huko nyuma kuna mjadala mkali kuhusu matumizi ya bendera ya taifa. katika kuuendeleza naomba kuuliza kama huyu dada kapatia ama kakosea kuvaa hivi?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 38 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 10, 2007

    hajakosea...there is nothing wrong with wearing ur flag as a shirt a dress or otherwise...i'd call it PRIDE.Bendera za wenzetu zinajulikana sana..because they wear them all the time..kwenye tshirts,kofia,wanabandika kwenye magari, and stuff like that.
    step out of Tanzania and no one knows much about our flag but us and a few neighbouring countries..the government or whoever is discussing such use as a MISUSE needs to check themselves before discussing this to the contrary..its PRIDE and its GOOD for the country as a whole..
    Flag of Jamaica,Italy, UK, USA and so forth..are all over this world..why not we wear ours and get it somewhere...she is very right and more of us should follw the lead..

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 10, 2007

    HAJAKOSEA. SOMA HOTUBA YA KWANZA YA RAIS BUNGENI TAREHE 30 DISEMBA 2005.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 10, 2007

    HAJAKOSEA. SOMA HOTUBA YA KWANZA YA RAIS BUNGENI TAREHE 30 DISEMBA 2005

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 10, 2007

    Kapatia sana na hakuna tatizo kabisa!

    Haba Bongo tunadanganyana: kila siku tunaona bendera kama za Marekani, Panama, UK, etc etc na wengine wamekufuru mpaka kuonyesha bendera kama ile ya confederate flag za Marekani, na mabasi mengine yana Swastika za Hitler na nimeona mtu kavaa t-shirt ina bendera ya SS ya wale askari wauwaji wa Hitler (yote haya ni kutokana na uelewa finyu wa wengi wetu!)Iweje hawa waonekane ni sawa na wananchi wetu waonekane wanafanya makosa wakivaa nguo zina bendera za nchi yetiu???!!!

    Sasa sioni tatizo la mtu kuvaa bendera yetu namna hii - in fact, inabidi ziwe nyingi zaidi na sio wakati wa Taifa Stars wakicheza!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 10, 2007

    Hajakosea, wengine inatakiwa tumuige huyu dada.Tusipovaa nguo zenye bendera ya Taifa letu wanataka tukavaa nguo zenye rangi za bendera za nje? Tutatakiwa tujivunie kuvaa nguo zenye rangi yabendera yetu na sio kuiogopa.Watanzania tunatakiwa tubadilike kwa hili.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 10, 2007

    mimi sioni kosa lolote,ingawa kila nchi ina sheria na taratibu zake kuhusu national emblems but still I see no offensive dressing like that.for restance here in the u.s.a the so said big and developed nation,the flag is even made to be won as bras,underweares and nobody qn abt that.tanzania tumefikia wakati tuwe na mitazamo ya kimaendeleo zaidi kulikoni kufuatilia vitu ambavyo havina kichwa wala miguu,kwa mfano kuna magwanda{military jezz} zinafanana na nguo za jeshi la tz zinauzwa hapa kwenye regular cloth stores,ukinunua na uzivae tz utajikuta polis or wanajeshi wanakukamata,je hio ni haki?kwa maaana nguo hizo zinauzwa na mtu kapendezwa nazo kanunua je hapo ni makosa ya aliyonunua or mtengenezaji?nasema hao wanajeshi na polis nadhani wanashughuli nyingi za maana zaidi ambazo walitakiwa wazitelekeze kulikoni kufuatilia mambo kama ambavyo nimeelza hapo juu.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 10, 2007

