NAPENDA KUTOA SHUKURANI ZA DHATI KWA WADAU WOTE 28 WALIOSHIRIKI KWENYE SHINDANO LA KUTAJA RANGI ZA BENDERA YETU YA TAIFA NA MAANA YA RANGI HIZO. KABLA YA KUTAJA WASHINDI NAOMBA NITOE MAJIBU KAMILI YA BENDERA YENYEWE. VILE VILE NATOA SHUKRANI HATA KWA WALE WALIOJIBU NDIVYO SIVYO, HALI KADHALIKA KWA MDAU 'NYAKYUSA' AMBAYE ALILALAMIKA KWAMBA MASWALI YA AINA HII NI YA KITOTO NA NISIWAPOTEZE WADAU MUDA WAO.
kwa uhakika zaidi juu ya majibu cheki http://www.tanzania.go.tz/profile.html
Uwiano wa Urefu Kwa Upana:-

Maelezo: Tatu kwa mbili, mfano ft.3 x ft.2, ft.6 x ft.4, ft.12x ft.8

Bendera ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina rangi nne nazo ni Kijani, Dhahabu, Nyeusi na Bluu. Rangi nyeusi imepita katikati ya bendera kuanzia pembe ya chini kwenye mlingoti na kuishia pembe ya juu kulia. Rangi hii huigawa bendera katika sehemu mbili zenye umbo la pembe tatu. Rangi nyeusi imetenganishwa na pembe tatu ya juu yenye rangi ya kijani na pembetatu ya chini yenye rangi ya bluu kwa mistari miwilimidogo yenye rangi ya dhahabu.
Viwango vya rangi na maana zake:

Nyeusi - Kiwango na. 9-103 - Watu
Kijani - Kiwango na. 0-010 - Ardhi
Bluu - Kiwango na. 0-012 - Bahari na Maziwa
Dhahabu - Kiwango na. 0-002 - Madini
Uwiano wa Rangi:
Rangi nyeusi kwa bendera ya Ft.6 x ft.4 ni 13/48 kwenda juu na Ft.13 upana. Mistari ya dhahabu ni 1/16 kwenda juu na3" upana kila mmoja.
SWALI HILO LINAPATIKANA KWENYE LINKI HII HAPA
http://issamichuzi.blogspot.com/search?q=bendera&x=59&y=11
KATI YA WATU 28 WALIOTOA MAJIBU NI WADAU WAIWLI TU NDIO WALIOJIBU KWA USAHIHI IKIWA NI PAMOJA NA PIA KUWEKA MAJINA YAO. WASHINDI HAO SI WENGINE ILA NI:
1. PIUS
2. WA - CHIRANGI
NATOA HONGERA ZANGU NYINGI KWA WADAU PIUS NA WA-CHIRANGI KWA KUSHINDA SHINDANO HILI. NAOMBA MNIAMBIE NI ZAWADI YA PICHA GANI MNAYOTAKA NA JE NIWATUMIE AMA NIBANDIKE BLOGUNI HUMU. WADAU WALIOSHINDA SHINDANO LILILOPITA WALA MSIKONDE. ZAWADI ZENU MTAPATA KABLA YA JULAI 20, TATIZO HAMJANIAMBIA NIWATUMIE AMA NIBANDIKE HUMU. NA KAMA NI KUWATUMIA NITUMIE EMAIL ZIPI? MIE NAPATIKANA KWENYE: issamichuzi@gmail.com
AHSANTENI KWA USHIRIKIANO
.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 16, 2007

    Mimi ninaapeal
    Kwanza dhahabu ni rangi gani? na lini ilianza kuitwa dhahabu?

    hata kuna wimbo tulifundishwa shuleni unasema manjano.

