baada ya kupima ngoma juzi pale mnazi mmoja, jk pia aliweka hadharani matokeo yake na ya mai waifu wake mama wa kwanza salma kikwete kwamba mambo yao ni mswano....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 44 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 17, 2007

    ktk haki ya kawaida lazima matokeo yatakuwa mazuri, unategemea Rais mzima atangazwe kuwa mgonjwa, NO WAY. Ikitokea hivyo basi mpimaji atafukuzwa kazi palepale?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 17, 2007

    Hivi viongozi wakubwa wakijua kwamba wako positivu watatangaza hadharani?

    ReplyDelete
  3. Nilipoenda kupima hapo Dar ,kilichokuwa kinanikera ni maswali yao.Walianza kuniuliza mpaka HIV ni nini? Na maswala kibao kiasi mpaka mtu unaweza kughairi kupima .Sijui kama sikuhizi wana tumia utundu mwingine.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 18, 2007

    majibu yake mbona yanajulikana huyu!!! hapa ni kiini macho tu

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 18, 2007

    wapiii waongo wote hao, unadhani wakiwa nao hao madoctor watasema anao si watamuandikia cheti kinginewe ili awadanganye umma wa kitanzania kwamba hana. wapi. bwana kupenda ngono huyu aisiwe nao kakambia nani.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 18, 2007

    Hahaha safi sana mh hv nyie mlidhani Jk ataenda pima ukimwi huku hajui status yake sio,no alikuwa anajua sana ndo amana kaenda pima.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 18, 2007

    Sasa anafurahia nini rais mzima? Inamaana alikuwa hajiamini? Chukua matokeo yako peleka nyumbani na kama kuna jambo iambie familia yako. Vilevile, kama unaona itaathiri utendaji wako au itawasaidia wananchi wako, waambie.

    Baba zima linatoka na matokeo juu juu kama toto dogo.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 18, 2007

    lakini sio sawa kutangaza afya yako kweni sababu ya kupima ni kujitangaza baada ya kupima? mi nilithani mtu anapima ili ujuwe afya yako ikoje ili ufaham hatua yakuchukua katika maisha yako kama vile jinsi ya kula vizuri, na madawa ya kurefusha maisha, pamoja na kama unaweza kufanya mapenzi na kujenga familia.....

    sasa jk kutangaza ndo anamaanisha kila mtu atagaze afya yake kwa jamii? hi picha ndo kama inaonyehsa hivyo ni kama ndo itakuwa hivyo basi watu wengi wata pata ubaguzi katika jamii zao wakifahamika wanao mdudu.

    wazo langu tu lakni.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 18, 2007

    kaka michuzi nimeshushwa na mambo ya jk inamanisha kwamba yeye mzima je wananchi ambao wameadhika watajisikiaje mimi ni daktari majibu yanabidi yapelekwe lab kwa wiki sita kabla vidudu havijaoneka au kuonekana hapa kuna utata sidhani kama mheshimiwa ametumia hakima kuna asilimia hasini ya watanzania ni wagonjwa hili swala si mchezo kuna yatima wengi ambao wamepoteza wazazi na baada ya majibu hayo inabidi ukapime tena baada ya miezi sita kuhakiisha kuwa uko clear very dispointed mh jk

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 18, 2007

    Haya waliokuwa wanaosha vinywa kwamba mweshimiwa ameyakanyanga sasa kipo wapi.. mambo hadharani mswano. Wabongo kwa kuosha vinywa hajambo

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 18, 2007

    Safi kabisa! Japo binafsi sikutaka hata waliopima hadharani waonyeshe na majibu yao hadharani, kwa hakika JK anawajua waosha domo! Cha kufurahisha na kushangaza ni kwamba bado wapo watakaoendelea kuchonga hata baada ya matokea kutolewa hadharani, patamu hapooo, LOL

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 18, 2007

    "MHUUU KAZAZII KWELIKWELI"
    HIVI KWA MFANO WANGEKUTA MAMBO YAKE PRESIDA HAYAKO MSWANO PIA ANGEWEKA FORM JUU HIVYO?AU KWA MFANO PRESIDA ANGEKUTA MAMBO MSWANO NA MAMA WA KWANZA KUMEHARIBIKA PANGETOSHA KWELI HAPO?
    MSHAURINI ARUDI TENA BAADA YA MIEZI 3 FOR CONFIRMATUION.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 18, 2007

