wadau kuuliza si ujinga. kwa nini kwenye ndoa mke humvisha pete mume na mume humvisha mke lakini kwenye ingejimenti ni mume tu amvishaye mke????

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 16, 2007

    du kaka michuzi hivyo ni vidole vyako kweli nidhani niko mwenyewe minanaonaga aibu sana kuonyesha madole yangu adhani wewe una moyo

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 16, 2007

    UNATAFUTA UGOMVI NA ABUBAKARI SADIKI!HAYAAAA!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 16, 2007

    Sio kila arenjimenti ya ndoa inafuata utamaduni wa namna hiyo!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 16, 2007

    Ni sawa na kuulisa kwa nini mume hulipa mahari na mke halipi....Wewe unafikiri jibu ni nini? Zinaweza zikawepo sababu kem kem kutokana na jinsi unavyotaka kuelezea. Traditionally, mwanamke ndiye anayekuwa "approached" kwa hiyo pete ni kama "red fag" kuonyesha "stop she is taken" Maelezo mengi ni kwa ajili ya desturi hamna right or wrong answer on this...

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 16, 2007

    hiyo ni utamaduni tuliouiga kutoka western coutries. Kuna nchi kibao za kusini mwa america na visiwa vyao hawavai hiyo engagement ring. Na kuna wengine humo kwa mvulana ndio anavaa.

    Na siku hizi wasichana wengi tu wanawanunulia wanaume hizo ring especially USA.
    Kwa hiyo huo ni utamaduni

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 16, 2007

    Dah.. Hiyo setting ya hiyo pete inanikumbusha masonara wababaishaji wa bongo, na we michuzi unamoyo kweli wa kuuweka huo mkono wako, nafikiri kuna kitu kimekosekana katika hiyo ngozi yako, bila shaka Lotion ya mama watoto imekweisha nini?

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 16, 2007

    Hivi kwani mashoga inakuwaje? Wanavikanaaga ingejimenti ringi? Naona wazo la wanaume kuvikwa hiyo ringi linaweza wafaa mashoga zaidi!!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 16, 2007

    KAKA...HIYO PETE IPELEKE WAKAISAFISHE...HALAFU MRUDISHIE AIVAE MPAKA LEO HUJACHUKUA JUMLA...

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 16, 2007

    Michuzi hebu weka swali lako vizuri! Hakuna mume anayemvisha mke pete ya uchumba sehemu yoyote duniani! Kijana wa kiume anaweza kumvisha kijana wa kike pete ya uchumba kama ishara ya kumuonesha kuwa amedhamiria kumuoa na lengo sio kubuzi buzi naye halafu akatokomea gizani! Nafikiri huo ni utaratibu tu. Vipi mzee ulitamani kuvishwa pete ya uchumba na mama nanihii?

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 16, 2007

    Michu, si wanawake tu huvalishwa ingejimenti ringi, jamaa wa asili ya Asia, hususani wadosi ni Mwanaume alivalishwa na kidosho wake.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 16, 2007

    michuzi...
    kuhusu ringi--yaani pete mimi nadhani kwa mtazamo wa zamani ilikuwa ni kuepusha kupigwa kumbo..yaani ilikuwa rahisi mwanamkwe kunyemelewa ila kwa mtazamo wa kisasa wote wanastahili kuvishana ringi[pete] kwani wanawindwa wote ...hii imepata sana umaarufu ila wanaita pete ya ahadi ...ila ya kiume haina kikofia cha juu!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 16, 2007

    Ziko ring za aina nyingi tu inategemea hela yako na unataka kudanganya vipi.
    1. friendship ring
    2. Promise ring
    3. Engagement ring

    Na still unaweza ukawa nazo zote na mtu akakuacha kwenye mataa...au uliyempa akakurudishia maring yako

    Ring rohoni jamani- haya mambo ya kumaliziana hela tu.

    Na wasichana wanaamini the low the diamond carat the less the love.

    Na US calture yao hilo rock la bibie ni lazima liwe sawa na three months income yako au zaidi. Sasa wewe kama tu mshahara chako kwa mwaka ni 40 basi lazima ununue ring ya $10000 and up. Nawaoneaga huruma kweli. Bora kwetu nashuka kwa sonara mhindi nimemaliza

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 16, 2007

    Michu, mbona unatufanya watu wote mapimbindio nini kuuliza jibu kama tangu lini mwanamke hakakutongoza sasa hii ndio jibu lako kama wewe ndio ulitongozwa basi uliafanya vibaya sana kutoa pete na kama ulitongoza na kuomba ndoa u a man... so plz plz tuletea mambo mazuri sio haya ya unafiki,

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 16, 2007

    yaani nabaki kucheka tu kwani yangu macho na masikio.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 17, 2007

    Sasa kama hana la kuweka mnataka awawekee picha za Idd. Si ndio mtalalamika mpka kesho.

    Niheri zake mara flag, mara ring hazimgusi mtu...umbeya hatutaki humu kijijini...Michuzi hivyo hivyo...

    ReplyDelete
  16. Kwasababu ni mwanaume ndie anaemuomba mwanamke waoane na sio mwanamke.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...