tovuti ya wananchi itakavyoonekana pindi itapozinduliwa. mambo yakienda mswano huenda ikaingia hewani julai mosi mwaka huu, kwa mujibu wa redio mbao

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 24, 2007

    TOVUTI HIYO NI KWA AJILI YA WANAOJUA KIMOMBO TUU?.
    KWA NINI ISITUMIKE LUGHA YA TAIFA NA BADALA YAKE KIINGEREZA AMBACHO KWA MWANANCHI WA KAWA ATAAMBULIA NINI?
    MBONA WABONGO TUNAJIPENDEKEZA SANA NA HII LUGHA. ANGALIENI NCHI ZINAZONGUMZA KIFARANSA, KISPANIA, KIRUSI, KIGIRIKI NA LUGHA NYINGINE, WOTE HUTUMIA LUGHA ZAO ZA TAIFA. KWANI HAWAJUI KIINGEREZA?
    ULIMBUKENI KITU KIBAYA SANA. NA KUNA HABARI KWAMBA DOLA NDIYO INAYOSHIKA USUKANI NA KUITUPA SHILINGI KWENYE BIASHARA. AMA KWELI LIMBUKENI HAJIKISI!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 24, 2007

    Nakubaliana na msemaji aliyetangulia kuwa hakuna mantiki ya tovuti hiyo kutumia kiingereza kama lugha ya mawasiliano. Aidha inasikitisha kwa wenye tovuti kutumia lugha mchanganyiko (kiswainglishi). Nashauri kiswahili ndo iwe lugha mama katika tovuti hiyo ili wananchi wengi waweze kutumia na kama ni lazima basi kuwe na kiunganishi cha kwenda kwenye version ya kiingereza kwa wale wanaopenda kutumia lugha hiyo.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 24, 2007

    Tumesikia juzi Bungeni kuwa serikali ya JK haifanyi kazi kwa kupitia "mtandao" (e-mails and the likes) sasa hi tovuti itakuwa ni kwaajili gani? Kama itakuwa wazi kwa wananchi kutoa malalmiko na dukuduku zao, zitafanyiwa kazi kweli? au ndio viini macho vya sirikali ya JK. Just one of those things to show that the Govt moves with time but in reality nothing will be done. Hebu ona majina ya wauza unga ya mheshimiwa AC mpaka leo jamaa anapiga danadana. Hamna kitu hapo!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 24, 2007

    Anony hapo juu, huu ukurasa unaweza kuchagua kutumia kiswahili au kiingereza, angalia vizuri upande wa juu kulia... kuna kitu kama KISWAHILI. nahisi ukiklik hapo unapata page ya kiswahili

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 24, 2007

    http://mzalendo-mzalendo.blogspot.com/

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 24, 2007

    Anon. wa June 24, 2007 6:13:00 PM EAT. Asiyefahamu kiingereza siyo tatizo kwao kwani hata access ya komputa hana, tishio kwao ni yule anaefahamu kiingereza na ndyo mlengwa hapa. Hawa ndiyo watu wanaojua madhambi, ubadhirifu na udhaifu wao. Walioandaa hii tovuti siyo wajinga...you need to know who's your customer.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 24, 2007

    technologia ya computer inahitaji uwe na ufahamu wa kingereza,hata kama utahitaji kufungua page ya kiswahili,sasa zaidi ya 90% wanaopitia website nikuanzia wanafunzi wa secondary na kuendelea,na kwa wale watoto ambao baba zao wanazo computer ndani na ni waprimary basi kwa namna moja ama nyengine wanaufahamu wa kingereza,so tovuti iwe kwa kiswahili au kingereza sawa tu,maana wengi wanaopitia webs wanazifahamu hizo lugha mbili,na wasiojua kingereza hata kidogo,hao hata computer ni nini hawajui.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 25, 2007

    Mijitu mingine bwana! Wewe anonymous wa kwanza kabisa, sijui unalalamika nini!!

    Kwa akili ya kawaida tu, unaweza kuona kwamba hapo pembeni kulia kuna sehemu imeandikwa "KISWAHILI". Kwa hiyo unaweza kuchagua lugha unayoipenda.