    Majibu yenyewe mbona ako mbali hivi!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 18, 2007

    kwa kweli namfagilia, big Up presidaa, viongozi wengine waige mfano wake. mama gwantusa

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 18, 2007

    Ni vizuri kwamba JK amepima ngoma na ni vizuri pia kwa vile ametangaza majibu. Hata hivyo suala la kupima na kutoa majibu bado vilikuwa ni vitu vya hiari kwake kufanya. Kampeni anazoendesha kiongozi huyu zina lengo la kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kupima kwa maisha yao wenyewe. Kwa mantiki hiyo,napongeza sana namna watu wengi walivyopokea na kuunga mkono juhudi za rais kwa manufaa ya wote.

    ReplyDelete
  16. Duuh kumbe walikuwa wanampazia tu mzee wa wa2.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 18, 2007

    waosha vinywa mpooooooo????

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 18, 2007

    Kweli nimeamini watanzania bado tuko nyuma na kufikiri kwetu kunatia shaka sana. Rais anapo pima UKIMWI na kujikuta hana anapaswa kushangilia? Is that a cause for celebration or celebration for cause? Na walio na virusi wafanyaje kama siyo kujiona kuwa wamekuwa condemned? Hii yote ni kutaka kujisafisha kutokana na maneno ya watu ambayo kamwe hayaishi. Sasa wataacha kusema?

    Significance ya cheti cha kutokuwa na virusi ni nini? Is it a shield or a sword? Kila kiongozi wa kitaifa akiamua kujitangaza nani atasema anao? Nani atasema hana? Sijawahi kusikia popote pale promotion ya watu KUTANGAZA kama wana ukimwi au hawana. Lengo la kampeni ya kupima kwa hiari siyo kutoa matangazo ni kila mtu kujua afya yake na kujilinda yeye na familia yake.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 18, 2007

    Nakupa big up mheshimiwa,japokuwa waoshavinywa hawawezi kuacha kuosha vinywa vyao ila mimi mhhhh.. piga ua garagaza hata kwa mtutu wa bunduki kupima no!

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 18, 2007

    Huu sasa mzozo, Rais wa nchi na mambo ya kiswahili, duh! Kweli wabongo kazi tunayo, sasa anamlingishia nani? Yeye mwenyewe kutokuwa mwaminifu katika ndoa yake, mpaka kuashiria kwenda kuhakikisha kama yupo salama ama la, anamtangazia nani sasa?
    Kama Rais wa nchi ana mambo mengi sana ya kufanya na sio hayo mazingaombwe. Safari zimeisha sasa anabuni nini afanye, kaangukia kuhakikisha je katika kimbia kimbia yake aliukwaa ama la?
    ISITOSHE, KWA WABONGO NINAVYOJUA HATA KAMA ANAO HAWAWEZI SEMA, WASEME WAFUKUZWE KAZI WE!HATA YEYE HAWAWEZI KUMWAMBIA, HIVYO WALA ASIJIDANGANYE.
    Mwangalie, eti na karatasi juu yaani HAAMINI? Inakuwaje hana na yeye ni Kiwembe!

    Pole sana JK!

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 18, 2007

    Doc wa 2:59 PM kweli mimi hata sifurahii kwanini ameonyesha matokeo yake. La muhimu ni kwahamasisha watu kupima na kujua stustus yao.

    Ila sio lazima kwa week sita. Kuna aina nyingi za kupima huu ugonjwa...quick test ikiona virusi ndio inapelekwa kwenye test nyingine n.k.
    You can have your results within three days

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 18, 2007

    Ni uamuzi wa mtu kutangaza matokeo yake hadharrani na hata yeye ni binadamu kupima sio lelemama na ukipima ukiona huna ngoma sherehe ni lazima kufanya. Ni wangapi tukienda kupima be honesty though unaishi maisha ya kawaida lakini siku ya kuchukua majibu ni tofauti.

    Na ingetakiwa liwe jambo la sheria au kawaida kuwa wenye virusi wawe tayari kuacknoledge. Ili watu wasiambukizwe kwa makusudi. Na waweze kusaidiwa au waliohusiana nao wapate muda wa kupimwa mapema.

    Tunatakiwa tubadilishe tabia ya kufikiri kuwa na virusi ni jambo la aibu na siri. Ni heri watu wawe na upeo wa kujua kuwa ukiathika siku hizi kuna dawa za kurefusha maisha. Na ni bora kujua mapema.

