katika kuongoza kwa mfano jk na mama wa kwanza salma kikwete leo wamekuwa watu wa kwanza kupima ngoma mara tu baada ya jk kuzindua rasmi kampeni ya kitaifa ya kupima kwa hiyari leo bustani ya mnazi mmoja gaden. tukio hilo lilirushwa laivu na kupokelewa kwa msisimko ambapo wadau wengi wamesema watapima baada ya kuona kumbe hamna noma wala nini endapo kama prezidaa mwenyewe na mai waifu wake wamefanya hivyo....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 14, 2007

    ama kweli kupima HIV kumwvamiwa, hata hivyo what a motivation kama president na wapinzani kina lipumba na Mbowe wamepima basi watu watajitokeza kwa wingi kujua status zao za ngoma. Ila bwana michu vipi majibu ya JK na mke wake? Na kina Lipumba na Mbowe je?
    watueleze majibu yao suala hapa si kupima tu ni kupima na kujua status au mnasemaje wadau?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 14, 2007

    Tunakusubiri Michuzi utupe kopi ya majibu yako wadau. Hii itaamasisha sanaaa watu kujitokeza kupinga ngoma saaaanaaaaa. Nakuaminia Michuuuuuuuuuzi

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 14, 2007

    sawa tumeona mh.prezidaaaa ametuonyesha njia ya kuelekea kupima tumekubali,sasa swali linakuja je,huyo mh.wetu akionekana anahawo washkaji kwenye mwili wake majibu yatatangazwa na wananchi wajue ili na wao wafuate mkondo wa mh?naomba kuwekwa bayana kwa hilo.kazi njema mkuu

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 14, 2007

    brother michuzi wewe umekwenda kupima?tunataka picha yako ukionekana unapima.
    thnx bro 4 gd work

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 14, 2007

    Hapo sio kuchukua Damu tuu wakienda kuimwaga baadae wapambe. Ilitakiwa mitambo yote ya kutest iwepo na process yote ya kuweka sample mpaka inaposoma matokeo iwe LIVE na kila mtu aone, ili iwe mfano kwa watakao kutwa wameathirika wasijifiche wajitangaze kwani kupima tu bila kuwa na hadhari ya kuwafanya walioathirika wawalinde wengine zoezi hili litakuwa halijafikia malengo yake

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 14, 2007

    hii propaganda,kajitosa sababu in private,alishapewa all is clear

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 14, 2007

    Hata akikutwa na ngoma nani atatangaza? Wacheni unywanywa!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 14, 2007

    Raisi mwenyewe awe mfano,lazima kila mtu apime. kama mama hana haimaanishi mzee naye hana. Kila mtu akapime

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 14, 2007

    samahani sikumuona mzee pale...saa tutajua majibu yao au siri yao :D

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 14, 2007

    A way to go.

    Tumuombe Mungu watu watakao pima majibu yakitoka asilimia isiwe kubwa sana ya watu wenye virusi.

    Mungu ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 14, 2007

    sawa,,lakiniiiii..

    watatangaza matokeo au ni *siri*,,kama kweli ni UWAZI?

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 14, 2007

    Great example.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 14, 2007

    Je majibu ya prezidwa yatatangazwa? Sababu kupima sio tatizo, unaweza ukapima na majibu ikawa siri yako, kama mtu unapima na kutangaza hapo poa.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 14, 2007

    the whole ya ya kupima sio kutangazia watu umzima au mgonjwa...point ni pima jua status yako mwenyewe then do the right thing kama mzima kuwa mwangalifu zaidi na kama positive anza kuishi lifestyle inayoshauriwa na wataalam ....sio upime then uanze kuwatangazia watu majibu yako ni yako tuu na daktari wako.

    ReplyDelete
  15. Prez - kapima... safi sana... lakini sidhani na wala sitegemei kusoma matokeo yake (hiyo siku itakuwa siku kweli)... by ze way - watasema tu "majibu siri ya mtu na dakitari wake" na hapo udodoso ndo utakuwa umepigwa breki

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 14, 2007

    Pamoja na kupima na kujua, itasaidia maambukizi, lakini waadhirika watatibiwa wao wapi na watapata wapi huduma nyinginezo. jengeni hospitali zenye vifaa sio kujipigisha picha eti mnapimwa.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 14, 2007

