baada ya handakizzz naona tuhamie kwenye miundombinu mingine ya dar ambayo inachekesha. siishi kujiuliza kwa nini bahari ya hindi wakazi wa dar wanaisikia kwenye bomba tu kwani imezungusshiwa senyenge yote kuanzia bandarini hadi feri. ukiuliza unaambiwa ni eneo la bandari na linahitaji kuwe na usalama. mbona awali walalahoi ndipo walikoponea kupunga upepo na kununua kacholi hapo mahali hata pakaitwa bombay? hapo sijaenda bado bustani ya mnazi mmoja gaden ambako kutwa inapigwa kufuli ati watu wataichafua. kukiwa na sherehe inafunguliwa. hahahaa bongo bwana.... sijui wahusika hawatembeleagi kwa wenzetu kama

kwa watani wetu wa jadi na kwa m7 waone jinsi walipa kodi wanavyofaidi jasho lao?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 10, 2007

    Chukua tano Michuzi. Maranyingi tunafanya vitu vyetu kinyume nyume.Kwa sisi wapanda daladala hiyo ndio ilikuwa Beach yetu ya karibu.Kwenda Coco na beach nyingine hunaitaji private car kwa sababu zipo mbali na vituo vya public transport.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 10, 2007

    yeah,its okay for them to lock the hell of it coz if they let it open to everyone,the bongos will go on pupp & pee on the ocean banks leaving a stinking smell

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 10, 2007

    kwa kweli kaka michuzi tanzania tunachekesha sana na si kwamba viongozi wetu hawatembelei nchi za nje hapana, bali wanatenbelea kwa manufaa yao tu na si ya wananchi, kwa mfano bustani ile ilitakiwa kuwa wazi kwa watu kupumzika na kujengewa sehemu za kukaa na walinzi na wafanya usafi wawepo muda woote, kwa mfano mie niko capetown, yaani kuna bustani kuuuubwa kwa ajili ya wananchi kukaa karibu na ofisi ya bunge na pia bandarini kwao panaitwa waterfront yaani ni pazuri na kuna entertainment za kila aina, ngoma zaidi ya 20, kuna malls zenye maduka zaidi ya 1000, hotelna kila kitu yaani watu ni kuingia na kutoka usalama wa kutosha, watalii hawakauki ndo maana wakati mwingine naona kama sisi tumejiloga wenyewe, lakini naamini kuna siku tutapata viongozi wenye nia kweli ya kuendeleze nchi na si wao wenyewe, tuombe Mungu tu

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 10, 2007

    Sababu nadhani unayo bwana Michuzi Ustaarabu ni kitu cha bure wala siyo lazima uwende shule upate shahada ya USTAARABU. Sasa kama tunashindwa kuufanya kwa vitendo wacha JIJI wafunge hayo maeneo. Unaona kwenda kujisaidia kwenye choo ni hatari mpaka ukajisaidie bustani ya Mnazi Mmoja nani atavumilia. Na tangu yafungwe hatujaona hata mtu mmoja kajinyea barabarani sababu Mnazi Mmoja imefungwa, hivyo basi kumbe kuna sehemu zingine mnaweza kwenda kujisaidia zaidi ya Feri na mnazi mmoja. Mtaona hayo maeneo kwa nje hivyohivyo mpaka mtakapojirekebisha. Na pole ziwaendee wale wastaarabu wachache wanaotumia bustani kwa matumizi yanayostahili kwa kukumbwa na tatizo hili lililosababishwa na watu waliokosa ustaarabu. Kwenda kwenye vyoo vya kulipia mnaona dili nenda basi kaombe kwenye nyumba za jirani na maeneno hayo mmalize shughuli zenu na muiache bustani iwe bustani, au beach iwe beach na siyo maficho wa vibaka na watumiaji wa madawa ya kulevya. Dawa ya moto ni moto tu, Keep it up JIJI

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 10, 2007

    Jiji wamefanya laama sana sana uchafu wa watu na ustaraabu mdogo watu wanafanya vyoo safiii Dar hoyeeeee jiji hoyeeeeee kidumu chama cha ......