    Na kwa mazingira yetu ukimwi sio lazima uambukizwe kwa njia inayojulikana sana tu. Nikiangalia ajali za barabarani kila siku na tulivyo wasamaria na magari ya wagonjwa au polisi wanafika kwenye tukia masaa 6 baada ya ajali. Ni casual civilians ndio huwa wanajitolea kila siku kuokoa majeruhi. Je wanavaaga protective gears zozote? Je wanao wasaidia ambao wanavuja damu na wamekatwa na maglass mwili mzima wanajulikana status zao? Utakuta watu wengine wanaambukizwa na virusi kwa wema wao.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 18, 2007

    Baba unajua hii? Mbona kama cheap deal? Hebu achana na matokeo hayo angalia huu mkataba kwa undani kama tumeuzwa vile land ya kilometa ngapi for only that money? Land yetu inaworth more than that hata kama ni wapi.

    Atomic Resources Acquires 5,200km sq Land in Tanzania

    Atomic Resources has entered into an agreement through its Tanzanian registered subsidiary Pacific Corporation East Africa, to purchase a further 5,200km sq of granted exploration ground within the current project area of Tunduru, Southern Tanzania. This brings the company's current concession holding in Tanzania to approximately 6,000km sq. Up to $US465,000 will be payable to the vendors.

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 18, 2007

    Unajua binadamu bwana hawaridhiki kabisa. JK amepima watu wakapiga kelele kwamba mbona hajatueleza matokeo yake, ametoa matokeo watu wanasema mambo mengine, mbona tunakuwa hivyo.

    JK ninamfagilia, maana hata kama umepima una ngoma sioni sababu ya kuchekwa, hiyo ndiyo hali halisi.

    FC

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 18, 2007

    Tatizo lipo kwa waathirika, na wanajisikiaje wanapopata matokeo mabaya.

    Raisi kukenua baada ya kupima ukimwi kunaonyesha kuwa na mzaha ktk suala hili.

    Raisi alitakiwa aonyeshe utu uzima kidogo ktk kuuelezea umma kuhusu majibu ya vipimo vyake.

    kwa upande mwingine tunashukuru kwamba Raisi hajaathirika na gonjwa hili lisilo na tiba.

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 18, 2007

    leave the president ALONE

    NYIE WAOSHA VINYWA KATI YENU NANI KAPIMA NGOMA, MNAOSHA TU VINYWA.. MNAJUA HIV STATS NA RATE YAKE KWA SASA? ACHENI PRESIDENT AWE MZALENDO KUFANYA ANAYOFANYA, ETI ANAO, ANAO NINI? MNAJUA KUOSHA TU, KUPIMA SI KAZI WANA NDUGU.... KAZI NI KUCHUKUA MAJIBU.. KALAGHA BAHO ! MSHINDWE NA MLEGEE !!

    ReplyDelete
  27. AnonymousJuly 18, 2007

    JK asitudaganye.Washikaji wake wengi wamekufa na ukosefu wakina muilini yeye ameponaje????????????????/

    ReplyDelete
  28. AnonymousJuly 18, 2007

    Alitumia Kondom!!

    ReplyDelete
  29. AnonymousJuly 18, 2007

    JK asituyeyushe hapa, basi aongoze vita vya Ukimwi wa Rushwa na sio kuwaachia majambazi walio katika Serikali yake na zilizopita wanaiibia nchi huku yeye anatabasamu tu.

    ReplyDelete
  30. AnonymousJuly 18, 2007

    Hata huyo jamaa kwenye picha anataka kuona vizuri.Tazama anavyokiangalia hicho cheti

