
kila jioni na asubuhi siku hizi hutumika 'njia tatu' kupunguza msongamano wakati wa kwenda/kurudi makazini ambapo magari mengine huruhusiwa kupita upande wa pili wa njia nne kama hivi. kiasi imesaidia. ila ambo bado kwani wadau wengi wanashauri vijia vidogo-vidogo vingekarabatiwa na kupitisha magari kupunguza wote kutumia njia moja
Kuhusu barabara za Dar,nachoshindwa kuelewa ni kwa nini wasiitwe wawekezaji kuja kuboresha njia za usafiri kwa wakazi wa jiji,badala ya kuwekeza eti kwenye maduka ya nguo au sanaa za waTz(vitu ambavyo twaweza fanya wenyewe)?Magari yanazidi kuingizwa mjini ya nini wakati barabara ni zile zile?Kuna bandari hapo ina pantoni la kwenda Kigamboni tu,kwa nini lisiwepo jingine kwa wakazi wa Kunduchi,Masaki Bahari beach nk???Nchi yetu imebarikiwa na mali asili kwanini hazitumiki ipasavyo???
ReplyDelete