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 10, 2007

    Anon hapo juu, sikubaliani nawe kwa sababu zifiatazo: Tunauaba wa vyoo vya public na kama vipo havitunzwi ndio maana watu wanajisaidia ovyo.Pili kukosekana usimamizi mzuri ndio maana hayo maeneneo yanakuwa machafu.Hao vibaka/wavuta bangi unaosema mbona´wakija nje wanafuata sheria?na wengine wanatumia beach/bustan kuvuta ndumu...na mbona haziharibiki. Tulichooungukiwa ni usimamizi mzuri wa hayo maeneo. Solution sio kufunga bali ni kuweka usimamizi mzuri..wananchi wanalipa kodi kwa kazi hiyo na sio kuendeshea seminar za kuwezeshana.Mtaendelea kufunga mpaka lini.Watu wa jiji wajifunze kwa watani wetu wanawezaje kutunza maeneo ya wazi.Bustani zenyewe mbili tu zinatushinda? sasa nini tutaweza. Ungefahamu nini maana ya public beach/garden usingewaunga mkono jiji kwa kuzungushia senyenge hapo Ferry.Pole sana.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 10, 2007

    Bado naendelea na mr Ombaomba.
    Jiulize kwa nini watanzania wanapenda kupata "maji ya mende"kwenye pub za wazi. Ni kwamba hatuna garden, sehemu pekee ni kwenye Bar tu ndio unaweza kukaa nje na kupata upepo.Nenda Sinza kaangalie watu wanavyopata shinda, hakuna garden matokeo yake wanarundikana kwenye mabar kila jioni.Hila kwa sababu akili zetu ni futi hili hatulioni tunaamini jamaa wana fweza za kulamba kilaji daily.Kma bado unielewi wasiliana nami nikupe lecture ya "urban space"nafikiri baada ya hapo utanielewa zaidi.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 10, 2007

    We ndugu yangu unaongelea bustani gani jiji sasa hivi lina vyoo vya kulipia vingi tu na vimezunguka bustani ya mnazi mmoja na vinafanyiwa usafi mzuri tu tena naona ni vizuri kuliko vya wale wanaojisaidia mule bustanini, ili vyoo hivi viwe kwenye hali nzuri ya usafi muda wote Jiji wameamua kucharge kwa kila mtu anapotaka kutumia shs 100 hapa ndiyo likaanza tatizo yaani anaona kulipa mia ya maintanace ni deal anaamua kwenda kujisaidia beach au bustani ya mnazi mmoja, kama huna pesa nenda nyumba zilizojirani waombe jamani nisaidieni nimeshikwa na haja nataka kujisaidia hakuna mtanzania atakeyekufukuza akwambie nenda kajisaidie bustani ya mnazi mmoja atakuruhusu tu, Huu ni utamaduni wetu watanzania kusaidiana kwenye shida na raha. Tatizo linakuja USTAARABU na mazingira tuliyokulia maana kuna makabila mengine ana choo ndani lkn kuna jinsia moja hairuhusiwi kutumia choo atatakiwa akajisaidie nje porini. Sasa tusipokuwa wastaarabu na kuwa askali wa kulinda bustani zetu kwa kila mmoja wetu basi JIJI wache wazifunge maana unamuona mtu anajisaidia kwenye bustani unapita tu humwambii kitu chochote unategemea nini? mshitaki kwenye vyombo vinavyohusika kama kweli ulitaka beach na bustani ziwe wazi kwa jamii. Ustaarabu siyo lazima twende shule jamani, na inatia aibu ukisiakia ustaarabu ulianzia afrika halafu tunashindwa kuuenzi kwa vitendo.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 10, 2007

