Home
Unlabelled
aga khan
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Duuh!! Mchonga kiboko...anacheka nae kumbe analipigia mahesabu jengo hilo.mara baada ya picha hii Agakhan anafika nairobi tu mchonga anatangaza kutaifisha jengo la IPS.
ReplyDeleteMnakumbuka?
Mchonga alikuwa mwanaume wa shoka. Haogopi. Alikuwa na hoja nzito na kali. Aliwathamimini wazawa bila kujali asili, rangi, dini au kabila.
ReplyDeleteNdiyo alitaifisha kwa maslahi ya UMMA. Alipotoka tu wakaanza KUUMA tena kwa kun'gata. Kumbuka NBC, Almas za Mwadui, Dhahabu na majumba ya msajiri. Alifanya kazi si mchezo.
Ndio namchukulia mwalimu kama binadamu mwingine yeyote yule kama kiumbe dhaifu kama viumbe vingine vyovyote vile. Kuna mazuri aliyoyafanya ndiyo na kuna mabaya vilevile aliyoyafanya ambayo hadi hivi sasa tunaonja adha yake. Tukirudi nyuma na kuanza kuchambua suala moja hadi lingine tutaonana ya kwamba mwananchi wa leo anateseka kwa ajili ya misingi mingine aliyoianzisha na hadi leo tunadidimia. Viongozi wetu wa leo wamekuwa wakulaumiwa kila kukicha lakini ukweli ni kwamba kuna wakati wanakosa jinsi kutokana na kufanya kazi kwa mazoea ya yale waliyokuwa wakiyaona. Ni vigumu sana kwa mtu ambaye amefanya kazi kwenye vipindi vitatu mfululizo vilivyopita kubadilika na kuwa mwadilifu kivitendo, kimaneno yes inawezekana maana hatulipii muda tuutumiao kuongea. Tutaendeleza yale yaliyoachwa na wasisi wetu umekukuwa wimbo ambao kamwe hautaisha pasipo watanzania wenyewe kuamua kubadili hali kama hii. Tanzania kila kunapokucha inakuwa ni afadhali ya jana. Sasa je haya ni maisha gani ndugu zangu. Leo hii unaambiwa elimu ya msingi ni bure, ndio nakubali lakini je darasa moja lina wanafunzi wangapi na walimu wangapi? Je sheria halisi ya idadi ya wanafunzi darasani ni ipi? Tunafanya jitihada za kila kata kuwa na shule ya sekondari, je walimu wako wapi? Au ndo tuanzishe mafunzo ya muda mfupi kwa wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne kwa ajili ya kufundisha sekondari? Sitaona ajabu maana yalishatokea mafunzo ya miezi mitatu kwa walio tuliokuwa tukiwaita wa UPE, waliofeli darasa la saba na kurudishwa kufundisha masomo yaleyale waliyoyashindwa. Simlaumu kiongozi wa sasa bali lawama zangu zitazidi kuwaendea wasisi wetu. Kuna wakati nafikia hatua nasema labda tuliwahi kupata uhuru na labda tuliulazimisha, maana historia haionyeshi kama Tanganyika hadi mwaka 1961 ilikuwa ni koloni, bali kinachoonekana ni kwamba ilikuwa ni territory, na juhudi zilikuwa zikifanywa kuwasomesha watu wachache kwa maandalizi ya kuwa viongozi. Baada ya kuelimika kidogo basi wakakurupuka na kusema tunaweza kujitawala sasa kwani kila kitu kipo tayari. Wao njooni baada ya miaka kumi muone tutakuwa tumifikia wapi. Haya, baada ya miaka hiyo kumi kati ya viwanda vingi vilivyokuwa vikifanya kazi ni vichache tu vilivyokuwa vikizalisha kama ilivyo hapo awali. Tatizo lilikuwa ni nini? hatukuwa na wataalamu wa kutoka! Je ni kitu gani kilitufanya tukimbilie uhuru? Kwa kweli inauma ngoja niishie hapa. Zidumu fikra za mwenyekiti.
ReplyDelete