    Sijui hiyo neno rangi ya dhahabu imeingia lini kwenye kamusi ya kiswahili

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 16, 2007

    Michuzi ulinifanyia ubaya siku hiyo, websaiti yako haikutaka kupokea komenti zangu siku hiyo. Ninajua nilikuwa nishinde

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 16, 2007

    Michu, wewe ni wangu galagaza piga uwa wewe na mimi forever! Ila wafuga Fisi wameniacha hoi kabisa.Lakini hayo majibu watu watalalamika sana nafuu ya mimi niliye sema ni maswali ya kitoto. Lakini Michuzi mbona mwalimu wangu wa darasa la siasa hakuwa anataka vipimo na mimi nilikuwa na pata hilo swali linapo ulizwa bila hata ya kutoa vipimo. Nafuu ungesema majibu yaambatane na vipimo au ujazo ra Rangi, Mimi naona swali lilikosewa na kila mtu ameshinda hata na mimi nimeshinda vilevile na picha ibandikwa humu humu kama zawadi yetu..Halafu umesama rangi ya dhahabu? Michuzi, hakuna kitu kina itwa rangi ya dhahabu katika official 'expressions'. watu husema golden goose,golden boy,golden egg,golden beach etc-ni kielelezo tu upo hapo-hiyo futa kabisa hiyo lakini officially hakuna kitu kama rangi ya dhahabu.Mimi nitaendelea kulalamika mpaka utoe zawadi kwa wote.
    Ila Mwanagu Wafuga Fisi wameniacha mdomo wazi.
    Ndaga fijo.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 16, 2007

    Michuzi, sina hakika kama kijani inawakilisha ardhi. Siku zote nilifundishwa kwamba kijani maana yake ni uoto mbalimbali wa nchi kama vile miti, mazao, misitu na kadhalika. Unaweza kuangalia vizuri hilo? Ardhi haiwezi kuingia katika eneo la madini?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 16, 2007

    Michuzi, hakuna rangi ya dhahabu! Bendera yetu ina rangi ya njano, ambayo maana yake ni madini yetu. Unaposema dhahabu una maana tuna madini mamoja? Na kwanza hakuna rangi inayoitwa dhahabu. Kuna madini yanaitwa dhahabu, na ndio huwa tunafaninishia vitu vyenye rangi inayofanana na madini hayo. Michuzi, namimi nina appeal.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 16, 2007

    HATA MIMI NASHANGAA, ETI RANGI YA DHAHABU!!WE MICHUZI WAKATI MWINGINE UNATIA HASIRA KWELIKWELI.
    HEBU ACHA KUPOTOSHA UMMA.
    MIMI NILIFUNDISHWA RANGI YA MANJANO NA MWANANGU KILA SIKU ANAIMBA ULE WIMBO WA BENDERA YETU HALAFU WEWE UNATULETEA MAMBO GANI HAYA!!??
    ACHA HZO.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 16, 2007

    Nakubaliana na mdau wa kwanza kabisa aliyekanusha madai ya michuzi eti rangi ya NJANO sasa imegeuzwa na kuitwa dha DHAHABU.
    Kama unataka kusema NJANO ni DHAHABU, basi hata PINKI nayo itaitwa NYEKUNDU au ZAMBARAU itaitwa BLUU.
    Rangi ya NJANO ni NJANO na itabaki hivyo milele kadhalika DHAHABU na rangi nyingine kama HUDHURUNGI na DAMWATI.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 16, 2007

    MICHUZI KAMA HAUKUTAKA KUPATA WASHINDI BORA USINGEWEKA SWALI LAKO HUMU. TOKA NAANZA DARASA LA KWANZA HADI NAMALIZA CHUO SIJAWAHI KUSIKIA HIYO RANGI YA DHAHABU UNAAYOSEMA WEWE, TULIFUNDISHWA BENDERA INA RANGI NNE NAZO NI KIJANI, MANJANO, NYEUSI NA BLUU.USIWAPOTOSHE WATANZANIA.NAJUA LENGO LAKO LILIKUWA NI KUPATA WASHINDI WACHACHE AU KUKOSA KABISA.WEWE NI MTU MZIMA SASA USIWAFANYE WATU WAZIMA KAMA WATOTO.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 16, 2007

    michuzi acha kutuyeyusha,hivi vipimo mara inch mara ratio umevipata wapi,kwenye katiba ya nchi au wapi?

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 16, 2007

    MICHUZI NILISEMA WATU WATALALAMIKA. SASA TOA ZAWADI KWA WOTE.
    NDAGA FIJO
    NYAKYUSA!