    Bwana michuzi hapa sioni ubaya huyo mama anaonenesha mapenzi kwa taifa letu na kujivunia utaifa wake.bwana mMichuzi ingelikua vizuri kama picha hii ungeiweka sambamba na picha ambazo zinonyesha bendera yetu inafutiwa miguu katika uwanja wa ndege wakati wa mapokezi ya viongozi mbalimbali kibaya zaidi ni kuona watu wanaoshiriki katika zoezi ili ni viongozi wa juu.Pia Bendera yetu ambayo inapashwa kuheshimiwa katika bunge unafutiwa miguu.Kama mimi ningelikua Rais au kiongozi wa juu au mbunge kama ningeshindwa kuwashawishi viongozi wenzangu kubadiri taratibu za kudhalilisha BENDERA yetu basi ningelikua navua viatu wakati wa kuwapokea viongozi wa juu wakati wa mapokezi ya Viongozi mbali mbali katika uwanja wa ndenge au katika jengo la bunge.Kama inabidi kusimama wakati wa kushusha na kupandisha bendera ninapoikuta bendera katika janvi jekundu katika jumba la bunge na viwanja vya ndege kwa vile iko chini basi inanibidi nitembe kwa mikono au kichwa miguu juu.Kitendo hiki nakifananisha na kupiga na kucheza wimbowa taifa katika disko au kilabuni.Hivyo naomba Bwana michuzi kama kunauwezekano ziweke picha hizo sambamba.MUNGU IBARIKI TANZANIA.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 10, 2007

    sioni kama kuna ubaya kwa mtu kuvaa rangi za bendera yako unless kama sheria za nchi zinakataza

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 10, 2007

    Kwanza kabisa amegeuza hiyo bendera juu chini, kijani huwa juu na bluu huwa chini.Angalau basi kama aneamua kuivaa bendera ya taifa angehakikisha iko sahihi.

    Njia nzuri zaidi ya kuonyesha uzalendo katika mavazi ni kuvaa rangi za bendera ya taifa na sio bendera yenyewe. Kwa kufanya hivyo, unakuwa umeonyesha uzalendo lakini pia heshima ya bendera inabaki pale pale. Tukiangalia nchi nyingi za wenzetu mara nyingi rangi ndio zinavaliwa na sio bendera yenyewe.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 10, 2007

    yaani huyo ndio kapatia kweli kweli, sio kama wale vijana wengine tunaovaa vilemba vya bendera ya marekani wakati hata kenya tu hatuna uwezo wa kufika. Mimi namfagilia sana. Suala sio kuvaa ukiwa umevaa suti, vaa hata kama uko bwiii kwa vile wewe ni mtanzania. Sasa niulize jamani, wewe kama baba yako sio mzuri anachemsha katika maisha yake, utamkataa alafu uchague baba wa mtu mwingine. No way, mimi nasema huyu amenifurahisha saaaaana.
    Tena naunga mkono jitihada za kuvaa mavazi yenye bendera ya kwetu. Tujulikane kidogo jamani

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 10, 2007

    Kulikuwa na enzi fulani ambapo kuwa M'bongo ilikuwa kama laana.
    Time zimebadilika,Mungu katuonyesha njia.Kuwa Mtanzania sasa ni Babkubwa.Na huyu mama namshukuru kwa pride aliyonayo ;Mungu ambariki.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 10, 2007

    Kapati sana , alafu katoka bomba sana, hadi mtindi umeonekana.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 10, 2007

    Huyu kakosea sana. Na kwa vile inaonekana kafanya kwa kukusudia basi afikishwe kwenye vyombo vya sheria bila dhamana na hukumu yake bila shaka ni kuninginizwa tu. Pia kesi yake iendeshwe haraka hata wengine wakinung'unika potelea mbali.
    Naomba kutoa hoja na sitaki matusi!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 10, 2007

    Yuko sawa!

    Hii nchi kwani ina wenyewe? Mbona haina dira? Kila kitu hovyohovyo kama vile all of its people are fools. I'm sorry but it's a fact. Madini yanavunwa wenyewe hawapati kitu. Rushwa zasemwa kila kukicha hakuna cha maana kifanyikacho.

    Mauzi mauzi mauzi tu mafuta juu eti wana nia ya kuzuia mfumuko wa bei! na nawaambieni msipoingia mtaani kupigania haki yenu mtakwisha! Wachache tu watatumia tigo zenu. Mtajiju!