    KILA UPANDE UFANYE HOMEWORK YAKE
    SERIKALI:FUNDISHENI WANANCHI MATUMIZI BORA YA FUKWE ZETU NA KUWEKA SHERIA KALI KWA WANAOKAIDI MATUMIZI BORA YA FUKWE WALE WOTE WANAOJISAIDIA, KUVUTA BANGI NA KUKABA WATU MAFUKWENI WASHUGHULIKIWE.
    WANANCHI kUWENI WASTAARABU NA MZITUMIE VIZURI FUKWE HII NI PAMOJA NA KUTOA TAARIFA KWA VYOMBO VYA DOLA KUHUSU WALE WOTE WANAOTUMIA VIBAYA FUKWE.
    CHIEF BURITO.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 10, 2007

    Hapa kinachotakiwa kuangaliwa ni utamaduni na umasikini wa watanzania.

    Nikianza na utamaduni ni kwamba watanzania hatuna utamaduni wa kuthamini sehemu zetu za public, unakuta mtu anajisaidia sehemu za kupumzikia kama beach na kama unakumbuka kuna siku radio moja ilikuwa inatangaza live jinsi bustani ya mnazi mmoja ilivyo na vinyesi vya binaadamu sio ndege wala paka!!

    Pili matumizi mabaya ya kodi za wananchi, kama jiji au halmashauri inakusanya kodi kweli nafikiri wangejenga vyoo vya kutosha na kuajiri watu wa kuvisimamia na vikawa bure sio vya kulipia, hii kulipia ndio inawafanya watu wajisaidie hovyo, na msimamazi kazi yake iwe inspection kabla mtu hajaondoka anakagua na kumruhusu au kumpa vifaa asafishe. hii itajenga utamaduni wa usafi.

    Tatu miundo mbinu, kweli ukiangalia vitu kama upatikanaji wa maji ya uhakika kungeweza kupewa kipaumbele zaidi kwani vyoo hivyo bila maji ya uhakika ni bure.

    Nne kupunguza umasikini miongoni mwa wananchi, watu wengi wamekata tamaa na maisha na hivyo ni kama frastrated ukimkuta mtu anajisaidia hovyo ukamsemesha maneno atakayokupa ni ya kukatisha tamaa, kwani haoni umuhimu wowote wa kuwa na mazingira safi wakati yeye analala chumba kimoja na kuku, mbuzi tena chini.

    Jambo lingine ni kuwa na hiden Cameras watu wanaofanya vitendo vya ajabu wawe exposed to the public kupitia luninga n.k hii itajenga utamaduni wa self respect.

    Hata huku walipoendelea watu wengi wamekuwa shaped na hiden cameras

    Mwisho uongozi wa watu wenye kujali maendeleo ya nchi badala maendeleo binafsi, ukiangalia haya yote ni matokeo ya ubinafsi wa viongozi wetu kuanzia ngazi chini mpaka juu, mtu kapewa fungu la matumizi la maendeleo anaona bora atumie 10% kuonesha kafanya kitu kwa umma na 90% inaingia mfukoni mwake na haulizwi na mtu.

    Mwisho Ningependa kutoa pendekezo moja Mtu asiwe kiongozi wa juu kama hana International exposure kuna watanzania wengi wana uwezo mkubwa wa kimataifa lakini kwa kuwa si mwenzetu hawapewi fursa ya kuibadili nchi.