    ReplyDelete
  31. AnonymousJuly 18, 2007

    Kaka Michuzi habari zako?
    Mie nashangaa watu wanaosema maneno makali juu ya Rais wao. Haswa hao wanaosema sijui ana wanawake wengi,sijui wengine wengi wamekufa,wao yanawahusu nini? Kama Rais ameamua kufanya kampeni ya wazi juu ya suala zima la Ukimwi,mi nafikiri ni vyema sana kama tukimuunga mkono katika suala zima la kujikinga na hata tukiweza kuokomesha Ukimwi kwa aslimia nyingi.
    Tatizo watu maskini hatuna mawazo endelevu kabisa,kila siku tunawaza ngono ngono ngono,hata hatujui mwisho wetu. Mi ninafurahia sana hawa wenzetu wa Malaysia,waaminifu kupita kiasi,wanajali familia zao na mambo mazuri ya kuinua uchumi wa nchi yao. Hata kama wapo wanaopenda uchizi basi si kwa asilimia nyingi,na kwa kuwa Serikali yao ni yenye utashi na sheria kali,basi wananchi huogopa kufanya tendo la ndoa hivyo hasa kwa watu waliooa au kuolewa. Lakini sisi tunawaza ni jinsi gani nitampata mwanamke yule au mwanaume yule hata kama mtu ana Mke/Mume wake mzuri tu nyumbani. Kwa kweli huo ni utumwa wa kijinga kabisa na ni kitu ambacho kinatufanya kujigongesha na GONJWA hilo hatari.
    Mi nafikiri badala ya kumgugumizia Rais maneno makali ni afadhali tufungue mawazo,ufahamu wetu na kuanza maisha ya kizazi kijacho vyema tena chenye maadili yote na hakika tutashinda hii vita ya dhidi ya Ukimwi.
    Namuunga mkono Mheshimiwa Rais kwa asilimia zote na hakuna ubaya wa yeye kusema hadharani matokeo yake.Namtakia maisha marefu na kazi njema ili aweze kulitumikia Taifa lake changa vyema na kwa uadilifu zaidi.Pia afahamu kwamba,binadamu tumeumbwa kwa kusema,bila ya kusema maisha hayaendi sawa.Kila mtu ana mtazamo wake katika maisha yake na ya jirani yake lakini siku zote naamini maisha bora anayo mtu kwa binafsi yake.
    KILA LA HERI KATIKA SAFARI YA KAMPENI HIZO ZA KUUPINGA UKIMWI NCHINI MWETU.

    ReplyDelete
  32. AnonymousJuly 18, 2007

    Wewe anony 5.50 pm unajiuliza ameponaje huyu....umeshazikia ulemsomo unaosema sio kila mwenye meno anakula nyama ya kuchoma basi ndio hivyo...

    Kama unavyojua mheshimiwa wetu hanywi pombe na research inaonyesha 85% ya watu wakilewa hawatumii condom

    ReplyDelete
  33. AnonymousJuly 19, 2007

    Wabongo msiwe na ROHO za kwanini.Kwanza ni lazima mjue JK alipima kwa sababu zipi na ndipo mtoe maoni yenu ya kipumbavu>>>>>>BIG UP JK umeonesha ujasiri ambao wengi hawana.Wenye donge wameze wembe.Nakufagilia na sera yako ya kutaka kuwasaidia waathirika, kwani wengi wanakufa kwa kukosa hata hizo dawa za kuwaongezea nguvu.

    ReplyDelete
  34. AnonymousJuly 19, 2007

    Off course, alikwenda pima sababu alikuwa kwanza sio mwaminifu na pili hakuwa akijiamini na ndio sababu baada ya kupata majibu akashangilia hadharani kwani hakutegemea kuwa mzima.

    ReplyDelete
  35. AnonymousJuly 19, 2007

    michuzi mwambie akupe scan ya majibu uweke huku tuone, nilijaribu ku-zoom in lakini sioni vizuri hiyo karatasi..kama ya mtu mwingine je :D

    ReplyDelete
  36. AnonymousJuly 19, 2007

    Huyo jamaa asitudanganye wa Tz. majibu haya ni fake, yote hiyo ni siasa tu ili tusahau maisha magumu na wizi wakina Balali. atimize ahadi zake za uchaguzi watu tufurahie. angetulia na kwendesha nchi asingekuwa na wasiwasi ya kupata ukimwi.au mama kaukwa nini???????/

    ReplyDelete
  37. MIMI SIPIMI NG'O!!!!

    Kwanza kwanini sisi wavuvi ndo tunaongoza kwa kuathirika na ugonjwa huu? naomba mnisaidie. au tukienda kuvua tunawaacha wake zetu na vimada wetu wanachukuliwa na wenzetu? au Tunapokwenda kutia nanga visiwa na pwani zingine huwa tunakutana na warembo wengine?

    NISAIDIENI JAMANI. ILA PIA NISAIDIENI UMUHIMU WA MIMI KUPIMA.