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 10, 2007

    Mbona suala hili lilishapitishwa na Rais Kikwete katika hotuba yake ya tarehe 30 Desemba 2005 na pia juzi tu tarehe 6 Julai 2007 wakati wa Maonesho ya SABASABA, Rais Kikwete alipotembelea banda la WIPE la akinamama alioneshwa fulana 'car wash' yenye mchoro wa bendera kama alivyovaa huyu dada na Rais akamuagiza yule mama mbunifu aliyefuma fulana hizo kutengeneza za kutosha wachezaji wote wa 'Taifa Stars' na yeye Mhe. Rais atawanunulia wachezaji wote zitakapokuwa tayari. Hapo ni kwamba Mhe. Rais alishatoa kibali na alikuwa anasisitiza. Kama Mhe. Rais ameshasema nani tena mwingine ataweza kuzungumza vinginevyo? katika picha ya hapo juu dosari ni kwamba huyu dada ni kweli bendera ameigeuza, rangi ya bluu siku zote huwa chini na ya kijani huwa juu, watu wengi hukosea.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 10, 2007

    Hakuna ubaya. Kavaa bendera na mwenge kwa makusudi maalumu...sherehe za taifa!

    Inatokana na nguvu mpya, nguvu mpya na kasi mpya za ku-instil uzalendo!

    ReplyDelete
  17. hakuna ubaya kuvaa ivo, na si hivyo tu inabidi hata serikali ikituuzi basi tuwe na haki pia ya kuichoma moto hiyo bendera. Kwa ivo isiwe tu kuivaa bali pia kuichoma moto ili kuionesha serikali kutokubaliana nayo ktk jambo fulani!

    ReplyDelete
  18. Hakuna dhambi kabisa katika hilo. Kwa wenzetu ni mambo ya kawaida kutanguliza bendera za taifa, sisi tunatanguliza za vyama. Si kwa kujali maslahi ya vyama , bali yetu binafsi. Niunafiki mtupu!

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 10, 2007

    Mara nyingi watu wana wanatoa mfano wa Wamarekani jinsi wanavyovaa bendera yao kama uzalendo. Ukweli wa mambo ni kuwa wanavunja sheria ya nchi yao. Mmarekani anasheria ambayo inakataza kuvaa flag na nimeinukuu hapa: The United States Flag Code Section 8 part d: The flag should never be used as wearing apparel, bedding, or drapery. It should never be festooned, drawn back, nor up, in folds, but always allowed to fall free. Bunting of blue, white, and red, always arranged with the blue above, the white in the middle, and the red below, should be used for covering a speaker's desk, draping the front of the platform, and for decoration in general.

    Just because wamarekani wengi wako ignorant na sheria zao haimaanishi kuwa tuwaunge mkono.

    Sasa najua wepesi wa kuandika watataka kunijibu na kuniuliza mbona hata Olympic Team zao zinavaa flag. Hiyo si kweli, katika "official events" unapoona american flag imevaliwa ukweli ni kwamba ni rangi za bendera, mistari na nyota, lakini sio bendera kamili. Ni muhimu watu watofautishe bendera na rangi za bendera. Kuna mtu ameongelea majamvi ya airport na bungeni, pale airport sinauhakika ni nini kimewekwa kwenye jamvi lakini bungeni kwenye janvi sio bendera bali ni rangi za bendera. Kumbukeni bendera yetu ina diagonal lines lakini kwenye jamvi la bunge zile rangi ni parallel not only that but the blue is disproportional larger than the other colours and to be precise the colours on the jamvi at bungeni are green-yellow-black- yellow-blue-yellow-black-yellow-green therefore it is not the flag.