    Enyi ndugu zangu mnaotaka kujua status za wenzetu walioko katika siasa Tanzania nyinyi mmeshapima na kujua status zenu? au mnaandika kuosha domo? FYI-FOR YOUR INFORMATION!kila mtu anawajibu wa kupima na kujua status yake kwa ufupi, suala la kutangaza majibu ya mtu kuwa negative/positive ni la mtu binafsi kama ilivyo katika kupima unaweza kaa kimya ukaenda kinyemela bila kujitangaza. Kwa waliopima wakishatangaza majibu yao kama wana ngoma au la nyinyi mtafanya nini katika maisha yao? wengi wao tayari wanasemekana wana ngoma hapo kati ya waliojitokeza kupima tokana na tabia zao katika jamii na mifano hai ya watu wangapi wamewauwa kwa kutembea nao... kila mtu ashike lake, hao ni wanasiasa na nyie ni wananchi mmnaonyeshwa mfano bora na vingozi wetu kwa ujumla nanyi fanyeni hima mkapime mjue kama safari zenu zitakua kwa ngoma au la! sio kutaka kujua watatangaza matokea au la! eeh wabongo! Noma! udaku kutwa! alieleta neno waosha vinywa hakukosea kwa kweli! duh! mmnachonga sana!

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 14, 2007

    Wabongo kwa kunung'unika. Hamna jema asingeenda kupima mngesema amekwenda kupima mmesimama juu kama nini. Suala lilikua kupima na sio kupima na kutangaza kwa watu. Majibu ukipewa ni wewe utajua la kufanya na Mungu wako au lawyer wako.

    Ila ningeomba serikali ifanye kuwa ni lazima mtu ukienda hospital kwa ugonjwa wowote lazima wakupime wajue ukoje.
    Nchi zingine wenye networks doctors file lako lina haya yote na kwenda emergency siku hizi ni lazima wanakupima pia. Ila hawamtangazii yeyote.

    Ila huo ndio mwanzo..Enough is enough jamani

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 15, 2007

    hihi ama kweli wabongo ndio kichwa cha wendawazimu sasa ya nini rais na mkwewe wanaende kupima na ata mbowe na viongozi wote wakienda kupima , hivi unaweza kutoa majibu ya kweli kama umeweza kuwaficha wala rushwa, wanaoiba kodi, wenye kuwatoza kodi ndogo na kuwa makapuni ya kigeni maliasili na hii ndio kitu kidogo kama watu wanataka kwenda kupima ni wajibu wao ila swala hapa ni hawa viongozi na watu wenye mapesa ndio wengi wao huu ugonjwa na pia wanaonga binti zetu, dada zetu wa pesa pesa swala hapa ni kuwaelimisha watu umuhimu wa ugonjwa huu sio viongozi kwenda kupima so what hata kama je wananchi ukweli watajua ...ili ni swali ?? je ...waandishi wa habari msigojea mpaka umeletewa habari na viongozi na mfanye kama wao wanavyotaka wajibu wa kazi yenu ni kutafuta ukweli na ushahidi wa habari ndio mzitoa kwenye vyombo vya habari hapo ni mtakuwa mmetumia proffesional yenu.. hihihihi mkereketwa yupo njia ...hihihi

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 15, 2007

    Swala la kampeni ya kupima Ukimwi SI kufahamu afya ya mtu mwingine, maana ukifahamu mtu ni HIV+ au -, haikusaidii maana watu wanapofanya ngono hatari huwa hawana takwimu ya kucheki, huyu nafahamu afya yake, huyu sifahamu. Dhima kubwa ni kuondoa ile hofu kuwa kupima hakuwezekaniki, wanaopima wanakufa nk. Pia ni kuongeza idadi ya watu wanaoptata ushauri nasaha, maana kabla ya kupima, ama utakubali au kukataa, kuna wasaa wa kuongea na mshauri na kupata mawazo tofauti na yako. Kwa hiyo, hilo swala la Kikwete anao au hana, itamhusu sana yeye ili ajue anajiandaa vipi kiafya na kifamilia, kama akiwa anao au hana. Tuwe tunaona mambo kwa umbali, na umbea wa kiswahili kuwa nani anao nani hana tuuache. By the way, sasa Ukimwi ukiwa nao unaweza kuishi miaka 20 (10 ya virusi kuwa ugonjwa, 10+ ya ugonjwa kuharibu mwili). Sasa Miaka 20 ya Ukimwi, linganisha na magonjwa yetu ya kila siku Tanzania (Malaria, Kansa ya mapafu, nk).

