makamu wa rais dk. mohamed ali shein akiwa katika sala kumuombea hayati sheikh nurdin hussein aliyefariki jumamosi jijini dar na kuzikwa leo huko kijijini kwake pande, kilwa. sala hii ilifanyika msikiti wa shaadhir, dar kabla maiti haijapelekwa kilwa kwa mazishi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Yaani Michuzi nilivyokuwa nimekumind hujatoa taarifa za kifo cha Sheikh Nurdin? we acha tu maana huyu mzee wetu! Mungu amuweke mahali pema peponi!

    ReplyDelete
  2. RIP mzee wetu

    ReplyDelete
  3. Hii blog sasa utafikiri chumba cha maiti yaani mortuary.Kila sehemu marehemu,marahemu wamejaa marehemu kila kona.Hivi Michuzi unapenda sana maiti wewe mwanga nini?

    kIla mahali marehemu! nitahama blogu lako tukuachie ukae na marehemu wako.

    ReplyDelete
  4. Mungu wape faraja wanafamilia wote wa Sheikh Nurdin

    ReplyDelete
  5. INNA LILLAH WAINAILAHI RAJIUN..sisi sote ni wa Mwenyezimungu na kwake tutarejea..Kaka Michu asante kwa taarifa.

    ReplyDelete
  6. August 27, 2007 11:08:00 PM Wewe weee haya sio vizuri shauri yako mimi naomba kaka michuzi utupe habari kila siku za misiba asiyejisikia kusoma ahame hakuna aliyeshikwa kamba mwenyewe michuzi anafanya kazi ya CHARITY

    ReplyDelete
  7. Mwenye enzi akuondole yaliyo mazito na akulipe uanyostahili ! R I P

    Mzushi

    ReplyDelete
  8. Inshalah!

    Mwenyezi Mungu atajua mwenyewe atakupeleka mahali gani ambapo anapojua mwenyewe wanastahili kukaa watu kama Sheikh Nurdin.Amin

    ReplyDelete
  9. Mwenyezi mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.AMEN

    ReplyDelete
  10. we anon wa aug,27 8:09:00 unafanya mchezo,usifanye masihara na kifo.huenda labda hayajakukuta,tushukuru angalau Michuzi anatupa nafasi ya kutoa salam za pole kwa ndugu zetu wafiwa hata kama hatuwajui kwa sura.ahsante Issa.

    ReplyDelete
  11. What's wrong with other people? Maana ya kuwa na hii blog ni kupeana habari nzuri na mbaya. Au huyo mshamba hapo juu hajawahi kufiwa? Michuzi keep it up! Tuletee habari zote, nondo, misiba, harusi na anything unachoona ni muhimu kwa jamii. Wewe unayetishia kuhama you can do it! Michuzi hata loose nothing! Kusema kweli hii ni blog amabyo naifungua kila nikiamka na kabla ya kwenda kulala it has been a source of all current events zinazotokea nyumbani, kwa sisi tuliombali at least unakuwa up to date na whats going on. Go Michuzi achana na watu wasiopenda maendeleo. They negative all the time and they can't do nothing!

    ReplyDelete
  12. Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi,amin.

    ReplyDelete
  13. Kwa utafiti niliofanya kwenye Blogu za watanzania hii ya Michuzi ndio inaongoza kwa kuwa na marehemu wengi.

    Mimi nimelia sana kulilia waliokufa kwenye hii blogu hadi nimechoka.

    Misiba kwenye hii blogu ni mingi kweli hata mtu hujui ulie upi na unyamaze upi.

    Mingine badala ya kulia unabaki tu kutoa kamasi maana machozi yamekauka.

    ReplyDelete
  14. Inna lillahi wa inna illahi raji'un,nilikuwa jana napitia tzuk.net ndipo nikaona habari za mzee wetu Sh.Nurdeen,nikajiuliza nimetoka kusoma blog ya Michuzi hajaweka habari za Sheikh lakini anatuwekea habari za 2 moons,kwahiyo leo ni faraja kuona umetutaarifu maendeleo ya maziko,tambua una watembelea site yako wa kila aina,kuna wanao penda wana muziki,kuna wanao wapenda wana siasa na vile vile kuna wanao wapenda ma sheikh na huyu ni mmoja katika ma sheikh wakubwa who will be sadly missed,it's a GAP very hard to fill the work he's done for the Muslim Society it's a big loss.Rest In Peace mzee wetu na pole kwa wafiwa M'Mungu awape subra nasi tuko nyuma yake.

    ReplyDelete
  15. kuna watu wengine naona bangi nyingi,hivi mnafahamu kama kifo ni part ya life na michuzi kazi yake kututaarifu,na ni wakati mgumu kwa wafiwa all you can do at times like this is to console not burden them with stupidity kuwa blog imejaa vifo wewe mwenyewe utakufa sasa tukuone nawe unakufa tuu machozi sie hatuna tena.

    ReplyDelete
  16. Watu wengine bwana ni hasara kabisa sijui vichwa vyao wameweka kamasi sasa mtu unaingia kwenye blogu kupata information sasa unapinga au ndio mila zenu yaani hata maana ya msiba hawajui Nimesikitika kusikia kifo cha sheikh nurdin Mola ailaze roho yake mahala pema peponi amen.

    ReplyDelete
  17. INNA LILLAH WAINAILAHI RAJIUN
    Ni msiba mkubwa sana. Mimi binafsi nimefaidika sana na mafundisho ya Sheikh Nurdin
    RIP

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...