    Tunaweza tuka argue kuwa dada kwenye picha hii hajavaa bendera kwa kuwa ameshola shati lake kwa kutumia bendera juu chini. Kwa mfano huu ambao Michuzi ameutoa, it could be argued that technically she is not wearing the flag.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 10, 2007

    Mheshimiwa Spika: Waheshimiwa Wabunge: Serikali ya Awamu ya Nne inakusudia, miongoni mwa mambo mengine, kuimarisha utaifa wetu kwa kufanya mambo kumi yafuatayo:

    Kwanza, kutumia mfumo wa elimu kujenga na kuimarisha umoja wa kitaifa, , ikiwemo kutenga shule za Sekondari za Kitaifa zitakazochanganya kwa makusudi wanafunzi wenye vipaji mbalimbali kutoka pembe zote za Tanzania;

    Pili, kuandaa mitaala ya somo la uraia itakayopanda mbegu za uzalendo na umoja wa kitaifa katika ngazi zote za elimu;

    Tatu, kuzipa changamoto shule za mashirika ya dini, isipokuwa seminari, kupokea wanafunzi wa dini zote;

    Nne, kuendeleza kazi nzuri iliyoanzishwa na Serikali ya Awamu ya Tatu ya kufufua Jeshi la Kujenga Taifa;

    Tano, kujenga muafaka baina ya vyama na makundi ya jamii juu ya utambuzi wa, na kuheshimu, tunu za kitaifa kama vile haki, usawa, umoja na mshikamano.

    Sita, kutumia michezo, nyimbo na sanaa kuimarisha hisia za utaifa na kujenga uzalengo na kuipenda nchi;

    SABA, KUENEZA NA KURUHUSU MATUMIZI YA ALAMA ZA KITAIFA KAMA MAMBO YA KILA RAIA KUJIVUNA NAYO NA KUYAHESHIMU SANA;

    Nane, kujenga na kuimarisha mahusiano kati ya dini, vyama vya siasa na makundi mbalimbali ya jamii;

    Tisa, kuteua Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais atakayeshughulikia mahusiano kati ya vyama vya siasa, dini na makundi mbalimbali ya jamii; na

    Kumi, kuimarisha utaratibu wa mazungumzo ili kutatua mapema migogoro katika jamii.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 10, 2007

    Anony wa July 10, 2007 9:41:00 AM EAT sikubaliani na wewe kuhusiana na nguo zinazofanania na za kijeshi.

    Kwa kawaida hizi zimeleta utatanishi kwa watu wengi sana hapa bongo kwani imeshatokea majambazi yamevaa combat feki na wananchi wakaelewa walikuwa wanajeshi!

    Vilevile, mbona sijawaona watu hao wakivaa "Dominoes Pizza Delivery" au "Mortuary Attendant" etc etc with pride ya kama wavaapo replica combat? And don't tell me eti hizi zina watu wake wanaofanya kazi huko - because so does combats zina watu ambao ni wanajeshi!!

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 10, 2007

    Michuzi,

    Hili sio swali la kuuliza--wakina Mkwawa, Kinjikitile na wengine waliokufa kwa ajili ya TZ nadhani watakuwa wanageuka huko makabulini saizi wanavyosikia huu mjadala. Ili tuenedelee lazima tujipende na tuonyeshe kwamba tunajipenda na kupeperusha bendela yetu ndio njia mojawapo yakuonyesha hilo. Naona Michuzi unaendeleza hii mjadale, CCM wamekutuma nini? Nadhani wao kinacho wasumbuwa ni kwamba sasa hata kama walala hoi kama sisi tutapeperusha bendela je wao the so called wakubwa watajulikana vipi? Tell them kuwa vijana tunaanza taratibu kudai uhuru wetu. Uhuru wakufanya chochote tunachotaka alimradi hatuja vunja sheria ambayo inaendana na wakati.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 10, 2007

    This looks great and we want to have as many as possible all around the world Tanzania hoyeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 10, 2007

    Kwakuwa sheria haijabadilika wala kufutwa, kisheria kakkosea. ila kijamii kapatia kabisa.

    ReplyDelete
  25. yaani hajakosea kabisaaaaaa...ila alichokosea ni bendera yenyewe....nadhani hakuna nchi yenye maji juu halafu ardhi ikawa chini...just kakosea hiyo rangi ya bluu na kijani.