    Kikubwa hapo ni Utamaduni wetu haurusu kuacha sehemu wazi cha kwanza ni kutransform attitude yetu then ndio tufungue hizo beach n.k

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 10, 2007

    Ukweli ni kwamba watendaji wa jiji letu la Dar hawana uzoefu na ubunifu wa mambo haya ya bustani na sehemu za ufukweni. Baadhi tunadhani watanzania ni wazito kiasi cha kutoweza kwenda kujisaidia kwenye vyoo vya uma hata kama vitakuwepo katika hizo bustani, mimi naamini kama watendaji wa jiji wengejipanga na kuweka vyoo na wasimamizi wa bustani na fukwe wakati wote hakuna mtu angefanya jambo la ajabu kama kujisaidia hovyo.Nchi inaendelea sasa huwezi ukatia seng'enge kuzuia walipa kodi wasipumzike kwenye bustani na fukwe za bahari kisa eti watachafua, wekeni wasimamizi na wafanya usafi kama bustani zingine zozote katika mataifa mengine-Cass

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 10, 2007

    MIMI NAISAPOTI SERIKALI KWA ASILIMIA MIA,WA TZ SIYO WASTAARABU KABISA,BUSTANI YA MNAZI MMOJA ILIKUWA NI CHAFU WATU WANAKOJOA KILA SEHEMU NI HARUFU MTINDO MMOJA,FERI WATU WALIKUWA WANAFANYA CHOO.HIYO NDIYO DAWA YA KUMUONGOZA MTU AMBAYE AJASTARAABIKA,SERIKALI KATIKA HILI MI NAWASIFU,FUNGA MPAKA WATU WASTAARABIKE!FUNGAAAAAAAAAAAAAAAAA!!!

    ReplyDelete
  13. Najiuliza hili swala mara nyingi!Nahisi kuna mhusika ambaye anaamua , ambaye hajawahi kufika bichi!Halafu nafikiri kutokana na ukweli Watanzania, mambo muhimu ni mengine. Bado hatuja fikia kugombania haki ya kwenda kuogelea.Tukifikia yoyote mwenye fensi tutazifungua

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 10, 2007

    UK bustani zote ziko wazi na wapo wafanyakazi wa halmashauri za miji wanazifanyia usafi kila siku asubuhi, na kuna mapipa ya kuweka taka (na pia yapo ya taka za vinyesi vya mbwa -maana hawa jamaa na mbwa ni kama chanda na pete).
    Tatizo letu TZ serikali za mitaa bado zinaongozwa na watu wa mwaka 47!!!

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 10, 2007

    Hapa bwana wakati mwingine hakuna haja ya kuilaumu serikali. Wananchi wenyewe siyo wastaarabu kabisa na matumizi ya bustani na fukwe za bahari. Maeneo hayo utakuta ndiyo vijiwe vya wahuni, kuvuta bangi na kuwekwa vyoo. Sasa serikali itazuia vipi, wakati sheria zipo mijitu yenyewe vichwa maji. Mimi naona serikali imefanya sawa kufunga hayo maeneo maana watu siyo wastaarabu kabisa.

    FC

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 10, 2007

    Mji wa New York kulikuwa na vyoo vingi kwa umma. Vilifungwa shauri vilibadilishwa mahali pa madawa ya kulevya, mahali pa kujificha kunywa pombe hadharani, na mambo mengine ya ngono!

    Aliyeumia ni mtumiaji wa kawaida.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 11, 2007

    Mkono ukichafuka hutakiwi kuukata.

    Kola la serikali na wananchi.

    Serikali iweke sheria ni mwiko kukojoa nje ya mahali panapoitwa choooni. 2. kodi ya jijini kama wananchi wakikubali iongozwe ili wafaidi matunda ya nchi kwa kuajiri watu wakusafisha na kuweka mapipa ya taka kila mahali. 3. wananchi tujifunze ustaarabu kusafisha mara tukimaliza kula lunch au kupanya picnic. 5. tujifunze kutotema mate au kukojoa kila mahali eapecially wanaume.6. tusiwe watumwa na kungonja kutumwa...tujitume wenyewe.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 11, 2007

    HUU UZIO WA BAHARI NA UZIO WA MNAZI MMOJA NI MASUALA MAWILI TOFAUTI.

    NI VIZURI WALIVYOWEKA ILA KUTENGWE MAHALI WANAPOTAKA KUWE BEACH NA KUWE NA LIFE GUARD. SEHEMU ZINGINE ZISIZO NA GUARDS BASI KUWE NA UZIO.

