mdau ndelamio wa bongo wa akiwa cape town ambako baada ya kupiga raundi akaenda kuvuta bima hili...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 18, 2007

    Huku sasa ndio tunauita ulimbukeni michu kuna watu wangapi wanavitu vya maana hawajitangazi?. mi nilifikiri apige picha kwenye kiwanda kikubwa aoneshe kuwa baada ya kupiga round kafungua kiwanda ambacho anaajiri watu kama 1,000 hapo kweli ningemuona mjasiliamali.

    Hii sasa itawafanya vijana wetu bongo kufiria mambo kama haya badala ya kufight na maisha home waanze kuzamia sauzi wakaishie maisha ya geto. Je sisi tutajuaje kuwa hilo si lake ni la mtu kapaki na kumwambia amuangalizia(security) yeye akaona ni opportunity ya kuchukua snap na kuwakoga jamaa aliowaacha kijiweni bongo!!, amekuletea na picha ya kadi ya gari michu???, Haya sisi hayatuhusu ni yeye tu na maisha yake.

    Kesho atamuomba mzungu apige nae picha na kutuambia kaoa mzungu Wabongo kweli bado tuna safari ndefu sana, tena sanaaaaaaaa!!!!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 18, 2007

    Being a sales person for past 5 years in UK that person touching the car is not a customer (no will he be in nxt few years)!
    He must be careful as he may scratch other peoples car bureee !and land in trouble trying to show off !
    Im ready to put money down incase he can prove me wrong
    Abdul

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 18, 2007

    Mzee hapa umechemsha, picha hii ina muhimu gani hapa???

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 18, 2007

    Michuzi mkubwa hii sio blog ya ubishoo bwana,ni ya kitaifa na watu wenye uchungu na taifa,sijaona sababu ya wewe kuweka picha za huyo muuza unga na hilo bima lake,je unataka na sisi tukutumie zetu tupo na maskoda yetu na alfaromeo.tunayo ilahatuoni kama ni kuna maana yoyote.hayo ni maoni yangu na sio chuki,kama nimekosea kumradhi wadau.
    Mkonge ndani ya EU

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 18, 2007

    Do we have to know this?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 18, 2007