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 10, 2007

    mimi bado dinosour bendera ya china haivaliwi kiovyoovyo wala ya n korea but kila mtu aijua ingebakia kama ilivyokuwa mwanzo you have to be fit and aproved kuvaa bendera ibakie kama nyara za serikali . mnajua kama bata maji wote uk ni mali ya queen?? it is special. lazima tuwe kivyetu bendera iwe ya timu ya taifa na wanariadha na watu wanao liwakilisha taifa or mashujaa na watu ,... ithink you can see ninakotoka. nawimbo wa taifa ubakie nyara pia nakuimba kwake tuwe wakakamavu kama tradition yetu na si kuweka mkono kifuani . then msemo wa "kanywa maji ya bendera" utaenda wapi? tusiige tu jamani tutapoteza tamaduni zetu hivihivi.bendera is not just piece of cloth man !!dos

    ReplyDelete
  27. AnonymousJuly 10, 2007

    BRO MICHU KUNA WATU WALIKUULIZA KUHUSU MPAKANJIA...

    wasome hii kutoka IPP

    Mpakanjia avunja ukimya

    2007-07-10 18:11:51
    Na Badru Kimwaga, Jijini


    Mfanyabiashara maarufu nchini na aliyekuwa mume wa Mbunge wa Viti Maalum-UVCCM, marehemu Amina Chifupa, Bwana Mohammed Mpakanjia amevunja ukimya na kushusha skadi zito kwa wale aliosema wanamuombea kifo.

    Akizungumza na gazeti hili mapema leo, Bw. Mpakanjia amesema anashangaa sana kusikia akiambiwa anaumwa na yu mahututi hospitalini wakati ukweli ni kwamba ni mzima wa afya na anaendelea na kazi zake.

    Bw. Mpakanjia maarufu kwa jina la Meddy, amesema hajui taarifa za kulazwa wodi maalum katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akiwa hali wala kunywa, watu wanazipata wapi na kwa malengo gani.

    ``Mimi mwenyewe nimeshtushwa na taarifa hizo ?ndugu yangu nashindwa kujua wanaodai mimi nimelazwa Muhimbili nikiwa hoi, sili wala kunywa wananitakia kitu gani, wakati mi ni mzima wa afya na ninaendelea na kazi zangu za kila siku za kulijenga taifa hili,\" Bw Mpakanjia akasema.

    Amedai kuwa amekuwa akipata usumbufu mkubwa toka kwa ndugu, jamaa na marafiki zake walioko ndani na nje ya nchi wakitaka kujua ukweli kuhusu afya yake.

    ``Nimekuwa nikipata usumbufu wa kupigiwa simu kuulizwa juu ya uzima wangu na ninapowajibu kuwa niko fiti, hubaki hawaamini,``.

    Amesema watu waliosoma taarifa kuhusu yeye kuwa mgonjwa, walipomuona jana akipita akiwa ndani ya gari lake, walimshangaa kiasi cha baadhi kumsimamisha na kumuuliza kulikoni.

    ``Niliwataka wapuuze uzushi wanaousikia kwani wanayemuona ni Meddy kamili na yuko fiti,`` akasema.

    Taarifa za kuumwa kwa Mpakanjia zilianza kuvuma siku chache baada ya kifo cha aliyekuwa mkewe ambaye alifariki dunia wiki mbili zilizopita na kuzikwa kijijini kwao Lupembe, wilayani Njombe mkoani Iringa.

    Mbunge huyo aliyekuwa machachari tangu aingie bungeni miezi 18 tu iliyopita, alifariki, siku ya kilele cha kupambana na dawa za kulevya.

    ReplyDelete
  28. AnonymousJuly 10, 2007

    HUYU KAKOSEA SAANA AFUNGWE SIO CHINI YA MIAKA 10 JELA! HII HAITAKIWI KUVAA BENDERA YA NCHI.

    ReplyDelete
  29. AnonymousJuly 10, 2007

    Amevaa rangi za Bendera yetu, Taifa stars wanafanya hivyo pia. Si lazima uvae Bendera yenyewe.

    Majority ya timu za taifa huvaa rangi za bendera yao, mfano Brazil au German. si lazima iwe ktk mpangilio wa Bendera halisi.

