kwetu) au kitu kingine kinachotoa sura ya utaifa siyo ubinafsi na unafiki wa kutoa majina kwa kuwa tu kiongozi wa nchi anapenda mpira,so what?
    Halafu jambo jingine ambalo watanzania bado hawajalijua ni kwamba ahadi alizotoa JK wakati wa uchaguzi hazitekelezeki na ahadi ambazo zingetolewa na rais wa nchi iliyoendelea siyo kwetu. Sasa ilikupoteza attention ya watanzania ame-focus kwenye kitu kinachoteka akili za watu MPIRA. Lakini hutuwezi kupata maisha bora kwa Taifa Stars kufanya vizuri (ni jambo jema but not first priority). Wananchi wa vijijini hawawezi kuuza mazao yao wakapata kukidhi mahitaji,huduma za afya,barabara mbovu na ongezeko la kodi lisiloeleweka n.k bado ni kipaumbele. Na JK anayaona hayo lakini MTANDAO wake unahitaji kula good times,government spending imeongezeka kupita wakati wowote na budgetary discipline haipo, KASI MPYA iko wapi?Au ni ya ulaji na ufujaji?
    Tafadhalini watanzania,tuache unafiki baadhi yetu tumeenda shule lakini haina msaada tunaogopa kuongea ukweli ili tuonekane wazuri, what is the point ya kuwa educated kama hatuwezi kufanya critical analysis on issues?Leo tunafuraha sana na probably miezi miwili mitatu ijayo lakini kuna miezi 12 ambayo tutaendelea kupata maisha duni na ahadi hewa.Hiyo ndiyo trade-off ya short term happiness.
    Mungu Ibariki Tanzania
    Naomba kuwasilisha hoja yangu.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 19, 2007

    Duh huu upumbavu waafrika tutauacha wapi? Nani hasiyewafahamu akina Bokassa, Mobutu, Idd Amin, etc ebu tuache ulimbukeni.....hata kama Rais anaamua kuvaa jezi na kuchezea timu ya taifa, ni wajibu wake kama mtanzania kuipeperusha bendera ya Taifa....tena yeye kama kiongozi ni lazima asaidie timu ya Taifa....sasa katimiza wajbu wake, wabongo mlishakuja na eti JK boys!!!! duh yaani ukoloni na ushamba my goodness utatuka lini????? nashangaa shule za mkapa, nyerere, oh askofu mkoba etc....for what? najua wengine mtakuja na mada eti mbona kuna G.Washington University, JF Kenedy University etc!!! but whats the point to do that? ni bora ufanye hivyo baada ya huyo mtu kaishaaga dunia ndo una-muenzi, mfano sishangai DIA siku hizi kuitwa JK nyerere int. airport...lakini mtu bado yuko hai, achana na dhana hizo mpaka hapo tuone mchango wake kamili.....tumia majina kuita mitaa ya bongo lakini si kitu kikubwa kama hichi........shule bwana!!!!! baba C hupo? komaa na cardn..health inc, hehehe

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 19, 2007

    Wabongo bwana kidogo tu mmeshalewa kama mmenyweshaw sijui hiyo kinjwaji ya south.

    Ingefungwa mngekimbilia kuibadili jina?

    Na akipenda kula dinner Kilimanjaro hotel only nayo mtabadilisha jina hiyo hotel?

    Acheni kupapatika vitu vya kijinga. Jina la Taifa Star lipo na nizuri sana. Kama mnaliona baya basi tutafute reasonable lingine.

    Kwa hiyo hili ndio la muhimu tu aliloonyesha toka aingie madarakani? Au vitabadilishwa vingi tu??? Au hili ndio tutamkumbuka nalo akiondoka madarakani?

    Hata watu wa nje watatucheka nchi yetu ikienda nje ya nchi halafu inaita JK boyz na maana ya ke wakipewa watasikitika sana..

    Akija raisi mwingine hiyo timu itaenda kuwakilisha nchi kwa jina hilo hilo aua itabadilishwa tena......kama mnaona nick name yenu inawapendeza it is okay lakini tulioko nje ya nchi tunaikumbuka na kuiita timu yetu TAIFA STAR

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 19, 2007

    ARE THEY BOYS OR MEN????

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 20, 2007

    Michuzi na wewe mchemfu saa zingine jamani! Unaboa kama nini. JK Boys, JK Boys, please!