    ReplyDelete
  11. Duuh sasa michuzi unatuyayusha mbona Pius ameandika bendera yetu ina rangi nne lkn alizozitaja ni tatu tu. sasa umempa ushindi kwa kigezo gani?

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 16, 2007

    NAMSHUKURU SANA MICHUZI KWA MAJIBU HALALI KABISA, NA WALE WANAOKATA RUFAA WANAPINGANA NA HABARI RASMI ZA SERIKALI, NAJUA YOTE NI KWA SABABU WALIMU WETU WALITUDANGANYA>>> MAJIBU YAKO HAPA

    http://www.tanzania.go.tz/profile.html

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 16, 2007

    HUYU JAMAA MICHUZI NYIE HAMJUI. UNAJUA HANA MJADALA MAALUM ILA INATAKA KUWAJAZA WATU KWENYE BLOG YAKE NA KUBISHANA VITU VISVYO NA MSINGI.
    HIYO YOTE NI KUWAPOTEZA MALENGO NA KUSAHAU KUMUULIZA MAMBO YA MUHIMU AMBAYO HUJITIA KIMBELEMBELE KUINGIZA HUMU, WATU WAKIMJIA JUU HUYEYUSHA KWA KISHINDANO FEKI.
    ANGALIENI SANA KILA ANAPOINGIZA SHINDANO, KUNAKUWA NA HOJA YA MUHIMU AMBAYO WATU HUIJADILI NA KUIFUNIKA KIAINA.
    BALALI ALIPOFUKUZA BAADHI YA WAANDISHI NA KUINGIZA ANAOWATAKA YEYE, HUO NDIYO UNGEKUWA MJADALA WA MUHIMU.
    LAKINI KWA VILE MICHUZI HUENDA AKAWA MMOJA WA WALIO KWENYE PAYROLL, ANAYEYUSHA TARATIBU NA HATA PICHA ZA WALIOTIMULIWA HAKUZITOA. (ANGALIA Abdallah Mrisho Blog utaona).
    NA KWA KUYEYUSHA ZAIDI, AKAINGIZA MJADALA WA BENDERA. HIVI WATU WAZIMA NA HESHIMA ZAO UNAWAULIZA RANGI YA BENDERA YA TAIFA? KWELI WEWE TUTUSA!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 17, 2007

    sasa hao washindi mbona hamna aliyesema neno dhahabu.....?????

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 17, 2007

    Kwa hiyo hizi tunazoziona kila siku zenye rangi ya manjano sio bendera legaly right?
    Kwa hiyo ruksa kuzibandika kila mahali kwa vile bendera ya TZ color yake ni dhahabu

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 17, 2007

    kuna huyo jamaa anaekazania waandishi walifukuzwa mbona hajibiwi?
    Hivi nani kamfunga kamba ya kuja kwenye hii blog?Radio One,RTD na Free Africa huwa wanamatangazo ya vifo,kwanini mtu afungulie clouds fm au East Africa Radio au kiss fm halafu aanze kutoa matusi eti hili redio pimbi kweli,kwanini haliweki matangazo ya vifo? Kwanini ukanunue kiu wakati wewe hutaki kusoma habari za kidaku? Haya tuseme untaka zile riwaya,sasa kinachokufanya ukasome na udaku halafu uanze kutoa matusi ni kitu gani?Mi nafikiri pimbi ni wewe unaetaka vitu kusikopatikana.Jambo forums na shy24 wao huwa wako na serious forums za siasa,sasa wewe pimbi kwanini usiende huko ukajadili hayo mambo?Mtu mwingine kaenda kwenye maoni ya Balali halafu anasema wewe michuzi tuletee mijadala ya maana,kwa mfano mambo ya ukimwi hivi. Cha kushangaza kuna ujumbe wa ukimwi kaupita juu wala hakutoa maoni yake.
    Hili ni ombi kwa michune na wote mpitiao hii blog,mnaonaje mtu akitaka kutoa maoni ya matusi aweke jina lake kamili na kontakti zake,halafu ampigie simu michuzi kudhibitisha hizo kontakti ni zake mtoa maoni hayo ya matusi,kinyume na hapo hamna kuweka maoni yenye matusi hewani!
    Mnaojua press law,hivi internet iko ekzemptedi kufuata sheria,mfano defamesheni? Mi nadhaniaga kwa kumoderate all comments that goes on air, moderater/web master muite upendavyo ilimradi humtusi, haimaanishi anachukua msalaba wa yote yaendayo hewani?