    Afya yangu nikiijua, halafu iweje? ndo ntapona? au Ntakufa tu hata nifanyeje? au hata kama nikiwa na ugonjwa sintakufa, sasa nijue ili iweje?

    SITAKI KUJUA, Cha muhimu ni kuwa makini.

    kwanza hata maelezo ya kitaalamu bado hayajitoshelezi kuhusu mbu, damu, malaria na HIV

    Kama mbu anaweza kubeba vijidudu vikubwa mno vya malaria, na magonjwa mengine kama Mbusha, matende etc, iweje ashindwe kubeba vijidudu vyenye ujanja wa hali ya juu, tena vyenye kubadilika badilika kama vya HIV? TUSIDANGANYANE

    Kwanini Duniani, Nchi zilizo kwenye mkondo wa Malaria (TROPICAL COUNTRIES) ndio nazo zinaongoza kwa AIDS na HIV? Kuna nini kinafichwa hapo?

    Kuna jambo linanishangaza kwa sisi Waafrica, eti watu wanawaza kupima, kujitangaza, na kupata misaada ya madawa etc!!!!! NI AKILI HII AU MATOPE? Hivi hamjui kwamba inadumaza ubunifu na uchunguzi wa kitaalamu wa Nchi zetu badala ya kuwaza kutafuta dawa, madaktari wanawaza kuwapima watu watoe ripoti na kupata misaada ya ARVs. Afrika haitaendelea kamwe kwa kupenda kupewa bure. Ukiangalia vyombo vya habari, kila kona misaada ya madawa, sijui nini. Ujinga mtupu, mnakalia kupokea misaada na kuandika papers ili mpewe misaada, badala ya kuwaza jinsi ya kupambana kivyenu. Mnadumazwa. Eti Bush kaongeza bajeti kwenye misaada ya madawa ya ARVs Africa. UPUMBAVU MTUPU. Na viongozi wetu wanashangilia sana ujinga huu. SALUTE KWA MUGABE

    ReplyDelete
  38. AnonymousJuly 19, 2007

    JK alikwa mzima toka alipo tangaza kuchukua form, isinge wezekana agombee Urahisi akiwa kama mwathirika.

    Nampa pole sana Mama Salma ,kwani bora wasinge pima na kuweka matokeo hadharani, maana mashakupe wa mjini wote sasa wamesha jua JK ni mzima, so hawata kua na wasiwasi tena , matokeo yake wata mwinda kwa udi na uvumba.

    ReplyDelete
  39. Ni zaidi ya miaka 25 leo tangia huu ugonjwa usikike naamini Rais kama wengine wengi alisha pima kujua status yake zamani tu lkn kama amepima tena alitaka kuwapa moyo raia wake wasiogope kupima ili mtu atakapo jua matokeo ajue aishije accordingly.

    Kutuoa majibu hadharani labda pia ni wa nia nzuri lkn sijui ni ipi?. ... Je hao walio na virusi wanajisikiaje? wakati afya ya mtu ni siri yake na daktari wake? (human rights).
    Kuna mahali nilipost kuuliza huduma zipi zinazotolewa na serikali kwa wale wenye virus? au TZ tunaishi na yale mawazo kwamba wenye virus wamejitakia wenyewe?Kama alivyo sema anon mmoja hapo juu hili gonjwa lina maajabu yake kuna makahaba niliwajua nikiwa mtoto bado wapo hadi leo na wamezeeka, kuna watu ameenda mara ya kwanza na mara moja anapata, kuna watoto wamezaliwa na gonjwa (kutoka kwa wazazi) hata hawajui leo wana miaka ishirini ni bikra ataolewa mara hoop eti wanaumwa yeye na mumewe lkn hakuna aliye kwenda nje ...

    Mi naona wenye virus ni wanyonge ambao hawana njia ya kujitetea na sisi TZ bado tuna wa bagua sana
    ingawa tunasema eti tusiwabague mara tuwashitaki wanaombukiza kwa makusudi (sijui kivipi) sasa itafika mahali tutapima watu tuta weka majibu hadharani tutaweka vijiji separate vya wenye virus na hapo ndipo tutakufa tena kwa wingi maana badala ya kuwa wazi watu watajificha tena zaidi sijui sasa tuta kuwa tumefanya nini?