    Mbongo asakwa na FBI kwa kudhuru

    Nafurahi kupata fursa hii. Naamini maoni yangu yaweza kuwa marefu kiasi lakini naamini it\'s worthy. Hii sasa inakuwqa toooo much maana sasa wanataka kuifanya nchi ionekane tofauti na ilivyo. Ni kweli kuwa asilimia kubwa ya vijana wanaotua hapa nchini hawakamilishi lengo lao la kwenda shule lakini inatokana na matatizo mbalimbali ambayo mengine yanazuilika na mengine ni ya kujitakia. Kama ilivyo katika filamu ya BONGOLAND ambapo jamaa asiye na kitu anaandika nyumbani kuwaeleza kuwa ana hili na lile, ndivyo ilivyo hata katika maisha hali ya baadhi ya watanzania waishio huku ambao wanaishi maisha tofauti na wanayosimulia nyumbani, wanapiga picha wakiwa kwenye magari na wakati mwingine hata nguo za kuazima ama kukodi wakisema ni zao wakati wana maisha magumu na baadae kinachofuata ni watu walio nyumbani kuomba tu-misaada twa hapa na pale na ili kijana ajidhihirishe kuwa mambo safi analazimika kufanya lolote awezalo kutimiza na hapo ndipo wanapoanza kujihusisha na biashara za ajabu na kuishia kwenye maugomvi ya ajabu. Nisingependa kuwalaumu saaana wazazi lakini naona niwakumbushe kuwa \"unapomtuma\" mwanao huku basi jitahidi kumfikisha katika mikono salama. Ninakuhakikishia kuwa sehemu anayofikia mtu ina zaidi ya asilimia Themanini kujenga mustakabali (future) wa nini atafanya, ata-behave na vipi atakuwa. Ukimleta akafikia kwa drug dealers hatakuwa na jinsi zaidi ya ukarimu siku za mwanzo na itakapofikia wakati wa kuijua nchi na mahali pa kwenda inakuwa tooo late na pengine anakuwa mtumiaji (kama sio muonjaji wao) na lazima ujue kuwa kila mtu huwa na marafiki wanaojuana na kufanana kitabia na kwa vyovyote watateteana katika kila wafanyalo, hivyo usitegemee mtu afikie kwa watu wema aangukie mikononi mwa wahuni right away ama afikie kwa wahuni kisha afahamiane na watu wema right away. Wazazi msiache kuwashughulikia wanenu wanaotaka kuja huku ilani suala la KUWA MAKINI KUJUA NI WAPI ATAFIKIA NA WATU HAO WAKOJE / WANAISHI VIPI. Ukweli wa mambo ni kuwa Wabongo wengi hapa US ni Party, Pombe, kinadada na Majigambo tena kwa vitu vilivyo juu ya uwezo wao. Si ndio maana wanachomana visu? Kama anataka kuwa juu yako lakini hana uwezo na anaamini kuwa yeye ndiye best atakupunguza ili aendelee kutawala. STUPID.....
    Kwa kweli inasikitisha na kutia aibu kama watanzania tumefikia situation yya kuuwana kwa kuchomana visu kisa ni wanawake au upuuzi wa kiringishiana pesa na vitu ambavyo vikifanyiwa tathmini havifikii hata 1/3 ya maisha ya mtu inatia kichefuchefu. na inazidi kuonyesha ni kiasi gani ni wajinga kwani tunaiga yasiyoo faa kuigwa wazazi wanajiua kwa kutoa kila walicho nacho ili watoto wao wapate elimu na la msingi zaidi ni kupata exposure, maana mtu anaspokwenda nchi za magharibi hatajifunza vya darasani tu kama ni mwendaji wa shule bali na experience ya kuishi na watu kutoka kila kona ya ulimwengu wenye culture mbalimbali ammbayo kutokana na ulimwengu kubadilika itasaidia sana ku adapt mazingira yoyote ya kazi na ukizingatia kuwa globalisation notion inainfluence kwenmye kila kitu, hata tz sasa kuna swala la privatization na makampuni mengi tu ya kigeni yanafunguliwa. Sasa kama kweli vijana tunaopata hiyo nafasi ya kwenda huko ikawa vizuri kukopi yalio mazuri na kurudisha nyumbani kuijenga nchi yetu rather than upumbavu tunao ufanya halafu wenye nchi zao utakapo amua kutuzui kuingia tutaanza kulalamika na kusema ni kinyume na kakiza binadamu wakati sisi wenyewe ndio tunaharibu kwa kugfanya makosa tena ya kutoana roho si dhani kuna mtu anaye taka kukaribisha majambazi kwenye nyumba yake.. KWELI NINGEWAASA VIJANA WENZANGU KUWA MAKINI NA KUFANYA VITU AMBAVYO LEO NA KESHO VITAWAFANYA WATU WAKUUMBUKE NA KUTAMANI UENDELEE KUWEPO. SIO LAZIMA VIWE VIKUBWA HIVYO NA KWA AJILI YA TAIFA NZIMA BASI JAPO KUWAFANYA WAZAZI WAKO NA WALE WATAKAO PATA NAFASI YA KUWA KARIBU NAWE WAJISIKIE \"MAKE THEM PROUD\" PLEASEEEEEEEEEEEEEEE WATANZANIA WENZANGU HASA VIJANA TULIO NCHI ZA UGENINI TUJARIBU KUCHANGE NA KUFANYA MAMBO YA MAANA MALI NA UMAARUFU UTAKUJA TU KAMA TUTAJIJENGEA MSINGI MIZURI WA MAISHA. YALIO TOKEAA HUKO USA DALASS SI YA KUJISIFU NA YATATUFANYA TUKOSE MENGI NA WAKATI MWINGINE WATU WAANZA KUFIKIRIA MARA MBILI KABLA WAHAJASEMA URAIA WAO NA NI JAMBO LA KUSIKITISHA TUTAKAPO ANZA KUUKANA URAIA WETU. NA NI KITU AMBACHO WENGI WA WATANZANIA KIKO NYUMA KABISA YA UBONGO WETU

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 18, 2007

    Bwana Michuzi mimi nafikiri jamaa aliingia showroom kufurahisha maccho yake, sababu ukiwa umeshanunua huwa wanalitoa gari nje wakati wewe unamalizia paper work, lakini hapo inaonekana kama vile anafurahisha macho yake. Hizo ni fikira zangu.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 18, 2007

    SOOO WHAAAAAAAAAAAAAT!!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 18, 2007

    hapana huu ni ushamba.....!!!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 18, 2007

    jamani kulikoni tena huko dallas,watanzania wamechinjana au?