    Michu wacha nitoe hoja.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 15, 2007

    Anko michuzzzzzzzzz!
    Hii kitu ya kuonesha mtu anapima ngoma live inaweza ikaleta matatizo makubwa sana... mie ni mdau ninayesoma psycholojia.. katika kitu kama hichi kinaweza kikasababishwa watu waone kuwa kupima ngona ni kitu cha lazima... itamfanya mtu aende akapima ati kwasababu mtu fulani fulani naye kaenda kapima na sio kuwa anataka kwa hiyari yake.
    Pia ukiangalia kwa upande mwingine inatoa maana kabisa ya VCT.... kwa watu ambao awafikirii kwa mbali wanaweza wakaona kuwa kitu kama hiki sio cha siri.... wakati kupima ngoma ni kitu kinachotakiwa kiwe cha siri sana na sio kuoneshwa kwenye kideo.... kama kweli angetaka kuonesha watu angeoneshwa anaingia kwenye chumba cha ushauri na kuoneshwa anatoka na sio kuoneshwa paka anatolewa damu...

    Naomba Tanzania tuangalie ivi vitu vidogo vidogo tunavyofanya vinaweza vikasababisha maafa makubwa katika akili ya mtu na kubadilisha tabia zake.
    Ningependa kuwakilisha.

    ReplyDelete
  22. hiko ni kiini macho tu, hivo vidamu walivyofyonza vya mhe. Rais wa jamhuri ya muuungano wa waTanzania vitachukuwaliwa na waliinzi wake wala havitafika maabara ya kidudu mtu yeyote.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 15, 2007

    Hivi wadau wa hii blog mna matatizo gani ? kwa nini mnapinga tuu hata kama jambo ni zuri ? nina imani kuna watu wanaweza kupinga JK hata akijenga barabara au hospitali kijijini kwao ! Let us be honest and give credit where it is due.

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 15, 2007

    anon wa july 15,2007 7:03:00AM
    napinga hoja yako.Hofu ya wengi ya kupimwa HIV siyo kule kujitokeza na kwenda kupimwa bali ni matokeo ya kupimwa.Kwahiyo unaposema kampeni ina lengo la kuwaondoa wananchi hofu kwavile tu watakapomuona Rais amekwishapima nao watahamasika si kweli.Hakuna mtu anayeogopa kupima.Swala la kwenda kutobolewa vein na kutolewa damu hakuna anayeliogopa,kwani haliui na wala halina maumivu ya kutisha.Watu wanachohofia ni matokeo ya kipimo,jee kama wataonekana HIV+,itakuwaje??Ndo maana wadau wengine wamesisitiza kuhusu kuwekwa wazi kwa matokeo ya waheshimiwa.Hii itasaidia pia hata kuondoa unyanyapaa kwa wagonjwa kwa sababu Kama nikijua mbunge wangu kwa mfano amepima na kugundulika kuwa anao nami itaniongezea kujiamini na kwenda kupima,nikijua jamii haitanishangaa na haitaninyanyapaa,kwavile hata viongozi pia nao wanaishi na virusi.Huku ndo kuwaondoa wananchi woga-kupima tu haitoshi,na majibu pia yasifichwe.
    Unaposema ukifahamu mtu ni HIV+,haisaidii unakosea sana,na nyinyi ndo mnasababisha watanzania tupukutike kama kuku wa mdondo kwa hili gonjwa.Tabia mbaya sana ya usiri tanzania.Kama tukiwa na dhati hasa ya kutokomeza hili gonjwa basi tuwe wazi,tusifiche.Tujue nani mgonjwa nani hana,nani kafa kwa HIV nani kwa malaria.
    naomba kutoa hoja michu

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 16, 2007

    Hivi wewe michuzi una matatizo gani? mbona huweki coments zangu? i see unaitia hasira kinomaaaa ngoja ntajaribu tena kutuma nisipooan utantibua natkautandika vibokoo haswaaa lione vile!

    ReplyDelete
  26. Rais amepima ili kuwapa moyo watu wapime. Majibu yaweje hayatuhusu. Mtu unapojua status yako ya afya unajua uiishije. Swali langu je serikali ina huduma gani inayotoa kwa walio positive? mfano nchi nyingine kwa wale walio positive wanatoa dawa za magonjwa yote bure, wanatoa madawa ya kuongeza maisha bure, wanatoa condoms bure, kwa wagonjwa ambao hawana kipato kabisa wanawapa at least once per month gunia la mchele, mafuta, sukari etc bure.

    Halafu wamejitahidi kueelimsha uma kwamba ni ugonjwa kama wowote hivyo watu wanaishi kwenye family zao bila kunyanyaswa. Tanzania hata kumpa mkono tu mtu mwenye virusi wanadhani wamesha ambukizwa sasa watu wataachaje kujificha? ndoo maana tunapukutika unfortuantely.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...