    KAMA NI VIWANJA VYA MNAZI MMOJA HIYO NI SHUGHULI NYINGINE NA LABDA NI KWAVILE WATU WAMEZIDI KUPACHAFUA TU. WAWALIPISHE WATU KIINGILIO ILI WAPATIKANE WATU WAKUSAFISHA PARKS AU JIJI LIKUBALI KUTOZA KODI ZAIDI. NA HIYO WATU WATAPIGA MAYOWE WAKIAMBIWA WACHANGIE KUSAFISHA PARK SEMBUSE JIJI

    IMEFIKA SIKU ZA KUANZA KUJITUMA NA SIO KUNGOJEA KILA KITU KOFANYWE NA SERIKALI. HAYO NI MAJUKUMU YA SERIKALI ZA MITAA. KILA MTAA UNATAKIWA KUTUNZA MAZINGIRA YAKE NA JINSI KUNAVYOKUA KUSAF NDIO JINSI WATU WENGI WATAPENDA KUTEMBELEA HIZO SEHEMU NA BIASHARA ZA HUO MJI ZITAPATA WATEJA KWA WINGI. SASA NI JUU YA WAFANYA BIASHARA KUANGALIA MASUALA HAYA NA KUCHANGIA PIA.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 11, 2007

    porojo nyingi fanyeni kweli basi watu vitendo

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 11, 2007

    Mojawapo ya kazi Kodi ni kuprovide public goods, nikimaanisha kama usalama, miundombinu kuitunza n.k., Sasa unaposema wananchi watozwe kodi zaidi jiulize kwanza hii ya sasa inafanya kazi gani?

    Ukipata jibu ndio unaweza sema kodi iongezwe au ibaki ile ile, kinachofanyika sasa ni kwamba kodi zinakuwa misalocated badala ya kupelekwa kwenye malengo yake zinaishia mifukoni mwa wanjanja nao wanaona njia pekee ni kuweka uzio hizi sehemu ili zisiwe na gharama ya kuzihidumia.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 11, 2007

    Tatizo la nchi yetu hatu tenganishi federal tax na state tax.

    Kodi inakusanywa lakini utakuta Dar wanalipa nyingi sana lakini inaenda mtwara au mikoani.

    Ingetakiwa kuwe na tax ya mkoa na matumizi yake yawe ya mkoani tu na tax ya nchi iwe inatumika kwa nchi nzima. Watu wengine wanafaidi bila kuchangia.

    Ingerudishwa kodi ya kichwa mama yangu aliniambia kulikua na kitu kama hicho you live you pay. hapo kila mtu atatafuta kazi na kuwajibika. manake kazi itakua kazi sio sasa hivi vijana wengi wametoka shule mwambie afanye kazi yeyote zaidi ya aliyosemea noooo...mtaani tu kwepu kwepu hakumbuki hata deni analodaiwa na kwa vile hamna cha kodi ya kichwa basi mambo yote poa.

    ReplyDelete
  22. Jamani hata kama hayo mabustani yakitengenezwa na kuwekewa vyoo ni kazi bure maana vyoo kama havitumiki kiistaarau,kama maji yanyewe shida, wasafishaji hawalipwi;sehemu za mapumziko kama hizo hazita fana.Angalia vyoo vya mashule tu utajua tukoje ktk maswala ya ustaarabu.
    Labda vyoo hivyo vitumike kwa malipo madogo;kila anayeingia analipa kisenti!
    Hata hivyo bora kuwekwe uzio kuliko kuuza sehemu hizo kwa watu wajenge mahoteli ya gharama na hivyo atakaye faidi ni yule mwenye pesa tu,wale wa hali duni watabaki kusikia harufu tu.
    Ni jambo linalobidi kutafakariwa vyema maana raia wanahaki ya kufaidi maliasili yao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...