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 18, 2007

    jamaa mshamba tu amesimama barabarani anashangaa shangaa. hii picha weka kwenye album yako uangalie na wenzako wa kijiweni... kiasaka!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 18, 2007

    huyu ndio kama yule mjinga aliye pandisha rangerover kwenye BA hilo gari atalipitishia barabara gani na kodi iliyo wekwa kwenye hiyo bajeti wazimu inayojadiliwa sijui kama ameconsider hilo

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 18, 2007

    Mwenye Gari ni yule jamaa mrefu nyuma ana sign paper..wewe bishororo unafurahia kupiga picha. Watu wamepaki hayo kama matatu hivi garage hawajatuma picha kwa michuzi wala nini acha ubishororo.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 18, 2007

    Michu,picha kama hizi zinachafua blogu!

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 18, 2007

    michuzi hiyo gari unakisia inaweza $$ ngapi ???

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 19, 2007

    ah ndugu zangu ,kosa lake ni kuwaonyesha gari lake au ?Basi kama mna hasira sanaaa wekeni ya kwenu!

    Kwani yeye hastaili kuwa na gari kama hilo au mwamuona mshamba?

    Kumbukeni Mdharau mwibaaaa.........

    Wadau kumbukeni hapa kwa michuzi vitu vingi vyaonyeshwa ,Nakumbuka yule mdau wa Uturuki aliyegraduate recently kaweka picha zake hapa pia alipondwa na wakatafuta mpaka shule aliyosoma ina rank ya ngapi,
    Sasa huyu katuonesha gari lake pia kosaaa.

    Kwa kweli wabongo tunapenda kuponda about everything ,mi binafsi nikiposti picha yangu mtanisasambua weeee mpaka nikonde .

    All in all hii blog ni ya Michu yeye ndo mwamuzi wa yapi ya kuweka au la.Tupunguze ukali ndugu zangu sio vyema Mungu hapendiii.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 19, 2007

    ni kweli blog hii ni ya michuzi, lakini nawe pia ungeheshimu mawzo ya wengine. Hakuna cha mdharau mwiba wala nini, hiyo picha inajieleza huyu mtu ni mgeni maeneo hayo. Namlaumu Michuzi kwa kumsingizia jamaa kanunua hiyo gari,Bwa Michuzi tupe proof hayo maneno kasema mwenye picha ili tumdharau rasmi.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 20, 2007

    Jamani mnaingia hapa buru, na taxes zenu hazifiki kwa Mr. Supu. Kama msanii anafanya anavyotaka yeye, na nyie ambao hata wateja siwezi kuwaita , mnaweza kuingia tena na kusoma na kuangalia hayo amiliki aliyoweka. Blogs nyingi zinakufa kwa kukosa "wateja". Michuzi kwa kuweka vitu tofauti na kutoa chance kwa wote (including wenye wivu na uswahili) ndo anafanya mie na wengine wengi kurudi tena hapa. HANDS OFF THIS SITE na kama mna cha maana fungueni zenu tuone. Blackmpingo

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 21, 2007

    Black Mpingo hilo unalosema ndio nilijaribu kulieleza hapo juu saa 2:14 june 19.Kwamba michu ndo mwenye last say kwenye blog yake hivyo ataweka chochote atakacho na kuminya chochote ,mbona comments kibao tunaandika hazitoa ni uamuzi wake,hamna anayemlipa kwa kazi za blog hii wala si mimi.Kule kwa Chemi niliona siku aliweka message kuelezea kwamba ile ni blog yake anafanya kazi kwa muda wake na maamuzi yote ni yake.Mi nakuomba ka michu endelea kuweka mambo yote kama utakayopenda kama mtu anaona maendeleo yake ni elimu anakuletea picha za Graduation zipublish kaka,kama ni kama huyo bro hapo juu kununua bima sijui nini we publish bro,hamna noma wala nini .
    All in all wapondaji na wasiopenda watu fulani kuwa na kitu kikubwa zaidi yao pia watapaka sana.

    To you michu najua una mamlaka yote na blog hii lakini kuminya comment inauma wewe lol.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...