    Ni sawa na ukitembelea website ya Taifa. Unaweza kuchagua "Kiswahili" ama"English". Acha ulimbukeni wa kukurupuka kutoa maoni kabla ya kufanya uchambuzi wa kina wa kitu unachotaka kukiongelea almradi tu umeandika.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 25, 2007

    hiyo website ni upumbavu mtupu na kuwafanya watu hawana akili...umefika wakati serikali kuacha blah blah na kufanya kazi serious,hiyo website inanikumbusha ule upuuzi wa kipindi cha MIKINGAMO serikali inayofanya kazi kwa majungu...shut down hiyo site na kila wizara au idara ya serikali iweke ya kwake ambayo itakuwa ni kwa ajiri ya huduma za kazi waliyopewa sio huo upuuzi ambao hujui unamwandikia nani na nani atakujibu

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 25, 2007

    Hiyo tovuti ya malalamiko ni upuuzi mtupu.

    JK anafahamu madukuduku ya wananchi lakini hafanyi kitu.

    Serikali kwanza inatakiwa itatue

    Richmond

    Mikataba ya madini

    Kesi ya Mahalu

    Kesi ya dito

    Ile email iliyozungumziwa bungeni wiki iliyopita

    ANBEN

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 25, 2007

    hiyo website ni upumbavu mtupu na kuwafanya watu hawana akili...umefika wakati serikali kuacha blah blah na kufanya kazi serious,hiyo website inanikumbusha ule upuuzi wa kipindi cha MIKINGAMO serikali inayofanya kazi kwa majungu...shut down hiyo site na kila wizara au idara ya serikali iweke ya kwake ambayo itakuwa ni kwa ajiri ya huduma za kazi waliyopewa sio huo upuuzi ambao hujui unamwandikia nani na nani atakujibu

    Nakubaliana kabisa na anony niliyemnukuu hapo juu. Ni Mikingamo na ile programa ya Mwinyi kukutana na raia mara moja kwa mwezi. Hivi kweli viongozi wetu wanafikiri sawasawa? Watu wenye kuijua hiyo website ni wachache sana na ni wale wa mjini tu, je serikali ni kwa ajili ya watu wa mjini tu. Matatizo makubwa ya nchi hii yako vijijini, siyo mijini. Pamoja na nia yako njema, please Mr President, Col. JK, be serious. Huu uongozi wa bla bla kweli utatufikisha pabaya. Utashangaa ukiambiwa kuwa gharama za kutayarisha hiyo website yaweza kuwa mamilioni ya pesa ambazo zingefanya jambo la maana zaidi kwa wananchi kwa namna nyingineyo.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 25, 2007

    Nasikia ktk hotuba ya Rais ya mwezi uliopita, Rais aliwauliza jamaa waliokuwa pembeni yake kama website ipo tayari, alikuwa anamaanisha website hii ama nyingine?

    ReplyDelete
  13. kuna anon mmoja hapo juu ana wrong perception juu ya lugha, kujua kingeraza si kuwa na akili, wala si kuwa mchambuzi wa mambo kingereza ni lugha kama lugha nyengine, huu ndo upumbavu wetu wa afrika wakimuona mtu anajua kingereza wanamuona anajua kila kitu wapo mabeach boy tele wanajua kingeeza lakin hawajui kuchambua mambo,na wapo watu wasiojua kingereza ambao ni wachambuzi wazuri wa mamabo na wenye falsafa pana ya maisha. Tusipende kuhukumu akili za watu kwa lugha.kwa mfano wadachi,wachina,wajapan na wajerumani hawajui kingereza vp nawao hawana akili? we anon usiwe mtumwa wa fikra pumbavu!!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 25, 2007

    Anon aliyesema eti technologia ya computer inahitaji uwe na ufahamu wa kingereza, ni mwongo mkubwa!

    Wachina na Wajapani na Warusi computer zao wanazi-access kwa lugha yao!

    Anonymous said...
    Tumesikia juzi Bungeni kuwa serikali ya JK haifanyi kazi kwa kupitia "mtandao" (e-mails and the likes) sasa hi tovuti itakuwa ni kwaajili gani?

    Hayo yana maana kuwa serikali haiwezi kuwa inayasikiliza yote yanayoandikwa kupitia mtandao...mengi huwa si ya kweli..kwa mfano yanayoandikwa kiblogu na kwenye chatrooms..

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 25, 2007

    1. kama hujui kingereza hata cha kuombea maji basi huwezi kuingia kwenye compute kabisa. Kama unadukuduku hizo options zilizowekwa hapo naamini utaelewa maana yake na hata ukijieleza kwa kiswahili "labda" utasikilizwa

    2. Ila ni wangapi wanacomputer au access ya computer? Kama kuna option njyingi za kueleza madoni , dukuduku na hii ni moja wapo basi hamna tatizo lakini kama hii ndio the only way to do that...This is bullshit.