    ReplyDelete
  17. 1. Kwa wanaosema hakuna rangi ya dhahabu au hawatofautishi rangi ya dhahabu na njano bofya hapa. http://www.pitt.edu/~nisg/cis/web/cgi/rgb.html
    Klomatikia (Sayansi ya rangi) ni fani pana sana kuliko zile rangi saba tu za upinde wa mvua tulizomegewa enzi hizo katika kiwango hicho. Kwa mujibu wa tarakibu ya Prof. Munsell na wengine wengi (ambayo hutumika sasa zaidi kuliko hata hiyo ya British Std Range of Colors – B.S ya 1955) kuna majina (utambulisho) anuwai zaidi ya 1000 ya rangi katika mfumo wa HSB / HSV. Yaani rangi hutofautishwa na nyingine kwa kutaja HUE (utofauti kutoka rangi nyeupe), SATURATION (ukolezo) na BRIGHTNESS /VALUE (jinsi gani ina giza au mwanga.

    2.Katika mfumo wa desimali-sita (Hexadecimal) wa kutambulisha rangi, rangi ya Njano ni ffff00 wakati ile ya Dhahabu ni ffd700. Kwa maelezo ya lugha rahisi rangi ya dhahabu ni njano-chungwa (yellowish orange color.

    3.Kwa kutegemeana na utamaduni wa watu na au fani husika, rangi uhabarisha sana. Hata hivyo karibu dunia nzima kuna baadhi ya maana na matumizi ya rangi ambayo yamekubalika (conventionally). Rangi ya dhahabu ndio mara nyingi hutumika kuashiria madini, machimbo au utajiri na sio rangi ya njano ambayo hutumika katika mawasiliano na barabara (kumbuka yellow school bus, yellow tax-cabs, yellow caterpillar, yellow railways, yellow pages, yellow post & telecommunications, yellow road sign n.k)
    4.Kutaja uwiano wa urefu na upana, viwango vya rangi na maelezo kamilifu ya mpangilio wa rangi za bendera ya nchi si tu muhimu ni LAZIMA. Kama si kufafanua ukolezo na au mipangilio ya rangi basi nchi zifuatazo zina bendera zinazofanana: Costa Rika & Thailand; Ivory Coast & Ireland; Monaco & Indonesia; The Netherlands na Luxembourg n.k. Aidha bifu la Chad & Romania juu ya alama hii ya Kitaifa pia ni mfano halisi.

    Ndio maana wengine tulisema kuwa hili ni swali zuri sana. Ni vema sasa Mitaala, Waalimu na Wanafunzi ngazi zote kukarafati utilio wao ili yumkini ulandane na kauli rasmi ya Serikali yetu.

    Ndg. Michuzi nastakabadhi kupokea ushindi. Tutaendelea kuwasiliana.

    Wa- Chirangi

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 18, 2007

    Anony 6:15 wengine tu old skull mweee. Haya mambo ya kuongeza na kupunguza kila siku sijui wataacha lini. Tu sayari chetu tulifundishwa kapo sasa hivi ni marehemu. Kapluto hakako tena sasa sijui Michuzi akituuliza hili swa tutajibu as old skull au ....Kesho utasikia hata earth sio sayari tena.

    I am glad nilikwenda shule zamani.

    Leo kila siku wanakuja na research zao...leo chocolate ni mbaya sana, kesho chocolate ni nzuri a piece a day is good for you health, mara a of wine is good for your health, ukiamka hata hujanywa kaglass kako mara ukiangalia news ....a journal of so and so ......wamefind drinking is bad for your health....It is toooo much better keep it simple....color yetu tulifundishwa manjano....I never heard that our flag is gold

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...