    Hili swali kwako kaka Michuzi, wewe binafsi unaona kuna nongwa gani kupenda na kuvaa rangi za taifa ?
    ..ukiweza saidia, sitisha mijadala ya aina hii .

    ReplyDelete
  30. Aisee yaani safi sana maendeleo sio kujenga barabara na stadium hili nalo ni moja ya maendeleo. hongera kikwete kwani kuna baadhi ya wa bongo hata bendera yao walikuwa hawaijui.

    ReplyDelete
  31. AnonymousJuly 10, 2007

    Huyo Dada kuvaa hivyo hana tatizo lolote, iwe inakatazwa na serikali au la. Kwasababu alichovaa si bendera ya taifa ni T-shirt yenye rangi zinazofanana na bendera ya taifa la tanzania.

    Na kwanini serikali ikataze au hata kama ilikuwa inakataza ni kwamba ilikuwa inakataza uzalendo. Lakini ya ccm rukhsa, hata kofia inatengenezewa.

    ReplyDelete
  32. AnonymousJuly 11, 2007

    Mimi nadhani kuwa hili swala wala hatupaswi kulijadili maana halina tatizo. Kuvaa bendera sii makosa. Nakumbuka mwaka fulani mwana riadha wetu alishinda medaliya dhahabu lakini bendera haikupatikana ilibidi itafutwe kama dk 15 na tano hivi lakini nchi nyingine zilikuwa zimetapakaza bendera zao inabidi tujivunie bendera yetu na tuionyeshe

    ReplyDelete
  33. AnonymousJuly 11, 2007

    Where is the pride, patriotism – Musirudishe u-communists, Hata CHUPI tengeneza na vaa, BE PROUD OF YOUR COUNTRY = “This will be the day when all of God's children will be able to sing with a new meaning, "My country, 'tis of thee, sweet land of liberty, of thee I sing. Land where my fathers died, land of the pilgrim's pride, from every mountainside, let freedom ring."

    ReplyDelete
  34. AnonymousJuly 11, 2007

    Mheshimiwa ISSA..HABARI ZA LEO KAKA..TUNASHUKURU KWA KAZI YAKO..BENDERA YA TAIFA INAHITAJI HESHIMA YAKE NA SIONI TATIZO KUIVAA K.M WANAMICHEZO AU MTANZANIA/MGENI ANAEJISIKIA...MZEE NAONA DADA KAKUSHAWISHI ANAFAHAMU KUCHEZA NGOMA HUYU..

    ReplyDelete
  35. AnonymousJuly 11, 2007

    mheshimiwa ISSA.HABARI ZAKO,MIMI NAONA HUYU DADA KOSA NILA FUNDI ALIESHONA NGUO HIYO.KAWAIDA RANGI BLUE INAKUWA CHINI NA KIJANI JUU. HII INAONYESHA WENGI HAYAJUI NEMBO ZA TAIFA LETU IKO HAJA NYIE WAANDISHI WA HABARI INABIDI MTUMIE ZAIDI NEMBO KTK MAKALA ZENU ILI LAU WAZOEE KUZIONA NAKUZIFAHMU
    PETER NSHISHI-POLISI KILIMANJARO

    ReplyDelete
  36. AnonymousJuly 11, 2007

    KWANZA AMEVAA RANGI SAWA NA BENDERA YA TAIFA, LAKINI MPANGILIO WA RANGI SIO BENDERA YA TAIFA.

    BILI TUWE SERIOUS KIDOGO, KWA SHERIA ZA SASA KUVAA BENDERA ZA TAIFA BILA KIBALI MAALUM NI KOSA LA JINAI, NDIO MAANA KWENYE MAAZIMISHO YA MIAKA 45 WAZIRI MKUU AIDHINISHA KWA MUDA.

    KWA HIYO KWA SHERIA ZA SASA HILO NI KOSA KUBWA

    ReplyDelete
  37. AnonymousJuly 14, 2007

    I'd hit that!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...