    3. Kama mtu akitoa dukuduku itakuwa inaonyeshwa hadharani na wote tuweze kusoma swali na jibu au ukishaclick send ndio hivyo tena swali linaenda na litakapoishia hulioni au hata kujibiwa ndio hivyo ufuatilie miaka yote.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 25, 2007

    Kufahamu kingerezasio kuwa na akili nadhani anony ameteleza ulimi. Ila kujua lugha zaidi ya moja IQ yako inakua sharp sharp na zaidi ya yule anayejua lugha moja. Sasa kama wewe unajua kiswahili na kimanyema holla, kiswahili na kipare hola. Mkumbuke watoto wa siku hizi hawajui hata lugha ya baba au ya mama ni kiswahili tu sasa ili IQ iwe up ni heri ajue basi hata kingereza.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 25, 2007

    Kassim ma-beach boy wanajua kiingereza gani? Huyu rais wako mwenyewe hajui kiingereza halafu unataka kutwambia beach boy anajua kiingereza. Hivi unaposema mtu anaijua lugha unamaana gani? Labda utueleze kabla hatujaendelea na huu mjadala

    Ninadhani issue ni lugha mbili au zaidi na lugha iliyotumiwa hapa ni kiingereza. Kwahiyo anaejua kiingereza ana advantage over asiyejua kiingereza. Fact: 1. Exposure ni mfano mmoja na ni tishio kubwa kwa wanasiasa wengi wa kitanzania.

    Fact: Ukiangalia nchi za kiafrika zilizofanya "mapinduzi" (South Africa, Rwanda, Burundi, Zaire) na nchi nyingine nyingi zimefaanikiwa baada ya ushirikiano wa wapinzani walio ndani na nje ya nchi. Hao wapinzani walio nje wakiomba misaada hawaongei kizulu au chinyarwanda, bali wanaongea lugha za watu wanaowaomba misaada. They don't even speak beach english but they do speak english.

    Kwahiyo, anaetoa kamisheni ya kutengeneza hiyo tovuti anajua anacho kifanya.

    Don't come here and misslead people with your pinhead argument.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 25, 2007

    Upande wa kulia wa sura ya hito tovuti ina sehemu ya Kiswahili...kwa maana kuwa ukibofya hapo tovuti hiyo hiyo itafunguka kwa Kiswahili!

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 26, 2007

    Administration ya JK haina credebility why bother, ana wasikiliza wazugu tu! ataku sikiliza wewe!

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 28, 2007

    Sad FACT

    that majority of the comments on this post feel as though Tanzanians should continue to communicate in their own language and oust the other communities and cultures that want to do business with the country. Completely SAD... Sisi wote mafala ndo maana tuna liwa... Because we are so dum we want to proclaim our own ignorance...

    I think many Tanzanians who cant speak English are just intimidated by learning and overcoming their set backs... I think we are so scared to come out and show our real selves..... our literacy level was the highest in the region a few years ago, meaning in comparison to other states, we could read and write (in swahili), but guess what the world just didn't care whether we were reading or writing swahili...

    Nimesikitika....

    I've often told Michuzi to Blog in English, to expand his reach, Michuzi is popular amongst Tanzanians at large but imagine what accolades he can accomplish if the entire globe could understand his rhetoric escapades and constant contemporary insurgence to document the culture of Tanzania.. the people, the life, the land and most of all the community.

    For as long as we live in this general fear, we will keep being robbed by our leaders (Wahindi na Wabongo wenzio in banks and high official positions) .... And we will always live in the DARK..

    I say more power to English speaking people, more power to the Government for Embracing the 20th Century... Its not that we don't respect or love Swahili.. We speak it.. we speak it very well.. but we acknowledge that its not the language that will lead us to become Global players...

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 28, 2007

    SO UNTRUE

    There are so many chinese, japanese blogs on net. Do you read all that?

    You need to help other people to learn your language.

    The market/popular language in the US used to be spanish, german/deutch, mandarin and french but now so many people are lerning chinese....Why .....????? Go figure......

    be proud of who you are and other people will respect you more.

    I am supporting a multi language website.

    If one can speak two languages is fine, three languages that is even better more than three is superb....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...