    Mawazo yangu: Tungefanya wale wenye virus wajiamini, waishi maisha ya kawaida wajue kwamba siri yao inasetiriwa, kwamba utapata msaada wa madawa na kwamba kama bado wana nguvu wana endelea na kazi... kwa kifupi kuwapa matumaini ya maisha.

    JK kwa kutoa majibu yake hadharani hatujui impact gani italeta, najua Nyerere angekuwepo asingefanya hivyo kuogopa labda itaumiza wengine, alitupenda sana watanzania bila kujali wenye virus na wasio nayo. Alitete sana wanyonge!


    Mungu ibariki TZ

    ReplyDelete
  40. AnonymousJuly 19, 2007

    Kuna tofauti gani majibu kuwekwa ktk kadi ndogo + mhuri, na kama haya ya mhe rais kwenye fomu?
    naomba ufafanuzi maana kuna waliopewa kadi na kupigiwa mhuri siku hiyo

    ReplyDelete
  41. AnonymousJuly 19, 2007

    KAMA WATANZANIA TUNAHAMINI CHETI BASI KILA MTU BONGO MZIMA,NASHANGAA WATU WANAPIGA DOMO KAMA WAGENI WA BONGO,KILA CHETI UNACHOTAKA KINAPATIKANA, KINACHOHITAJIKA NI MTU ALIYOMFANYIA VIPIMO VYA NGOMA MHE: RAIS HATOKE KWENYE TV AUTANGAZIE UMMA WA WATANZANIA KWAMBA KILA KITU MSWANO KAMA WATU WENGINE MNAVYOSEMA NA KAMA CHOCHOTE KITATOKEA MBELENI YEYE NDIO ATAWAJIBIKA KWA KUWADANGANYA WATANZANIA.

    ReplyDelete
  42. AnonymousJuly 19, 2007

    MVUVI KAMA UKO SEROUS NA UNACHOONGEA BASI ELIMU KUHUSU UGONJWA HUU BADO INAHITAJIKA SAN.

    SISEMEI KUHUSU WEWE KUTAKA KUPIMA AU LA NAZUNGUMZIA JINSI YA UPEO WAKO KUHUSU HUU UGONJWA.

    JK ASANTE NA MICHUZI ASANTE KW AKUWEKA HII TOPIC. NILIKUA NASIKIA TU KUWA KUNA WATU BADO HAWAJUI UKIMWI NINI NINI NA JINSI UNAVYOAMBUKIZWA NA TOFAUTI YA VIRUSI HIVI NA VINGINE LEO NIMEJIONEA MWENYEWE. MWAKA 2007 BADO MTU ANASEMA HIVYO

    KWELI RAISI WETU MPENDWA KAZI UNAYO NA PIA LA MUHIMU NI ELIMU KUHUSU HUU UGONJWA KWANZA. AFRICA BADO HATUJUI LOLOTE KUMBE...OMG

    ReplyDelete
  43. AnonymousJuly 20, 2007

    kwa kweli hata mie huyoo mvuvi alinishangaza sanaaaaaaa!....yaani mpaka nimeshtuka hapa!....KWELI BADO TUKO NYUMA SAANA KWEYE MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI!...na issue hapa wala sio UKIMWI!issue ni IGNORANCE!..people are sooo illiterate!....kiasi unaogopa..kha!jamani hata km hukupata nafasi ya kuingia shule!..jaribu kujifunza mambo kupitia vyombo mbali mbali...internet,jisomee magazeti,vitabu na vijarida mbali mbali UELIMIKE!!!!!!la sivyo mnatutia AIBU!!!!!....TRUE----NO OFENCE!!!

    ReplyDelete
  44. Ni kweli kabisa wadau, elimu kuhusu HIV/AIDS inahitajika sana hasa kwa sisi watu wa kawaida, kama huku feri na mashambani. Naomba mnitoe ushamba sasa kwa kunielimisha hapa na si kunilaumu, MIE ELIMU SINA, na labda niongee kwa niaba ya wasioelimika kama mimi. Tusaidieni. Mimi nadhani gharama za kampeni za upimaji, matangazo ya ANGAZA, magari ya TACAIDS, masherehe ya UKIMWI nk ni kubwa kuliko gharama za uelimishaji. Ukiangalia katika mitaala ya elimu ya msingi na sekondari, UKIMWI umepewa nafasi ndogo mno, wasomi mnaoelewa tusaidieni jamani.

    Mvuvi toka Feri.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...