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 20, 2007

    MICHUZI SASA UNATUYEYSHA BWANA, WEWE NA HUYO JK HADI MNATAKA KUTUBOA KABISA,
    NADHANI UMEONA MAONI YA WATANZANIA WALIO WENGI WANAPINGA TIMU YA TAIFA KUITWA JINA LA HUYO JAMAA(SIKUPENDA KULITAJA MAANA NITAKUWA KAMA NA MIMI NAIITA HIVYO)HUU NI MJADALA UMEANZISHA,SASA NATAKA KUWE NA HITIMISHO ILI HILI JINA TULIKOMOSHE KABISA,NI BORA HATA TUKAIITA TIMU YA TAIFA MKWAWA BOYS.
    MKONGWE NDANI YA EU

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 20, 2007

    WADAU INAONEKANA MOZAMBIQUE NAO SIO MCHEZO MPAKA SASA WAMEKUBALI MECHI MOJA TUU KUFUNGWA .http://cafonline.com/competitions.php?head=Nations%20Cup&loc=competitions/nations_cup/matches.htm

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 20, 2007

    Kaka Michuzi, hivi hatuna lingine la kuzungumza mpaka kila siku Taifa Staz, Taifa staz!?!
    Mbona tunakuwa MALIMBUKENI hivi? Na huo ni ushindi tu wala sio UBINGWA.
    Hebu tuletee mambo mengine achana na hayo ya Taifa staz yameshapita sasa.

    ReplyDelete
  28. AnonymousJune 20, 2007

    Hebu tuacheni mambo ya ajabu na aibu jamani. Sawa, Kikwete anapenda michezo ieleweke wapo baadhi ya watu pia wanapenda sana michezo hata zaidi ya Kikwete, tofauti ni kwamba hawana uwezo ama hawajulikani kwa namna moja ama ingine. Nisichonge sana, point ni kwamba, hii timu na iendekee kuitwa tanzania Taifa stars, hakuna cha JK wala mwengineo atayekuja baada ya Kikwete.
    nawakilisha!

    ReplyDelete
  29. AnonymousJune 20, 2007

    NA WABONGO WOTE MTAKULA SOKA, MTALALA KWENYE UWANJA WA SOKA, MTAAMKIA SOKA, MKITEMBEA SOKA, MKISIMAMA SOKA KILA KITU SOKA!
    HAMKUMBUKI CHOCHOTE JUU YA UCHUMI WA NCHI YENU. WAULIZENI KENYA WALIPOJENGA MOI KASARANI NA BAADA YA MASHINDANO YA KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA WALIAMBULIA NINI...SOKA (DENI KUBWA).
    BADO NYIE NA KAJIWANJA CHENU CHA TAIFA. JAMAA (WACHINA) WANAVUTA MUDA KIDOGODO DENI LIWE KUBWA MSHINDWE KULIPA, MPELEKE MADINI NA MAZAO MUHIMU KWAO...KISA, SOKA. (UWANJA MPYA).

    ReplyDelete
  30. AnonymousJune 21, 2007

    As Jornalist mzee Michuzi lazima uwe shujaa, mwadilifu na usiwe muoga. Muhimu sana usijipendekeze na tumia lugha watu wote wanaielewa. Achana na lugha ya kihuni isiyo na mahana. Dunia nzima sasa tunasoma hii glob.
    JK doesn't deserve anything, Taifa Stars inashinda mechi lakini haijawa structured professionally. Si muda mrefu itaenda chini tena. Ukitaka kujua viongozi wanastahiri sifa angalia hapa Australia walivyotengeneza Soccer team yao. Watch out for Aus team. Hutasikia ujinga kama huo eti the team ipewe jina la PM hapa. What JK is doing is his job. Angekuwa intelligent ange-implement hizi change kupitia minister responsible. Kama minister hawezi kazi anamuondoa kama wanavyofanya wenzetu. Mimi naona JK anajitafutia umaarufu. Wa-TZ kwa vile bado wamelala na hawana tabia ya kuangalia nchi nyingine wanamuona JK shujaa.
    How many people benefit from soccer? There are serious issues that JK should deal with. Mfano umeme, bogus contracts nchi imeingia, unemployment, corrupted officials (big fishes) sio wadogo kama makatibu kata ambao JK anawa-target. Uchumi ukiwa imara michezo yote itaendelea na sio soccer pekee

    ReplyDelete
  31. Hakuna lolote la ajabu alilofanya JK katika timu ya Taifa zaidi ya KUTIMIZA WAJIBU WAKE.Si aliomba mwenyewe majukumu hayo? Raha za lile jengo jeupe malipo yake ni kufanya kila kitu kwa bidii,maarifa, uaminifu nk. la sivyo tunamfukuza 'upangaji'. Taifa Starz ndio jina la timu.Full Stop.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...